Zaidi ya waumini 100 wa Kanisa Katoliki wamekabidhi Ubalozi wa Vatican nchini Tanzania barua rasmi ya malalamiko kwa Papa dhidi ya Askofu Mkuu wa Dar es Salaam, Jude Thaddeus Ruwa’ichi, na Katibu Mkuu wa TEC, Padri Dkt. Charles Kitima.
Kwa Padri Kitima, waumini wanadai amejihusisha na siasa kwa upendeleo, kusababisha mgawanyiko ndani ya Kanisa, na kushindwa kulinda umoja na uaminifu wa waumini kinyume na Sheria za Kanisa.
Dhidi ya Askofu Ruwa’ichi, wanadai matumizi ya lugha ya kudhalilisha hadharani, kuwaaibisha waumini kutoka madhabahuni, na kukiuka Canon Law pamoja na mafundisho ya Kanisa kuhusu heshima, upole na ulinzi wa waumini.
Waumini wanamuomba Papa achunguze madai hayo na kuchukua hatua stahiki kulinda heshima ya waumini, umoja na uaminifu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania, wakisisitiza kuwa hatua yao ni ya kikanisa na si uasi.