Waungwana nimerudi.....sikuwepo muda mrefu poleni....jamani...hebu sikilizeni,tumieni akili na MSIWE WANAFIKI:...NGO yetu ina deal na watoto yatima..tulipewa cheque kama msaada kwa ajili ya watoto ili tuweze kuwapa mahitaji yao ya lazima ya kila siku ikiwa pamoja gharama za shule ....benki ambayo ni convinient kwetu kimazingira ni Barclays ..na kwa kuwa hatukuwa na akaunti ya chama na kwa kuwa hatukutegemea kupata ugumu kama tulioupata ,nikawashauri wenzangu tufungue akaunti Barclays...just imagine ni cheque ya Septemba mwaka jana ....kwa hiyo tangu kipindi hicho mpaka nilipoandika hoja yangu kwa mara ya kwanza..ilishapita kama miezi mitatu...lakini katika kipindi hicho usumbufu ulikuwa mwingi sana ..ila kila mara tulikuwa tukihakikishiwa akaunti itakuwa tayari soon!!!muda ukaenda na ukaenda...bahati mbaya signatories wengine walikuwa na majukumu mengine huku wakiamini mambo ya akaunti yapo shwari..,haikuwa rahisi kuwapata tena wote ili tufungue sehemu nyingine...narudia tena...sababu pale tulihakikishiwa !!!!.Wakati huo huo watoto kule kituoni wanateseka na njaa na wengine wameshindwa kwenda shule sababu ya kukosa mahitaji muhimu...kama uniform,madaftari,nauli nk....hivyo tumekuwa tunakopa au kutoa mifukoni mwetu wakati hela ipo ila hatuwezi kuitumia....ni katika mchakato huo basi ikabidi tuwaulize wanataka kitu gani ili tuimalize fedheha hii.... labda 'soda'....nikamwambia yule mfuatiliaji labda akimpa soda mhusika mambo yatakwenda(KAMA ILIVYO MILA NA DESTURI YETU!,WACHENI UNAFIKI HAPA!!!!)..soda alipewa na danadana ikaendelea..(sasa ilifika kipindi tukaanza kumdai yule tuliyempa hela ya kutoa soda labda hakutoa ndio maaana tunapata kadhia hii!!!)...anyway...lakini mungu si athumani...pamoja na kwamba pale tulichemsha...documents zilezile tumetumia kufungua akaunti benki nyingine baada ya wiki tatu...(juzi tarehe 8 ) ingawa bado kunataratibu za kibenki zinamaliziwa...
BULL --- UMENICHEKESHA SANA KUBEBA BANGO KUHUSU BRIBE,KWANI UNAISHI WAPI WEWE???
JE UNGEKUWA WEWE KATIKA MAZINGIRA KAMA HAYA YETU UNGEFANYA NINI???