Ndumbayeye
JF-Expert Member
- Jan 31, 2009
- 7,413
- 4,020
Wakuu nilifungua akaunti mpya barclay kwa sh. 50000 januari 2009, leo naangalia salio nakuta 12000, gharama zao zikoje kwa mwenye kujua?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wakuu nilifungua akaunti mpya barclay kwa sh. 50000 januari 2009, leo naangalia salio nakuta 12000, gharama zao zikoje kwa mwenye kujua?
Mkuu hujaeleza ni account gani ulifungua..kuna account za aina tatu hapo...kwa kuangalia tu ulivyo changanyikiwa..utakuwa ulifungua ile account ya makato ya 10,000 kwa mwezi..na hujaangalia leo utakuwa uliangalia mwezi ulio pita.....so ungefungua ule ya makato 3500 kwa mwezii usinge kuja na malalamiko hayo..au ulikwenda na pesa mingi pale....
Wakuu nilifungua akaunti mpya barclay kwa sh. 50000 januari 2009, leo naangalia salio nakuta 12000, gharama zao zikoje kwa mwenye kujua?
Nashanga.......Yaani unaweka ela benki halafu inakatwa..!
Tz kweli ni shamba la bibi..lol
Nashanga.......
Yaani unaweka ela benki halafu inakatwa..!
Tz kweli ni shamba la bibi..lol
Nafikiri ni bora kuwa safe cabinets ndogo ndogo kwa kuhifadhi pesa otherwise it does not make sense at all. Ukikopa fedha benki riba kibao. Ukiweka fedha hasa hii BARCLAYS riba sifuri. Wezi kweli kweli na maana nzima ya kibenki inaisha. Kwa msingi huu kukomboka na umaskini ni tabu kabisa.
Du! enzi za Julius ukiweka fedha nbc kila mwezi unawekewa interest, lakini sasa ukiweka akaunti ya akiba wewe ndo utawalipa benki kila mwezi mpaka kisumni kiishe!
Ndumbayeye,
Barclays ni benki ya matajiri. Kima cha chini cha makato kutokana na maoni ya watu wengine hapa inaonekana ni 3000/= kwa mwezi. Kutokana na utafiti wangu mdogo nimegundua kuwa benki isiyo na makato mengi kwa TZ kwa sasa hivi ni Exim. Hawakati kwa mwezi wala hawakati ukichukua pesa zako na wanakupa faida ya 2% kwa mwaka kwa akaunti ya akiba (savings akaunti) labda wawe wamebadilika hivi karibuni. NMB wao hukata 200/= kila mwezi wakati CRDB wao hukata 400/= kila mwezi na kila ukichukua pesa hukata 300/= iwe kwenye kaunta au kwenye ATM.