Barua ya Adam Malima kumpinga Spika!

Barua ya Adam Malima kumpinga Spika!

Status
Not open for further replies.
Tanzanianjema partly wrote to ES..........

"...............Na nani kakuambia kuwa vikao vilifanyika Karimjee?...."

Ndugu yangu Tanzanianjema kama jambo hulijui ni bora ukae kimya.

ni ushauri tu
 
Masatu, Mzee Es na Tanzanianjema,

..................
Ninachojua mimi ni kwamba Mzee Ndesa ana tepu ambayo ina sauti ya EL akimwambia Mengi afute kesi kwani Manji kahonga sana wabunge. Hiyo ipo na nimewahi kuisikia mwenyewe. Naamini Ndesa ameitoa katika mahojiano yake kule PCB ambayo tayari yamefanyika.

Hapa kuna utamu kweli kweli. Masikio yangu yako katika form nzuri sana kusikia maamuzi ya awamu ya nne kuhusiana na hili.
 
Mzee ES

Shukran kwa maelezo yako murua

Quote from ES

(1). Ni kwanini Ndesamburo, alijitoa kwenye kamati na hata kuweza kuwashutumu wabunge wa ccm kuwa wamekula ruhswa, tena hadharani bila ya kuogopa? Na kwanini kama hana ukweli mpaka leo hajakamatwa, maana can you imagine kuwashutumu wabunge wa ccm na tuhuma nzito namna hiyo bila kukamatwa? END

Ndesamburo hajakamatwa kwa sababu pamoja kuwa Tanzania demokrasia yetu bado changa, taratibu lazima zifuatwe. Spika ameshachukua hatua za kupeleka kesi ya madai ya rushwa ya Mzee Ndesa PCB na wanayafanyia kazi. Majibu kutoka PCB ndiyo yatakayo determine hatua ya kuchukua dhidi ya Mzee Ndesa. Katika mambo haya watu huwa hawakurupuki tu na kukamata watu ovyo.

Quote from ES
(2). Swali langu la pili kwao ilikuwa ni kwanini Spika naye alikubali kui-refer hiii kesi kwa pcb? Na ni kwa nini mpaka leo wabunge wanaotuhumiwa kula rushwa hawajasema kitu kujibu tuhuma hizo? Kamati ilimuona Malima hana kosa, sasa ikawaje Malima tena anaenda ccm kulia? END

Spika alipeleka kesi hii PCB kwa sababu ndio chombo rasmi cha kiserikali cha kushughulikia rushwa. Ama kuhusu wabunge wanaotuhumiwa kula rushwa kwanini hawajasema chochote, hapa kuna utata kwanza mpaka sasa Mzee Ndesa mwenyewe amejichinganya mwanzo alisema kamati ndio imehongwa na baadae akasema Bunge lote limehongwa! Sasa Mzee ES unaposema wabunge "watuhumiwa" hapa sijui una maanisha wepi? Hata hivyo nadhani wabunge/kamati wameona wasubiri waitwe na PCB huko ndio wakaseme ukweli ulivyo.

Hili la kama kamati ilimuona Malima hana hatia kwanini aliende "kulia" CCM, jibu ni kuwa pamoja na kamati kumuona hana hatia, Spika amemtia hatiani na ndio maana amepeleka "kilio" chake cha Spika CCM na sio "kilio" chake kwa Kamati.

Quote from ESNdipo nilipopata majibu nyeti niliyoyatoa huko juuu yaliyokuvuta kuja na majibu yako, ya kutaka kuonyesha kuwa maneno yangu si sahihi, great, sasa hebu tumabie mkutano uliomuhusisha el mpaka kuambiwa na sendeka kuwa amekula rushwa ulifanyika wapi? au tumuulize Zitto? Na el alipokuwa anamuita Mengi masaa ya usiku mara mbili nayo tumuulize Zitto kama ilikuwa ni Karimjeee? END

Kwa kadiri nijuavyo EL sio mjumbe wa kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge, kwa maana hiyo huo mkutano wake na Sendeka kwenye mjadala huu hauna nafasi labda walikutana "just for a cup of tea" same aplies for "mkutano" wa masaa ya usiku mara mbili baina Mengi na EL.

Quote: from ES
Je Mbunge Zitto alihudhuria vikao vyote vya hiii kesi au alifahamishwa kila wakati vinafanyika wapi? Je ulishawahi kuona posting yangu huko nyuma kabisaaa hata kabla hii kasheshe haijaanza ambapo nilisema kuwa siku moja Malima, Dua (NSSF), na Kingunge walionekana masaa ya usiku kwenye viwanja vya bunge, unafikri walionekana Karimjeee? END

Nilimuingiza Mh Zitto hapo ili apate kusaidia ufahamu wake kuhusu suala hili. Na posting yake nadhani umeiona. Hilo la Dau, Malima na Kingunge kukutana Karimjee sina elimu nalo pengine ndio ktk "for just a cup of tea"

Quote: from ES
Ukweli ni kwamba kuna mikutano ilifanyika Dodoma na kuna iliyofanyika Dar, lakini critical kama ya kuonyeshwa mikanda ilifanyika Dodoma kwa hiyo huo ufafanuzi wako ni mzuri lakini sio sahihi, Zitto hahusiki na vikao vya hiyo kamati, ndio maana niliposema ile nyeti ya kutaka kumhusisha Mengi na kesi ya treason endapo angeshindwa hii kesi, hata Zitto aliiijua kwangu kwa hiyo Mbunge Zitto tusianze kumuhusiha na asiyohusika nayo, halafu kwa taarifa yako ninazo nyeti nyingi za hii kesi kuliko ninazozitoa ila ninakuwa careful maana mimi sio mgeni na siasa bongo, ninajua what time is? The matter of fact hata maoni ya wabunge wawili ninayo pia, wananchi hapa tunataka kuijadili hii kesi kwa undani na kujua shillingi millioni mia zimetumikaje, huu mjadala is not about me Mzee Es! END

