Barua ya Adam Malima kumpinga Spika!

Barua ya Adam Malima kumpinga Spika!

Status
Not open for further replies.
Mwanakijiji

Unjaua niliposema kuwa you can do better than that ni kutokana na heshima yako na chombo chako cha habari ambacho kina umaarufu mkubwa tuu.

Lakini tatizo ni pale unapotegemewa kuwa impartial na kuweza kujenga arguments ambazo zinaangalia both sides of the issue lakini of recently umekuwa huji na hoja bali umekuwa overwhelmingly biased hoja zako mwanzoni wakati hii thread ilipoanza ulisema kuwa MALIMA KAAJIRIWA NA MANJI. I mean how do you expect watu wakuchukulie serious na chombo chako cha Habari kama na wewe unarukia bandwagon ya kusema jambo bila ya kuwa na uhakika nalo?

Dont get me wrong inawezekana ni kutokana na frustrations lakini kila mtu yuko frustrated lakini kwa status yako katika jamiii we expected more of you instead of coming up with unsubstantiated claim ambazo zimepelekea wewe kuonekana kuwa umekuja na narrow range of debate

That said, ningependa ku clarify kuwa SIJAKULAUMU KUWEKA HII BARUA humu bali hiyo bandwagoning yako inanitisha

Aliyesema Malima ni mwajiriwa wa Manji ni Mzee Es!
 
- Suala la Malima limegeuka kuwa kubwa na la Kikatiba kwa sababu Spika hakufanya kile ambacho alipaswa kufanya na baadaye akaamua kutumia mitishamba ya "busara" zake ili kunyamazisha jambo hili. Watu waliposema ripoti ijadiliwe Bungeni aligoma na kusema yeye ndiye Spika!! Leo hii maji yamefika shingoni ati sasa watalizungumza suala hili Bungeni, what the f...!

- Hivi hawa wabunge wetu wanakunywaga ulanzi kwenye vikao? Haiwezekani watu walioapishwa kulinda Katiba ya Nchi wanasita sita kutekeleza jukumu lao!!
Mwanakijiji hilo nililisema hapo nyuma kidogo kama ifuatavyo:
Halafu Kosa jingine Kwanini ile ripoti hakuiwakilisha Bungeni na wabunge wakaichambua pamoja na matokeo yake Lakini kwa UBABE ULEULE ALISEMA TUME ILIKUWA YAKE NA RIPOTI NI YAKE, Sasa anapotaka kulipeleka tena swala Bungeni Kwani hiyo tume kwasasa imegeuka kuwa ya wabunge na si ya spika tena. Anyway, Anavuna alichopanda................Ajifunze sheria na kanuni zipo kwa wote ndani ya ukumbi wa bunge na Yeye ni msimamizi wa kuhakisha zinachukua mkondo wake kwa wote wanaongozwa nazo ndani ya bunge hilo Tukufu. Hapa labda kuna Ambacho kimejificha ambacho Mh. Adam anakijua sisi hatukijui na ndiyo maana anaendeleza chokochoko Lakini Kama si Leo basi masiku ya usoni tutalielewa
 
Masatu,
Ndiyo maana nikauliza labda kamati ilikuwa inachunguza suala lingine. Lakini Spika alizungumzia kwa kirefu kuhusu tuhuma za Malima dhidi ya Mengi kwamba ITV humtangaza zaidi Mengi kuliko viongozi na masuala ya kitaifa. Spika alieleza kwamba Mh.Malima alishindwa kuthibitisha kauli hiyo.

Sasa katika mazingira kama hayo kamati ilishindwa vipi kumtia hatiani? katika mazingira kama hayo kwanini Spika hakumchukulia hatua za kinidhamu?

