Jaji Mark Bomani aliongeza, hilo linasababishwa na udhaifu wa sheria ya madini. Bahati mbaya sana kwa sababu ya uchache wa wa wabunge wa upinzani, hoja zote zenye maslahi mapana ya Taifa zinanyongwa na wanyonyaji hawa ccm kwa kuitetea serikali yao dhalimu. Wanakuja na utetezi muflisi ooh, tukivunja mikataba tutashitakiwa na endapo tutashindwa kesi itakula kwetu. Well and good! Tunasema tuache kuingia mikataba mipya chini ya sheria zilizopo, ili mikataba tuliyoifunga ikiisha au ikifa ife na sheria yake, tutunge sera na sheria mpya kwa ajili ya mikataba mipya kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo, hawako tayari kwa sababu wanakuwa wameshawekana ssawa kwenye Party Caucas- maslahi ya Chama kwanza, ya Taifa majaliwa! Kwenye Bunge liloisha leo Mbunge Zungu aliainisha vizuri kwa kulinganisha mapato yatokanayo na biashara ya mawasiliano baina ya nchi wanachama wa Afrika Mashariki kwa mwaka 2010 ambapo KENYA walikusanya Dola Mmiloni 79, UGANDA Dola Milioni 31, RWANDA Dola Milioni 14, (watumiaji wa simu 30,000) TANZANIA yenye watumiaji simu 48,000 ilikusanya Dola Milioni 1.7 tu! Inauma sana. Cha ajabu wakati wabunge wengi tena wa CCM walipoongezeka kuibeba hoja, mwanzoni naibu Spika alionekana kushtushwa na kuahidi ufuatiliaji wa kina kwa Wizara inayohusika, lakini sijui alipitishiwa kimemo! ghafla mwishowe hoja aliichinjia baharini.