Bado nasisitiza kuwa mikutano ya Kamati ilifanyika ofisi za Bunge Dar Es Salaam na katika hili naomba pia kumuuliza Mh Zitto anaposema mikutano ilifanyika Dar Es Salaam katika Speaker' s room. Je hiyo speaker' s room si ipo katika ofisi za Bunge Dar Es Saam? hivyo kauli yangu ya awali ina stand tall.. Ushahidi ktk hili ni huu:


Team quizzes committee interrogates Malima, Mengi
KILASA MTAMBALIKE
Daily News; Thursday,September 07, 2006 @00:05
THE Mkuranga MP (CCM), Mr Adam Malima and the IPP Executive Chairman, Mr Reginald Mengi, yesterday took oaths before the Parliamentary Privileges, Ethics and Powers Committee at the Parliament offices in Dar es Salaam.
The two have lodged complaints against one another and the committee is meeting for three weeks to work on their complaints.
Reliable sources said the duo spent less than an hour before the committee where they were also debriefed on the conduct of the proceedings.
Mr Mengi was the first to arrive at the Parliament offices yesterday almost ten minutes before 3pm. Carrying heavy dossiers, Mr Mengi was accompanied by his lawyer.
Mr Malima arrived at the Parliament offices a few minutes before 3pm.
Mr Mengi has complained about the debate in the National Assembly during the budget session that ended in Dodoma last month over prioritisation of stories in prime time news bulletins by some media houses.
He has protested that Mr Malima was unfair to his company when debating the Ministry of Information, Culture and Sports budget estimates.
Mr Malima sought the Speaker's guidance following Mr Mengi's decision to refute what was said in the House in paid up advertisements.

He felt Mr Mengi had been unjust to him. End

Swali kwa Mh Zitto Speaker's room haipo ktk parliament office Dar?

Mzee ES,

Unaposema unazo nyeti nyingi kuliko unazozitoa na unakuwa careful kwa sababu unajua siasa za bongo, huu ni mkwara wa kitoto! if ur MAN ENOUGH mwaga hizo nyeti if u cant it is as good huna hizo the so called nyeti.
chukua hii challenge ya Mwanakijiji hapa;

Quote: from Mwanakijiji
Mzee ES... I would love to be "mwenye ungo".. nyie nipenyesheeni tu.. I can take care of the rest...End
__________________
Hoja Hujibiwa kwa Hoja!

Kama wewe unaogopa Mwanakijiji kajitolea kumfunga "paka kengele" mpenyeshee basi. Acha mikwara ya kizamani!.

Quote:: from ES
Kwakumaliza ni kwamba ninaona unajaribu sana kuigeuza hii ishu kuwa personal on me, ila hiyo nafasi sitakupa maana at this point ninazo nyeti nyingi ya hii ishu na ukweli wa ishu, kwanza ulikuwa unajaribu kuifanya ni ishu ya mimi kukataa kuhusu Spika alichoikabidhi pcb, sasa umegeuka kuwa sikukubali kuwa Spika amevurunda, NONESENSE, vikao vilikofanyika au kutofanyika I could careless, ila ninajua kuwa Ndesamburo ana tepu ambazo zina kila kitu kama nilivyosema huko nyuma, ndio maana mpaka leo hajaguswa na sheria na ndio maana alim-convince Spika kuipeleka hii kesi pcb,End

Mimi sijaifanya hii ishu ni personal on u on contrary u have made this issue personal on ur own! Kila wakati unatisha watu eti nina nyeti mara nimeongea na wabunge mwaga vitu ooh nazijua politics za Bongo, Mwanakijiji anakwambia mpe yeye hiyo tenda he will take care the rest!

Kuhusu alichopeleka spika PCB kila mtu anajua ni madai ya Rushwa ya Mzee Ndesa, asiejua hivyo katika forum hii ni wewe tu mwenye "nyeti" na unazikalia!

Spika kuvurunda the same, amevurunda na hata wewe mwenyewe umekubali hapa.

Hili la Mzee Ndesa kuwa na tape tunaomba ushahidi. Mh Zitto kasema tepu alioisikia yeye ni mazungumzo baina EL na Ndesa. Na cha kushangaza Mzee Ndesa huyo huyo amemwambia Spika kaambiwa na Mengi ambaye ndie alieongea na EL kuhusu rushwa. Hapa inaonekana Mzee Ndesa ni muongo na kigeugeu ndio maana madai yake ya rushwa yanaonekana ni uwongo alio uzua mwenyewe.


Quote: From ES

Kwahiyo wewe ni kuchangia tu what you know kuhusu hii kesi, lakini kujaribu kunirukia mimi haitakusaidia maana nitaendela kumwaga ukweli au nyeti, sitaogopa kitu wala mtu hapa na siajawahi hata siku moja kumuogopa mtu hapa, kama unamtetea Malima, then ulipaswa kumuwambia mapema kabla hajajiiingiza kwenye hii kesi kuwa asingeweza kufika popote na hii kesi, na sasa he is in big trouble, maana mtu yoyote anyeijua kamati kuu ya ccm, anajua the last thign unataka ni kamati hiyo kukaa chini na kuongelea ishu kama hii, amuulize Idd Simba, Mbilinyi na mzee Salmin alipotaka kuongeza muda kule visiwani, what happened? End

Yes, mimi nachangia kama wanavyochangia wengine ukiwemo wewe. Hii kwamba nakurukia wewe, sina tatizo lolote na wewe, sikujua hunijui tumekutana humu basi. Kama ambavyo humuogopi mtu nami vivyo hivyo simuogopi mtu.