Natamani ningeiona ripoti ya Kamati ya Maadili. Isije ikawa kamati hiyo iliweka kando kanuni na sheria za bunge, na badala yake kutumia "busara za kamati" kufikia uamuzi wake.

zaidi, natamani Mh.Malima angetoa mwanga zaidi wa kuhusu maoni ya hao dissenters wa kamati ya maadili, na kwanini anaona wamekosea. nadhani Mh.Malima ame-base zaidi kwenye idadi/uchache wa dissenters kuliko maoni yao.
 
KNKCU,Mzee ES,Masatu,Mwanakijiji,
Spika alitamka kwamba Malima alishindwa kuthibitisha kauli yake aliyoitoa bungeni. Kwa kanuni za Bunge hilo ni KOSA. Sasa Sijui kwanini Kamati ya Maadili ilimuona hana hatia yoyote, unless ilikuwa inachunguza jambo tofauti.

Hata Malima mwenyewe hazungumzii kabisa kushindwa kwake kuthibitisha matamko aliyoyatoa ndani ya bunge. Anachokisisitiza ni haki ya wabunge kuzungumza kwa "uhuru" wanapokuwa ndani ya bunge.

Mimi nilifikiri "busara za Spika" ni ule uamuzi wa Mzee Sitta kutokumchukulia hatua za sheria za bunge Mh.Malima kwa kutoa madai ya uongo dhidi ya Bw.Mengi na ITV. Mimi nadhani Malima angekubali kukutana na Mengi hata kama yeye binafsi hana ugomvi naye. Hili suala limejadiliwa mpaka na kamati ya bunge, kwa msingi huo there are some issues/differences that need to be sorted/ironed out btn Mh.Malima na Bw.Mengi
JOKAKUU!
Wakati ninachanghia huko nyuma kuhusu hili nilandika kama ifuatavyo:
Hii tulisema toka awali kwenye Manji VS Mengi Kwamba Mh. Spika alipindisha kanuni ktk kutoa Hukumu au Maamuzi ikiwa yeye na kamati walioiunda wanakubali Malima alilidanganya Bunge Hapa ni kwamba wamemtia hatiani na Kama wamemtia hatiani nini kilitakiwa kufanywa?

Ni kumuadhibu kwa mujibu wa kanuni zilizopo kama tulivyoshuhudia watu waliongea ndani ya Bunge hilo hilo na kuadhibiwa tena yeye ilitakiwa Kwanza Afute kauli yake aliyeitoa,pili amuombe msamaha aliyemsingizia yaani mengi, Kama ilivyoamuliwa kwenye swala Mh. Cheyo Na Mh. Shibuda kutokana na kauli ya cheyo aliyeitoa kwa shibuda kuhusiana na fedha zilizotumika ktk ujenzi wa shule huko Shinyanga.

Sasa kwanini hili halikufanyika hii ni Tabia ile ile ambayo tumejionea kwa Mh.Spika kuwa mwepesi kufuata sheria zinapowahusu Wapinzani na Hapa kilichomponza ni Huo Umwamba na kuacha kufuata kanuni husika tena kwa huyu kijana Mh. Adam isingeishia hapo kama mimi ningekuwa spika ningempa Adhabu ya kulipa na Fedha za walipa kodi alipokuwa Anadanganya na kuombwa toka awali afute kauli yake aligoma na kufikia hadi kuundwa kwa tume iliyotugharimu walipa kodi.

Sasa Mh. amembeba mtu asiyebebeka pamoja na kutopenda kumuadhibu kijana amemgeuka na kumuona hajui kazi yake kama alivyoonyesha ,Sasa hivi Mh.Spika analalamika nini kwamba kachafuliwa Jina kwani alikuwa hajui alichokifanya kilikiuka kanuni kwa kutomuadhibu mtu ambaye ushahidi unaonyesha kwamba ana kosa.

