Barbershop girls pose a new threat to marriage

hahahaha, nimefurahishwa sana na hiyo sentensi kiongozi. sio wewe tuu inawatokea wengi...imagine anakusugua shingoni kama anaelekea mabegan halafu wanatumia muda mwingi sana. mim huwa nawaambia basi unatosha. wengine wanakupaka mpaka lip balm. kweli kunahitaji ujasiri na uvumilivu wa hali ya juu huko barbershops

 
Haya weee....yale yale, hawa watu wanaojiita wazaire ndo sitaki kabisaaa kuwasikia:angry:



 
Kwa sie 'wagonjwa' wa vifua, ukiegeshwa pale kifuani unatamani zoezi lisiishe mapema..lol.

But on a serious note,ipo haja ya kuanza kuregulate hii biashara kwa ukaribu zaidi....risk inayopose kwa afya ya jamii inaakuwa kubwa. Usafi, aina ya vipodozi na namna wanavyotoa huduma hizi za salon... kwa hakika vinahitaji kutizamwa kwa karibu ili kuilinda jamii.
 
Hawa wa kina dada ni hatari, week end hii kuna mmoja alikuwa anaomba namba yangu ya simu pale Sinza Mori, pamoja na kumwambia kwamba sikai Dar lakini akawa ameniganda anataka namba na vituko vilikuwa wakati wa scrub, niliondoka bil kudai chenji...
 

Kuna ujumbe uliofichika hapa. I bet your former bf is your hubby now.
 
Kiukweli ukiwa MWENDEKEZAJI wa Totoz (hasa za kusomba njiani) hawa wa barbershop hutowaacha!!! Wanajua kujilegeza na kutia majaribu makubwa sana katika sehemu ya kazi yao!! Huna ushahidi kuwa anakujaribu ila kwa mwenye akili timamu huhitaji KUAMBIWA KARIBU KULA🙂

Ni wewe mwenyewe na roho yako!! Siyo kila tunapokwenda BAR tutoke na Bar maid.....
 
kwa kweli hizi Barbershop ni wizi mtupuu sio kwa kina dada tu( maana hawa ni wezi wa waume na wachumba za watu) hata kwa kina kaka mabraza men wanaofanya kazi ya kunyoa nywele, maana week end hii nilienda pale Victoria kwenye kona ya kwenda mwenge kuna saloon pale niliingia kunyoa na kufanya srub, baada ya kumaliza kila kitu yule dada akanimbia vipi jamaa kakwambia bei nikamuuliza yuko wapi nimlipe? yuledada "akasema ametoka" nikamuuliza shilingi ngapi? akaniambia elfu kumi na mbili, nikamuuliza yaani nimenyoa upara na kufanya scrub ndio bei yote hiyo? akasema ndio nikampa ile pesa nikaoondoka.
huu ni wizi katika ma sallon na nimesema sitarudi tena katika saloon ile tena.
 

Conclusion: Many barbershop have been turned into commercial sex zones, men’s are not dealing with Barmaid, and this is the threat for many marriage.

Dah! Barbershops was the most safest place ukiagwa akija unakagua kichwa..
Naona tumeongezewa sehemu nyingine pa kua wary....

Kweli it is hard being a wife in Dar and most difficult to be a man...
 
Mh... sis'

Yani kila kinachompa mwanaume comfort sasa si kitakua threat to marriage?? to me a threat to any marriage is the marriage itself!

MTM...hapa umeongea kaka yangu...kusema ukweli tunakoelekea itakuwa hata wanawake wanaoendesha magari na vimini mapaja wazi tutaimba kuwa ni threat kwa ndoa zetu. Mimi nafikiri ni muhimu tukaziangalia nasi namna tunavyoziendesha na kuzihadle ndoa zetu. Kama mtu ukiwa na mumeo ndani mnapetiana petiana, mara moja moja mnascrubiana na kupeana massage kwa mpangilio maalumu ........hivi kweli ataona nini cha ajabu akienda scrubiwa na hao vinyozi??

