Barua ya majibu ya Msekwa kuwajibu Kinana na Makamba hii hapa

Amini nakuambia awamu ya pili ya JPM itakuwa na kishindo kikubwa mno na watu hawataamini kitakochotokea

Mark my words
 
Mkuu naona unatoa kashfa nyingine tena kwa kuhusisha masuala binafsi ya mtu.
Tatizo nini?
Nini kifanyike basi kutatua tatizo ulionalo lipo?
 

You can sense the danger of plotting against the king, from this letter, full of wisdom. Wazee wetu hawa, Kinana na Makamba, kwanini wasichukue busara za wengine walioamua kukaa kimya? Kuna mengi watayapata kwa kufanya hivyo kuliko kujaribu kumpindua mfalme. Sio kitu rahisi. Na historia inatufunza kwamba, pale ambao mapinduzi yanashindikana, wale waliopanga mapinduzi wanapewa zawadi.
Enzi zile za zamani, vichwa vyao au wananing'inizwa juu ili watu waone na kufikiria vizuri wakiamua kufanya hivyo tena.
 
Wakati hili baraza linaundwa awamu ya jana kama sikosei kulikuwa na minong'ono ya ni kama mbinu za kuwaweka Wastaafu wa ngazi za juu pembeni ili wasitie kauzibe katika vikao rasmi vya chama. Ndio utaona huto tuvifungu twa ajabu twa ushauri unaombwa, unaweza uzingatiwe au upuuzwe na mambo mengine ya juujuuu tu hivi na yasiyo ya msingi. Na fikiri clip itawakumbusha nani ni muumini wa sera za juu juu.



Lakini hujafa hujaumbika Msekwa naye kawajibu kijuu juu kama msingi wa kuanzishwa baraza leyewe ulivyo kusudia. Na msingi utaona ni Wazee Wastaafu washirikishwe kijuu juu tu.
 

Truth be told, hivi unaujua vizuri muundo wa chama cha mapinduzi? Ule unaoonekana na usioonekana? Msekwa amekaa kwenye siasa na mifumo ya uongozi ya ncho hii muda mrefu kujua hatari ya kujaribu kufanya baadhi ya mambo.

Tatizo letu kubwa ni kukosa ubunifu na kupenda kujisomea...hatuwezi kukiondoa cha dola kwa mbinu ambazo toka zianze hazibadiliki na hazijatoa tija yoyote.

Unamshauri Mzee nini sasa? Ajifunge Kamba shingoni akajining'inize kama yeye naye ni shujaa wa kihehe anayeona fahari kufa kisa kamfumania mkewe, bila kujua anahalalisha ndoa ya wawili hao yeye akishaenda chini futi sita?
 
Hongera mzee Msekwa kwa hekima msjibu ya awali na huenda yakawa ya mwisho, kwani umenawa baraza halina maamlaka! Hivyo basi mtalitupa zigo juu kwa uongozi uliopo .
 
Huku bavichaa wako bize na audio feki za ccm
 
Yote haya ni kwa sababu hakuwaunga mkono akina Kinana? Ni tatizo la akili, hili! Kila siku tunawinda nani amkomoe rais, huyo ndo shujaa. Ili iweje? Kama unazijua taratibu za CCM kuliko zilizoelezwa, basi toa majibu! Ajabu ni kwamba hata wana CHADEMA sasa wanatafuta msaada CCM!
 
Mzee kajibu kisheria sana na kakwepa sana.
Ishu itawadodea kina Kinana
 
Acha kukwepa wajibu wako! Nyerere alimkemea Mwinyi bila woga na bila kujali hoja za kijinga kama hizi!
 
Reactions: Qwy
Unataka akufurahishe wewe kamanda wa ufipa, au?
 
Kama kawa Jk anajifanya mtoto wa mjini kwa kuzuga anakagua viwanja vyake huko dom wkt anajua saga lote.

Kama alivyomruka Lowassa kwenye richmond amaenda kuwaruka wakina Nape tena.
Yaani umenifanya nicheke ghafla
 
Jamaa analinda Ukumbi wake pale dodoma usije ukavunjwa, Ukumbi wa Pius Msekwa, lazma acheze na upepo
 
Maajabu! Barua ya Msekwa imevuja kabla hata hajai-sign! Au wazee wa baraza la wazee huwa hawasign documents zao?

Hata hivyo nimeona tatizo la kisarufi ambayo si rahisi ifanywe na Mzee Msekwa ambaye amewahi kuandika hata vitabu:

'Ndugu Abdurahaman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM mstaafu' badala ya .......Kinana, Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM. Hali kadhalika kwa mzee Makamba. Hii kitu inaitwa 'CCM mstaafu' sijui nini.....maana ni kuwa CCM ilishastaafu. Nachelea kusema hii barua si genuine kwa sababu haina sahihi ya mwandishi lakini pia tatizo la sarufi inaonesha imeandikwa na Bashite classic.
 

Mzee Pius Msekwa una akili na busara sana. Umejibu vema. Mungu akubariki.
 
Msekwa nae amezuuuuuka tu hakuna jipya, anashauri hayo kwani Musiba ni mwana ccm? Mwenyewe anajiita mwana harakati sasa kwa nini ajadiliwe kwenye vikao vya chama? Kumbe Membe ana akili na busara kuliko hawa wazee?! Mahakamani ndio mahali pa kushughulika na mtuhumiwa wako sio vikao vya chama...Musiba yake mahakama tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…