Barua ya majibu ya Msekwa kuwajibu Kinana na Makamba hii hapa

Barua ya majibu ya Msekwa kuwajibu Kinana na Makamba hii hapa

Msekwa nadhani ndio kiongozi Mstaafu muoga kuliko wote , hana ujasiri wowote ule na wala hawezi kutenda haki kwenye sakata hili , hii ni kwa sababu hajawahi kujitegemea na hajawahi kuhangaikia maisha yake nje ya ccm , anaiabudu ccm kuliko Mungu , kwake " mwenye bia nyingi mezani " ndiye wake , hata mke aliyenaye alimpata kwenye jumuiya za chama .
Busara kama hizi za mzee msekwa huwezi kuzikuta ufipa pale.

Hili saga lingekuwa limetokea upande wa ufipa sasa hivi kila mtu angekuwa anatoa tamko, huku kina Lema na Msigwa wakiendelea kutoa matusi Twitter wakichangiwa na makamanda uchwara kama wewe.

Igeni hizi Busara toka ccm
 
Busara kama hizi za mzee msekwa huwezi kuzikuta ufipa pale.

Hili saga lingekuwa limetokea upande wa ufipa sasa hivi kila mtu angekuwa anatoa tamko, huku kina Lema na Msigwa wakiendelea kutoa matusi Twitter wakichangiwa na makamanda uchwara kama wewe.

Igeni hizi Busara toka ccm
kitu cha msingi sana ni kwamba umenielewa , hii inatosha
 
yaani wewe ndo unaakili saaan kupita wao
Mkuu hata mtu mwenye akili nyingi sana anaweza kuto itumia vizuri akitawaliwa na tamaa au hisia flani.

Emotional intelligence (EQ) ni kitu muhimu sana wakati wa kufanikisha malengo flani.
Wakati mwinge pengine ni muhimu kuliko IQ.

Na ndio maana unakuta asie soma au mtu mwenye elimu ya msingi tu, anaweza kufanikiwa sana kimaisha kuliko mhadhiri wa chuo kikuu.

Hilo kundi la akina Nape kuna walioshikwa na hisia za hasira kutumbuliwa, kuachwa kando meza kuu ya karamu, kuzuiwa madudu ya kifisadi, kukosolewa awamu yao kwa uzembe, kukosa uraisi au tamaa ya kupata uraisi n.k.

Hivyo wengi hapo si wavumilivu na kupangilia mambo kwa makini. Emotionally hawako stable ni vile wanakurupuka, wapo desperate.

Hivyo inawezekana wana akili (IQ) kubwa kuliko mimi lakini hawapo emotionally stable kuliko mimi. Wanakosa utulivu katika fikra wakati wanapanga mikakati.
 
Sio uoga...wanapambania maslahi binafsi. Makamba anataka mtoto wake awe Rais. Kinana anataka empire yake iendelee kula vya bure. Sidhani kama hao wanaipenda hivyo Tanzania

Hongera Makamba na Kinana. Zama za uoga zimepitwa. A new era has begun. Kama Jiwe anamtuma Musiba kutukana watu na aambiwe... That is the crux of the matter. Hayo mengine ni kelele tu.
 
Mkuu ujumbe umefika lakini hii sio barua labda useme maelezo ya barua! Otherwise piga picha au scan uitume!
 
Barua hata usipo address mtu katibu ataifungua na kuipekeka kunakohusika.
which means huna haja ya kui address kwa Katibu...

matokeo yake ndio haya sasa, Katibu kajibu

ingekuwa addressed kwa Chairman au Baraza, Msekwa asingepata balls wala uhalali wa kutoa "majibu ya awali..."

tuache kufanya vitu kwa mujibu wa mwalimu wa somo la Uandishi wa Barua darasa la nne... darasa la nne unakaririshwa vitu vya kiofisi ambavyo huna uwezo wa kuvichambua wewe wala mwalimu wako
 
Tarehe15 Julai, 2019.

Nakiri kupokea barua yenu ya tarehe 15 07/ 2019 ambayo mliisaini wote wawili, na ikawasilishwa kwangu kwa mkono na Mhe. Nape Nnauye (Mb), jana tarehe 14/07/ 2019
 
Msekwa nadhani ndio kiongozi Mstaafu muoga kuliko wote , hana ujasiri wowote ule na wala hawezi kutenda haki kwenye sakata hili , hii ni kwa sababu hajawahi kujitegemea na hajawahi kuhangaikia maisha yake nje ya ccm , anaiabudu ccm kuliko Mungu , kwake " mwenye bia nyingi mezani " ndiye wake , hata mke aliyenaye alimpata kwenye jumuiya za chama .
Duh!! hii kweli kiboko
 
