Bariadi: Askari polisi aliyegonga gari la RPC Chatanda afariki dunia

Laana inawatafuna jeshi la Polisi wanaanza kupasuana wenyewe. Ewe Mwenyezi Mungu tuamulie huu ugomvi kati yetu na jeshi la Polisi
 
Timoth Philipo, askari polisi wilayani Busega amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Mkoa wa Simiyu baada ya gari alilokuwa akiendesha kugongana na gari lililokuwa likiendeshwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Blasius Chatanda.

Taarifa iliyotolewa na kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Shadrack Masija leo Jumatano Oktoba 5, 2022 inaeleza kuwa ajali hiyo ilitokea Oktoba 2, 2022 eneo la Mizani Nyakabindi ikimhusisha Chatanda na Philipo.

"Toyota Harrier ilikuwa ikiendeshwa na ACP Chatanda iligongwa na Toyota Mark II ikitokea Bariadi kwenda Lamadi ikiendeshwa na Philipo na kusababisha majeraha kwa madereva wote wawili pamoja na H. 7123 Pc Emmanuel ambaye ni msaidizi wa Chatanda," amesema.

Amebainisha kuwa majeruhi wote walifikishwa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya matibabu na kubainisha kuwa chanzo cha ajali ni uzembe wa Philipo ambaye alihama upande na kwenda upande wa kulia na kisha kuligonga gari liliokuwa likiendeshwa na Chatanda.

Amesema Philipo alifariki dunia Oktoba 3, 2022 akiwa anapatiwa matibabu ikielezwa kuwa sukari ilishuka.
Katika taarifa hiyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limetoa pole kwa ndugu na familia ya marehemu na taratibu za mazishi zinafanyika kwa kushirikiana na familia na mwili utasafirishwa kwenda Wilaya ya Magu Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya mazishi.

Chanzo: Mwananchi
Hii inaitwa "MBWA KALA MWANAE"
 
Watuambie chanzo cha ajali na ni nani alikuwa mzembe. Ajali za kugongana mara nyingi mmoja wa madereva kafanya uzembe wa kutofuata sheria. Sasa nani alifanya hivi kati ya hawa wawili, maana wao wanajua kulima watu fine -- ooh ume-overtake kwenye solid line. Sasa nani kasababisha hii ajali hapa ikiwa wote wawili wanapaswa kuwa vinara wa kufuata sheria?
Chatanda, ila Bwana ameshampumzisha.
 
Inasikitisha kifochochote kutokea, kiwe cha raia a,a cha mlinda usalama upande wangu ninaona tumepoteza Mtanzania mwenzetu.

Natoa pole kwa jeshi la polisi na familia ya marehemu.
 
Sas huko lamadi kunaa magari gani had wagongane uso kwa uso

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Mkuu huyo askari alikua kalewa sana maana pia walimpima kiwango cha ulevi kilikua juu, yeye ndo mwenye makosa alihama njia na kifata gari la RPC japo rpc alipata tuu michubuko kdgo akatibiwa na kuruhusiwa wala sio kwamba kasingiziwa.
 
Timoth Philipo, askari polisi wilayani Busega amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Mkoa wa Simiyu baada ya gari alilokuwa akiendesha kugongana na gari lililokuwa likiendeshwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Blasius Chatanda.

Taarifa iliyotolewa na kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Shadrack Masija leo Jumatano Oktoba 5, 2022 inaeleza kuwa ajali hiyo ilitokea Oktoba 2, 2022 eneo la Mizani Nyakabindi ikimhusisha Chatanda na Philipo.

"Toyota Harrier ilikuwa ikiendeshwa na ACP Chatanda iligongwa na Toyota Mark II ikitokea Bariadi kwenda Lamadi ikiendeshwa na Philipo na kusababisha majeraha kwa madereva wote wawili pamoja na H. 7123 Pc Emmanuel ambaye ni msaidizi wa Chatanda," amesema.

Amebainisha kuwa majeruhi wote walifikishwa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya matibabu na kubainisha kuwa chanzo cha ajali ni uzembe wa Philipo ambaye alihama upande na kwenda upande wa kulia na kisha kuligonga gari liliokuwa likiendeshwa na Chatanda.

Amesema Philipo alifariki dunia Oktoba 3, 2022 akiwa anapatiwa matibabu ikielezwa kuwa sukari ilishuka.
Katika taarifa hiyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limetoa pole kwa ndugu na familia ya marehemu na taratibu za mazishi zinafanyika kwa kushirikiana na familia na mwili utasafirishwa kwenda Wilaya ya Magu Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya mazishi.

