Unamfahamu Ronaldinho Gaucho?
Alicheza Barcelona, akaondoka Barcelona ikabaki kua moja ya timu bora kabisa katika historia ya mpira wa miguu.
Labda tu nieleze kidogo.
Katika mpira wa miguu, huwezi kumreplace world class player yeyote!
Ni nani alieweza kumreplace Ronaldo De Lima?
Nani kamreplace Zinedine Zidane?
Nani kamreplace Xavi Hernandez?
Jibu ni hakuna.
In football, we don't seek to replace players. Mpira wa miguu unamifumo mingi ambayo hubadilika kutokana na hali iliyopo.
Neymar ni mmoja kati ya vipaji vikubwa katika ulimwengu wa soka. Lakini kuondoka kwake sio mwisho wa barca kushinda makombe.
Aliondoka Xavi, lakini barca ikashinda treble.
Kwenye Mpira, mfumo ambao timu inautumia ndio msingi mkuu na sio mchezaji mmoja mmoja.
- KANA -