Hapana, njaa ndiyo inatufanya tufanyekazi sisi wote, na hii ni kwa viumbe vyote. Lakini Haji hakosi chakula ninavyomuona kwa macho ya nyama. Mtu mwenye wafuasi zaidi ya 4m Instagram bila shaka ni mtu maarufu kwa kibongobongo. Kwanini watu wana m follow, lazima anacho kitu cha ziada. Siku ya yanga day nilihudhuria wakati Haji ikijulikana kuwa amefungiwa na tefutefu asishiriki mpira. Yanga akawa na ma MC wengine pale uwanjani akina Dakota, Kitenge na Zimbwela ambao walionekana kupwaya kabisa pale uwanjani. ghafla Manara akaibukia uwanjani kutoka kusikojulikana, watu wooote walilipuka kwa shangwe na uhai ukarejea pale uwanjani. Nataka tu kusema mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, Manara anajua kuliko watu wengi sana kwenye tasnia yake.
Majina kama Mwamba wa Lusaka ambayo yanavuma hadi leo pale simba ni zao la huyu bwana. Manara anazifahamu haki zake na anajua kuzidai kitu ambacho wafanyakazi wa tanzania wakiwemo ma professor wakubwa wanashindwa kudai haki zao, wanapunjwa na waajili wao kama mazuzu na kuishia kutoa huduma hafifu na kupokea rushwa kutoka kwa wanaowahudumia kama njia mbadala ya kuishi.