Simtetei Malima natetea ukweli na haki na napinga dhulma, uongo na uonevu. If he is in trouble it has nothing to do with me!

Quote: from ES
Hiii ishu ni kubwa na very educating kuliko kunendelea kunihusisha mimi na kutaka kuigeuza kuwa upinzani kati yangu na wewe, ndio maana ninasema tunasubiri kitabu cha Ndesamburo, ambacho tayari Spika anakipiga vita sana kisitolewe, lakini tutakipata tuu hata akikisitisha! END

Sina sababu ya kuweka upinzani na wewe. Kitabu cha Ndesa ni chake mwenyewe all the best! amesha prove ni kigeu geu na muongo what should we expect from that "book"?

Quote: from ES
Hizo nyeti ni nyeti mno kuzipenyeza bro, kumbuka kuwa sasa hivi anatafutwa mchawi you do not want to be the one, yaani mchawi! END

Kishakwambia "he will take care the rest" jibu hapa HUNA hizo nyeti mkwara mbuzi tu!

Mungu Ibariki Tanzania
 
Masatu/Tanzania njema,

Sina muda wa kuwapotezea wanachi hapa na maneno mengi wakati point ni chache, cha msingi kwenye post yako ya majibu iliyopita ulidai mikutano ilifanyika Dar na kama ninabisha aulizwe Mbunge Zitto,

(1). Mbunge Zitto ametoa majibu kama nilivyosema kuwa vikao vilifanyika Dar na Dodoma, na kama nilivyoambiwa na wajumbe wawili wa kamati hiyo, the matter of fact siku ya ku-present videos au tepu, Mengi aliendesha mwenyewe gari lake mpaka Dodoma, kwa maneno ya mjumbe mmoja wa kamati hiyo, hii ndo the main point ya majibu yako na majibu yangu na majibu ya mbunge Zitto,

(2). Nilisema Ndesamburo ana tepu, na Mbunge Zitto uliyetaka aulizwe amekuhakikishia kuwa kuna ambazo amezisikia mwenyewe kwa masikio yake, sasa what else do you want kama sio kuwapotezea wananchi muda wao na kushusha heshima ya hii forum na credibility yake?


(3). Kumpa nyeti Mzee MMJ, huo ni uamuzi wangu sio wako period! The matter of fact sitampa ili nione what can you do!

Mzee naona ndio kwanza unaanza kuirukia forum, sasa kaa chonjo mana you ain' seen anything yet na ninaikaribisha challenge yako kwa mikono miwili ili ujifunze kama wengine kabla yako, ninaona sehemu nyingi za majadiliano unajaribu kuwa kiranja wa kuwaambia seniors what to say, hapana mimi ni mtu huru na hutoa vitu vyangu on my pace and my time tena vya uhakika, Mbunge wa taifa uliyetaka aulizwe amekujibu very clear kuwa kila nililosema ni kweli, sasa ni aibu mtu mzima kuendelea ku-create none ishu wakati ishu zimejibiwa tayari, kwa hiyo samahani mzee wangu, mimi sio shushu mimi ni mwana-forum wa long time hapa dedicated kuelimishwa na kuwaelimisha wanachi na siku zote nina uwezo wa kufikia sehemu za siasa ya bongo ambazo hazifikiki na kuwaletea wananchi wachambue pumba na mchele uko wapi, umaarufu kwenye forum huletwa na kukata ishu sio kurukia senor members na kutaka kuwaambia what to say and what not to say,

Uanaume wangu hauwezi kupimwa na nyeti za siasa, mana inaonekana wako hupimwa na how much you know kuhusu nyeti za siasa za bongo, ambazo ukweli ni kuwa huna sasa kaa pembeni upewe!

Kama una nyeti zitoe, kama huna kaa pembeni ule data hapa! na usivuruge mjadala wa wananchi! maana umesema aulizwe Mbunge Zitto, sasa tena unataka hata kumsuta mbunge huyo huyo, halafu unajaribu hata kumkashifu the hero wa kesi Mbunge Ndesamburo, what is your point?

Wewe ni kutulia pembeni ule data, kwa tarifa ni kwamba ukumbi wa bunge Dar kwa jina lingine huitwa Karimjee Hall!

Posting: 1,367 - 80 = 1,287 Long way to go!

Ahsante!
 
Masatu ni mchangiaji mzuri tu; tena mchambua hoja wa nguvu.
Mzee Es yeye ni mtu wa nyeti nyingi.
The point of contention hapa ni hafifu sana and not worth the waste of effort.
Wote wanatoa michango mhimu JF.
 
Mzee ES,

Shukran kwa majibu yako.Naona umekuwa mkali kidogo ktk majibu yako, hata hivyo ndio kawaida mjadala unapopamba moto jazba za hapa na pale hazikosekani I dont blame u.