Mi naombea wazidi kuparuana mpaka wapate majeraha nje na ndani ya mwili
 
which means huna haja ya kui address kwa Katibu...

matokeo yake ndio haya sasa, Katibu kajibu

ingekuwa addressed kwa Chairman au Baraza, Msekwa asingepata balls wala uhalali wa kutoa "majibu ya awali..."

tuache kufanya vitu kwa mujibu wa mwalimu wa somo la Uandishi wa Barua darasa la nne... darasa la nne unakaririshwa vitu vya kiofisi ambavyo huna uwezo wa kuvichambua wewe wala mwalimu wako
Katibu alitakiwa ajibu kuwa kwa niaba ya Baraza ninatoa majibu yafuatayo Lakini ona alichoandika Ni as if yeye Ndie mtoa majibu mwenyewe!!!! Chochote anachojibu alitakiwa Aseme kwa niaba .Lakini kwa kuwa hakuwashirikisha kutoa majibu ndoo unaona Mzee msekwa akijikanyaga ohh natoa sehemu tu ya majibu ohh majibu kamili wazee wakikaaa SI angesubiri wakae haraka ya Nini?
 
Msekwa nadhani ndio kiongozi Mstaafu muoga kuliko wote , hana ujasiri wowote ule na wala hawezi kutenda haki kwenye sakata hili , hii ni kwa sababu hajawahi kujitegemea na hajawahi kuhangaikia maisha yake nje ya ccm , anaiabudu ccm kuliko Mungu , kwake " mwenye bia nyingi mezani " ndiye wake , hata mke aliyenaye alimpata kwenye jumuiya za chama .
Attacking personalities is one of horrible shortfalls in argument. I is absolutely fallacious.
 
Maajabu! Barua ya Msekwa imevuja kabla hata hajai-sign! Au wazee wa baraza la wazee huwa hawasign documents zao?

Hata hivyo nimeona tatizo la kisarufi ambayo si rahisi ifanywe na Mzee Msekwa ambaye amewahi kuandika hata vitabu:

'Ndugu Abdurahaman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM mstaafu' badala ya .......Kinana, Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM. Hali kadhalika kwa mzee Makamba. Hii kitu inaitwa 'CCM mstaafu' sijui nini.....maana ni kuwa CCM ilishastaafu. Nachelea kusema hii barua si genuine kwa sababu haina sahihi ya mwandishi lakini pia tatizo la sarufi inaonesha imeandikwa na Bashite classic.
Bora umeliona hilo, the billion dollar question is who is controlling this whole shit?
Kuna mtu au kikundi cha watu wanoichezesha hii game na inaenda kadri utashi wao, hata kama kiranja mkuu hausiki moja kwa moja lazima kutakuwa na blessings zake. Si rahisi kuwachezea wazee heavyweights kama hao na kila mtu akaogopa japo hata kuonyesha kukerwa na kinachoendelea.
 
BARUA YA MAJIBU YA AWALI.

Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu;

Ndugu Yussuf Makamba, Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu;

DAR ES SALAAM.

Tarehe15 Julai, 2019.

Nakiri kupokea barua yenu ya tarehe 15 07/ 2019 ambayo mliisaini wote wawili, na ikawasilishwa kwangu kwa mkono na Mhe. Nape Nnauye (Mb), jana tarehe 14/07/ 2019.

Baada ya kuisoma kwa makini, nimetambua kwamba malengo makuu ya barua hiyo, yalikuwa ni mawili yafuatayo:

(i) Kuwasilisha kwa pamoja malalamiko yenu dhidi ya mtu aitwaye Cypriian Musiba; ambaye “amekuwa akitoa maelezo yenye kuwatuhumu na kuwazushia uwongo ninyi, na viongozi wengine wastaafu wa CCM na wa Serikali waliostaafu na walioko madarakani, kwamba eti mnamhujumu Rais kutekeleza majukumu yake” (ukurasa wa kwanza, para ya pili).

(ii) Kuomba Baraza la Viongozi Wakuu Wastaafu wa CCM “walishughulikie jambo hili, kwa namna ambayo wazee wenyewe wataona kuwa inafaa”. (ukurasa wa pili, para ya mwisho).

Zaidi ya hayo, nimezingatia maelezo yenu ya kuwa “tuliamini kwamba, kama utaratibu wa CCM ulivyo, kazi ya kulinda heshima ya CCM ni pamoja na kukemea vikali, pale viongozi wake wakuu wa sasa na waliostaafu wanapochafuliwa. Kwa hiyo basi, tulitegemea wahusika ndani ya Chama watazikemea kauli zake , na kumuasa asitumie jina la Mwenyekiti wa CCM kuchafua na kudhalilisha watu, au kumchukulia hatua nyingine muafaka. Kwa bahati mbaya, hili halikufanyika”. (ukurasa wa kwanza, para ya tatu).

