Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,478
- Thread starter
- #21
JC:
Nakubaliana katika ufafanuzi wako. Na kwa kutumia ufafanuzi wako, serikali ya majimbo ni muhimu kwa nchi kama Tanzania ambayo ina diversity ya ethnic groups.
Kuna study inayoonyesha kuwa nchi masikini kama Tanzania, zinatumia sehemu kubwa ya mapato yao ku-pacify ethnic tensions. Kwa mfano wilaya za Tanzania zimegawanywa kimakabila. Wakati wa Nyerere kulikuwa na wilaya kati ya 120 na hiyo ni sawa na idadi ya makabila. Vilevile majimbo ya ubunge yamefuata makabila.
Baraza la mawaziri la kwanza la Kikwete lilikuwa na mawaziri karibu 60. Na wengi walikuwa kama wawakilishi wa maeneo fulani au dini fulani.
Matokeo ni gharama kubwa ya uendeshaji wa serikali.
Wabunge wengi wa sasa ni wakazi wa DSM, wanagombe ubunge kwa sababu ya uhusiano wa kikabila na sio kuwa na ukazi au interests katika maeneo hayo. Na matokeo yake ni kuwa na wabunge wenye kuhitaji VX, kwa sababu atakuwa na uhakika wa kwenda kwenye jimbo lake, Dodoma kwenye vikao na kurudi nyumbani DSM.
Uzembe unaouona kwa viongozi wetu unatokana na kuwa hawawajibiki kwa wale wanaowatawala. Njia moja ya kuwafanya wawajibike ni kuzipa local authority madaraka makubwa. Viongozi wachanguliwe na locals.
Mkuu wa mkoa anayeteuliwa na Rais, interests zake ni kumsikiliza rais na sio wananchi. Na hicho cheo anaweza kupewa kama zawadi na sio sifa za kiutendaji.