Barbara Gonzalez na Wallace Karia wateuliwa CAF

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,775
Reaction score
29,746
FB_IMG_16638671190320476.jpg

=====

Watanzania wanne wameteuliwa kuwa wajumbe kwenye Kamati mbalimbali za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ameteuliwa kuwa mjumbe kwenye Kamati mbili.

Kamati hizo ni ya Maandalizi ya Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) pamoja na Kamati ya Fedha.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athumani Nyamlani ameteuliwa kwenye Kamati ya Soka la Ufukweni (Beach Soccer).

Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Barbara Gonzalez ni Mjumbe katika Kamati ya Mashindano ya Klabu.

Mjumbe katika Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya CAF kutoka Tanzania ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha.
 
Tuacheni ushamba, kamati zoote za CAF wajumbe au viongozi wake wanatoka katika FA za nchi mbalimbali Afrika. Tumekua na wajumbe katika kamati za CAF tangu Enzi za Said Elmaamly, Leodigar Tenga n.k Tena wajumbe wa kudumu achana na awa ambao Leo unateuliwa kesho katibu wa CAf akiwa mwingine unaondolewa.
Lakini hiyo yote haijawahi kubadili kiwango Cha mpira wetu. Mabadiliko ya Soka letu hayataletwa na Teuzi za watu wetu uko Caf.
Kunahitajika viongozi safi wenye kuweza kushawishi uwekezaji na mazingira rafiki katika mpira wetu.
 
Ambao hao viongozi wanapatikana kwa mabingwa wa historia.
 
Tuacheni ushamba, kamati zoote za CAF wajumbe au viongozi wake wanatoka katika FA za nchi mbalimbali Afrika. Tumekua na wajumbe katika kamati za CAF tangu Enzi za Said Elmaamly, Leodigar Tenga n.k Tena wajumbe wa kudumu achana na awa ambao Leo unateuliwa kesho katibu wa CAf akiwa mwingine unaondolewa.
Lakini hiyo yote haijawahi kubadili kiwango Cha mpira wetu. Mabadiliko ya Soka letu hayataletwa na Teuzi za watu wetu uko Caf.
Kunahitajika viongozi safi wenye kuweza kushawishi uwekezaji na mazingira rafiki katika mpira wetu.
Punguza makasiriko acha watu wafanye kazi
 
Ndio unajua leo hiyo yote haijawahi kubadili kiwango cha mpira wetu?!

Hatutaki makasiriko yenu.
 
Nilichogundua;
Baada ya juzi Waziri kumteua Ally Mayai mwenye uyanga kuwa Kaimu Bosi kule kwenye Wizara ya michezo

CAF nao wamejibu mapigo; nao wamefanya teuzi toka kwa watu wenye mapenzi na Simba na Coast union.
 
Back
Top Bottom