Barnabas Classic, " Diamond aliniuliza unataka sifa au unataka pesa?"

Barnabas Classic, " Diamond aliniuliza unataka sifa au unataka pesa?"

Barnaba Classic aka Mopao aka Mtukazi ambaye kesho anaachia album yake yenye hadhi ya kimataifa album inayoandaliwa kwa ajili ya international market.

Amesifu namna Diamond Platnumz alimpokea na kumuunga mkono kwenye kusimamia project nzima ya album yake ya Love Sounds Different.

Maneno anayoyakumbuka siku amekutana na Diamond Platnumz kwa discussion alimuuliza "unataka pesa au unataka kujulikana?".

Ili swali lina maana kubwa sana kwenye biashara ya sasa hivi ya muziki ambayo imejaa chuki na mashambulizi yenye mlengo wa kauzibe.

Barnaba ni msanii mkubwa sana na fundi wa muziki, ila ameamua kuweka ego pembeni na kufuata support ya name of the game Chibu Dangote. Kuna watu wanaweza kuona anajishusha ila wenye akili wanaelewa Barnabas kaamua kufanya biashara.

Watoto kama Rayvanny na Harmonize hawawezi kabisa levels za music za Barnabas lakini wamewekwa juu na management ya Diamond na wanapiga hela mpaka kesho.

Mimi naisubiri kwa hamu album ya Barnabas na wimbo ninaosubiri kwa hamu ni aloimba na Diamond Platnumz inasemekana video yake haijawai kutokea toka Tanzania ipate uhuru.

Mwamba kabisa Barnaba kayasema maneno hayo kwa kinywa chake kwenye interview hii hapa


Bandiko limekaa kichawachawa ..... Halijengi
 
Barnaba hana nyota,nyimbo zake zitaishia nananga na sirari na tunduma
 

Barnaba ana sauti ambayo akiifanya show ya live na msanii yoyote yule, ni lazima amtie aibu.

Nimeona wasanii wote alioimba nao jana ni kama vile alikuwa anawafundisha muziki.

Kijana ana kipaji cha hali ya juu.
 
Muziki unamhitaji sana Diamond akisema asuse akae pembeni afanye projects zake tu bongofleva itayumba sana. Acha afanye maana hata asipofanya hawatoacha kumsema vibaya vya kumsema vipo vingi hawajaanza leo na hawatomaliza leo.

Barnaba anaenda kuiona sasa pesa ya muziki.

View attachment 2324085
WCB ni kiwanda aisee..

Hongera Barnaba kwa maamuzi sahihi..
 

Barnaba ana sauti ambayo akiifanya show ya live na msanii yoyote yule, ni lazima amtie aibu.

Nimeona wasanii wote alioimba nao jana ni kama vile alikuwa anawafundisha muziki.

Kijana ana kipaji cha hali ya juu.
Amechelewa sana...alikuwa kwa wanyonyaji. Sasa atachomoka.
 
Sasa Barnabas umaskini kwaheri. Mwambieni Alli kiba amtafute Mondi ampe akili ya kuwa bilionea sio kila siku kutembea na gari used from Japan
kwani wewe hautaki gari jipya kama walilopewa lokole na issa azam[emoji28][emoji28].

au tayari umeshapewa??

kama kiba ana gari used la milioni zaidi ya 100 wacha kumjadili kifala fala hapa.
 
Back
Top Bottom