Quote: from ES

1). Mbunge Zitto ametoa majibu kama nilivyosema kuwa vikao vilifanyika Dar na Dodoma, na kama nilivyoambiwa na wajumbe wawili wa kamati hiyo, the matter of fact siku ya ku-present videos au tepu, Mengi aliendesha mwenyewe gari lake mpaka Dodoma, kwa maneno ya mjumbe mmoja wa kamati hiyo, hii ndo the main point ya majibu yako na majibu yangu na majibu ya mbunge Zitto, End

Vikao kufanyika ofisi za Bunge Dar Es Salaam hili nimelitolea ushahidi, hata hivyo tuchukulie mfano vimefanyika Dodoma. Tujadili the subject matter. Madai yako ni kuwa vikao vilivyofanyika ndani ya ukumbi vimerekodiwa na tepu anayo Mzee Ndesa. Swali hapa wabunge wepi hao? wajumbe wa Kamati? na kama ndio hivyo, Mh Sendeka nae kala rushwa kwani ni Mbunge wa CCM pia! Kama ilikuwa ni informal meeting ya wabunge wa CCM ushahidi wa kimazingira unashawishi mtu kuamini si kweli, haiingii akilini watu wajadili mshiko ktk ofisi za bunge it is as if anaejua kuwa kuna vinasa sauti ni Ndesa tu? labda tu tukumbushane hapa ni akina nani wajumbe wa Kamati ya Haki, Kinga na maadili ya Bunge. Wafuatao wana form kamati hiyo:


1. Mh Juma N’hunga Seleiman – Mwenyekiti - CCM
2. Mh Wilson Mutagaywa Masilingi – Makamu wa Mwenyekiti - CCM
3. Mh William Mganga Ngeleja – Mjumbe - CCM
4. Mh Maneno Ramadhani Athumani – Mjumbe – CCM
5. Mh Haroub Masoud Said – Mjumbe - CCM
6. Mh Dr James Alex Nsekela – Mjumbe – CCM
7. Mh Christopher Ole Sendeka Olonyokie – Mjumbe – CCM
8. Mh Anna Margareth Abdallah - Mjumbe – CCM
9. Mh Tatu Mussa Ntimizi – Mjumbe – CCM
10. .Mh Dr Lucy Nkya Saware – Mjumbe – CCM
11. Mh Fatma Mussa Maghimbi – Mjumbe – CUF
12. Mh Philemon Ndsesamburo – Mjumbe – CHADEMA
13. Mh Anne Kilango Malecela – Mjumbe – CCM
14. Mh Juma Hassan Kilimbah – Mjumbe – CCM
15. Mh Athumani Said Janguo – Mjumbe - CCM

Humo yumo Waziri wa zamani ofisi ya Rais (Utawala bora ), naibu waziri, mkuu wa Mkoa, mkuu wa wilaya na mwenyekiti jumuiya wa wanawake nk.

Hivi hawa hata kama ni kweli wamechukua rushwa basi ndio "wajadiliane" kuhusu hiyo rushwa katika kumbi za Bunge? Hivi hawa hawajui kuwa kuna vinasa sauti humo?. Mtafute wa kumwambia huo uwongo wako.

Quote: from ES(2). Nilisema Ndesamburo ana tepu, na Mbunge Zitto uliyetaka aulizwe amekuhakikishia kuwa kuna ambazo amezisikia mwenyewe kwa masikio yake, sasa what else do you want kama sio kuwapotezea wananchi muda wao na kushusha heshima ya hii forum na credibility yake? END

Hiyo habari hapo juu ni maarufu, hakuna jipya hapo madai ya Mh Ndesa kuhusu mazungumzo ya EL na Mengi ni ya siku nyingi, hivyo kuwepo kwa tepu sio jambo jipya. Tunachotaka hapa ni tepu ulizosema Mzee Ndesa anazo za "kikao cha siri" cha wabunge wa CCM kuhusu wao kupewa rushwa. Kama kuna kuwapotezea watu muda ni huku unakukofanya wewe unatoa madai halafu washindwa kuyathibitisha.


Quote: from ES
3). Kumpa nyeti Mzee MMJ, huo ni uamuzi wangu sio wako period! The matter of fact sitampa ili nione what can you do! END

The fact hapa ni kuwa HUNA hizo unazoziita nyeti bila vitisho tu! Nitakacho kifanya hapa ni kukuona mzushi na muongo basi.

Quote: from ES
Mzee naona ndio kwanza unaanza kuirukia forum, sasa kaa chonjo mana you ain' seen anything yet na ninaikaribisha challenge yako kwa mikono miwili ili ujifunze kama wengine kabla yako, ninaona sehemu nyingi za majadiliano unajaribu kuwa kiranja wa kuwaambia seniors what to say, hapana mimi ni mtu huru na hutoa vitu vyangu on my pace and my time tena vya uhakika, Mbunge wa taifa uliyetaka aulizwe amekujibu very clear kuwa kila nililosema ni kweli, sasa ni aibu mtu mzima kuendelea ku-create none ishu wakati ishu zimejibiwa tayari, kwa hiyo samahani mzee wangu, mimi sio shushu mimi ni mwana-forum wa long time hapa dedicated kuelimishwa na kuwaelimisha wanachi na siku zote nina uwezo wa kufikia sehemu za siasa ya bongo ambazo hazifikiki na kuwaletea wananchi wachambue pumba na mchele uko wapi, umaarufu kwenye forum huletwa na kukata ishu sio kurukia senor members na kutaka kuwaambia what to say and what not to say,END

Huu ni mkwara ya kitoto. Kumbuka mtu mzima hatishiwi nyau! who r the so called seniors? is that u? u can be senior kwa mkeo na watoto wako sio hapa.

Quote: from ESUanaume wangu hauwezi kupimwa na nyeti za siasa, mana inaonekana wako hupimwa na how much you know kuhusu nyeti za siasa za bongo, ambazo ukweli ni kuwa huna sasa kaa pembeni upewe! END

Wewe ulienazo hizo "nyeti" umesema hutoi ili uone mimi nitafanya nini! big joke! kwa hiyo wanikomoa sio!

