Barua ya Adam Malima kumpinga Spika!

Barua ya Adam Malima kumpinga Spika!

Status
Not open for further replies.
ile makala yangu ya "jinamizi la CCM litamkaba Malima?" bado ina ukweli!! wakati wote mnafuatilia hili la Malima.. macho yangu yote yako kwenye suala la Richmond!!
 
Wandugu

Kitu ninachopenda hapa JF ni watu wanavyokuwa wanaacha ushabiki na kuzungumzia FACTS. ule ushabiki wa wanaosema ndiyo waseme ndio, ndioooooooooo nknk , i.e. ushabiki wa Simba na Yanga hapa JF si MAHALI pake

The Content of the material tells the fact kwamba Mh Malima alisema UONGO period. other than that ni USHABIKI ambao ni waste of time kama ambavyo sasa huyu kid kilaza anajitahidi kufanya (kwenda kwa Makamba). and afterall ITV sio TVT!!!

kwa mabye hakuona hebu soma hapa chini..................
SPIKA ALISEMA---Kauli ya Mhe. Malima kwamba:-
“Nimewahi kushuhudia mimi Rais wa Jamhuri ya Muungano ana habari nzito kwenye taarifa ya habari ya saa mbili anapewa dakika moja na nusu, Waziri Mkuu anataka kuzungumzia njaa anapewa dakika moja na nusu, watoto wa ‘Primary’ wanakuja kutoka Zanzibar kutembelea Kiwanda cha Coca-Cola wanapewa dakika kumi. Mmiliki wa TV anakwenda kuongea na watoto wa Madrasa Msasani kwa ajili ya kugombana na Sheikh mmoja anapewa dakika kumi.”

SPIKA AKAENDELEA, "Inadhihirisha wazi na kushawishi kuwa Mhe. Malima alikuwa anatoa taarifa ya jambo alilolishuhudia yeye mwenyewe.

Katika kauli yake, Mhe. Malima alikuwa anazungumzia kitu cha kitaalam, yaani muda wa kurusha matangazo hewani (Air time), ambapo muda hupimwa kwa sekunde. Kamati ilifanya uchunguzi kwa kuangalia kanda za televisheni za matukio yote yaliyokuwa yametajwa Bungeni na Mheshimwa Malima. Imedhihirika kwamba, kanda za pande zote mbili yaani za Bw Mengi na alizoziwasilisha Mhe Malima. Imebainika kuwa, si kweli kwamba, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipewa dakika moja na nusu, watoto wa Primary kutoka Zanzibar waliotembelea Kiwanda cha Coca-Cola walipewa dakika kumi na Mmiliki wa ITV alipokuwa anaongea na watoto wa Madrasa Msasani alipewa dakika kumi.

Katika ushahidi wa kanda iliyowasilishwa na Bw. Mengi, tukio la Bw. Mengi kutembelea Madrasa ya Msasani lilirushwa hewani kwa dakika 4.21, tukio la ziara ya watoto wa Laurent International ya Zanzibar kutembelea ITV Mikocheni lilirushwa hewani kwa dakika 3.17, tukio la Waziri Mkuu akizungumzia njaa lilirushwa hewani kwa dakika 5.04 na tukio la ziara ya Rais Msumbiji lilirushwa hewani kwa dakika 3.31.

7.2.6 Katika ushahidi wa kanda iliyowasilishwa na Mhe. Malima, tukio la ziara ya Rais Msumbiji lilirushwa hewani kwa dakika 3.20, tukio la Waziri Mkuu akizungumzia suala la njaa lilirushwa hewani kwa dakia 4.28, na matukio ya Bw. Mengi kutembelea Madrasa ya Msasani na lile la watoto wa ‘Primary’ ya Zanzibar kutembelea ITV na Coca-cola yalirushwa hewani kwa dakika 5.50 kwa ujumla wake.

7.2.7 Matokeo hayo ya uchunguzi wa Kamati hiyo ya Bunge yanaonesha wazi kuwa, matamshi ya Mhe. Malima hayakutimiza masharti niliyoyataja kwenye aya ya 5.4.2.1 hapo juu, yaani kwamba, yamevunja na kukiuka masharti na matakwa ya Kanuni ya 50(1) ya Kanuni za Bunge (Toleo la 2004) ambayo, pamoja na mambo mengine, inapiga marufuku Mbunge yeyote kusema Uwongo Bungeni."


Kwa uelewa mzuri, Kanuni hiyo inatamka kwamba:-

“Ni marufuku kabisa kusema uwongo Bungeni. Kwa sababu hiyo, Mbunge yeyote anapokuwa akisema Bungeni, atawajibika kuwa na hakika kwamba, maelezo anayoyatoa ni sahihi, na siyo mambo ya kubuni au ya kubahatisha tu;”…

Ukweli huo unatusaidia kujibu hoja ya pili kwamba, kutokana na kukiuka masharti ya Kanuni ya 50(1) ya Kanuni za Bunge, matamshi ya Mhe. Malima aliyoyatoa Bungeni hayana kinga inayotolewa na Ibara ya 100(1) ya Katiba na Kifungu cha 3 cha Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, 1988.

