BARUA KUTOKA JELA
Kuna mbaba mmoja, mwanae lifungwa jela,
Jina lake sitotaja, nakataliwa na mila,
Machozi yakamvuja, mfukoni hana hela,
Barua kutoka jela, ilimkomboa baba.
Aliandika barua, kwa mwanae gerezani,
Dhumuni ni kumwambia, meshindwa lima shambani,
Nguvu zake mepungua, hawezi jembe shikeni,
Barua kutoka jela, ilimkomboa baba.
Baba na aliamua, barua kuiandika,
Gerezani ikatua, kwa mwana ikasomeka,
Babayo sina afia, shamba letu kulimika,
Barua kutoka jela, ilimkomboa baba.
Mwana lishikwa uchungu, sijue afanye nini,
Limuomba sana Mungu, atolewe gerezani,
Akazalishe mikungu, ili auze sokoni,
Barua kutoka jela, ilimkomboa baba.
Mwana akapata wazo, baba kumsaidia,
Barua yenye ujazo, baba limuandikia,
Ningekuwa na uwezo, jela ningeikimbia,
Barua kutoka jela, ilimkomboa baba.
Lingine aliandika, mwana kwa ile barua,
Shambani kwenye vichaka, hela nyingi lifukia,
Lizoiba kwenye duka, kwake Mwarabu bandia,
Barua kutoka jela, ilimkomboa baba.
Wale jela askali, wakaisoma barua,
Wakaitamani mali, shambani alofukia,
Usiku maaskali, shambani mule lijaa,
Barua kutoka jela, ilimkomboa baba.
Shamba lote wakalima, hela wakifukuzia,
Asikali wakahema, pesa hawakuambua,
Ila shamba wamelima, vizuri kupindukia,
Barua kutoka jela, ilimkomboa baba.
Baba tena liandika, barua kwenda kwa mwana,
Furaha imemshika, shamba limelimwa sana,
Mwana nae akacheka, ujanja wenye maana,
Barua kutoka jela, imemkomboa baba.
Nae mwana liandika, kwa baba yake barua,
Kama shamba melimika, panda njugu na bamia,
Askali liwateka, shambani mekulimia,
Barua kutoka jela, ilimkomboa baba.
Denny Jeremias Kitumbika
Mtunzi wa mashairi na ngano za Kiafrika
Mufindi Tanzania 24.7.2017
Kuna mbaba mmoja, mwanae lifungwa jela,
Jina lake sitotaja, nakataliwa na mila,
Machozi yakamvuja, mfukoni hana hela,
Barua kutoka jela, ilimkomboa baba.
Aliandika barua, kwa mwanae gerezani,
Dhumuni ni kumwambia, meshindwa lima shambani,
Nguvu zake mepungua, hawezi jembe shikeni,
Barua kutoka jela, ilimkomboa baba.
Baba na aliamua, barua kuiandika,
Gerezani ikatua, kwa mwana ikasomeka,
Babayo sina afia, shamba letu kulimika,
Barua kutoka jela, ilimkomboa baba.
Mwana lishikwa uchungu, sijue afanye nini,
Limuomba sana Mungu, atolewe gerezani,
Akazalishe mikungu, ili auze sokoni,
Barua kutoka jela, ilimkomboa baba.
Mwana akapata wazo, baba kumsaidia,
Barua yenye ujazo, baba limuandikia,
Ningekuwa na uwezo, jela ningeikimbia,
Barua kutoka jela, ilimkomboa baba.
Lingine aliandika, mwana kwa ile barua,
Shambani kwenye vichaka, hela nyingi lifukia,
Lizoiba kwenye duka, kwake Mwarabu bandia,
Barua kutoka jela, ilimkomboa baba.
Wale jela askali, wakaisoma barua,
Wakaitamani mali, shambani alofukia,
Usiku maaskali, shambani mule lijaa,
Barua kutoka jela, ilimkomboa baba.
Shamba lote wakalima, hela wakifukuzia,
Asikali wakahema, pesa hawakuambua,
Ila shamba wamelima, vizuri kupindukia,
Barua kutoka jela, ilimkomboa baba.
Baba tena liandika, barua kwenda kwa mwana,
Furaha imemshika, shamba limelimwa sana,
Mwana nae akacheka, ujanja wenye maana,
Barua kutoka jela, imemkomboa baba.
Nae mwana liandika, kwa baba yake barua,
Kama shamba melimika, panda njugu na bamia,
Askali liwateka, shambani mekulimia,
Barua kutoka jela, ilimkomboa baba.
Denny Jeremias Kitumbika
Mtunzi wa mashairi na ngano za Kiafrika
Mufindi Tanzania 24.7.2017