Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
- Thread starter
- #221
ile makala yangu ya "jinamizi la CCM litamkaba Malima?" bado ina ukweli!! wakati wote mnafuatilia hili la Malima.. macho yangu yote yako kwenye suala la Richmond!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wandugu
Kitu ninachopenda hapa JF ni watu wanavyokuwa wanaacha ushabiki na kuzungumzia FACTS. ule ushabiki wa wanaosema ndiyo waseme ndio, ndioooooooooo nknk , i.e. ushabiki wa Simba na Yanga hapa JF si MAHALI pake
The Content of the material tells the fact kwamba Mh Malima alisema UONGO period. other than that ni USHABIKI ambao ni waste of time kama ambavyo sasa huyu kid kilaza anajitahidi kufanya (kwenda kwa Makamba). and afterall ITV sio TVT!!!
kwa mabye hakuona hebu soma hapa chini..................
SPIKA ALISEMA---Kauli ya Mhe. Malima kwamba:-
Nimewahi kushuhudia mimi Rais wa Jamhuri ya Muungano ana habari nzito kwenye taarifa ya habari ya saa mbili anapewa dakika moja na nusu, Waziri Mkuu anataka kuzungumzia njaa anapewa dakika moja na nusu, watoto wa Primary wanakuja kutoka Zanzibar kutembelea Kiwanda cha Coca-Cola wanapewa dakika kumi. Mmiliki wa TV anakwenda kuongea na watoto wa Madrasa Msasani kwa ajili ya kugombana na Sheikh mmoja anapewa dakika kumi.
SPIKA AKAENDELEA, "Inadhihirisha wazi na kushawishi kuwa Mhe. Malima alikuwa anatoa taarifa ya jambo alilolishuhudia yeye mwenyewe.
Katika kauli yake, Mhe. Malima alikuwa anazungumzia kitu cha kitaalam, yaani muda wa kurusha matangazo hewani (Air time), ambapo muda hupimwa kwa sekunde. Kamati ilifanya uchunguzi kwa kuangalia kanda za televisheni za matukio yote yaliyokuwa yametajwa Bungeni na Mheshimwa Malima. Imedhihirika kwamba, kanda za pande zote mbili yaani za Bw Mengi na alizoziwasilisha Mhe Malima. Imebainika kuwa, si kweli kwamba, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipewa dakika moja na nusu, watoto wa Primary kutoka Zanzibar waliotembelea Kiwanda cha Coca-Cola walipewa dakika kumi na Mmiliki wa ITV alipokuwa anaongea na watoto wa Madrasa Msasani alipewa dakika kumi.
Katika ushahidi wa kanda iliyowasilishwa na Bw. Mengi, tukio la Bw. Mengi kutembelea Madrasa ya Msasani lilirushwa hewani kwa dakika 4.21, tukio la ziara ya watoto wa Laurent International ya Zanzibar kutembelea ITV Mikocheni lilirushwa hewani kwa dakika 3.17, tukio la Waziri Mkuu akizungumzia njaa lilirushwa hewani kwa dakika 5.04 na tukio la ziara ya Rais Msumbiji lilirushwa hewani kwa dakika 3.31.
7.2.6 Katika ushahidi wa kanda iliyowasilishwa na Mhe. Malima, tukio la ziara ya Rais Msumbiji lilirushwa hewani kwa dakika 3.20, tukio la Waziri Mkuu akizungumzia suala la njaa lilirushwa hewani kwa dakia 4.28, na matukio ya Bw. Mengi kutembelea Madrasa ya Msasani na lile la watoto wa Primary ya Zanzibar kutembelea ITV na Coca-cola yalirushwa hewani kwa dakika 5.50 kwa ujumla wake.
7.2.7 Matokeo hayo ya uchunguzi wa Kamati hiyo ya Bunge yanaonesha wazi kuwa, matamshi ya Mhe. Malima hayakutimiza masharti niliyoyataja kwenye aya ya 5.4.2.1 hapo juu, yaani kwamba, yamevunja na kukiuka masharti na matakwa ya Kanuni ya 50(1) ya Kanuni za Bunge (Toleo la 2004) ambayo, pamoja na mambo mengine, inapiga marufuku Mbunge yeyote kusema Uwongo Bungeni."
