Bariadi: Watu 7 wafariki katika ajali iliyohusisha Bajaji na lori

Bariadi: Watu 7 wafariki katika ajali iliyohusisha Bajaji na lori

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Watu 7 wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa kutokana na ajali iliyohusisha lori aina ya Scania lenye namba za usajili T172 AUP, ambalo liligongana na Bajaj yenye namba za usajili MC 426 CFQ.

Bariadi.jpg

Watu saba wamefariki dunia na wengine nane wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha Lori kugonga pikipiki ya matairi matatu (Bajaji) jana Jumapili March 27, 2022 katika eneo la mtaa wa Kidulya nje kidogo ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.

Akizungumza na Mwananchi Digital Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Simiyu, Faustine Mtitu amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva wa lori uliosababisha kugonga bajaji.

"Baada ya lori hilo kuigonga bajaji inayokisiwa kuwa ilikuwa imebeba abiria sita na lori likiwa na watu takribani 12, bajaji iliwaka moto na lori kupinduka," amesema Mtitu.

Chanzo: Mwananchi
 
Watu saba wamefariki dunia na wengine nane kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha lori aina Scania, Trekta na Bajaji katika eneo la Mtaa wa Kidulya nje kidogo ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu ambapo katika ajali hiyo Bajaj iliwaka moto na kuteketea kabisa huku chanzo cha ajali hiyo kikitajwa kuwa ni mwendokasi wa dereva wa lori uliosababisha kugonga Bajaji.

FO7iIKRXEAA7REx.jpg


Chanzo: ITV
 
Back
Top Bottom