Halafu Kosa jingine Kwanini ile ripoti hakuiwakilisha Bungeni na wabunge wakaichambua pamoja na matokeo yake Lakini kwa UBABE ULEULE ALISEMA TUME ILIKUWA YAKE NA RIPOTI NI YAKE, Sasa anapotaka kulipeleka tena swala Bungeni Kwani hiyo tume kwasasa imegeuka kuwa ya wabunge na si ya spika tena. Anyway, Anavuna alichopanda................Ajifunze sheria na kanuni zipo kwa wote ndani ya ukumbi wa bunge na Yeye ni msimamizi wa kuhakisha zinachukua mkondo wake kwa wote wanaongozwa nazo ndani ya bunge hilo Tukufu. Hapa labda kuna Ambacho kimejificha ambacho Mh. Adam anakijua sisi hatukijui na ndiyo maana anaendeleza chokochoko Lakini Kama si Leo basi masiku ya usoni tutalielewa
 
Jokakuu,

Unaposema kuwa Spika alizungumza kwa kirefu kesi hii ni sawa. Lakini swali je aliechunguza kesi na kutoa ripoti ni tume sio spika!. Sasa kama Spika alikuwa ana uwezo wa kufanya kazi ile vizuri zaidi kwanini aliipeleka kwenye kamati in the 1st place?

Inaonyesha una mashaka na maamuzi ya kamati, lakini ukweli utaendelea kubaki hivyo hivyo kuwa kamati imemuona Mh Malima hana hatia.

Itakuwa jambo la busara pia mbali na jambo hili kujadiliwa tena bungeni watu wa bunge wa post Hansard za proceedings za kamati kwenye web yao ili na sisi wananchi tuchambue pumba na mchele. Huu uamuzi wa Kamati based on what we will see ktk Hansard tutajua kama uamuzi wao ni questionable or what. Huu ni ushauri wa mjadala kuwa mpana zaidi na kuwaondoa wananchi mashaka.

Mungu Ibaraki Tanzania
 
Zitto said:
Aidha, uamuzi wa Malima kuamua kumshitaki Sitta nje ya utaratibu na kanuni za Bunge, nao umesababisha kuibuka kwa maswali mengi miongoni mwa wabunge, ambao baadhi yao wameshaanza kukiona kitendo hicho kuwa ni cha kulidhalilisha Bunge kimamlaka (Contempt of Parliament).
Nilisema huko nyuma kuwa hata kama Malima alionewa na spika hatua yake ya kuhoji madaraka ya spika na kumshitaki nje ya bunge ni kosa kubwa sana. Kuna utaratibu wa wa wazi kabisa wa kukabiliana na makosa ya spika siyo kujifanyia mambo kienyeji enyeji tu. Kitendo alichofanya Mheshimiwa malima kinatokana na siasa za kizamani za Chama kushika hatamu na kinadhalilisha bunge zima kwa jumla ikiwa ni pamoja na yeye mwenywe kama mbunge. Nadhani atachukuliwa hatua thabiti za kinidhamu ili kulinda heshima ya bunge.

Watu tunataka Bunge lenye nguvu la kuweza kuhoji utendaji wa serikali halafu mheshimiwa huyu yeye anataka kulifanya Bunge kama kikao cha CCM; bado wanaingalia nchi hii kama ile ya miaka ya sitini na sabini ambako viongozi wa serikali walikuwa bado wanajituma kwelikweli. Serikali ya leo inahitaji kudhibitiwa sana na bunge, hivyo mamlaka yote ya bunge hayahitaji kuhojiwa nje ya bunge.
Zitto said:
Habari kutoka ndani ya duru za wabunge wa CCM zinaeleza kuwa, moja ya vifungu walivyotumia ni sheria namba 3 ya mwaka 1988, iliyo katika Ibara ya 24 (D) ambayo inapinga kuhojiwa kwa mamlaka ya Spika na chombo kingine chochote nje ya Bunge.

Zitto said:
Aidha wabunge hao wamepanga pia kutumia kanuni namba 60 ya Bunge iliyo katika toleo la mwaka 2004 ambayo pia inatoa mamlaka kwa maamuzi ya Bunge kutohojiwa na chombo kingine cha nje.