Quote: from ES
Kama una nyeti zitoe, kama huna kaa pembeni ule data hapa! na usivuruge mjadala wa wananchi! maana umesema aulizwe Mbunge Zitto, sasa tena unataka hata kumsuta mbunge huyo huyo, halafu unajaribu hata kumkashifu the hero wa kesi Mbunge Ndesamburo, what is your point?

Wewe ni kutulia pembeni ule data, kwa tarifa ni kwamba ukumbi wa bunge Dar kwa jina lingine huitwa Karimjee Hall!

Posting: 1,367 - 80 = 1,287 Long way to go! END

Niliyonayo nimeyaweka hadharani msondo wameimba "mambo hadharani" nyeti zako wewe unazo mwenyewe na hutoi ili uone mimi nitafanyaje!

Mzee Ndesa hana u hero wowote zaidi ya kujichanganya mwenyewe.

Sijazungumzia "ukumbi wa bunge Dar" nimezungumzia ofisi za Bunge Dar, hivyo ni vitu viwili tofauti na vipo sehemu tofauti Dar. Ni wewe ulieshindwa kutofautisha na kuleta habari za Karimjee!

Hapa hatupimi umefanya posting ngapi? tunapima uzito wa hoja! unaweza ukawa na posting hata milioni "MR SENIOR" lakini kama mwendo wenyewe ndio huu, Im sorry 2 say its full load of rubbish..!

Kilwa jazz waliimba "Mtoto acha kupiga mayoweee wacha watu waone wenyeweee"

Umgu Ibariki Tanzania
 
Finally, kwa maneno yako mawili,

"2" na "Nyau" nimeshajua kuwa wewe ni yule yule jaamaa sasa umekuja na jina lingine. kwa hiyo nitaendelea na ishu za mjadala tu,

Suala la tepu kuwa maarufu huko uliko sielewi unasema nini, na kwa nini hukusema kabla sijasema kama ulikuwa unajua, nyeti nimeziweka kwenye post yangu very clear, hazipo forum yoyote wala gazeti lolote Tanzania, na nilifanya makusudi ili kukupa elimu kwa kupandisha gia, cha kujibu huna sasa unalilia logic tu, hayo tumeyazoea hapa forum, lakini always hakuna competition,

Mzee tulia pembeni ule data hapa, hiyo kufura kwa pweza ni mazoea hapa kwa wasiokuwa na data! waliojaribu kuleta full of rubbish walishabadili majina na wengine hawapo tena hapa , lakini walituacha hapa hapa!

Sasa hivi unachojaribu kufanya ni kuuharibu tu huu mjadla na logic zako against ukweli, "Nyeti", Mzee MMJ, anajua kuwa nyeti zikiwa haizna noma huwa ninmpenyezea zikiwa na noma NO,

mzee wangu ni vigumu jogooo la shamba kuwika mjini maana sasa unakutana na baba yao, hiyo Kilwa iliimbwa na Juma Mrisho, alipohamia Urafiki Jazz yaani "Chua Ngoma" alikutana sisi "Magoma Kita Kita" watoto wa Ilala Mchikichini yaani baba ya muziki mpaka leo tunaendelea, na Jogooo la shamba Mzee Gurumo, baba ya muziki! Jogooo la shamba Mzee Kilwa Juma Mrisho alishaacha muziki siku nyingi!

Umejaribu matusi umeshindwa kwa jina lingine, sasa again unajaribu hoja na nyeti umeshindwa, maneno yale yale ila majina tu unabdili, kweli wewe mkali ndugu yangu unachonitakia ni nini blaza? Hebu angalia nyuma utaona mahali ulipotumia hayo maneno yako ambayo huwa huwezi kuachana nayo

yaani: "2", "Mwendo Mdundo", "Nyau", "Bata"

unafikir kuna watoto wadogo humu kwenye forum? Ahadi yangu bado ni ile ile tukutane uso kwa uso tuyamalize badala ya kupotezea watu muda wao humu!
 
Masatu

Huu ni mkwara ya kitoto. Kumbuka mtu mzima hatishiwi nyau! who r the so called seniors? is that u? u can be senior kwa mkeo na watoto wako sio hapa.

This is uncalled for - Huna sababu ya kuandika hivi.
 
Mzee ES,

Shukran kwa majibu yako murua.

Quote: from ES

"2" na "Nyau" nimeshajua kuwa wewe ni yule yule jaamaa sasa umekuja na jina lingine. kwa hiyo nitaendelea na ishu za mjadala tu, END

Ni nani "yule" jaamaa? Nadhani sasa umechanganyikiwa na u r looking for way out.

Quote: from ES


Suala la tepu kuwa maarufu huko uliko sielewi unasema nini, na kwa nini hukusema kabla sijasema kama ulikuwa unajua, nyeti nimeziweka kwenye post yangu very clear, hazipo forum yoyote wala gazeti lolote Tanzania, na nilifanya makusudi ili kukupa elimu kwa kupandisha gia, cha kujibu huna sasa unalilia logic tu, hayo tumeyazoea hapa forum, lakini always hakuna competition, END

Nenda kasome tena nilichoandika kabla huja kurupuka na kuleta madai ya ajabu. nimesema hakuna jipya kuhusu madai ya Mh Ndesa ktk mazungumzo ya EL na Mengi. Unless hapa unataka tuamini ulijua madai ya rushwa ya Mzee Ndesa kabla ya yeye Ndesa hajasema kwenye vyombo vya habari. Nasisitiza hili si jambo jipya na kama ndio "nyeti" ulizokuwa unazificha ndio hizi si nyeti kitu zilishakuwa un-nyeti longtime ago!