Ogah umenena Huko nyuma kwenye thread hii nilisema Spika Ametumia Ubabe ule ule wa kutomuadhibu mkosaji kwasababu kuendeleza uchama,Kwani Kosa la malima na lile la c heyo lilitofautiana nini? Lakini Cheyo aliadhibiwa kwa kanuni za kifungu hicho hicho lakini Malima aliambiwa watapatanishwa?

(upotovu na ukiukwaji wa taratibu husika ndani ya Bunge na aliyefanya ni mtu aliyepewa jukumu la kusimamia taratibu hizo)Angalia swala la cheyo na shibuda halikuundiwa tume kwanini la Mengi na Malima liliundiwa tume? Kwa mtazamo wangu kimsingi maswala yote yalikuwa karibu yanafanana na ni wabunge wawili kutoa tuhuma kwa watu wawili tofauti, tuhuma ambazo hazikuwa na ukweli.Sasa ilikuwaje wabunge hawa wawili maswala yao yakapewa uzito tofauti hadi moja likapelekea kula au kutafuna fedha za walipa kodi kwa kiwango cha juu sana?Unajua nini?

Ndiyo maana nilisema Spika anavuna alichopenda kwa kuendeleza ubabe tena kwa kumbeba mtu asiyebebeka.Kuna watu walisema uwezo wake kama spika unampa haki hiyo,HAPA NINASEMA AMEITUMIA VIBAYA HAKI YAKE HIYO NA SASA KIVULI CHAKE KINAMKIMBIZA PUTA.Huko nyuma nilisema adhabu ya Malima ingekuwa kali zaidi kwasasa kama swala litarudi bungeni kwa Mh. Spika kukubali kumeza matapishi yake mwenyewe huko apewe adhabu kali sana ikiwemo ya kulipia gharama ya fedha ya walipa kodi iliyopotea kwa yeye kulidanganya Bunge huku akielewa kwamba alichokuwa akisimamia ni uongo.

Spika na wabunge wote hawakuwa makini toka awali,kwasababu mtu anapotoa tuhuma kwamba mmiliki anapewa dakika kumi kwenye kurusha habari zinazomuhusu yeye kwenye taarifa habari na Rais anapewa dk.1-2,Hivi mnaoangalia taarifa ya habari ni TAARIFA YA HABARI GANI INAYOCHUKUA DK 10 TU KUZUNGUMZIA KITU KIMOJA,JE MUDA HALISI WA KURUSHA TAARIFA HABARI YOTE HEWANI NI MUDA GANI?Hapa hapakuhitaji hata kufika huko mbali kubaini hakuna ukweli?Lakini ikawa hoja na kutufikisha mabonde kuinama na kupoteza fedha kibao ambazo zingetumika kwa shughuli za maendeleo.

Sijui kuna sheria gani ya kumuadhibu spika Lakini nafikiri na yeye alistahili kupewa adhabu kali kwa kutumia madaraka yake vibaya na kutosimamia kanuni za uendeshaji bunge ktk maamuzi aliyoyatoa pamoja na Mh Malima kulidanganya Bunge, hili limeshusha credibility yake na kutusababishia hasara kama walipa kodi kwa kujifanya ametumia buasara wakati mwisho wa siku hatuioni busara bali tunaona maamuzi yote toka awali hayakuzingatia uchambuzi yakinifu kuanzia ya kuunda tume hadi ya maamuzi ya mwisho.

Hapa kama kweli wapinzani wangekuwa na nguvu nafikiri walitakiwa waunganishe mambo na kuweka uwepo wa kutokuwa na imani na spika kwani naamini ndiyo huyu aliyemhukumu cheyo kwa kusema uongo(mpinzani)kumuacha malima kwa kusema uongo (kutoka chama chake).
 
Kazi et al,
Sakata la Malima na Mengi ni tofauti na lile la Cheyo na Shibuda na huenda ilikuwa sahihi kutumia njia tofauti kuyashughulikia:
KUMBUKA, baada ya Malima kusema (kudai?) bungeni kuwa kituo fulani cha TV hakitoi kipaumbele kwa habari za kitaifa kulinganisha na habari za mmiliki wa kituo hicho, Mengi (ambaye pasi na shaka ndiye huyo mmiliki wa hicho kituo japo hakutajwa wazi wala kwa jina) akawasilisha MALALAMIKO yake kwa Spika kudai kuwa Malima hakumtendea haki KUMJADILI au KUMZUNGUMZIA yeye huku akijua kuwa hayumo bungeni na hivyo hawezi kujitetea.

Kabla ya kuwasilisha malalamiko rasmi kwa spika, vyombo vya Mengi vikatoa kauli kali dhidi ya Malima kuhusu kauli yake bungeni. Kuona hivyo, Malima naye akawasilisha MALALAMIKO yake kwa spika kuhusu mtu/asasi nje ya bunge kumlalamikia mbunge kwa taarifa/kauli aliyoitoa bungeni.

Kwangu mimi hapo ndipo UMUHIMU wa kamati kuangalia madai ya Mengi, ambaye si mbunge, upo. Na pia kamati kuangalia kama madai ya Malima yana hoja.
Swali kuu ni je, Bunge lina mipaka gani kumjadili mtu aliye nje ya bunge bila kumpa nafasi ya kujitetea? Linalofanana na hilo, ila kwa upande wa pili wa shilingi, ni je, MTU/ASASI nje ya Bunge anaweza kulishtaki au hata kulilalamikia bunge? Hiyo ndiyo ilikuwa test case.

Tukumbuke huko nyuma wakati wa spika Msekwa, kuna baadhi ya watu waliwahi kuonywa na bunge (kwa haraka namkumbuka Mama Tery) kwa kutoa kauli nje ya bunge ambazo wabunge/bunge halikuridhishwa nazo na likawataka waombe msamaha baada ya kuitwa na kuhojiwa na kamati kwa kauli zao hizo.
Nakumbuka pia, baadhi ya vyombo vya habari viliwahi kukaripiwa na bunge kwa "kujadili" mwenendo wa bunge. Hata IGP Mahita aliwahi kukemewa na bunge baada ya kuwashutumu wabunge nje ya bunge kwa kulalamikia "kitu wasichokijua"; ilibidi anywee.

Wakati anapokea malalamiko ya Mengi, Spika alisema wazi kuwa, bunge lina mipaka yake na kusisitiza kuwa wabunge lazima wawajibike kwa kauli na matendo yao.

Suala la kina Cheyo na Shibuda, ni kwamba wote ni wabunge, na mmoja (Cheyo) alidai kuwa Shibuda kasema uongo kuhusu matumizi ya pesa za wakulima (wa Shinyanga) kutumika vizuri, ikiwa ni pamoja na kujenga shule. Cheyo alidai kuwa pesa zimeliwa na wajanja. Shibuda akamtaka Cheyo athibitishe kauli yake kwa takwimu. Ndipo spika akampa muda Cheyo, na aliposhindwa kuthibitisha madai yake, akaambiwa afute kauli yake na amuombe msamaha mbunge mwenzie. Kwa hiyo wahusika wakuu katika sakata hili walikuwemo bungeni na walipata nafasi ya kutetea hoja zao. Hiyo na tofauti na suala la Mengi na Malima.
 
Kazi et al,
Sakata la Malima na Mengi ni tofauti na lile la Cheyo na Shibuda na huenda ilikuwa sahihi kutumia njia tofauti kuyashughulikia:
KUMBUKA, baada ya Malima kusema (kudai?) bungeni kuwa kituo fulani cha TV hakitoi kipaumbele kwa habari za kitaifa kulinganisha na habari za mmiliki wa kituo hicho, Mengi (ambaye pasi na shaka ndiye huyo mmiliki wa hicho kituo japo hakutajwa wazi wala kwa jina) akawasilisha MALALAMIKO yake kwa Spika kudai kuwa Malima hakumtendea haki KUMJADILI au KUMZUNGUMZIA yeye huku akijua kuwa hayumo bungeni na hivyo hawezi kujitetea.

Kabla ya kuwasilisha malalamiko rasmi kwa spika, vyombo vya Mengi vikatoa kauli kali dhidi ya Malima kuhusu kauli yake bungeni. Kuona hivyo, Malima naye akawasilisha MALALAMIKO yake kwa spika kuhusu mtu/asasi nje ya bunge kumlalamikia mbunge kwa taarifa/kauli aliyoitoa bungeni.

Kwangu mimi hapo ndipo UMUHIMU wa kamati kuangalia madai ya Mengi, ambaye si mbunge, upo. Na pia kamati kuangalia kama madai ya Malima yana hoja.
Swali kuu ni je, Bunge lina mipaka gani kumjadili mtu aliye nje ya bunge bila kumpa nafasi ya kujitetea? Linalofanana na hilo, ila kwa upande wa pili wa shilingi, ni je, MTU/ASASI nje ya Bunge anaweza kulishtaki au hata kulilalamikia bunge? Hiyo ndiyo ilikuwa test case.

Tukumbuke huko nyuma wakati wa spika Msekwa, kuna baadhi ya watu waliwahi kuonywa na bunge (kwa haraka namkumbuka Mama Tery) kwa kutoa kauli nje ya bunge ambazo wabunge/bunge halikuridhishwa nazo na likawataka waombe msamaha baada ya kuitwa na kuhojiwa na kamati kwa kauli zao hizo.
Nakumbuka pia, baadhi ya vyombo vya habari viliwahi kukaripiwa na bunge kwa "kujadili" mwenendo wa bunge. Hata IGP Mahita aliwahi kukemewa na bunge baada ya kuwashutumu wabunge nje ya bunge kwa kulalamikia "kitu wasichokijua"; ilibidi anywee.

Wakati anapokea malalamiko ya Mengi, Spika alisema wazi kuwa, bunge lina mipaka yake na kusisitiza kuwa wabunge lazima wawajibike kwa kauli na matendo yao.

Suala la kina Cheyo na Shibuda, ni kwamba wote ni wabunge, na mmoja (Cheyo) alidai kuwa Shibuda kasema uongo kuhusu matumizi ya pesa za wakulima (wa Shinyanga) kutumika vizuri, ikiwa ni pamoja na kujenga shule. Cheyo alidai kuwa pesa zimeliwa na wajanja. Shibuda akamtaka Cheyo athibitishe kauli yake kwa takwimu. Ndipo spika akampa muda Cheyo, na aliposhindwa kuthibitisha madai yake, akaambiwa afute kauli yake na amuombe msamaha mbunge mwenzie. Kwa hiyo wahusika wakuu katika sakata hili walikuwemo bungeni na walipata nafasi ya kutetea hoja zao. Hiyo na tofauti na suala la Mengi na Malima.

msingi wa swala zima umelalia pale pale tofauti yao ni kwamba kwenye swala hili mmoja mbunge mwengine si mbunge kwaninini baada ya kusiliza malalamiko ya pande zote mbili wasingeomba vielelezo vya udhibitisho kwa kutoka pande mbili zinazotuhumiana?Ushughulikiaji wake ndiyo haukua sahihi kwa muono wangu na ndiyo uliotuingizia hasara walipa kodi,Nafikiri wangeleta vielelezo tokea awali kabla ya kukurupuka kuunda tume ,tusingefikia tulipofikia Leo.Mbivu na mbichi zingejulikana katika hatua za awali na tungenusuru mafedha yetu ,muda na malumbano yasiyo na msingi.Na mkosaji angeadhibiwa kwa kanuni husika basi.
 
KNCU,

Tofauti iliyopo ni kubwa na ya msingi kama alivyosema Mwanagenzi. Kwa kuwa mlalamikaji/mlalamikiwa sio mbunge na mwingine ni mbunge, Spika asingweza kulishughulika sawa na kesi ya Cheyo, Wangwe nk.

Kulipeleka suala hili kwenye kamati ilikuwa sahihi, alichovurunda mzee six ni kuto heshima maamuzi ya kamati yake mwenyewe na kuja na "mtishamba wa busara zangu"

Mungu Ibariki Tanzania
 
Masatu,
majority wa wajumbe wa kamati wamemuona mh.malima hana makosa. sasa ni vigezo vipi wamevitumia wakati ushahidi wake, according to spika, haukuweza kuthibitisha madai yake ndani ya bunge? kwa maneno mengine ni kwa msingi upi majority ya wajumbe wa kamati wameshindwa kumhukumu malima kwa kusema uongo?

yaani i am so curious kuona opinions zote mbili za wajumbe wa kamati ya maadili. suala hili kama lilivyo sasa hivi linanipa kigugumizi.
 
Mzee Joka,

Heshima mbele mkuuu, Spika hataki maoni ya wabunge wawili waliopingana na wenzao ndani ya kamati yatoke kwa wananchi, lakini tunayo wanachodai ni kwamba kulikuwa na rushwa kwa upande wa wenzao wanaopingana nao,

Ndicho cha msingi kwenye maoni yao, na wanadai Malima hakuwa na kesi isipokuwa aliwapotezea muda wa bure wabunge na taifa zima kwa ujumla, kwa sababu tepu hazikuthibitisha madai yake, ambayo ndio iliyokuwa kesi ya msingi kwenye hiyo kesi ya kamati ya bunge!

Ndani ya kikao hicho mbunge Sendeka aliwaonya wenziwe sio mara moja kuwa anaamini wamekula rushwa, na wakti mmoja hata el aliitwa humo kwenye kikao na akamuoanya kuwa anaamini na yeye pia amekula rushwa,

sasa mzee wangu ngoja niseme the real nyeti ya hii kesi ambazoi sikutaka kusema siku zote,

Ni kwamba ndani ya bunge jipya kuna vyombo vya kisasa vya kunasa kila kinachoendelea ndani ya mikutano ya bunge na wabunge kwenye kamati, vyombo hivyo hunasa hata sauti ya kukohoa au sauti yoyote ile ya binadamu ndani ya kikao, inasemekana wakati wa vikao vya siri vya wabunge wa ccm peke yao mambo yote yalikuwemo humo kwenye hivyo vyombo, Ndesamburo inasemekana ana kopi za hiyo mikutano ya siri kutoka kwenye hivyo vyombo, ambazo zinaeleza wazi juu ya mabishano hayo ya rushwa kuwa nani amekula nini, ndio maana hakuwa na wasi wasi kujitoa kwenye kamati na kuipeleka kesi yake PCB, na pia alimuonyesha Spika, ndio mana naye ikabidi aipeleke pcb,

Ndesamburo na Mengi, walikuwa wakiwasiliana all the time wakati wa kesi, el alimuta Mengi mara mbili wakati kesi ikiendelea, mara ya kwanza alimuambia kuwa Manji amewahonga wabunge ili wamuuue Mengi, mara ya pili alimuita na kumuambia ajitoe kwenye hiyo kesi kwani hawezi kushinda, inasemekana kwenye vikao vyote viwili na el Mengi alimrekodi mkuuu bila ya yeye kujua kutokana na kushuriwa na washauri wake kabla ya kwenda kumuona, Ndesamburo made very clear kwa Spika kuhusu yote haya na hata kwa pcb,........... siwezi kwenda ndani zaidi maana ni nyeti mno..............!

Je unashangaa kwa nini ilitumika "mitishamba ya busara?" je pcb kweli watakuja na majibu halali kwa wananchi na taifa kwa ujumla? Nafikiri hii kesi imeshaisha kabla hata haijaanza!
 
KNCU,

Tofauti iliyopo ni kubwa na ya msingi kama alivyosema Mwanagenzi. Kwa kuwa mlalamikaji/mlalamikiwa sio mbunge na mwingine ni mbunge, Spika asingweza kulishughulika sawa na kesi ya Cheyo, Wangwe nk.

Kulipeleka suala hili kwenye kamati ilikuwa sahihi, alichovurunda mzee six ni kuto heshima maamuzi ya kamati yake mwenyewe na kuja na "mtishamba wa busara zangu"

Mungu Ibariki Tanzania
Nasema umakini haukuwepo kulipeleka swala kwenye Tume bila ya kufanya screening ya ushahidi kwani wangefanya screening ya ushahidi kutoka pande zote mbili yaani toka kwa mengi na Malima tusingefikia kwenye kuunda tume kwani tukumbuke ushahidi ulikuwa mikanda ingeangaliwa bungeni na hata mengi kualikwa kwani ni watu wangapi wanaaalikwa bungeni siku hizi?Kuna wabunge wengi wanaalika watu wao kwenye ukumbi wa bunge na spika hutoa utambulisho kwanini hili la kualikwa mengi kuhudhuria shauri lake limeshindikana?Matokeo ya kukurupuka kwenye tume ni HASARA KUBWA AMBAYO KAMA NINGEKUWA SPIKA NISINGEFIKA HUKO NA NINGEOKOA FEDHA YA WALIPA KODI KWA KUFANYA SCREENING..................Na hili lingemalizika hapo na kwa ukweli tulionao mpaka sasa ningemuadhibu malima kutokana na kanuni husika Full Stop!Hayo mengine yote yameletwa na maamuzi mabovu ktk kulishughulikia swala husika.
 
Mzee ES,

Respect Br., kanyaga twende mzee, thanks for the deep infs, sasa tutawaachia watu wachague wapi ni kwenye pumba na wapi upo mchele.

KNKCU
Well said man!!, yaani narudia tena kusoma hicho kipengele chako hapo juu ni very Clear. yaani Mzee Six kajiingiza mwenyewe katika COBWEB, na hiyo ndio mitishamba yenyewe!!, one has to look at bottomline of the issue na SIO USHABIKI.

Respect to you All
 
Mzee Joka,

cha msingi kwenye maoni yao, na wanadai Malima hakuwa na kesi isipokuwa aliwapotezea muda wa bure wabunge na taifa zima kwa ujumla, kwa sababu tepu hazikuthibitisha madai yake, ambayo ndio iliyokuwa kesi ya msingi kwenye hiyo kesi ya kamati ya bunge!!
Absolutely right,Na hapa ndipo ninaposema hiyo mitishamba ya busara ndiyo ilitakiwa itumike kufanya screening ,Na ukweli ungejulikana mapema kwamba malima ameshidwa kuproof madai yake then the issue could be eliminated for further hearing.Hapa Tungeokoa muda na kikubwa Fedha yetu milioni mia moja huku kuna watu wanakufa kwa kukosa dawa,hospitali ya TAIFA HAINA VITANDA VYA KUTOSHA TUNGEWEZA HATA KUWEKA VITANDA KWENYE WODI ZOTE ZA HOSPITALI YA TAIFA,WANAFUNZI HAWANA MADAWATI YA KUKALIA TUNGEPUNGUZA KADHIA HII KWA BAADHI YA SHULE.
Ndani ya kikao hicho mbunge Sendeka aliwaonya wenziwe sio mara moja kuwa anaamini wamekula rushwa, na wakti mmoja hata el aliitwa humo kwenye kikao na akamuoanya kuwa anaamini na yeye pia amekula rushwa,

sasa mzee wangu ngoja niseme the real nyeti ya hii kesi ambazoi sikutaka kusema siku zote,

Ni kwamba ndani ya bunge jipya kuna vyombo vya kisasa vya kunasa kila kinachoendelea ndani ya mikutano ya bunge na wabunge kwenye kamati, vyombo hivyo hunasa hata sauti ya kukohoa au sauti yoyote ile ya binadamu ndani ya kikao, inasemekana wakati wa vikao vya siri vya wabunge wa ccm peke yao mambo yote yalikuwemo humo kwenye hivyo vyombo, Ndesamburo inasemekana ana kopi za hiyo mikutano ya siri kutoka kwenye hivyo vyombo, ambazo zinaeleza wazi juu ya mabishano hayo ya rushwa kuwa nani amekula nini, ndio maana hakuwa na wasi wasi kujitoa kwenye kamati na kuipeleka kesi yake PCB, na pia alimuonyesha Spika, ndio mana naye ikabidi aipeleke pcb,

Ndesamburo na Mengi, walikuwa wakiwasiliana all the time wakati wa kesi, el alimuta Mengi mara mbili wakati kesi ikiendelea, mara ya kwanza alimuambia kuwa Manji amewahonga wabunge ili wamuuue Mengi, mara ya pili alimuita na kumuambia ajitoe kwenye hiyo kesi kwani hawezi kushinda, inasemekana kwenye vikao vyote viwili na el Mengi alimrekodi mkuuu bila ya yeye kujua kutokana na kushuriwa na washauri wake kabla ya kwenda kumuona, Ndesamburo made very clear kwa Spika kuhusu yote haya na hata kwa pcb,........... siwezi kwenda ndani zaidi maana ni nyeti mno..............!!!
Hapa ndiyo patamu kama Mh. sendeka alionya toka awali na NATUMAI ALIMTAHADHARISHA HATA SPIKA JUU YA HILO ,Sasa hapa ni sehemu nyingine ambayo Decision making ilikuwa poor,Kama kulikuwa na fununu za uwepo wa Rushwa au HATA MAZINGIRA YA RUSHWA kwanini spika Hakuivunja hiyo tume hata kabla ya kufika mbali kwani tungeokoa angalau kiasi fulani cha fedha Hii ni sehemu nyingine Busara ya Spika kama anavyodai ilitakiwa itumike Lakini aliiponyosha nafasi hiyo.
Je unashangaa kwa nini ilitumika "mitishamba ya busara?" je pcb kweli watakuja na majibu halali kwa wananchi na taifa kwa ujumla? Nafikiri hii kesi imeshaisha kabla hata haijaanza!
Hakuna kinachoshangaza kutumika mitishamba ya Busara kwenye Dakika za mwisho za kesi kwani busara halisi zilipotakiwa kutumika halikufanyika Busara usainii ndiyo zikachukua mkondo na lengo kubwa ilikuwa si kumlinda malima tu bali kuwalinda na wanatume ambao walikuwa wanatuhumiwa na kubeba credibility ya chama chake.sasa hapa ndipo alipokosea zaidi kwani Malima anahakika kwa kibunda kilichotolewa na mchochezi mada(Manji)kwa kuwanunua karibu wote waliotegemea kutoa haki kwa kumuona Malima hana Kosa,kwa kiswahili fasaha kwenye kesi kama hii unapomuona Malima hana kosa basi kwa maneno mengine Mengi ana Kosa ,Na kwasababu Malima anajua nini kiliamuliwa na kamati ndiyo maana kwa kufuata ushauri wao hao wachochezi mada akatunisha kifua kwamba Spika Kachemsha na hakumtendea haki tena wapi? kwa Rafiki yake Manji mwengine Makamba ili atumie nafasi yake kuu kichama amdhibiti Spika.
 
Masatu,
majority wa wajumbe wa kamati wamemuona mh.malima hana makosa. sasa ni vigezo vipi wamevitumia wakati ushahidi wake, according to spika, haukuweza kuthibitisha madai yake ndani ya bunge? kwa maneno mengine ni kwa msingi upi majority ya wajumbe wa kamati wameshindwa kumhukumu malima kwa kusema uongo?

yaani i am so curious kuona opinions zote mbili za wajumbe wa kamati ya maadili. suala hili kama lilivyo sasa hivi linanipa kigugumizi.

Jokaa Kuu: Ni swali la msingi sana. Je, kamati ilitumia vigezo vipi kumwona Malima kuwa hana kosa la kusema ukweli, licha ya kuwepo ushahidi wa hiyo mikanda?
Tukiweza kupata ushahidi mhimu uliotumika kufikia uamzi huo, tutakuwa tumefumbua kitendawili. Kwa sasa tunaweza kuamini kuwa ni rushwa iliyofanya kazi, au upendeleo wa aina fulani ndani ya kamati. Na hili linatupeleka katika hatua nyingine kuhusu umakini na 'integrity' ya wabunge wetu kwa ujumla. Kama kamati nzima, isipokuwa wajumbe watatu tu (nao pengine kwa sababu zisizokuwa za msingi sana, kama za ukabila au udini wao) wameonyesha uozo mkubwa kiasi hiki, kweli tunaweza kujivuna kuwa tuna viongozi?

Mzee Es, inanibidi niungame wazi kuwa mara nyingi huwa ninashindwa kuielewa vizuri baadhi ya michango yako. Nitajitahidi sana kuendelea kujifunza ili niweze kukupata vizuri.
 
Mzee Kalamu,

Heshima mbele mkuu, mimi ni zigg zagg! bro ninakuja kueliimishwa na kuelimisha, na ni mwanachama hai wa ccm ila sipendi uozo hata kama umo ndani ya chama changu licha ya upinzani,

Mwanzoni nilidhani Spika was right jinsi alivyoi-handle hii kesi, lakini the more ninavyoelimishwa na mimi mwenyewe ninavyotafuta info za hii kesi, ninaanza kujisikia kutapika na mwenendo wa Spika katika hii kesi, pamoja na kwamba anatoka chama changu, lakini ukweli kwangu ni muhimu sana mbele ya public na hasa kutoka hii forum, ambayo sasa imeanza kuwa chombo kizito sana cha habari za ndani za nchi yetu kwa jamii,

Nadhani nimekusaidia katika quest yako ya kujaribu kuielewa michango yangu, kama haitoshi sina tatizo kuongeza ndugu yangu, the point ni kuwa sitaki uozo na hasa ndani ya chama changu, media imenunuliwa kwa hiyo mahali pa sisi wanyonge kuwatwanga watawala ni hapa!

Yaaani kumkoma nyani giladi!
 
Mzee ES,

Nashukuru unakubali sasa kuwa Spika kavurunda ktk hili.

Quote from ES
sasa mzee wangu ngoja niseme the real nyeti ya hii kesi ambazoi sikutaka kusema siku zote,

Ni kwamba ndani ya bunge jipya kuna vyombo vya kisasa vya kunasa kila kinachoendelea ndani ya mikutano ya bunge na wabunge kwenye kamati, vyombo hivyo hunasa hata sauti ya kukohoa au sauti yoyote ile ya binadamu ndani ya kikao, inasemekana wakati wa vikao vya siri vya wabunge wa ccm peke yao mambo yote yalikuwemo humo kwenye hivyo vyombo, Ndesamburo inasemekana ana kopi za hiyo mikutano ya siri kutoka kwenye hivyo vyombo, ambazo zinaeleza wazi juu ya mabishano hayo ya rushwa kuwa nani amekula nini, ndio maana hakuwa na wasi wasi kujitoa kwenye kamati na kuipeleka kesi yake PCB, na pia alimuonyesha Spika, ndio mana naye ikabidi aipeleke pcb, END

Naomba tu kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hilo hapo juu. Kwa ufahamu wangu (na ndio ukweli ulivyo) ni kuwa vikao vyote vya kamati kwenye kesi hii vilifanyika ofisi ya bunge DAR ES SALAAM na sio Ukumbi mpya wa Bunge DODOMA. (Mh Zitto anaweza kuthibitisha hili) Hivyo habari ya vinasa sauti it sounds sio sahihi, hata hivyo kama hivyo vinasa sauti pia vimefungwa ofisi ya Bunge Dar then sina ubishi ktk hilo
 
It is about time... mtu anipitishie nakala.. it is about time kuanza kutumia teknolojia kuwaumbua hawa viongozi!!!
 
Mzee Masatu,

Heshima yako mkuu, aliyenipa hizi habari ni wajumbe wawili wa kamati hiyo ambao waliajribu sana kumsihi Ndeasmburo asijitoe kwenye kamati, ndipo akawapa hayo niliyoyasema huko juu,

Mikutano ya kamati au anything ilifanyika wapi sijui, tulifika hapo baada ya mimi kuwauliza,

(1). Ni kwanini Ndesamburo, alijitoa kwenye kamati na hata kuweza kuwashutumu wabunge wa ccm kuwa wamekula ruhswa, tena hadharani bila ya kuogopa? Na kwanini kama hana ukweli mpaka leo hajakamatwa, maana can you imagine kuwashutumu wabunge wa ccm na tuhuma nzito namna hiyo bila kukamatwa?

(2). Swali langu la pili kwao ilikuwa ni kwanini Spika naye alikubali kui-refer hiii kesi kwa pcb? Na ni kwa nini mpaka leo wabunge wanaotuhumiwa kula rushwa hawajasema kitu kujibu tuhuma hizo? Kamati ilimuona Malima hana kosa, sasa ikawaje Malima tena anaenda ccm kulia?

Ndipo nilipopata majibu nyeti niliyoyatoa huko juuu yaliyokuvuta kuja na majibu yako, ya kutaka kuonyesha kuwa maneno yangu si sahihi, great, sasa hebu tumabie mkutano uliomuhusisha el mpaka kuambiwa na sendeka kuwa amekula rushwa ulifanyika wapi? au tumuulize Zitto? Na el alipokuwa anamuita Mengi masaa ya usiku mara mbili nayo tumuulize Zitto kama ilikuwa ni Karimjeee?

Je Mbunge Zitto alihudhuria vikao vyote vya hiii kesi au alifahamishwa kila wakati vinafanyika wapi? Je ulishawahi kuona posting yangu huko nyuma kabisaaa hata kabla hii kasheshe haijaanza ambapo nilisema kuwa siku moja Malima, Dau (NSSF), na Kingunge walionekana masaa ya usiku kwenye viwanja vya bunge, unafikri walionekana Karimjeee?

Ukweli ni kwamba kuna mikutano ilifanyika Dodoma na kuna iliyofanyika Dar, lakini critical kama ya kuonyeshwa mikanda ilifanyika Dodoma kwa hiyo huo ufafanuzi wako ni mzuri lakini sio sahihi, Zitto hahusiki na vikao vya hiyo kamati, ndio maana niliposema ile nyeti ya kutaka kumhusisha Mengi na kesi ya treason endapo angeshindwa hii kesi, hata Zitto aliiijua kwangu kwa hiyo Mbunge Zitto tusianze kumuhusiha na asiyohusika nayo, halafu kwa taarifa yako ninazo nyeti nyingi za hii kesi kuliko ninazozitoa ila ninakuwa careful maana mimi sio mgeni na siasa bongo, ninajua what time is? The matter of fact hata maoni ya wabunge wawili ninayo pia, wananchi hapa tunataka kuijadili hii kesi kwa undani na kujua shillingi millioni mia zimetumikaje, huu mjadala is not about me Mzee Es!