Kwa maelezo hayo, barua yenu inachukua sura ya “rufaa kwa Wazee” hawa, kutokana na kuona kwamba Chama “kimeshindwa kukemea vikali jambo hili”.

Majibu ya awali.

Kama mnavyofahamu, Baraza hili hufanya kazi kwa njia ya vikao rasmi, na kwamba Katibu peke yake hana mamlaka ya kutoa maamuzi yoyote. Kwa hiyo, nitawasilisha barua yenu kwa Wajumbe wa Baraza, ili kupata maelekezo yao juu ya nini kifanyike. Lakini wakati tunasubiri, naweza kutoa majibu ya awali, yakiwa ni ya kukumbushana mambo ya msingi yafuatayo ambayo yanapaswa kuzingatiwa, (ambayo mimi na ninyi tulisimamia utekelezaji wake, wakati tulipokuwa madarakani kama viongozi wakuu wa Chama):

(1) Wajibu wa kutii Katiba na Kanuni zilizopo.

Jambo la kwanza linahusu mamlaka ya kutenda kazi, au ‘ jurisdiction’, ya Baraza letu, kama yalivyowekwa na Katiba ya Chama, Kama mnavyojua, Katiba ya Chama cha Mapinduzi imekipangia kila Kikao cha Chama kazi zake mahsusi za kufanya. Na kazi mahsusi ya Baraza la Ushauri la Viongozi Wakuu Wastaafu wa CCM, zimetajwa na kuainiishwa katika Ibara ya 127 (3) ya Katiba hiyo, Toleo la 2012, kuwa ni “kutoa ushauri kwa Chama cha Mapinduzi, na kwa Serikali zinazoongozwa na Chama hicho”. Lakini kazi zile za kuangalia mwenendo wa wanachama na Viongozi wake, na kuchukua hatua stahiki pale inapobidi; hizo zimepangiwa vikao vingine vya Chama, vikao ambavyo ni vya utendaji (administration) ; kama ilivyoainishwa katika Ibara zinazohusu Vikao hivyo. Maana yake ni kwamba Kikatiba, Baraza la Ushauri halikupewa mamlaka, au ‘jurisdiction’, ya kutenda kazi hizo, ambazo ni za ki-uendeshaji. Badala yake, jukumu hilo limetolewa kwa vikao vingine, ambavyo ni vya viongozi walioko madarakani.

(2) Jambo la pili linahusu umuhimu wa kuzingatia miiko ya utoaji ushauri (ambayo ndiyo kazi mahsusi ya Baraza hili); ambayo ni hii ifuatayo:

(i) Kwamba ushauri huombwa. Ushauri kamwe hauwezi kushinikizwa kwa mshauriwa, au kutolewa kwake

kama amri ! Ndiyo kusema kwamba ushauri hauwezi kutolewa pale ambapo hauhitajiki. Na mwenye kuamua kuwapo kwa hitaji hilo, ni yule anayehitaji kupata ushauri, SIYO yule anayetaka kutoa ushauri.

(ii) Hata pale ushauri unapotolewa, tusisahau kwamba unaweza ama kukubaliwa; au kukataliwa. Pale unapokubaliwa, thamani yake inakuwa ni kubwa, kwa maana ya kuondoa tatizo lililokuwapo. Lakini pale ushauri unapokataliwa, thamani yake inakuwa ni sifuri kabisa, kwa maana ya kutatua tatizo lililopo.

(3) Jambo la tatu, ni kwamba jukumu la mtu yeyote aliyetuhumiwa la kusafisha jina lake, ni la mtuhumiwa mwenyewe.

Barua yenu imeeleza kwamba “Mlitafakari suala la kujitokeza hadharani ili kutoa yaliyo moyoni mwenu katika kujibu uwongo wake, kusafisha majina yetu, heshima yenu, na rekodi nzuri ya utumishi wenu, lakini mkaona kuwa ni vyema kwanza mkawasilisha malalamiko yenu kwenye Baraza la Ushauri la Viongozi Wakuu Wastaafu wa CCM, ili jambo hili lishughulikiwe”.

Sasa ki-utaratibu, siyo sahihi kujaribu kukwepa jukumu hilo la watuhumiwa wenyewe kujisafisha kwa kukanusha tuhuma zinzowahusu, na kujaribu kulihamishia jukumu hilo kwa watu wengine . Hii ni kwa sababu watuhumiwa wenyewe ndio wanaojua ukweli kuhusu tuhuma hizo, na kama kweli hazina msingi, ni wajibu wao kufichua ukweli wanaoujua.