Quote from ES
Sasa hivi unachojaribu kufanya ni kuuharibu tu huu mjadla na logic zako against ukweli, "Nyeti", Mzee MMJ, anajua kuwa nyeti zikiwa haizna noma huwa ninmpenyezea zikiwa na noma NO, END

Unae uharibu mjadala ni wewe unaesema una nyeti kumbe HUNA!

Quote: from ES
Umejaribu matusi umeshindwa kwa jina lingine, sasa again unajaribu hoja na nyeti umeshindwa, maneno yale yale ila majina tu unabdili, kweli wewe mkali ndugu yangu unachonitakia ni nini blaza? Hebu angalia nyuma utaona mahali ulipotumia hayo maneno yako ambayo huwa huwezi kuachana nayo END

Sijawahi kukutukana na sina sababu ya kufanya hivyo. Kama ambavyo sina sababu ya kubadili jina. Kama test yako ni misemo then u got it wrong kuna misemo common humu kwenye forum mfano kukata ishu nk kama kila ataesema hayo ni mtu mmoja then forum yote ni mtu mmoja bali majina ndio mbalimbali.

Quote: from ES
unafikir kuna watoto wadogo humu kwenye forum? Ahadi yangu bado ni ile ile tukutane uso kwa uso tuyamalize badala ya kupotezea watu muda wao humu! END

Tukutane mimi na wewe tuyamalize uso kwa uso? yepi hayo? sikujua kuwa tunapoteza muda humu ndani na heri tukutane uso kwa uso "tuyamalize" I think I have to contact PCB! sasa (joke)

Mungu Ibariki Tanzania
 
Niliandika kuhusu Jinamizi la Nidhamu ya Chama.... http://www.habaritanzania.com

Malima sasa adaiwa mtovu wa nidhamu
Taarifa maalum kuwasilishwa bungeni
NA MWANDISHI WETU

KITENDO cha Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, mkoani Pwani, Adam Malima kuwasilisha malalamiko yake dhidi ya Spika Samuel Sitta, katika Chama Cha Mapinduzi kimedaiwa ni udhalilishaji wa Bunge na utovu wa nidhamu.
Kwa mujibu wa habari ambazo gazeti hili imezipata, huenda katika mkutano wa Bunge unaoanza mjini Dodoma leo, katika moja ya vikao vyake kutawasilishwa taarifa maalum inayoainisha ni kwa namna gani Malima amelidhalilisha Bunge na kuvunja uhuru wa chombo hicho kwa kumshitaki Spika Sitta kwenye Chama chake cha siasa.

Sitta na Malima wote ni wabunge wa kuchaguliwa kupitia Chama Cha Mapinduzi. Spika ni Mbunge wa Urambo Mashariki mkoani Tabora.
Februari 8, mwaka huu katika kikao cha Bunge, Spika Sitta akitoa uamuzi wa sakata la Malima na Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi alisema hakukuwa na mshindi kati yao.
Katika hitimisho la uamuzi huo, alisema atatafuta muda muafaka awakutanishe kwa ajili ya kutafuta suluhu miongoni mwao, lakini Malima hakukubali na kuandika barua aliyoiwasilisha kwa Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba akilalamikia uamuzi huo wa Spika kuwa haukumtendea haki.

Chanzo chetu cha habari kinaeleza kwamba, Mbunge Malima alikuwa na haki ya kupinga au kukataa uamuzi huo wa Spika, lakini kwa kufuata kanuni za Bunge.
"...endapo mbunge yeyote hataridhika na uamuzi wa Spika, anaweza kuwasilisha sababu za kutoridhika kwa mwenyekiti wa kamati ya kanuni za Bunge ambayo itatakiwa ikae mara moja kufikiria na kutoa uamuzi wake kwa spika juu ya jambo hilo, na spika atalijulisha Bunge uamuzi huo uliotolewa.
"Isipokuwa spika hatakuwa mwenyekiti wa kamati ya kanuni za bunge wakati inapojadili jambo linalomuhusu," kilifafanua chanzo hicho.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, inadaiwa kwa makusudi Mbunge Malima anajaribu kupotosha suala hilo kwa kulipekeleka katika Chama, hatua ambayo ni kinyume cha sheria na utaratibu uliowekwa na kanuni za Bunge.
Imedaiwa kwamba barua ya malalamiko ya Malima si kukata rufani dhidi ya uamuzi wa Spika, bali ni kuhoji uamuzi huo na kuonyesha msisitizo amekataa kutii na kutekeleza maelekezo ya Spika, kitendo ambacho ni kosa la utovu wa nidhamu.

"Kitendo cha kupinga uamuzi wa Spika ni kitendo ambacho kinakwenda kinyume cha misingi ya uhuru wa Bunge na uhuru wa spika, katika kutoa uamuzi kuhusu utaratibu wa masuala ya bunge, na pia ni kitendo cha kulidhalilisha bunge kama chombo cha uwakilishi wa wananchi; wanachama na wasio wanachama wa chama chochote," kilifafanua chanzo hicho.
Kitendo hicho cha Malima pia kimedaiwa ni cha uvunjaji wa Katiba, kwa sababu kinavunja uhuru wa utaratibu katika Bunge, ambao kwa mujibu wa Katiba, haupaswi kuvunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika mahakama au mahali pengine nje ya Bunge.

"Spika wa Bunge anapaswa kuwa huru katika kutekeleza majukumu na mamlaka yake; anapaswa awe huru katika kutoa maamuzi yake kuhusu utaratibu bungeni. Katika kutekeleza majukumu yake, spika hapaswi kuwekewa shinikizo za kisiasa...
"Spika anapotoa uamuzi au mwongozo, hafanyi hivyo kwa kuzingatia itikadi ya chama chochote cha siasa, na wala haongozwi na mashinikizo ya kisiasa...
"Ni kinyume kabisa cha utaratibu wa uendeshaji wa masuala ya bunge, na pia ni uvunjaji wa katiba, kwa uamuzi, mwongozo au maelekezo yanayotolewa na spika au wenyeviti wa bunge kuhusu masuala ya utaratibu bungeni, kupingwa au kukatiwa rufani kupitia vyama vyao vya siasa," kilifafanua chanzo hicho cha habari.

Chanzo hicho kilisema ni dhahiri kwamba, tafsiri ya masuala ya utaratibu bungeni haiwezi kufanywa au kuamuliwa na kamati ya chama cha siasa.
"Kamati ya chama cha siasa itafikiaje maamuzi kuhusu masuala kama hayo, kwa mamalalamiko tu bila ya kuwa na ushahidi unaotokana na mwendendo mzima wa suala husika?" kilihoji chanzo hicho cha habari.

Chanzo hicho kilihoji kuwa katika Bunge lenye wabunge wanaotokana na vyama mbalimbali na spika akitoka katika chama kimojawapo, je mbunge ambaye spika hatoki kwenye chama chake, iwapo hataridhika na uamuzi, mwongozo au maelekezo ya spika atapeleka wapi malalamiko yake.
Hata hivyo, Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akitoa ufafanuzi kufuatia kauli za baadhi ya vyombo vya habari kulikuza jambo hilo kwamba sasa ni mgogoro ndani ya CCM, alisema Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM itajadili malalamiko ya Malima hivi karibuni.

Makamba alisema Malima na Sitta wote ni wabunge wa CCM na masuala yao yanaweza kujadiliwa kwa dhati ndani ya vikao vya CCM.
Alisema Malima alichofanya ni kutafuta msaada ndani ya Chama na kwa kufanya hivyo mtu wa kumkimbilia ni Katibu Mkuu, ambaye ndiye anayepanga ajenda za vikao vya Chama ili aone suala hilo alipeleke kikao gani cha Chama.
 
Makala iliyoandikwa Uhuru na kuletwa hapa na Mwanakijiji inaelekea kukubaliana na nilivyokuwa nikisema huko nyuma kuwa Malima alikiuka kanuni za bunge na ku-understimate madaraka ya spika. Vile vile makala hii inaelekea kukubaliana na mchangiaji mwingine aliyesema kuwa Malima kwenda kwa Makamba kulitokana zaidi na urafiki wao na alikuwa anatafuta kinga ya kiupendeleo, siyo kutafuta haki kwani hakuwa kanyimwa haki yoyote na spika kwa vile kuna utaratibu wa kutolea malalamiko yake bungeni kama anadhani kaonewa na spika.
 
Kama Adam Kigoma Malima anaharibu, kitu ambacho nakubaliana nacho asilimia mia moja ni wazi kuna umuhimu wa kuangalia kwa umakini suala zima la urithishaji nguvu za kisiasa (reduplication of elite) katika nchi yetu.

Ama unaesemaje Mzee ES?

Naomba mchango hapa!!!

Tanzanianjema
 
Naomba mchango hapa!!!

Tanzanianjema

Mchango wangu,

Tumpe nguvu Mtikila ili kuondoa ukiritimba wa kugombea kupitia vyama. Kamati kuu ambayo imejaa wakina nanihii ndiyo inayopitisha majina ya watu wa namna hii na kuwaengua wale wanaofaa.
 
Mzee Ole,

Na wenzako, hivi ni kwanini mnaruhusu huyu jaama anakuja kuiharibu hii forum wakati kule kwenye forum yake hafanyi hizi fujo anazoleta huku? Mzee nenda kwenye forum yako kule uendeleze hayo mabishano yako ya bila hoja,

Hapa inaonekana hupawezi bro maji ya shingo haya, huu mchezo tuliauanza siku nyingi ndugu yangu, mjini hupawezi hapa huu uwanja ni mpana mno rudi kule shambani kwenye forum yako, iliyobaki jina tu!

Mzee Tanzania njema, pharmacy na siasa haviwezi kuchanganywa pamoja halafu siwezi kuongea siasa na mtu wa aina yako maana hata Karimjee Hall hujui kuwa ndio majengo ya bunge la zamani Dar, sasa tutaongea nini? Nashangaa na hizo obsession zako na mwenzako na jina langu vipi mna shida gani?

Kule kwenye ile forum siwezi kurudi na hapa siwezi kutoka, kwa hiyo mnahitaji kusuka au kunyoa, mimi wembe ni ule ule tu siyumbishwi namtu hata siku moja, mzee huko nyuma umesema maneno mengi sana pamoja na kurekebishwa bado tuu hamsikii sasa nyie wawili muendelee na mjadala mimi nitajadili na wanaoelewa siasa ya bongo, lakini muda wa kupoteza na nyinyi na kuwapotezea wananchi wengine sina.

Isipokuwa nitaendelea na mjadala wa Spika, Malima, na Mengi, kama unataka mjadla wa Malima as a person kaanzishe thread yake, lakini huu mjadla ni tofauti na hayo unayoyataka, lakini kwa kifupi Malima ni Mtanzania kama wengine wote ana hakli ya kugombea nafasi yoyote nchini, halafu what is Malima tunapongelea taifa letu? Inaonekana una matatizo sana watoto wa viongozi, mzee hao ni binadamu kama wewe tu usiwe inferior kwao na kuwaona kuwa sio binadamu, wakiamua kuwa viongozi ni haki yao uongozi sio lazima uwe umetoka kwenye familia ya masikini, hayo tulishayapita siku nyingi!

Ahsante!
 
Mzee ES,

Shukran kwa ujumbe wako murua.


Quote: from ES
Na wenzako, hivi ni kwanini mnaruhusu huyu jaama anakuja kuiharibu hii forum wakati kule kwenye forum yake hafanyi hizi fujo anazoleta huku? Mzee nenda kwenye forum yako kule uendeleze hayo mabishano yako ya bila hoja, END

Jamaa gani huyo mzee wa "nyeti" hebu tupe kidogo au na hii pia huwezi kuitoa ili uone nitafanya nini?

Fujo gani anazoleta humu? na mabishano gani hayo bila hoja?


Quote: from ES

Hapa inaonekana hupawezi bro maji ya shingo haya, huu mchezo tuliauanza siku nyingi ndugu yangu, mjini hupawezi hapa huu uwanja ni mpana mno rudi kule shambani kwenye forum yako, iliyobaki jina tu! END

Mbona haya ni maji "kukuguba" au maji "kukutu" tu haya! mji upi na shamba ipi?


Quote: from ES
Kule kwenye ile forum siwezi kurudi na hapa siwezi kutoka, kwa hiyo mnahitaji kusuka au kunyoa, mimi wembe ni ule ule tu siyumbishwi namtu hata siku moja, mzee huko nyuma umesema maneno mengi sana pamoja na kurekebishwa bado tuu hamsikii sasa nyie wawili muendelee na mjadala mimi nitajadili na wanaoelewa siasa ya bongo, lakini muda wa kupoteza na nyinyi na kuwapotezea wananchi wengine sina. END

Forum ipi hiyo? hapa bado tunakuhitaji usitoke kwani hizo "nyeti" tutazipata wapi kama utaondoka? Pls usisusie mjadala utapunguza msisimko bado tunahitaji elimu yako ya "nyeti" tunajifunza mengi tu. Usimsusie shamba nguruwe atalimaliza!

Mzee ES hivi unanifananisha na nani? utapata taabu sana kutaka kunijua kama ambavyo sikujui wewe, usipoteze muda kutaka kunijua mimi. Tukate ishu au sio... mtu mzima hatishiwi nyau... hahaha!


Si unakumbuka kuwa una "tepu" za kikao cha siri cha wabunge wa CCM wakikiri kupokea rushwa ya Manji wakiwa katika "ukumbi wa bunge Dodoma" bado tunaisubiri.

Na pia una "nyeti" nyingine nyingi tu nazo twazisubiri.

Mr Senior mwaga vituz!

Mungu Ibariki Tanzania
 
Ndugu wanaforum, Hivi Mengi anaobligation ya aina yoyote ile kuwapa airtime viongozi wa serikali kama anavyohoji mheshimiwa Malima? naauliza kwa sababu all along nilijua IPPMEDIA ni PRIVATE conglomerate ya Mengi na shareholders wake, sikujua kamwe kama serikali ina ubia wowote mpaka kiongozi mwandamizi kama Malima alalamike bungeni! Kwa uelewa wangu mdogo I thought (rightly or wrongly) kwamba Mengi na vyombo vyake wana haki ya kubroadcast news kadri wanavyoona inafaa as long hawavunji sheria za nchi!

Sasa waungwana baada ya kufuatilia huu mjadala inaonekana Mengi (has implied legal duty to the governemnt) kwamba inabidi viongozi wa serikali wapewe nafasi katika TV na Redio! Naomba nieleweshwe..huu wajibu wa Mengi kwa Lowasa, JK et al...uko grounded katika sheria ipi? Maana kabla hatujaanza kuhukumu watu, kwanza tukate issue ya umiliki wa hivi vyomba na sheria zinazomlinda bwana Mengi. Hivi Bush au Nancy Pelosi wanaweza kulalamika kwamba hawapewi mda CNN or CBS? (Just saying...). Nashindwa kuelewa kabisa huu mjadala maana kitu kama ni private property ya mtu..sidhani kama kuna wajibu wa kuwapa hata dakika moja hawa wakubwa serikalini!! Nilijua mda wote kwamba Tido Mhando na crew yake ya TVT ndo yenye huo wajibu !!!

Please whoever can enlighten me on this...will appreciate... Au Mengi kabla hajapewa leseni ilikuwa mojawapo ya masharti kwamba inabidi atoe airtime ya kutosha kwa viongozi wa serikali..au serikali inalipia hiyo airtime...sielewi kabisa...Help....
 
Mikuki, hilo ndilo lilikuwa swali la Mhe. Malima kwa Waziri wa Habari!! ndio mwanzo wa kasheshe hili...!!
 
you know what..? we all forgot about the answers.. inabidi nirudie hansard the bunge..
 
Mzee Ole,

Mzee Tanzania njema, pharmacy na siasa haviwezi kuchanganywa pamoja halafu siwezi kuongea siasa na mtu wa aina yako maana hata Karimjee Hall hujui kuwa ndio majengo ya bunge la zamani Dar, sasa tutaongea nini? Nashangaa na hizo obsession zako na mwenzako na jina langu vipi mna shida gani?


Inaonekana una matatizo sana watoto wa viongozi, mzee hao ni binadamu kama wewe tu usiwe inferior kwao na kuwaona kuwa sio binadamu, wakiamua kuwa viongozi ni haki yao uongozi sio lazima uwe umetoka kwenye familia ya masikini, hayo tulishayapita siku nyingi!

Ahsante!

Mhhh,

Mzee ES, ughaibuni huwa mnasema NOTHING PERSONAL na ndivyo nionavyo.

Siasa kwangu sio mchezo kama udhaniavyo, uchambuzi wa siasa ni fani yangu, na nimeiendea shule chini ya mabingwa na sio wababaishaji .......

Tanzanianjema
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom