Barua maalum kwa Kanisa Katoliki na Kanisa la Kilutheri: Tusaidieni kupata Katiba Mpya na kutetea haki za kikatiba za kila mtu

Barua maalum kwa Kanisa Katoliki na Kanisa la Kilutheri: Tusaidieni kupata Katiba Mpya na kutetea haki za kikatiba za kila mtu

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Ndugu Maaskofu wetu.

Amani ya Bwana iwe nanyi.

Sina wasiwasi na Viongozi wetu wa dini wa Kanisa Katoliki na Kanisa la Kilutheri kuwa soon mtatupa muongozo wenu, kuhusu suala hili la katiba mpya ambalo serikali ya CCM inajaribu kulikwepa.

Mababa askofu nawaandikieni barua hii kwa sababu CCM pamoja na ubabe wao wote lakini nyinyi pindi mkitoa kauli, huwa wanawasikiliza

Mababa askofu, siku zote nyie mmekuwa mkisimamia haki, kushauri na kuonya, tuna imani kuwa kama mfanyavyo siku zote basi mtasimama na sisi wananchi kwenye matakwa yetu haya ya msingi ya katiba mpya.

Mababa askofu, ninaomba mtusaidie kuweka sauti ya kudai katiba mpya kwa sababu zifuatazo.

1. Katiba mpya ni mchakato ulioko kisheria
Mababa Askofu, mtakumbuka kuwa tuna sheria inayosimamia suala hili, hata hivyo serikali ya CCM inakwepa kutimiza wajibu wa kutekeleza sheria hii. Pamoja na ukweli kuwa suala la mchakato wa mabadiliko ya katiba yslichukua muda mwingi wa kukusanya maoni ya wananchi, fedha nyingi zilitumika na sheria ya mabadiliko ua katiba ikatungwa, lakini serikali ya CCM imekuwa ikipiga chenga utekelezaji wa sheria hii. Tunawaomba mababa Askofu muingilie kati kuwaambia CCM waheshimu sheria ya nchi hususan kwrnye jambo hili.

2. Mababa Askofu, Jambo la pili ni kuwa katika nchi yetu kuna katiba mbili zinazotawala moja ni ya muungano, na nyingine ni ya Zanzibar. Hizi katiba mbili zinakinzana
Zinakinzana hasa kwenye vifungu vinavyohusu muundo wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambapo katiba ya nchi yetu bado inatambua muundo wa zamani wenye rais wa Zsnzibar na Waziri kiongozi, wakati sasa hivi kuna Makamu wawili wa rais. Tunaomba muikumbushe serikali ya CCM umuhimu wa kuwa na aina ya uongozi nchini unaotambulika katika katiba. Pia katiba ya Zanzibar imepoka mamlaka ya Mahakama ya rufaa ambalo ni jambo la muungano, lakini katiba ya Zanzibar imelimit makosa ya Wazanzibar yanayoruhusiwa kuamuliwa ktk mahakama hiyo ya rufaa, ambapo imezuia makosa ya haki za binadamu yaliyoamuliwa na mahakama kuu ya Zanzibar kuweza kukatiwa rufaa mahakama ya rufaa. Huu ni ivunjifu wa katiba ya Muungano wa wazi

3. Katiba ya sasa ni katiba ya chama kimoja
Mababa askofu, Kama ambavyo wanataaluma wa Kanisa katoliki walivyowahi kuandika kwenye waraka wao juu ya umuhimu wa katiba mpya. Walisema wazi kwenye waraka wao kuwa katiba ya sasa hsikidhi haja kwa sababu ni ya chama kimoja. Mababa askofu, ukweli huu bado upo kwa sababu katiba hii bado ni ileile haijabadilika, wakati mazingira ya kisiasa nchini ni ya vyama vingi.

4. Mababa askofu, katiba ya sasa inawapa wanasiasa madaraka makubwa, wananchi tunahitaji katiba mpya ili madaraka yarudi kwetu wananchi
Mababa askofu, kwa mfumo wa nchi yetu, mayai yetu mengi yamo kwenye kapu la mtu ashikaye cheo cha Urais, pindi tukipata rais wa hovyo, katili, dhalimu, fisadi, muonevu hatuna namna nzuri ya kumdhibiti na anawrza kuiharibu nchi yetu kijamii, kiuchumi na kisiasa. Tunahitaji katiba mpya ili kuilinda nchi yetu dhidi ya crisis ya watawala mafikteta na madhalimu.

Naambatanisha waraka wa mwaka 2013 wa wanataaluma wa kanisa katoliki juu ya umuhimu wa mbadiliko ya katiba.

1191676_Waraka_wa_Katiba-01.jpg


1191677_Waraka_wa_Katiba-02.jpg


1191678_Waraka_wa_Katiba-03.jpg


1191678_Waraka_wa_Katiba-03 (1).jpg
 
Hizi ni taasisi za dini zenye nguvu na ushawishi mkubwa ila zisizojitambua na kutambua wajibu wao, kazi yao ni kukaa kimya tu, wanategea, wategeaji mpaka waone mambo yameharibika ndo wajitokeze.
 
Ummeanza kutegemea walimapadri wa kichaga wawasaidie ,yule shoo na na ruaich

It's secular national mpunguze mihemko

USSR
 
Wamuandikie barua ya noni wakati maaskofu wa kanisa katoliki kafanya nao kikao wiki jana na akala nao lunch.
 
Ombi langu kwa makanisa: yawatenge CCM (wana CCM wasipewe huduma za kiroho)
Sasa wote si watahamia kwa Gwajima, Mwamposa na Bakwata!! Na wengine watenda kwenye Mlima wa Moto hata kama Mwanzilishi alishatangulia mbele za haki.
 
Wataambiwa msiingilie mambo ya siasa, CCM wako predictable sana, halafu itatumiwa propaganda kuliamsha lile kundi jingine lijione halina msemaji/limepuuzwa, matokeo yake hilo kundi litaibuka kusimama upande wa CCM, then hii biashara ya Katiba Mpya ndio itaishia hapo.

Binafsi, ningependa kuona kwenye hii barua yako ukiyahusisha makundi mengine zaidi, mfano, hata kama BAKWATA hawaminiki, ungetafuta viongozi wengine wanaoaminika toka upande huo uwahusishe kwenye hii barua yako, mfano. Sheikh Ponda na wengine wa calibre yake.

Then from there, vipi wale wasio na dini, hawana chama chao au viongozi wao, huwa nafahamu kuna wale waganga wa asili, ila sijui kama kuna chama cha wanaoamini dini za asili, japo kundi hili linaweza kuonekana dogo, ila ni vyema likahusishwa pia kama lipo.
 
Hili jambo naona linakuwa serious

Sio linakuwa serious mkuu, ni serious tayari. Cdm washikilie hapo hapo, wananchi wengi wa nchi hii husubiri hamasa ya wanasiasa ndio nao wafuate mkumbo.

Na kwenye jambo hili cdm wana ushawishi mkubwa. Unapokuwa unapiga kelele ya haki, waouvu hujaribu kupotosha ili kupunguza makali, lakini kelele ikizidi lazima kieleweke. Kwa alichokifanya rais aliyepita sioni ni kwa jinsi katiba isipatikane.
 
Ummeanza kutegemea walimapadri wa kichaga wawasaidie ,yule shoo na na ruaich

It's secular national mpunguze mihemko


USSR

Kwenye hili la katiba mpya hata mawe yatapaza sauti. Ogopa sana takwa la haki. Kelele zinatakiwa ziwe kama zote, vyombo vya habari vyote inatakiwa hiyo iwe habari isiyokauka.
 
hizi ni taasisi za dini zenye nguvu na ushawishi mkubwa ila zisizojitambua na kutambua wajibu wao, kazi yao ni kukaa kimya tu, wanategea, wategeaji mpaka waone mambo yameharibika ndo wajitokeze.
Mungu akusamehe mkuu
 
Back
Top Bottom