Chanzo: Mwananchi
Huyu askari ni tofauti na yule aliefariki kwa ajali juzi hapo hapo lakini ni askari wa Maswa na atazikwa Kisesa Magu?
 
Mkuu huyo askari alikua kalewa sana maana pia walimpima kiwango cha ulevi kilikua juu, yeye ndo mwenye makosa alihama njia na kifata gari la RPC japo rpc alipata tuu michubuko kdgo akatibiwa na kuruhusiwa wala sio kwamba kasingiziwa.
Ndio huyu alieagwa Leo Maswa na wanasafirisha mwili kwenda kuzika Kisesa Magu?
 
Ila kusema sukari ilishuka[emoji848][emoji848] kua alikua hali chakula au alikua na tatizo la sukari.
Kama ni huyo inasemekana alikuwa chapombe kutokana na stress za kuzinguana na mkewe na mpaka anafariki mkewe hawakuwa pamoja yaani mke Hana hata mawasiliano na ukweni na hapajui so ikawa wanatafuta ufumbuzi wapi akazikwe maana hawapajui na mke hapajui...
Mungu atusaidie sana haya maisha ya kuishikisela kutana kimjini mjini
 
Yawezekana sababu ni hawa askari kujikuta Sheria za barabarani hazi wahusu Wana fanya wanavyo jisikia, hapo ni both team to score 🚶🚶🚶🚶🚶🚶🚶🚶🚶🚶🚶
 
Timoth Philipo, askari polisi wilayani Busega amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Mkoa wa Simiyu baada ya gari alilokuwa akiendesha kugongana na gari lililokuwa likiendeshwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Blasius Chatanda.

Taarifa iliyotolewa na kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Shadrack Masija leo Jumatano Oktoba 5, 2022 inaeleza kuwa ajali hiyo ilitokea Oktoba 2, 2022 eneo la Mizani Nyakabindi ikimhusisha Chatanda na Philipo.

"Toyota Harrier ilikuwa ikiendeshwa na ACP Chatanda iligongwa na Toyota Mark II ikitokea Bariadi kwenda Lamadi ikiendeshwa na Philipo na kusababisha majeraha kwa madereva wote wawili pamoja na H. 7123 Pc Emmanuel ambaye ni msaidizi wa Chatanda," amesema.

Amebainisha kuwa majeruhi wote walifikishwa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya matibabu na kubainisha kuwa chanzo cha ajali ni uzembe wa Philipo ambaye alihama upande na kwenda upande wa kulia na kisha kuligonga gari liliokuwa likiendeshwa na Chatanda.

Amesema Philipo alifariki dunia Oktoba 3, 2022 akiwa anapatiwa matibabu ikielezwa kuwa sukari ilishuka.
Katika taarifa hiyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limetoa pole kwa ndugu na familia ya marehemu na taratibu za mazishi zinafanyika kwa kushirikiana na familia na mwili utasafirishwa kwenda Wilaya ya Magu Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya mazishi.

Chanzo: Mwananchi
Hapo kwenye sukar kushuka baada YA ajali wataalam naomba mnifahamishe
 
Mh,hiki kisa lazima kitakuwa na wivu wa mapenzi ndani yake.
 
Sijui kwa nini, lakini kwa jinsi habari za hawa watu zisivyo aminika eti nimekaa hapa najiliwaza na Chibuku basi mawazo yakanipitia kwamba, usikute Philipo alikuwa na hasira na mukulu akawa aliamua akammalize hivyo akahamisha gari upande wapili ili amrestishe.
Bahati mbaya yeye ndio kajeruhiwa na wasivyo na dogo wakajua alikuwa na nia mbaya wakamfanya kama Panyalodi wa Makongo. Habari ya kushuka sukari mmh!
Anyway, hii Chibuku sijui imechanganywa na nini ona inavyoharibu ubongo wangu! Naiacha

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Gari za serikali huwa wanajiona wao hawafi.

Jana Mataa ya Morocco kuna Gari lenye plate namba ya SU lililazimisha kupita kwenye Mataa wakati hawajaruhusiwa. Ilibaki kidogo Sana itokee ajali mbaya ya kugongana na Lori lilikuwa linatokea kinondoni.

Madereva WA magari ya serikali mtaisha.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom