Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Masatu, Mzee Es na Tanzanianjema,
..................
Ninachojua mimi ni kwamba Mzee Ndesa ana tepu ambayo ina sauti ya EL akimwambia Mengi afute kesi kwani Manji kahonga sana wabunge. Hiyo ipo na nimewahi kuisikia mwenyewe. Naamini Ndesa ameitoa katika mahojiano yake kule PCB ambayo tayari yamefanyika.
Huu ni mkwara ya kitoto. Kumbuka mtu mzima hatishiwi nyau! who r the so called seniors? is that u? u can be senior kwa mkeo na watoto wako sio hapa.
Taarifa maalum kuwasilishwa bungeni
NA MWANDISHI WETU
KITENDO cha Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, mkoani Pwani, Adam Malima kuwasilisha malalamiko yake dhidi ya Spika Samuel Sitta, katika Chama Cha Mapinduzi kimedaiwa ni udhalilishaji wa Bunge na utovu wa nidhamu.
Kwa mujibu wa habari ambazo gazeti hili imezipata, huenda katika mkutano wa Bunge unaoanza mjini Dodoma leo, katika moja ya vikao vyake kutawasilishwa taarifa maalum inayoainisha ni kwa namna gani Malima amelidhalilisha Bunge na kuvunja uhuru wa chombo hicho kwa kumshitaki Spika Sitta kwenye Chama chake cha siasa.
Sitta na Malima wote ni wabunge wa kuchaguliwa kupitia Chama Cha Mapinduzi. Spika ni Mbunge wa Urambo Mashariki mkoani Tabora.
Februari 8, mwaka huu katika kikao cha Bunge, Spika Sitta akitoa uamuzi wa sakata la Malima na Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi alisema hakukuwa na mshindi kati yao.
Katika hitimisho la uamuzi huo, alisema atatafuta muda muafaka awakutanishe kwa ajili ya kutafuta suluhu miongoni mwao, lakini Malima hakukubali na kuandika barua aliyoiwasilisha kwa Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba akilalamikia uamuzi huo wa Spika kuwa haukumtendea haki.
Chanzo chetu cha habari kinaeleza kwamba, Mbunge Malima alikuwa na haki ya kupinga au kukataa uamuzi huo wa Spika, lakini kwa kufuata kanuni za Bunge.
"...endapo mbunge yeyote hataridhika na uamuzi wa Spika, anaweza kuwasilisha sababu za kutoridhika kwa mwenyekiti wa kamati ya kanuni za Bunge ambayo itatakiwa ikae mara moja kufikiria na kutoa uamuzi wake kwa spika juu ya jambo hilo, na spika atalijulisha Bunge uamuzi huo uliotolewa.
"Isipokuwa spika hatakuwa mwenyekiti wa kamati ya kanuni za bunge wakati inapojadili jambo linalomuhusu," kilifafanua chanzo hicho.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, inadaiwa kwa makusudi Mbunge Malima anajaribu kupotosha suala hilo kwa kulipekeleka katika Chama, hatua ambayo ni kinyume cha sheria na utaratibu uliowekwa na kanuni za Bunge.
Imedaiwa kwamba barua ya malalamiko ya Malima si kukata rufani dhidi ya uamuzi wa Spika, bali ni kuhoji uamuzi huo na kuonyesha msisitizo amekataa kutii na kutekeleza maelekezo ya Spika, kitendo ambacho ni kosa la utovu wa nidhamu.
"Kitendo cha kupinga uamuzi wa Spika ni kitendo ambacho kinakwenda kinyume cha misingi ya uhuru wa Bunge na uhuru wa spika, katika kutoa uamuzi kuhusu utaratibu wa masuala ya bunge, na pia ni kitendo cha kulidhalilisha bunge kama chombo cha uwakilishi wa wananchi; wanachama na wasio wanachama wa chama chochote," kilifafanua chanzo hicho.
Kitendo hicho cha Malima pia kimedaiwa ni cha uvunjaji wa Katiba, kwa sababu kinavunja uhuru wa utaratibu katika Bunge, ambao kwa mujibu wa Katiba, haupaswi kuvunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika mahakama au mahali pengine nje ya Bunge.
"Spika wa Bunge anapaswa kuwa huru katika kutekeleza majukumu na mamlaka yake; anapaswa awe huru katika kutoa maamuzi yake kuhusu utaratibu bungeni. Katika kutekeleza majukumu yake, spika hapaswi kuwekewa shinikizo za kisiasa...
"Spika anapotoa uamuzi au mwongozo, hafanyi hivyo kwa kuzingatia itikadi ya chama chochote cha siasa, na wala haongozwi na mashinikizo ya kisiasa...
"Ni kinyume kabisa cha utaratibu wa uendeshaji wa masuala ya bunge, na pia ni uvunjaji wa katiba, kwa uamuzi, mwongozo au maelekezo yanayotolewa na spika au wenyeviti wa bunge kuhusu masuala ya utaratibu bungeni, kupingwa au kukatiwa rufani kupitia vyama vyao vya siasa," kilifafanua chanzo hicho cha habari.
Chanzo hicho kilisema ni dhahiri kwamba, tafsiri ya masuala ya utaratibu bungeni haiwezi kufanywa au kuamuliwa na kamati ya chama cha siasa.
"Kamati ya chama cha siasa itafikiaje maamuzi kuhusu masuala kama hayo, kwa mamalalamiko tu bila ya kuwa na ushahidi unaotokana na mwendendo mzima wa suala husika?" kilihoji chanzo hicho cha habari.
Chanzo hicho kilihoji kuwa katika Bunge lenye wabunge wanaotokana na vyama mbalimbali na spika akitoka katika chama kimojawapo, je mbunge ambaye spika hatoki kwenye chama chake, iwapo hataridhika na uamuzi, mwongozo au maelekezo ya spika atapeleka wapi malalamiko yake.
Hata hivyo, Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akitoa ufafanuzi kufuatia kauli za baadhi ya vyombo vya habari kulikuza jambo hilo kwamba sasa ni mgogoro ndani ya CCM, alisema Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM itajadili malalamiko ya Malima hivi karibuni.
Makamba alisema Malima na Sitta wote ni wabunge wa CCM na masuala yao yanaweza kujadiliwa kwa dhati ndani ya vikao vya CCM.
Alisema Malima alichofanya ni kutafuta msaada ndani ya Chama na kwa kufanya hivyo mtu wa kumkimbilia ni Katibu Mkuu, ambaye ndiye anayepanga ajenda za vikao vya Chama ili aone suala hilo alipeleke kikao gani cha Chama.
Kama Adam Kigoma Malima anaharibu, kitu ambacho nakubaliana nacho asilimia mia moja ni wazi kuna umuhimu wa kuangalia kwa umakini suala zima la urithishaji nguvu za kisiasa (reduplication of elite) katika nchi yetu.
Ama unaesemaje Mzee ES?
Naomba mchango hapa!!!
Tanzanianjema
Mzee Ole,
Mzee Tanzania njema, pharmacy na siasa haviwezi kuchanganywa pamoja halafu siwezi kuongea siasa na mtu wa aina yako maana hata Karimjee Hall hujui kuwa ndio majengo ya bunge la zamani Dar, sasa tutaongea nini? Nashangaa na hizo obsession zako na mwenzako na jina langu vipi mna shida gani?
Inaonekana una matatizo sana watoto wa viongozi, mzee hao ni binadamu kama wewe tu usiwe inferior kwao na kuwaona kuwa sio binadamu, wakiamua kuwa viongozi ni haki yao uongozi sio lazima uwe umetoka kwenye familia ya masikini, hayo tulishayapita siku nyingi!
Ahsante!