Kwakumaliza ni kwamba ninaona unajaribu sana kuigeuza hii ishu kuwa personal on me, ila hiyo nafasi sitakupa maana at this point ninazo nyeti nyingi ya hii ishu na ukweli wa ishu, kwanza ulikuwa unajaribu kuifanya ni ishu ya mimi kukataa kuhusu Spika alichoikabidhi pcb, sasa umegeuka kuwa sikukubali kuwa Spika amevurunda, NONESENSE, vikao vilikofanyika au kutofanyika I could careless, ila ninajua kuwa Ndesamburo ana tepu ambazo zina kila kitu kama nilivyosema huko nyuma, ndio maana mpaka leo hajaguswa na sheria na ndio maana alim-convince Spika kuipeleka hii kesi pcb,

Kwahiyo wewe ni kuchangia tu what you know kuhusu hii kesi, lakini kujaribu kunirukia mimi haitakusaidia maana nitaendela kumwaga ukweli au nyeti, sitaogopa kitu wala mtu hapa na siajawahi hata siku moja kumuogopa mtu hapa, kama unamtetea Malima, then ulipaswa kumuwambia mapema kabla hajajiiingiza kwenye hii kesi kuwa asingeweza kufika popote na hii kesi, na sasa he is in big trouble, maana mtu yoyote anyeijua kamati kuu ya ccm, anajua the last thign unataka ni kamati hiyo kukaa chini na kuongelea ishu kama hii, amuulize Idd Simba, Mbilinyi na mzee Salmin alipotaka kuongeza muda kule visiwani, what happened?

Hiii ishu ni kubwa na very educating kuliko kunendelea kunihusisha mimi na kutaka kuigeuza kuwa upinzani kati yangu na wewe, ndio maana ninasema tunasubiri kitabu cha Ndesamburo, ambacho tayari Spika anakipiga vita sana kisitolewe, lakini tutakipata tuu hata akikisitisha!

Mzee MMJ,

Hizo nyeti ni nyeti mno kuzipenyeza bro, kumbuka kuwa sasa hivi anatafutwa mchawi you do not want to be the one, yaani mchawi!

Ahsante kwa ufafanuzi ila nyeti za ishu ni kubwa kuliko huo ufafanuzi!
 
Mzee ES... I would love to be "mwenye ungo".. nyie nipenyesheeni tu.. I can take care of the rest...
 
Tatizo Mzee Es unapenda kujifanya wewe ni shushu namba moja matokeo yake unaharibu.

Masatu amekuuliza Swali zuri sana ambalo ukweli ni kuwa linaonyesha kuwa ingawa unajitahidi sana kupata habari hata kama kijiografia upo mbali na jikoni tabia ya kutaka kuonyesha unajua mengi ina kuingiza matatizoni. Jibu swali hivyo vitu vya kurekodi vipo katika Kumbi za Ofisi za Bunge Dar Es Salaam. Na nani kakuambia kuwa vikao vilifanyika Karimjee?

Taratibu kaka, you have a long way to go.......hatupendi kazi ya kukurithisha Uchifu kule nanihii ikawa ngumu zaidi ya hali inavyo onyesha sasa.

Samahani kaka naweza kuwa mdogo kwako lakini kwa kuwa nina kuthamini sina budi kukueleza mapungufu yako.

Tanzanianjema
 
Hivi ndugu yangu Mzee Es unajua ukaribu wa Dr Dau na Adam Malima? Unadhani kuonekana kwa Dr Dau, Malima na Mzee wa Mjini Kingunge ni kitu cha ajabu kiasi cha kuanzan kujenga conspiracies.

Dr Dau kuwepo bungeni ilikuwa ni wajibu wake kama Mkurugenzi wa NSSF wakati wa bajeti ya Wizara mama yake....na ndivyo ilivyokuwa

Tanzanianjema
 
Kama Adam Kigoma Malima anaharibu, kitu ambacho nakubaliana nacho asilimia mia moja ni wazi kuna umuhimu wa kuangalia kwa umakini suala zima la urithishaji nguvu za kisiasa (reduplication of elite) katika nchi yetu.

Ama unaesemaje Mzee ES?
 
Masatu, Mzee Es na Tanzanianjema,

Vikao vyote vya kamati ya kinga, haki na madaraka ya Bunge vilifanyika Dar ukumbi unaoitwa Speaker's room ambao upo equiped na technolojia ya kunasa sauti. Baadhi ya vikao vilifanyika pia Dodoma.

Ofisi za Bunge Dar es Salaam ni kamati nne tu ndio hufanya vikao vikao vyake katika kumbi zenye teknolojia ya sauti. Kamati ya fedha, kamati ya ulinzi na usalama, kamati ya hesabu za serikali na kamati ya hesabu za serikali za mitaa.
Vile vile Spika ana ukumbi maalumu unaopakana na ukumbi wa kamati ya fedha unaoitwa Adam Sapi Mkwawa. Katika ukumbi huu wa Spika ndipo kamati ambazo si za kisekta kama kamati ya kanuni na kamati ya haki,kinga na madaraka ya bunge hukutana. Juzi kamati ya ulinzi na usalama ilikutana hapa pia wakati ikimhoji IGP na DIS kuhusu hali ya usalama nchini.

Hivyo, inawezekana kabisa Mzee Es akawa sahihi katika maelezo yake.

Ninachojua mimi ni kwamba Mzee Ndesa ana tepu ambayo ina sauti ya EL akimwambia Mengi afute kesi kwani Manji kahonga sana wabunge. Hiyo ipo na nimewahi kuisikia mwenyewe. Naamini Ndesa ameitoa katika mahojiano yake kule PCB ambayo tayari yamefanyika.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom