Baridi la Makete

Baridi la Makete

Napenda baridi sana sana!
Ehh Mwenye Enzi Mungu ilete hiyo baridi ya Makete Dar es Salama walahi![emoji2972]
 
Hata huku kwetu ikifika saa nane usiku kunakuwa na baridi kali sana mpaka huwa naamuka kuvaa suruali,sweta na kujifunika ndo nalala

Upweke shida/tabu sana
 
Wakinga jengeni kwenu muwe kama wachaga wenzenu mnavimbaaa huku mjini kwenu pa ki............e sana
 
Inategemea na pahala umefikia. Kama umefikia sehemu comfortable, chumba kizuri cha kisasa, madirisha ya vioo,kumepigwa ceiling nzuri. Ndani kuna umeme, TV nzuri kubwa ,kinga'muzi kilicholipiwa na External Hard drive yenye movie za kutosha,kitanda kina blanketi nzuri nzito za kukupa joto.

Jikoni kuwe na chakula especially bites za kutosha kama biscuits, karanga, tambi, zabibu kavu, matunda mbali mbali, kahawa nzuri kama Nestle, maziwa, asali, tangawizi ya unga, heater ya maji, upate na internet hapo aaaaaah wewe hautataka kuondoka hilo eneo.
Bila kuongeza demu kwenye list umebugi
 
Inasaidia kwa baridi wakati wa kulala lala nao
Snapchat-1256287213.jpg
 
tafiti zinaonyesha ni rahisi na ni nafuu kupambana na baridi kuliko joto,joto linasababisha mpaka stress likikubali,wakazi wa dar wanajua.
Facts

Joto kulikabili lina hitaji gharama ukiwa home utahitaji fan, ac au utulie kivulini chini ya mti ambapo napo hapo utakuwa unapata kaubaridi kwa mbali kasikokidhi mahitaji.

Ukiwa njiani unatembea unaweza pata hadi fangasi kutokana na jasho halafu ni mazingira rafiki kwa nagonjwa nyemelezi.

Sehemu yenye baridi hata umbu huwakuti lakini kwenye joto kila kitu kimejirahisisha
 
Back
Top Bottom