Barclays: Nimekoma!

Barclays: Nimekoma!

Ndumbayeye

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2009
Posts
7,413
Reaction score
4,020
Wakuu nilifungua akaunti mpya barclay kwa sh. 50000 januari 2009, leo naangalia salio nakuta 12000, gharama zao zikoje kwa mwenye kujua?
 
Mkuu hujaeleza ni account gani ulifungua..kuna account za aina tatu hapo...kwa kuangalia tu ulivyo changanyikiwa..utakuwa ulifungua ile account ya makato ya 10,000 kwa mwezi..na hujaangalia leo utakuwa uliangalia mwezi ulio pita.....so ungefungua ule ya makato 3500 kwa mwezii usinge kuja na malalamiko hayo..au ulikwenda na pesa mingi pale....
 
Katika kila bank kuna account za aina mbalimbali, ni vyema kwa mtu yeyote ambaye anafungua account ajue features na charges zote za hiyo account, most of the time they will try to push you into opening a certain type of account ambayo ina maslahi zaidi kwao but its your choice, kwa uhakika zaidi ni vizuri siku ya kwanza uchukue hata bronchures au leaflets ukazisome fresh, uamue account gani inakidhi matakwa yako then urudi siku nyingine ndo ufungue hiyo account.
 
Mkuu hujaeleza ni account gani ulifungua..kuna account za aina tatu hapo...kwa kuangalia tu ulivyo changanyikiwa..utakuwa ulifungua ile account ya makato ya 10,000 kwa mwezi..na hujaangalia leo utakuwa uliangalia mwezi ulio pita.....so ungefungua ule ya makato 3500 kwa mwezii usinge kuja na malalamiko hayo..au ulikwenda na pesa mingi pale....

Yaani unaweka ela benki halafu inakatwa..!

Tz kweli ni shamba la bibi..lol
 
Wakuu nilifungua akaunti mpya barclay kwa sh. 50000 januari 2009, leo naangalia salio nakuta 12000, gharama zao zikoje kwa mwenye kujua?

ndumbayeye, ulufungua akaunti ya aina gani? kuna prestige akaunti na kuna standard akaunti. prestige wanakata 12,000/= kwa mwezi na standard wanakata 3,000/= kwa mwezi.
 
Yaani unaweka ela benki halafu inakatwa..!

Tz kweli ni shamba la bibi..lol

Nafikiri ni bora kuwa safe cabinets ndogo ndogo kwa kuhifadhi pesa otherwise it does not make sense at all. Ukikopa fedha benki riba kibao. Ukiweka fedha hasa hii BARCLAYS riba sifuri. Wezi kweli kweli na maana nzima ya kibenki inaisha. Kwa msingi huu kukomboka na umaskini ni tabu kabisa.
 
Taib,

Kiukweli hamna sababu ya msingi ya benki kumkata ela mteja. Huu ni uwizi wa mchanamchana, na waTz nadhani dunia nzima waizi wanaambizana 'twendeni TZ..shamba la bibi !'. Hebu tuzingatie haya;

1. Cash card inakula kwa mteja, ingawa wanaandika disclaimer kabisa eti kadi ni mali ya benki! Tena kadi yenyewe unazungushwa kichizi kuipata.

2. Ukitumia ATM inakula kwa mteja!

3. Gharama za stationary, inakula kwa mteja!

4. Baadhi ya benki, ukituma ela hapahapa nchini ,inakula kwa mteja!

5. Kuna baadhi ya benki, ukifungua akaunti kwenye matawi fulanifulani wanakata extra fees.

Yaani ni tabu moja kwa moja.
 
Du! enzi za Julius ukiweka fedha nbc kila mwezi unawekewa interest, lakini sasa ukiweka akaunti ya akiba wewe ndo utawalipa benki kila mwezi mpaka kisumni kiishe!
 
tuwe na uzalendo zaidi wa kufungua akaunti katika mabenki ya kizalendo-NMB ,TPB nk
 
Du! enzi za Julius ukiweka fedha nbc kila mwezi unawekewa interest, lakini sasa ukiweka akaunti ya akiba wewe ndo utawalipa benki kila mwezi mpaka kisumni kiishe!

Ndumbayeye,
Barclays ni benki ya matajiri. Kima cha chini cha makato kutokana na maoni ya watu wengine hapa inaonekana ni 3000/= kwa mwezi. Kutokana na utafiti wangu mdogo nimegundua kuwa benki isiyo na makato mengi kwa TZ kwa sasa hivi ni Exim. Hawakati kwa mwezi wala hawakati ukichukua pesa zako na wanakupa faida ya 2% kwa mwaka kwa akaunti ya akiba (savings akaunti) labda wawe wamebadilika hivi karibuni. NMB wao hukata 200/= kila mwezi wakati CRDB wao hukata 400/= kila mwezi na kila ukichukua pesa hukata 300/= iwe kwenye kaunta au kwenye ATM.
 
Bank ya Postal makato yao yakoje? Pse anayejua anifahamishe.
 
Ndumbayeye,
Barclays ni benki ya matajiri. Kima cha chini cha makato kutokana na maoni ya watu wengine hapa inaonekana ni 3000/= kwa mwezi. Kutokana na utafiti wangu mdogo nimegundua kuwa benki isiyo na makato mengi kwa TZ kwa sasa hivi ni Exim. Hawakati kwa mwezi wala hawakati ukichukua pesa zako na wanakupa faida ya 2% kwa mwaka kwa akaunti ya akiba (savings akaunti) labda wawe wamebadilika hivi karibuni. NMB wao hukata 200/= kila mwezi wakati CRDB wao hukata 400/= kila mwezi na kila ukichukua pesa hukata 300/= iwe kwenye kaunta au kwenye ATM.

Barclays ni international bank na wanadai huduma inayotolewa nchi zote kwenye matawi ni sawa. Hivyo basi kama wana acount zinazochargiwa Tshs.3000 watakuwa hawako fair. kwani haitalingana na charges wanazocharge nchi nyingine. Mimi nina Saving Account Barclays wanancharge £5 kwa mwezi hivyo kama wanawachargi chini ya Tshs.10,000 basi hawatutendei haki huku kwa queen.
 
Back
Top Bottom