nikatoa kitu kidogo ...huduma iende spidi ikawa hola
kwa nini hukufungua branch nyingine umewang'ang'ania? halafu unaniharibia siku kwa kusema umetowa RUSHWA...🙁Jamani...
Sijui tatizo kama ni langu na watu walio karibu yangu..au ni vipi....kwa kweli huduma za benki za Barclays zinanitia kichefuchefu mno....
Nimejaribu kufungua akaunti personal sasa yapata mwezi wa tatu haijawezekana.... tena baada ya kuchoshwa na tawi la Ubungo plaza ..nikatoa kitu kidogo ...huduma iende spidi ikawa hola (mhusika jina ninalo)..nikajaribu tena tawi la pale Sea Cliff...usumbufu nilioupata nimenyoosha mikono...
Kama haitoshi ikatokea NGO ninayojishughulisha nayo imepewa msaada wa hela (cheque) na sababu hatukuwa na akaunti tuka jaribu kufungua akaunti pale Barclays downtown....tangu December 2009 mpaka leo...leta hiki, leta kile, haukuleta kile, sasa ulete kile, baada ya wiki uje mambo yatakuwa tayari... ukienda unakuta kimtu kingine kabisa kinakwambia ulisahau kuleta kile... basi..stori goes on and on!!!!...kutwa kuchwa.... sometimes simu wanapiga lakini hakuna kinachoendelea...
Baada ya kuchoshwa nikawa nalalamika mbele ya watu wachache,... kumbe nao yamewakuta kama haya.... nimeambiwa nisithubutu tena...ndivyo walivyo....kumbe hata hatua ya kufungua matawi mengi ni very hopeless move sasa nimekubali....sina uhakika kama uongozi unayajua haya... nimewanyooshea mikono...tunajiuliza hivi na nchi nyingine wapo hopeless hivi hivi? nimenawa...
Zamazamani nawe ni fisadi?
Fisadi sio anaepokea pekee bali hata mtoajio rushwa nae nifisadi, Kitendo cha Zamazamani kutoa rushwa iliafunguliwe account kinanipa wasiwasi sana, akiwa yeye kama mmoja wa viongozi wa NGO, wasiwasi wangu ni:
1) Atawezaje kuongoza NGO kwa kutoa rushwa badala ya kukemea? maadili yako wapi?
2) NGO yako inhusika na mambop gani?
3) Rushwa uliyotoa utaiweka kwenye P&L/Balancesheet ya NGO au inatoka kwenye mshaharawako?
Naomba majibu.
karibu sana Diamondtrust Bank,tawi lolote lile unakaribishwa
Waungwana nimerudi.....sikuwepo muda mrefu poleni....jamani...hebu sikilizeni,tumieni akili na MSIWE WANAFIKI:...NGO yetu ina deal na watoto yatima..tulipewa cheque kama msaada kwa ajili ya watoto ili tuweze kuwapa mahitaji yao ya lazima ya kila siku ikiwa pamoja gharama za shule ....benki ambayo ni convinient kwetu kimazingira ni Barclays ..na kwa kuwa hatukuwa na akaunti ya chama na kwa kuwa hatukutegemea kupata ugumu kama tulioupata ,nikawashauri wenzangu tufungue akaunti Barclays...just imagine ni cheque ya Septemba mwaka jana ....kwa hiyo tangu kipindi hicho mpaka nilipoandika hoja yangu kwa mara ya kwanza..ilishapita kama miezi mitatu...lakini katika kipindi hicho usumbufu ulikuwa mwingi sana ..ila kila mara tulikuwa tukihakikishiwa akaunti itakuwa tayari soon!!!muda ukaenda na ukaenda...bahati mbaya signatories wengine walikuwa na majukumu mengine huku wakiamini mambo ya akaunti yapo shwari..,haikuwa rahisi kuwapata tena wote ili tufungue sehemu nyingine...narudia tena...sababu pale tulihakikishiwa !!!!.Wakati huo huo watoto kule kituoni wanateseka na njaa na wengine wameshindwa kwenda shule sababu ya kukosa mahitaji muhimu...kama uniform,madaftari,nauli nk....hivyo tumekuwa tunakopa au kutoa mifukoni mwetu wakati hela ipo ila hatuwezi kuitumia....ni katika mchakato huo basi ikabidi tuwaulize wanataka kitu gani ili tuimalize fedheha hii.... labda 'soda'....nikamwambia yule mfuatiliaji labda akimpa soda mhusika mambo yatakwenda(KAMA ILIVYO MILA NA DESTURI YETU!,WACHENI UNAFIKI HAPA!!!!)..soda alipewa na danadana ikaendelea..(sasa ilifika kipindi tukaanza kumdai yule tuliyempa hela ya kutoa soda labda hakutoa ndio maaana tunapata kadhia hii!!!)...anyway...lakini mungu si athumani...pamoja na kwamba pale tulichemsha...documents zilezile tumetumia kufungua akaunti benki nyingine baada ya wiki tatu...(juzi tarehe 8 ) ingawa bado kunataratibu za kibenki zinamaliziwa...
BULL --- UMENICHEKESHA SANA KUBEBA BANGO KUHUSU BRIBE,KWANI UNAISHI WAPI WEWE???
JE UNGEKUWA WEWE KATIKA MAZINGIRA KAMA HAYA YETU UNGEFANYA NINI???
kioja kilichomchangaza mtu yoyote ni kutoa bribe ili akaunti ifunguliwe[itakuwa iliwafanya wakutilie shaka motives zako]....kwa sababu siku hizi mabenki yanabembeleza watu wafungue akaunti..iweje uwape pesa..!!..hata ukienda pale sokoni kariakoo kwa wale wanaofungulia akaunti wateja kwenye miavuli....ukiwapa pesa ..watapokea lakini ni lazima watakushangaa sana na watamuambia supervisor wao..utakuwa blacklisted[ushauri wa bure]...kwani watu wa benki siku hizi wanafungwa sana...na hiyo pesa uliyowapa walihisi itawatokea puani ...ikitokea mfano umeiba...kuanzia aliyefungua akaunti ,meneja hadi teller huwa wanaisaidia polisi ...lazima waogope!!pole..kama hukua na nia mbaya!!
\Unarun NGO kwa misaada halafu unafungua account kwa kutoa rushwa. Credibility yako iko wapi? I'm building some doubt here bro..
\
Veery credible......wakale walisema "Penye uzia penyeza rupia" ...unafikiri walikuwa wajinga??? Yaani watoto wafe na njaa ,washindwe kwenda shule kwa sababu ya vizingiti vya kijinga???? ...mazingira yenyewe yalionyesha hivyo..ingawa hatukufanikiwa!!!!...Just keep on building doubts there.....