Barclays is closing down 7 branches and Standard Chartered two branches are closed in Kenya.

mulisaaa

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2017
Posts
6,969
Reaction score
7,027
Kenya uchumi unayumba ukizingatia migomo inaongezeka ya kazi. Kutoka kwa manesi nasasa wakufunzi wa vyuo wanagoma wakiitaji pesa. Nikama serikali ya Jubilee imeshindwa kuendesha nchi. Na sasa tunaona international banks zinafunga branch zao kwa wingi. Je NASA ndosuluhisho??
 
Tatizo ni lugha au ni uvivu wa kusoma? Kwa maelezo kutoka website ya Barclays na wewe mtoa mada umeweka screenshot ni kwamba branches zinamaamishwa na kupelekwa sehemu zinapohitajika zaidi, wafanyakazi wataamishiwa kwenye hizo branches mpya.
Acha kupotosha watu...
 
Wewe ndio mgumu wa kuelewa kweli, "jobs at risk" unadhani walimaanisha nini au ndo unajipa moyo..!!??
 


Ati uchumi wa Kenya unayumbayumba? Ha! You wish. Uchumi wa Kenya unakuwa kwa asilimia 6% kwa mwaka, unayumbayumba wapi?

Tangu ujifunze kutake screenshots hivi majuzi, umekuwa ukitumia huo uwezo visivyo!

Habari ndio hii...

Barclays set to exit African business
 
Mtoa mada ni mpotoshaji mkubwa,hii bank BARCLAYS ipo katika kipindi cha mpito ambacho kinatokana na bank mama ya UINGEREZA kuuza hisa zake hasa hili tawi la AFRICA,tutashughudia mabadiliko makubwa kwa bank hii ndani ya AFRICA,kuna uwezekano mkubwa kwa ABSA(SA) kuwa itakuwa mmiliki mkubwa wa hii BARCLAYS TAWI LA AFRICA,kwa hiyo ufungaji na shifting ya branches ndani ya KENYA utatokea hadi kwetu,ila wenye accounts wasiwe na wasiwasi their money will be safe.
 
Uelewe barclays is planning to exit African market in 3yrs...it got nothing to do with Kenya's economy
 
Walipeni basi pesa kama mpo vizuriView attachment 535170
Bongo umesha sikia mgomo?? Au international bank kufunga branch??
Migomo hufanyika kila mahali, haimanishi nchi iko taabani kiuchumi. Hawa wanaogoma wanapigania maslahi yao tu.

Inasemekana ya kwamba wafanyi kazi wa umma Kenya wanapata mshahara nyingi kuliko hawa wa Tanzania, madaktari Kenya hata kabla ya kuongezewa mshahara baada ya ule mgomo walikuwa wakipata mshahara zaidi ya 2x ya watanzania.
Hata hawa manesi nasadiki wanapata mshahara zaidi ya wenzao wabongo.

Lakini wako mgomoni kutokana na mkataba fulani walipitisha na serikali ambayo haijapata kutimizwa.

Kwahivi komesha huu upoteshaji, benki ya Barclays ilipanga tangu mwaka jana kuexit Africa kutokana na sababu zao, sio eti kwasabu uchumi wa Kenya ama taifa lolote lile barani ina matatizo ya kiuchumi. Kama ni hivyo, wangekuwa wametoka Kenya kiyambo sana, nyakati zile uchumi wa Kenya haukuwa ukikuwa hata kwa 1%
 
Walipeni basi pesa kama mpo vizuriView attachment 535170
Movie yenu ya vichwa vya treni vibovu imefikia wapi, naskia TRL wamevikana ilhali vina rangi zao.

Hiyo nchi yenu kama bongo movie vile, yaani vichwa vya treni hadi vinashushwa kutoka kwa meli na haijulikani mmliki nani. Ndio maana mnaliwa kwenye madini hadi mumebaki mahandaki matupu na umaskini mwingi. Mnaishi kwa kiki na vioja kila siku...mkae na kujiuliza aliyewaroga kama bado yupo.

 
Mimi binafsi kama mteja wa Barclays, nilipata julisho kupitia SMS na bila shaka kwenye barua rasmi kuhusu kuhama tawi langu la Moi Ave hadi Queensway. Kwa hiyo najiandaa kuenda hilo tawi mpya kila mara. Mleta mada una upuzi wa kimataifa, au labda kiingereza changamoto. Soma taarifa yako tena, na ujionee jinsi unavyotia aibu bila usaidizi wowote.
 
Hii ni vituko, yaani locomotive zima linafika na hawajui nani mmiliki?
 
hahahaaa...pengine wamebadilisha rangi ya manjano,samawati na kijani....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…