Barbara na MO wakiziujulu Manara atarejea Simba?

Barbara na MO wakiziujulu Manara atarejea Simba?

Kwani Mo anaondoka kwenda wapi. Ana safari ya kwenda wapi. Nani alipata taarifa kutoka kwake au ni hisia binafisi. Wabongo bwana wanashindwa kufanya mambo ya msingi na kujadili mada jadidi za kimaisha badala yake wanaishia kumjadili mtu.
Hebu sema ukweli, huyu mo ndie ameomba yeye kuwa mdhamini Simba au Simba ndio wamemuomba mo awe mdhamini Simba?
 
Manara wa kwenu hakuna anayemtaka Simba bila kujali Babra na Mo wapi au wameondoka
Huo mkutano wa kumkataa manara simba mlikaa lini? wajumbe wangapi walimkataa kati ya wajumbe wangapi? usijitoe ufahamu, sema "mimi" simtaki manara sio useme "hakuna anaemtaka"
 
Kwa hiyo Manara akirudi Simba ana uwezo wa kuifadhili Simba? Wewe nadhani akili yako iko huko chini kwenye mbupu na makalio!
wewe kuna kitu umekikalia kina kusumbua. Manara si ndie aliyekuwa anawaimbisha nyinyi wote, "mara do or die" mara kile? alikuwa mfadhali wakati akiwaimbisha? Unajuwa wewe kwanini anafungiwa kila uchao?
 
kabla ya Mo na Babra, Simba haikuwepo? Manara yupo GSM anapiga kazi, Manara anaangalia Maslah tu wakimwita afanye nao kazi kwa dau zuri ataenda kwani we unamuonaje yule jamaa?
binafsi ninamsifu kwa hilo, wengine wanashangilia tu kama mazuzu wakati watoto wao wanapiga miayo. Mpira una fani nyingi sana ambazo kila mtu lazima anufaike nazo. Mpira lazima ukupe ajira kwa njia tofautitofauti kama vile wachezaji na viongozi kulipwa, mdhamini kujitangaza, kuuza wachezaji na zawadi za kushinda makombe, wachambuzi wa mpira, wauza jezi, wauza tiketi, wanaoonyesha na kutangaza mpira, wauza mavuvuzela, maji uwanjani na madaladala kupeleka watu uwanjani, mama ntile uwanjani, nk. Ukiona wewe unashabikia tu bila kuingiza chochote ujue wewe ni bwege.
 
Manara hatakiwi Simba hizi timu Zina tamaduni zake ambazo alizivunja
Huyu manara amefanya kufukuzwa tu na barbara, vinginevyo asingeondoka Simba, msikie mwenyewe akilalamikia kufukuzwa kwake, Barbara hayupo sasa, what next.

 
Huyu manara amefanya kufukuzwa tu na barbara, vinginevyo asingeondoka Simba, msikie mwenyewe akilalamikia kufukuzwa kwake, Barbara hayupo sasa, what next.


Nani amekuchagua kuwa msemaji wa Simba Sasa hivi unatakiwa kumzungumzia Manara na yanga yake Simba walishaachana naye
 
Huo mkutano wa kumkataa manara simba mlikaa lini? wajumbe wangapi walimkataa kati ya wajumbe wangapi? usijitoe ufahamu, sema "mimi" simtaki manara sio useme "hakuna anaemtaka"
Wewe ndio unajitoa ufahamu ulishasikia Kuna mtu kajitoa Simba sababu ya Manara
 
Kwavyovyote vile Manara anavinasaba na Simba, aliipenda Simba, alihudumu Simba na ana kadi ya Simba. Sote tunafahamu alifikaje Yanga aliko sasa hivi.

Je, kuondoka kwa Barbara na MO Simba kunaweza kumrudisha Manara Simba? Kwanini arudi Simba na kwani aendelee kubaki Yanga?
atalipwa na nani?
 
Huyu ni njaa tupu kama sisi
Hapana, njaa ndiyo inatufanya tufanyekazi sisi wote, na hii ni kwa viumbe vyote. Lakini Haji hakosi chakula ninavyomuona kwa macho ya nyama. Mtu mwenye wafuasi zaidi ya 4m Instagram bila shaka ni mtu maarufu kwa kibongobongo. Kwanini watu wana m follow, lazima anacho kitu cha ziada. Siku ya yanga day nilihudhuria wakati Haji ikijulikana kuwa amefungiwa na tefutefu asishiriki mpira. Yanga akawa na ma MC wengine pale uwanjani akina Dakota, Kitenge na Zimbwela ambao walionekana kupwaya kabisa pale uwanjani. ghafla Manara akaibukia uwanjani kutoka kusikojulikana, watu wooote walilipuka kwa shangwe na uhai ukarejea pale uwanjani. Nataka tu kusema mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, Manara anajua kuliko watu wengi sana kwenye tasnia yake.

Majina kama Mwamba wa Lusaka ambayo yanavuma hadi leo pale simba ni zao la huyu bwana. Manara anazifahamu haki zake na anajua kuzidai kitu ambacho wafanyakazi wa tanzania wakiwemo ma professor wakubwa wanashindwa kudai haki zao, wanapunjwa na waajili wao kama mazuzu na kuishia kutoa huduma hafifu na kupokea rushwa kutoka kwa wanaowahudumia kama njia mbadala ya kuishi.
 
Ninachokijua

Manar hana elimu ya kurud simba kilichomtoa ni unprofessional over
 
Back
Top Bottom