Ni kweli Malima kaenda kinyume na vifungu kadhaa vya sheria na anaweza kuwajibishwa kwa makosa hayo.
Zitto said:
Walipoulizwa sababu hasa za kufikia hatua hiyo, wabunge hao walisema taarifa walizonazo zilikuwa zikionyesha kuundwa kwa mtandao mpya ndani ya mtandao wa wana CCM wenye lengo la kuhakikisha Sitta anawekwa katika mazingira magumu kabisa kikazi.

Katika hili mimi namlaumu rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye aliyeanzisha hizi "siasa za makundi" kwa kuweka wanoitwa "wana mtandao." Siasa za makundi huwa ni hatari sana katika jamii na sasa hivi umekuwa kama utamaduni kwenye CCM. Makundi yatagawanyika pole pole na baadaye tutishia kuwa na makundi ya aidha kidini au makundi ya kikabila. Mzee Kawawa alikuwa akisistiza sana wana "CCM kuwa na mshikamano" lakini sasa naona hiyo imekuwa ni historia. Hebu ngoja tusubiri tuonae mambo haya ya mgawanyiko yataishia wapi.
 
Ila jamani ni wapi ambapo Malima alimtaja Mengi Bungeni au kutaja chombo chochote cha habari cha Mengi?
 
.....hata kama mbinu ni chafu. CCM imekwishaingiliwa. Makundi aliyoyazungumzia Kichuguu hapo chini sasa yamo kazini. Lisilofikiriwa na wala watu hawataki kulizungumzia ni mkono wa chama cha upinzani kipi unaojihusisha na mapambano yanayofurukuta ndani kwa ndani kichama sasa hivi. Wakizinduka, it will be too late!
Strategy ya hali ya juu kabisa hiyo; maanake hivi hivi kwa njia za kawaida tu CCM itatawala milele! Sasa dawa yao ipo jikoni.
 
MHE. ADAM K. A. MALIMA: Mheshimiwa Spika, awali ya yote, naomba
nimpongeze kwa dhati kabisa Ndugu yangu, Kaka yangu, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Muhammed Seif Khatib, kwa hotuba yake nzuri ambayo kweli kabisa ina mwelekeo wa utekelezaji wa malengo ya sera za Habari, Utamaduni na Michezo. Mheshimiwa Spika, naomba niwapongeze sana Manaibu Waziri wa Wizara hii, Mheshimiwa Joel Bendera, Mbunge na Kocha wa Timu yetu ya Wabunge na pia Mheshimiwa Dr. Emmanuel Nchimbi, ambao wote kwa pamoja wamejidhihirisha hapa katika Bunge lako na huko nje wakiwa wanatekeleza majukumu yao kuwa ni viongoziwazuri sana, tena sana.

Mheshimiwa Spika, naomba niseme yafuatayo kuhusu Sekta ya Habari:-
Mheshimiwa Spika, Tanzania imepiga hatua kubwa sana katika maendeleo ya
Sekta hii katika sehemu zote TV, Radio, Magazeti katika kipindi kifupi sana. Pia,
naamini kuwa Vyombo vya Habari vinafanya kazi katika mazingira mazuri
yanayowaruhusu kutekeleza majukumu yao kwa uhuru bila kubughudhiwa na Mamlaka. Lakini pia lazima tukubali kwamba uhuru wa kutoa habari una mipaka. Una viwango! Huwezi kwa sababu ya kumiliki Vyombo vya Habari ukatumia nafasi hiyo kwa ajili ya kudhalilisha Watanzania wenzako kwa kusema maneno ya uongo, au kwa kutoa habari zinazopotosha kwa makusudi. Utoaji wa habari ni huduma ya jamii. Naomba maelekezo ya kina, Muswada wa Sheria wa Vyombo vya Habari
uliotajwa na Mheshimiwa Waziri Ibara ya 19 ya hotuba yake itakuwa tayari, itakamilika lini?

Pia, naomba maelezo. Ni chombo gani cha kitaifa kinachohusika na usimamizi
wa viwango vya utangazaji na habari kwa mfano katika baadhi ya Televisheni zetu,
taarifa nyeti zenye umuhimu wa kitaifa za Rais, Waziri Mkuu, Bunge zinapewa dakika mbilimbili kila moja. Habari za mmiliki wa TV kwenda kwa watoto wa Madrasa Msasani ili kuendeleza ugomvi wake na Sheikh mmoja wa Msikiti wa Kariakoo peke yake unachukua dakika 10, za kipindi cha habari za kitaifa ambazo jumla zina dakika 20. Ni nani mhusika mkuu wa kusimamia viwango vya utangazaji? Mheshimiwa Spika, naomba katika hayo nizungumzie suala la utamaduni. Naomba sana Serikali ya Awamu ya Nne iandae rasimu ambayo itachangiwa na Wabunge kuhusu ni nini utamaduni wa Mtanzania kwa tafsiri pana ya utamaduni. Serikali iingie gharama na kwa makusudi kabisa wasimamie mikakati ya kuwafanya Watanzania wao. Napenda kutambua mchango wa Chuo cha Sanaa, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), BAKITA.

Mfuko wa utamaduni una mchango gani na mipango gani katika kuchangia mikakati hii ya utambuka wa utamaduni wa Mtanzania? Mheshimiwa Spika, mwisho naomba niongezee mchango wangu kwenye suala la michezo. Michezo iko ya aina nyingi Tanzania. Tuna vipaji vya wanamichezo katika michezo mbalimbali. Naomba tufanye utafiti wa kitaifa ili tujue ni gharama gani na kutoka maeneo gani ambayo Serikali itafanya ili katika miaka ijayo ya karibu tuone mabadiliko yatakayosimamiwa na Baraza la Michezo (BMT).

Migogoro ya mpira wa miguu haswa katika vilabu vikubwa vinaleta sura mbaya
sana. Naomba tupate maelezo ya Serikali, ni mikakati gani inayoeleweka ya kupata
ufumbuzi wa haraka? Mfano, kule Hispania migogoro ya Real Madrid na Barcelona
huingiliwa kati moja kwa moja na Serikali kwa kutambua umuhimu wa klabu hizi kwa
jamii na utulivu ndani ya jamii.

Mheshimiwa Spika, naomba nisisitize kwamba kuwe na uwekezaji unaokusudiwa
wa kunyanyua viwango vya michezo, kuanzia ngazi za kijana/watoto. Hii ni namna moja ya kumsaidia Kocha mpya wa Taifa wa kandanda kutekeleza kazi yale.
Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.
 
Ni mimi ndiye niliyesema kuwa Malima, Mbunge ni mkrugenzi katika kampuni za Manji, kama walivyo wabunge wengi wa taifa letu, sasa hili lisitake kugeuzwa kwa sababu Malima an sooo la Manji, NO! Malima ni mkurugenzi wa kampuni za Manji, kama Spika wa bunge lililopita alivyokuwa kwenye kampuni za RA, Vodacom, na ninaweza nikawatja wabunge wote ambao ni wakurugenzi kwenye kampuni za wawekezaji, tena kuanzia CCM mpaka wa upinzani, sasa ikitokea soo wasianze kukwepa wajibu wao, ninarudia tena niliyesema kuwa Malima ni mkurugezni katika kampuni za Manji ni mimi, FULL STOP,

Na ndio hasa kilichokuwa kiini cha Azimio la Znzibar, lililovunja Azimio La Arusha, ilikuwa kuwapa mwanya viongozi waswe masikini kwa kuwa na kazi zaidi ya ubunge! Spika Msekwa aliwezaje kuwa mkurugenzi kwenye kampuni ya mbunge mwenziwe? Mbona hakulia mtu, why now sasa kusikia Malima ni mkurugenzi wa kampuni za Manji, mimi sina tatizo na Malima nothing, lakini siku zote ninasimamia ukweli pamoja na kwamba Malima ni mbunge wa chama changu, mimi sioni dhambi ya yeye kuwa mkurugenzi wa Manji, maana kisheria anaruhusiwa,

sasa anayelalamika kuhusu hilo ninaomba kuelewa analalamika kwa misingi gani, au kwa hoja gani?

kwa wale mnaomtetea Malima ninasema kwamba, Malima alipaswa kuelewa kuwa sasa yuko kwenye siasa za taifa, sasa zinapohussha matajiri ambao wote ni wachangiaji wa chama kimoja cha siasa, kwa mtu kama yeye kuingizwa kati kati, ilikuwa very politically naive of him na hii ni the price he is paying for, na hapa nitawap mfano mmoja mzito,

Wakati wa uchaguzi wa mwisho wa CCM wa wajumbe wa halmashauri kuu, Dr. Huseein Mwinyi alitaka kugombea ujumbe huo kwa mkoa wa Pwani, alichukua foum akajaza, kabla ya kuirudisha alitumiwa ujumbe na mtandao kuwa hawataki competition huko na mgombea wao, meaning kwamba hawataki kushare attention huko na mtu mwenye jina kama yeye la mtoto wa rais wa zamani kwa hiyo akaambiwa kwa hiari yake airudishe ile fomu, Hussein akaenda kwa vigogo wawili wa CCM na kuwauliza kabla hata hajamwambia baba yake, wakamwambia kijana kubali yaishe irudishe hiyo fomu, akairudisha ndio akamwambia baba yake ambaye kwa kuelewa upepo wa siasa unavyogeuka hakubisha kitu, ndio maana leo Hussein ni waziri, sasa Malima needs to learn this lesson, uliza kwanza ndugu yangu, kwa sababu look at this at mwisho wa hii kesi hao waliomtuma watamuacha kwenye mataaaaa, ni very simple siasa nashangaa kuwa hakuweza kufikiri angalau kidogo tu!
 
News Update:

Hadi hivi sasa, suala hili halijaletwa kwenye kamati ya Wabunge wa CCM.
 
Mzee Masatu,

Ninajaribu kukuelewa, Spika Sitta at this point pamoja na yote bado anasubiri uchunguzi wa PCB, na sina uhakika kuwa PCB watachunguza only part ya hiyo kesi, badala ya kesi nzima kama unavyosema kama ninakuelewa vizuri, Sitta ametoa kitabu kuhusu hii kesi ninacho, sasa tunasubiri kitabu cha Ndesamburo kuhusu hii kesi ambacho kipo njiani kutoka nikikipata tu nitakuarifu,

Katika kitabu cha Sitta, kuna mahli anadai kuwa Mengi pia ana makosa ya kumshambulia Mbunge Malima, katika vyombo vya habari, na ana matatizo manei sana na mbunge Ndesamburo, kwa hiyo kitabu cha huyu mbunge kinasubiriwa san kwa hamu ili kukata mzizi wa fitina,

Isipokuwa kwa maoni yangu, Spika kama alifikia uamuzi wa mwisho kuhusu hii kesi na kumuona Malima ana hatia kwa kanuni za bunge, basi angemuwajibisha kama alivyooombwa na wabunge wawili Anne/Sendeka, kwenye hilo bado sijamuelewa Spika,

Pili ninaiheshimu hii kesi kwa kuwa kwanza ni kesi ya kwanza na aina yake bongo, ambayo inanipa moyo na kusogelea kwetu kwenye demokrasia yaani kuheshimu Due Process. Spika ana madaraka makubwa sana na uwezo wa kuzima mswaada au ishu yoyote ile ndani ya bunge, na pia kamati za bunge zinao huo uwezo, isipokuwa ishu ikishaenda kuzungumziwa kwenye kamati ya bunge baada ya kuruhusiwa na Spika kwa kutangazwa rasmi to the public at large, hapo Spika hawezi ku-turn arround na kurudisha saaa nyuma, ni lazima aende na ishu mpaka mwisho wake, ndio maana ninasema kwenye hii kesi Spika asikwepe wajibu wake, aimalizie hii kesi, au ipelekwe kwenye fulll bune na kupigiwa kura, as a final resort na kupewa mandate na bunge ili atoe adhabu, ndio kilichobaki, lakini at this point hawezi kuingiza busara zake, no that is NONESENSE!.

Kwa wale wenzangu wanaosema kuwa hii ishu ni waste of time ninasema kuwa tunaelekea kwenye demokrasia na huu ni mwanzo tu, haturudi nyuma tena, halafu tuwe macho huu uwanja ni mkubwa na unaangaliwa na dunia nzima na hasa majirani zatu wa Kenya, Uganda na Warundi pia kwa hiyo tuwe makini na tunayosema hapa!
 
Mzee Es
Heshima yako mkuu . Ulisema hoja Malima kuwa Mkurugenzi na juzi katika mahojiano alikataa kujibu hili swali . Naungana nawe Mzee Es kwamba kuna jambo na kwa nini Malima hakuna ndiyo au hapana?
 
Mzee Lunyungu,

Heshima mbele mkuu, ukweli ni ukweli na mimi sioni sababu ya yeye kukataa sasa kwa sababu ya sooo, the matter of fact anapokataa ndipo anatufanya wananchi tuanze kuwa na wasi kuwa kuna nini?

Tena bravo kwa Mzee Mwanakijiji kwa kumuuliza hilo swali, hakukuwa na ubaya wowote ule!
 
Masatu,
Maelezo ya Hansard yametoa mwanga kuhusu nini kiliendelea. Hansard inathibitisha kwamba Malima hakumtaja Mengi kwa jina wakati alipozungumza bungeni.

Sijui kilichotokea mpaka kulazimisha suala hili kufika mbele ya kamati ya bunge. Kinachonishangaza, kutokana na maelezo ya Spika, ni Malima kulazimika kutoa ushahidi wa kuthibitisha kauli yake bungeni kwa kamati ya maadili. Spika anadai vielelezo vya Malima vilishindwa kuthibitisha kwamba Raisi na Waziri Mkuu walipewa jumla ya dakika 4, na mmiliki wa TV alipewa dakika 10--nusu ya muda wa habari za kitaifa!!

Sasa pamoja na kwamba Malima hakumtaja kwa jina, je ni kwanini Mengi amelilamikia suala hili? Je, maelezo ya Malima yalikuwa yanatosha kujua kwamba alikuwa akimzungumzia Mengi bila kumtaja jina?

Kwa kweli ingekuwa vizuri kama maelezo ya kamati ya maadili, pamoja na maoni ya dissenters yangepatikana. Tungeweza kujua ukweli uko wapi; tungeweza kuelewa kwanini Spika ameamua kuiweka kando ripoti ya kamati na kutumia "busara za spika" kutatua "mgogoro" huu.
 
Mzee Joka,

Kitabu cha Spika, kinayo yote unayoyasema ni chekundu hivi kidogo kina kurasa 32, wabunge wawili walimpata Malima kuwa na hati akulidanganya bunge, kama Malima hakuwa anamsema Mengi kwenye malalmioko yake bungeni, basi kusingekuwa na kesi kabisaaa!

Muda wa kukiweka kitabu chote hapa sinao, lakini ninaweza kuki-print na kumtafuta mtu yoyote wa hapa akiweke hapa. Ingawa mpaka sasa sina uhakika kama kinaruhusiwa ila nitauliza hilo kwanza!

Ila for the record kinakuja kitabu cha Ndesamburo, patamu sana hapo!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom