Bariadi: Askari polisi aliyegonga gari la RPC Chatanda afariki dunia

Bariadi: Askari polisi aliyegonga gari la RPC Chatanda afariki dunia

Nawaza sio kwamba huyu poti alikuwa amepanga kuondoka na mkubwa wake labda Kuna terms hawakuwa sawa
 
Watuambie chanzo cha ajali na ni nani alikuwa mzembe. Ajali za kugongana mara nyingi mmoja wa madereva kafanya uzembe wa kutofuata sheria. Sasa nani alifanya hivi kati ya hawa wawili, maana wao wanajua kulima watu fine -- ooh ume-overtake kwenye solid line. Sasa nani kasababisha hii ajali hapa ikiwa wote wawili wanapaswa kuwa vinara wa kufuata sheria?
Mbona imeelezwa hapo kwenye uzi. Umesoma vizuri au umekimbilia kuandika tu[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Mkuu huyo askari alikua kalewa sana maana pia walimpima kiwango cha ulevi kilikua juu, yeye ndo mwenye makosa alihama njia na kifata gari la RPC japo rpc alipata tuu michubuko kdgo akatibiwa na kuruhusiwa wala sio kwamba kasingiziwa.
Je maelewano ya huyo Askari na RPC huko kazini kwao yalikuaje kabla ya ajali!!? Isije kua walikua wana beef hata ya kuvhukuliana Wanawake!!??
 
Kama ni huyo inasemekana alikuwa chapombe kutokana na stress za kuzinguana na mkewe na mpaka anafariki mkewe hawakuwa pamoja yaani mke Hana hata mawasiliano na ukweni na hapajui so ikawa wanatafuta ufumbuzi wapi akazikwe maana hawapajui na mke hapajui...
Mungu atusaidie sana haya maisha ya kuishikisela kutana kimjini mjini
Sasa Kama office hajui muajiriwa wake anatokea wapi na anaishi wapi,hicho kibarua Cha upolice kapewaje!!??
 
Ndio safari yake kaimaliza, pole kwa familia yake
 
Timoth Philipo, askari polisi wilayani Busega amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Mkoa wa Simiyu baada ya gari alilokuwa akiendesha kugongana na gari lililokuwa likiendeshwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Blasius Chatanda.

Taarifa iliyotolewa na kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Shadrack Masija leo Jumatano Oktoba 5, 2022 inaeleza kuwa ajali hiyo ilitokea Oktoba 2, 2022 eneo la Mizani Nyakabindi ikimhusisha Chatanda na Philipo.

"Toyota Harrier ilikuwa ikiendeshwa na ACP Chatanda iligongwa na Toyota Mark II ikitokea Bariadi kwenda Lamadi ikiendeshwa na Philipo na kusababisha majeraha kwa madereva wote wawili pamoja na H. 7123 Pc Emmanuel ambaye ni msaidizi wa Chatanda," amesema.

Amebainisha kuwa majeruhi wote walifikishwa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya matibabu na kubainisha kuwa chanzo cha ajali ni uzembe wa Philipo ambaye alihama upande na kwenda upande wa kulia na kisha kuligonga gari liliokuwa likiendeshwa na Chatanda.

Amesema Philipo alifariki dunia Oktoba 3, 2022 akiwa anapatiwa matibabu ikielezwa kuwa sukari ilishuka.
Katika taarifa hiyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limetoa pole kwa ndugu na familia ya marehemu na taratibu za mazishi zinafanyika kwa kushirikiana na familia na mwili utasafirishwa kwenda Wilaya ya Magu Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya mazishi.

Chanzo: Mwananchi
Inadaiwa ajali hadi kifo cha Timoth kuna utata,alikua na ugomvi na RPC.nipo kisesa ndugu wa Timoth wamekataa kupokea manīti
 
Shamba la bwana kheri mali ya bwana kheri
 
Hawa watu wanaendesha rafu Sana, afadhali haikuhusisha raia.
 
Mbona imeelezwa hapo kwenye uzi. Umesoma vizuri au umekimbilia kuandika tu[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Kuhama na kuingia upande wa pili sio chanzo cha ajali. Jaribu kuwa deeper.

Ni sawa na ndege inaanguka unaulizwa kwa nini ndege ilianguka unajibu ilishindwa kuendelea kuwa angani.
 
Back
Top Bottom