I think there is a need of evaluating and renewing and updating the art of loving within our marriages......hii mambo ya kuwa tunaoana, tunapata familia, tunatafuta maisha.......thats enough......... tuyaache. mara moja moja tujipendelee (kama tulivyo shauriwa na Mbu) tuzipe uhai ndoa zetu! Ama sivyo duh tutatishiwa mpaka na wanyama wasovaa nguo
 
Reactions: Mbu
Kuku ni kuku tu hawezi kuwa bata!
 

Mie siku hizi nakaa pembeni mwa Tanzania, hivi karibuni nilingia mjini huko Dar, nimejionea mwenyewe hali ilivyo tete katika hizo barber shops. Yaliyosemwa hapa nakubaliana nayo. Laiti kama siyo u-solid wangu nilikuwa matatani. Namshukuru Mungu nilitoka salama salimin. Majaribu mengine ni makubwa kiasi cha kushindwa kuvumilia. Kama kaka una ndoa yako ni vyema ukajiandaa kisaikolojia unapokwenda kwenye hizo barber shops, ukiingia kichwa kichwa bila shaka utafanya ngono isiyotarajiwa. Hao akina dada wenyewe ni hatari, hebu tafakari ni wateja wangapi wanahudumiwa pale kwa siku, ni wangapi wanafanya nao ngono? Je wote hawa wanajali hasa ukizingatia hakuna maandalizi ya kufanya kitendo hicho? Bila shaka wengi hawajali na kama itafanyika research zaidi ya 60% watakuwa wameathirika. Chonde chonde ndugu usipoteze maisha yako kwa tamaa za muda mfupi zilizoamshwa bila matarajio.
 
...my soulmate is a masseuse, she is a barber, she is a manucurist... Shauri zenu nyie wenye mioyo midogo na saloon lazima!
 
...my soulmate is a masseuse, she is a barber, she is a manucurist... Shauri zenu nyie wenye mioyo midogo na saloon lazima!
Mbu huyu soulmate mpya unampenda sana eeee, kama unampenda mwachishe hiyo kazi kuna mabazazi ya kufa mtu, yanaweza yakambadili ukajutia tena nafsi, sipendi kukuona unasuffer tena kama kipindi kileeeeeeee
 
...ha ha, Gaga, tatizo sio soulmate. Binafsi nishakwenda sana saloon za uchokozi, wanavisa sana wale kina dada lakini kama lengo nia na madhumuni ya kwenda saloon yalikuwa kunyoa nywele na ndevu, sikuwahi kudhalilishwa nao hata siku moja.

Mara ya mwisho nilikuwa nakwenda saloon moja pale mwenge. Mdada hajui maskini, yeye hufinya hasa..nami ndo nilikuwa namchagua kwani anakata kabisa stimu!
 
Nasikia Wazaire wanaotengeneza kucha wanakufunika taulo wanafanya massage za miguu mkono unapenyezwa mpaka karibu kabisa na chu*i kwa muda wa kama nusu saa. Walio pembeni hawajui kinachoendelea. Massage ikiisha hapo dada anarembua, Mzaire ana erection. Na pia wapo watoa massage kwa wanawake ambao ni wanaume, basi safari za saluni ndiyo maana haziishi.
 
Yusufu alipo ona mke wa mfalme anataka kumbaka alikimbia,wewe je.Unasubiri mpaka ubakwe,run!Kama usipokimbia unataka wakubake ,don't complain.Kwanza why should you go to such horrible places if you like and respect yourself.Umejipeleka mwenyewe kwenye mdomo wa Simba,
ngoja akutafune.
 
aisee 'chungu kama ngorotik', hiyo fleva imekaaje aisee?
 
Mghhhhhhhhh kuna mwanaume anabakwa
 
...my soulmate is a masseuse, she is a barber, she is a manucurist... Shauri zenu nyie wenye mioyo midogo na saloon lazima!

Lucky is her kwa kweli..........but ina maana she is working huko kwa babashopu au huduma hiyo waipata kwake? maana hii tungo tata kaka!
 
Reactions: Mbu
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…