Umuhimu wa jambo ili unatokana na kuwapo kwa dhana inayosema kwamba “silence means consent”; ambayo maana yake ni kwamba ‘ukinyamaza kimya bila kukanusha tuhuma zilizoelekezwa kwako, ukimya wako huo unachukuliwa kwamba umekiri ukweli wa tuhuma hizo’. Nafurahi, na kuwapongeza, kwamba tayari mumetekeleza wajibu huo kupitia vyombo vya habari.

TAHADHARI: Msiruhusu machungu ya tuhuma hizo yakawasahaulisha misingi hii, mkashawisika ‘kutafuta njia za mkato’ za kuyashughulikia, ambazo kumbe zinakiuka Katiba ya Chama chetu.

Madhumuni ya maelezo haya

Naomba ieleweke kwamba madhumuni ya kukumbushana juu ya mambo haya ya msingi , ni kuonesha tu ugumu uliopo wa ki-Katiba, kwa Baraza la Ushauri la Viongozi Wakuu Wastaafu wa CCM kushughulikia malalamiko yenu, kama mlivyoomba. Ugumu huo unatokana na kuzingatia kuwa:

kwanza, Katiba ya Chama haikutoa jukumu la kufanya kazi za ki-uendeshaji (administration) kama hii ya kusikiliza malalamiko yenu, kwa Baraza hili. Lakini pili, Baraza letu pia halikupewa mamlaka ya kusikiliza rufani zinazotolewa dhidi ya Chama, kama hii ya kwenu.

Ni muhimu vile vile, kuzingatia kwamba Baraza la Viongozi Wakuu Wastaafu wa CCM, ni chombo maalum cha Chama hicho , kilichoundwa na kupewa kazi maalum, iliyotajwa katika Katiba ya Chama. Baraza hili siyo kundi lolote tu la “wazee wa Chama” (kama yalivyo yale “Mabaraza ya wazee” mengine, yaliyotajwa katika Ibara ya 128 ya Katiba ya Chama), ambayo wajumbe wake wanatajwa kuwa ni “wazee wote wana-CCM, wenye umri kuanzia miaka sitini”; ambao, kwa kuwa hawakupangiwa jukumu lolote maalum, wanadhaniwa kuwa wanaweza kushiriki tu katika utekelezaji wa shughuli zozote za Chama “kwa kutumia busara za uzee wao, kama watakavyoona wao kuwa inafaa”!

Nahitimisha kwa kurudia kusema, kwamba haya ni majibu ya wali tu. Nawajibika kusubiri maelekezo ya wajumbe wa Baraza.

Pius Msekwa.

KATIBU, BARAZA LA USHAURI LA VIONGOZI WAKUU WASTAAFU WA CCM.

Kwa majibu haya ya Msekwa, ambayo Musiba amepata nakala yake, kilichobak ni kumwaga ugali, kwani wao wamesha mwaga mboga.
Hakuna jiwe litakao salia juu ya jiwe.
 
Msekwa nadhani ndio kiongozi Mstaafu muoga kuliko wote , hana ujasiri wowote ule na wala hawezi kutenda haki kwenye sakata hili , hii ni kwa sababu hajawahi kujitegemea na hajawahi kuhangaikia maisha yake nje ya ccm , anaiabudu ccm kuliko Mungu , kwake " mwenye bia nyingi mezani " ndiye wake , hata mke aliyenaye alimpata kwenye jumuiya za chama .
Hayo ya Msekwa binafsi tuyaepuke. Ila kwakweli hajakidhi kiwango (as a matter of principal) kwenye kutetea katiba ya chama chao tu.
Kwenye Katiba ya Nchi hiyo principal yake au ya chama chao HAIHUSIKI!!!!
Vinginevyo ni kigugumizi cha backbenchers wote wa CCM kinachotokana na mfumo mzima unaowaweka madarakani.
 
Tayari hapo kuna tatizo inaonyesha musiba ana uhakika na anachokisema kutokana na maelezo ya msekwa kuwa wajisafishe wenyewe na wao wanajua wakijaribu huenda yakasemwa mengi
 
Msome vizuri tena.
Hakuna mahali ametoa hitimisho au majibu ya mwisho.

Yeye kama katibu anao wajibu wa kuwajulisha wahusika kuwa amepokea barua yao, na kisha kutoa maoni yake au kukumbusha taratibu, kanuni, sheria na katiba vinasema nini na nani wa kutolea mahamuzi ya madai ya kwenye barua.


Kwanini ushauri wake asinge toa baada ya majibu ya kikao cha kamati yao? Huoni hapo kama hakuna haja tena ya kikao chao kwasababu yeye kesha maliza kila kitu? Ni mtazamo tu.
 
Back
Top Bottom