Kwa uelewa mzuri, Kanuni hiyo inatamka kwamba:-
Ni marufuku kabisa kusema uwongo Bungeni. Kwa sababu hiyo, Mbunge yeyote anapokuwa akisema Bungeni, atawajibika kuwa na hakika kwamba, maelezo anayoyatoa ni sahihi, na siyo mambo ya kubuni au ya kubahatisha tu;
Ukweli huo unatusaidia kujibu hoja ya pili kwamba, kutokana na kukiuka masharti ya Kanuni ya 50(1) ya Kanuni za Bunge, matamshi ya Mhe. Malima aliyoyatoa Bungeni hayana kinga inayotolewa na Ibara ya 100(1) ya Katiba na Kifungu cha 3 cha Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, 1988.
Kazi et al,
Sakata la Malima na Mengi ni tofauti na lile la Cheyo na Shibuda na huenda ilikuwa sahihi kutumia njia tofauti kuyashughulikia:
KUMBUKA, baada ya Malima kusema (kudai?) bungeni kuwa kituo fulani cha TV hakitoi kipaumbele kwa habari za kitaifa kulinganisha na habari za mmiliki wa kituo hicho, Mengi (ambaye pasi na shaka ndiye huyo mmiliki wa hicho kituo japo hakutajwa wazi wala kwa jina) akawasilisha MALALAMIKO yake kwa Spika kudai kuwa Malima hakumtendea haki KUMJADILI au KUMZUNGUMZIA yeye huku akijua kuwa hayumo bungeni na hivyo hawezi kujitetea.
Kabla ya kuwasilisha malalamiko rasmi kwa spika, vyombo vya Mengi vikatoa kauli kali dhidi ya Malima kuhusu kauli yake bungeni. Kuona hivyo, Malima naye akawasilisha MALALAMIKO yake kwa spika kuhusu mtu/asasi nje ya bunge kumlalamikia mbunge kwa taarifa/kauli aliyoitoa bungeni.
Kwangu mimi hapo ndipo UMUHIMU wa kamati kuangalia madai ya Mengi, ambaye si mbunge, upo. Na pia kamati kuangalia kama madai ya Malima yana hoja.
Swali kuu ni je, Bunge lina mipaka gani kumjadili mtu aliye nje ya bunge bila kumpa nafasi ya kujitetea? Linalofanana na hilo, ila kwa upande wa pili wa shilingi, ni je, MTU/ASASI nje ya Bunge anaweza kulishtaki au hata kulilalamikia bunge? Hiyo ndiyo ilikuwa test case.
Tukumbuke huko nyuma wakati wa spika Msekwa, kuna baadhi ya watu waliwahi kuonywa na bunge (kwa haraka namkumbuka Mama Tery) kwa kutoa kauli nje ya bunge ambazo wabunge/bunge halikuridhishwa nazo na likawataka waombe msamaha baada ya kuitwa na kuhojiwa na kamati kwa kauli zao hizo.
Nakumbuka pia, baadhi ya vyombo vya habari viliwahi kukaripiwa na bunge kwa "kujadili" mwenendo wa bunge. Hata IGP Mahita aliwahi kukemewa na bunge baada ya kuwashutumu wabunge nje ya bunge kwa kulalamikia "kitu wasichokijua"; ilibidi anywee.
Wakati anapokea malalamiko ya Mengi, Spika alisema wazi kuwa, bunge lina mipaka yake na kusisitiza kuwa wabunge lazima wawajibike kwa kauli na matendo yao.
Suala la kina Cheyo na Shibuda, ni kwamba wote ni wabunge, na mmoja (Cheyo) alidai kuwa Shibuda kasema uongo kuhusu matumizi ya pesa za wakulima (wa Shinyanga) kutumika vizuri, ikiwa ni pamoja na kujenga shule. Cheyo alidai kuwa pesa zimeliwa na wajanja. Shibuda akamtaka Cheyo athibitishe kauli yake kwa takwimu. Ndipo spika akampa muda Cheyo, na aliposhindwa kuthibitisha madai yake, akaambiwa afute kauli yake na amuombe msamaha mbunge mwenzie. Kwa hiyo wahusika wakuu katika sakata hili walikuwemo bungeni na walipata nafasi ya kutetea hoja zao. Hiyo na tofauti na suala la Mengi na Malima.
Nasema umakini haukuwepo kulipeleka swala kwenye Tume bila ya kufanya screening ya ushahidi kwani wangefanya screening ya ushahidi kutoka pande zote mbili yaani toka kwa mengi na Malima tusingefikia kwenye kuunda tume kwani tukumbuke ushahidi ulikuwa mikanda ingeangaliwa bungeni na hata mengi kualikwa kwani ni watu wangapi wanaaalikwa bungeni siku hizi?Kuna wabunge wengi wanaalika watu wao kwenye ukumbi wa bunge na spika hutoa utambulisho kwanini hili la kualikwa mengi kuhudhuria shauri lake limeshindikana?Matokeo ya kukurupuka kwenye tume ni HASARA KUBWA AMBAYO KAMA NINGEKUWA SPIKA NISINGEFIKA HUKO NA NINGEOKOA FEDHA YA WALIPA KODI KWA KUFANYA SCREENING..................Na hili lingemalizika hapo na kwa ukweli tulionao mpaka sasa ningemuadhibu malima kutokana na kanuni husika Full Stop!Hayo mengine yote yameletwa na maamuzi mabovu ktk kulishughulikia swala husika.KNCU,
Tofauti iliyopo ni kubwa na ya msingi kama alivyosema Mwanagenzi. Kwa kuwa mlalamikaji/mlalamikiwa sio mbunge na mwingine ni mbunge, Spika asingweza kulishughulika sawa na kesi ya Cheyo, Wangwe nk.
Kulipeleka suala hili kwenye kamati ilikuwa sahihi, alichovurunda mzee six ni kuto heshima maamuzi ya kamati yake mwenyewe na kuja na "mtishamba wa busara zangu"
Mungu Ibariki Tanzania
Absolutely right,Na hapa ndipo ninaposema hiyo mitishamba ya busara ndiyo ilitakiwa itumike kufanya screening ,Na ukweli ungejulikana mapema kwamba malima ameshidwa kuproof madai yake then the issue could be eliminated for further hearing.Hapa Tungeokoa muda na kikubwa Fedha yetu milioni mia moja huku kuna watu wanakufa kwa kukosa dawa,hospitali ya TAIFA HAINA VITANDA VYA KUTOSHA TUNGEWEZA HATA KUWEKA VITANDA KWENYE WODI ZOTE ZA HOSPITALI YA TAIFA,WANAFUNZI HAWANA MADAWATI YA KUKALIA TUNGEPUNGUZA KADHIA HII KWA BAADHI YA SHULE.Mzee Joka,
cha msingi kwenye maoni yao, na wanadai Malima hakuwa na kesi isipokuwa aliwapotezea muda wa bure wabunge na taifa zima kwa ujumla, kwa sababu tepu hazikuthibitisha madai yake, ambayo ndio iliyokuwa kesi ya msingi kwenye hiyo kesi ya kamati ya bunge!!
Hapa ndiyo patamu kama Mh. sendeka alionya toka awali na NATUMAI ALIMTAHADHARISHA HATA SPIKA JUU YA HILO ,Sasa hapa ni sehemu nyingine ambayo Decision making ilikuwa poor,Kama kulikuwa na fununu za uwepo wa Rushwa au HATA MAZINGIRA YA RUSHWA kwanini spika Hakuivunja hiyo tume hata kabla ya kufika mbali kwani tungeokoa angalau kiasi fulani cha fedha Hii ni sehemu nyingine Busara ya Spika kama anavyodai ilitakiwa itumike Lakini aliiponyosha nafasi hiyo.Ndani ya kikao hicho mbunge Sendeka aliwaonya wenziwe sio mara moja kuwa anaamini wamekula rushwa, na wakti mmoja hata el aliitwa humo kwenye kikao na akamuoanya kuwa anaamini na yeye pia amekula rushwa,
sasa mzee wangu ngoja niseme the real nyeti ya hii kesi ambazoi sikutaka kusema siku zote,
Ni kwamba ndani ya bunge jipya kuna vyombo vya kisasa vya kunasa kila kinachoendelea ndani ya mikutano ya bunge na wabunge kwenye kamati, vyombo hivyo hunasa hata sauti ya kukohoa au sauti yoyote ile ya binadamu ndani ya kikao, inasemekana wakati wa vikao vya siri vya wabunge wa ccm peke yao mambo yote yalikuwemo humo kwenye hivyo vyombo, Ndesamburo inasemekana ana kopi za hiyo mikutano ya siri kutoka kwenye hivyo vyombo, ambazo zinaeleza wazi juu ya mabishano hayo ya rushwa kuwa nani amekula nini, ndio maana hakuwa na wasi wasi kujitoa kwenye kamati na kuipeleka kesi yake PCB, na pia alimuonyesha Spika, ndio mana naye ikabidi aipeleke pcb,
Ndesamburo na Mengi, walikuwa wakiwasiliana all the time wakati wa kesi, el alimuta Mengi mara mbili wakati kesi ikiendelea, mara ya kwanza alimuambia kuwa Manji amewahonga wabunge ili wamuuue Mengi, mara ya pili alimuita na kumuambia ajitoe kwenye hiyo kesi kwani hawezi kushinda, inasemekana kwenye vikao vyote viwili na el Mengi alimrekodi mkuuu bila ya yeye kujua kutokana na kushuriwa na washauri wake kabla ya kwenda kumuona, Ndesamburo made very clear kwa Spika kuhusu yote haya na hata kwa pcb,........... siwezi kwenda ndani zaidi maana ni nyeti mno..............!!!
Hakuna kinachoshangaza kutumika mitishamba ya Busara kwenye Dakika za mwisho za kesi kwani busara halisi zilipotakiwa kutumika halikufanyika Busara usainii ndiyo zikachukua mkondo na lengo kubwa ilikuwa si kumlinda malima tu bali kuwalinda na wanatume ambao walikuwa wanatuhumiwa na kubeba credibility ya chama chake.sasa hapa ndipo alipokosea zaidi kwani Malima anahakika kwa kibunda kilichotolewa na mchochezi mada(Manji)kwa kuwanunua karibu wote waliotegemea kutoa haki kwa kumuona Malima hana Kosa,kwa kiswahili fasaha kwenye kesi kama hii unapomuona Malima hana kosa basi kwa maneno mengine Mengi ana Kosa ,Na kwasababu Malima anajua nini kiliamuliwa na kamati ndiyo maana kwa kufuata ushauri wao hao wachochezi mada akatunisha kifua kwamba Spika Kachemsha na hakumtendea haki tena wapi? kwa Rafiki yake Manji mwengine Makamba ili atumie nafasi yake kuu kichama amdhibiti Spika.Je unashangaa kwa nini ilitumika "mitishamba ya busara?" je pcb kweli watakuja na majibu halali kwa wananchi na taifa kwa ujumla? Nafikiri hii kesi imeshaisha kabla hata haijaanza!
Masatu,
majority wa wajumbe wa kamati wamemuona mh.malima hana makosa. sasa ni vigezo vipi wamevitumia wakati ushahidi wake, according to spika, haukuweza kuthibitisha madai yake ndani ya bunge? kwa maneno mengine ni kwa msingi upi majority ya wajumbe wa kamati wameshindwa kumhukumu malima kwa kusema uongo?
yaani i am so curious kuona opinions zote mbili za wajumbe wa kamati ya maadili. suala hili kama lilivyo sasa hivi linanipa kigugumizi.