Barua ya wazi kwa Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi: Manung'uniko ya Waislamu lazima yafanyiwe kazi

Barua ya wazi kwa Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi: Manung'uniko ya Waislamu lazima yafanyiwe kazi

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Ndugu Bashiru Ally,
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi

Mimi ni mwananchi, raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nimeamua kuchukua wasaa huu kukuandikia haya yafuatayo, kwani kwa haya niyaandikayo naamini ni ya msingi sana katika kukuza umoja na mshikamano wa Taifa letu vitu ambavyo ni muhimu sana katika kuimarisha amani ya Taifa letu. Kwa muktadha huu kuna nukta chache ningependa kukueleza ili chama chako cha Mapinduzi ambacho wewe ni mfuatiliaji mkuu wa utekelezaji wa Ilani yake ni lazima uzielewe na uhakikishe chama chako kinazifanyia kazi.

Ndugu Ponda alisoma waraka mzito sana, waraka wenye mambo mengi yanayohusu Taifa letu kiujumla na mengine exclusively yanayowahusu waislamu. kwa hiyo mimi nitakijikita katika yale yanayowahusu Waislamu.

1. Mosi kuna malalamiko ya muda mrefu ya kuhusu Waislamu kufanywa raia daraja la pili nchini.
Kwa miaka mingi tangu uraisi wa Mwalimu Nyerere, kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa waislamu, kuwa kuna ubaguzi wa kimfumo dhidi yao, miaka ya zamani walikuwa wakitolea mifano kwenye nafasi za elimu ya juu, kuwa inakuwaje Wanaoanzishwa shule darasa la kwanza kuna mamilioni ya vijana wa kiislamu, lakini ukiangalia huko kwenye elimu ya juu vyuoni, waislamu ni wachache sana?

Madai haya ya waislamu yamekuwepo, wengi wamekuwa wakimrejea Kighoma Malima kuwa alisaidia kufanya reforms kadha wa kadha alipoteuliwa na Rais wa awamu ya pili kuwa waziri wa Elimu, Mimi sitaki kujadili ukweli au uongo wa haya madai, bali nataka nikueleze kuwa hizi sentiment zipo katika jamii, waislamu wamekuwa wakizizungumza hizi habari kwa muda mrefu kama sehemu ya historia yao katika harakati za kutafuta namna ya kunufaika na matunda ya uhuru. Ubaya wa historia ni kuwa historia haifi.

Ndugu katibu mkuu ipo haja ya Chama cha Mapinduzi kuja mbele, kuweka rekodi sawa kiwaeleze waislamu kuwa chenyewe kama chama ambacho kwa kauli ya muasisi mwenyewe wa chama hiki aliwahi kukiri waislamu kuwa nyuma kielimu wakati wa uhuru, kije kiwaambie Waislamu, sisi kama chama tumefanya kadha wa kadha juu yenu na sasa hivi tumepata mafanikio kadha wa kadha kwenye suala hili la Elimu. Kwanini hii hoja ya elimu ni muhimu sana? Kwa sababu Elimu inaambatana na ajira, na teuzi mbalimbali serikalini na katika utumishi wa umma. Kwa maana mara nyingi waislamu wanapouliza swali kuwa mbona proportion yetu kwenye teuzi na ajira haiakisi wingi wetu wamekuwa wajibiwa kuwa hamjasoma!

2. Chama cha Mapinduzi lazima kiitake serikali yake itende haki kwa makundi yote ya kijamii
Kwa mujibu wa waraka uliosomwa na Sheikh Ponda, unaoonyesha uwiano wa teuzi kati ya Watanzania wenye imani ya Kikiristo na Watanzania wenye Imani ya Kiislamu ni kwa uwiano wa asilimia 80% wakiristo, na 20%Waislamu.
Ndugu Katibu mkuu by all standards hii haijakaa sawa hata kidogo. Haiyumkiniki katika Taifa ambalo populationwise kila kundi kati ya hayo mawili ndani ya jamii lina idadi kubwa ya kutosha tu ya watu katika jamii lakini linapokuja katika utumishi wa umma na teuzi za serikali kundi moja liko overrepsented huku jingine likionekana likiwa na idadi finyu sana, Kwa namna zozote zile hii asilimia ya 80% kwa 20% haiakisi uhalisia wa demography ya wananchi kwa muktadha wa makundi ya imani zao.

Chama cha Mapinduzi kinapaswa kuja na kuwaangalia waislamu machoni kiwaambie, wao wana shida gani kwa nini ni wachache katika teuzi hizi za serikali, wao hawana nini ambacho wenzao wanacho kiasi kwamba kundi jingine likiwa jingi katika nafasi hizo za teuzi kuliko wao? Zimekuwepo hoja kuwa hateuliwi mtu kwa sababu ya dini yake bali vigezo vingine, Tunataka chama cha mapinduzi kiwaambie waislamu kuwa labda hawana elimu, siyo wazalendo, ni mafisadi, ni wavivu sana, Au kiwaeleze sababu zozote zenye mashiko kwa nini wingi wao katika jamii hauakisi uwepo wao katika utumishi wa serikali?

Ndugu katibu mkuu, Chama cha mapinduzi kinaweza kuamua kukaa kimya utadhani hili tatizo halipo, lakini mimi ningependa kukiambia kuwa, uwepo au kutokuwepo kwa tatizo hilo siyo hoja, hoja ni kuwa waislamu wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu na sisi tunaoitakia amani nchi hii, tunaona kuwa hili ni bomu linalosubiri kupasuka kama ama rekodi zisipowekwa sawa au kufanyiwa kazi na serikali.

Ndugu katibu mkuu, Chama chako cha mapinduzi au serikali zake kamwe zisidhani kuwa madai haya ya waislamu yataisha iwapo kila siku wanakaa wanaona teuzi za serikali moja baada ya nyingine anateuliwa mtu wa imani nyingine huku wao wakiambiwa eti watu hawateuliwi kwa dini zao bali vigezo vingine, kwa nini hivyo vigezo viwe kwa wingi kwa watu wa imani moja tu?

3. Udini ni ufa mkubwa sana wa jamii yetu na ni lazima wote tuungane kuupiga vita
Ndugu katibu mkuu, kama kuna ufa mkubwa zaidi katika nchi yetu basi ni suala la udini, hili ni tatizo ambalo hatupaswi kulipiga vita kwa maneno bali kwa vitendo, na katika kulipiga vita tatizo hilo lazima tulipige vita huku kila mtu akiona kabisa kuwa tuna dhati ya kufanya hivyo, vipo viashiria nchini kuwa watu wa imani moja wanawekwa kwenye mizania tofauti pindi wanapofanya mambo fulani yenye kuashiria udini, na mambo haya yanawafanya watu wa dini nyingine wajihisi kuwa ni kutokana na mfumo kuinua kundi fulani ndiyo maana kundi hilo linajihisi kufanya mambo with impunity.

Katibu mkuu nitakupa mfano, Mkuu wa mkoa wa mmoja nchini anatoa kauli kuwa Nchi hii iko chini ya kanisa, hasemi iko chini ya Mungu, anasema iko chini ya kanisa na wala hashughulikiwi na serikali ya chana chsko kwa uchochezi. Waziri mmoja mwandamizi anafanya kampeni katika kanisa kwa kutandika bendera ya chama ndani ya madhabahu, Viongozi wa imani moja wakikemea serikali kwa kauli na maandishi (Japo ni haki yao) hawakamatwi lakini kiongozi wa dini ya Kiislamu anaposimama na kutumia haki yake ya kutoa mapendekezo na maoni yake anakamatwa na kuswekwa ndani bila kufikishwa mahakamani ndani ya muda maalumu kinyume cha sheria.

Ndugu katibu mkuu, katika muktadha huu kwa nini Waislamu wasikiwekee chama chako na serikali yake alama ya kuuliza kuwa huenda vinalea na kuendekeza udini wa imani mmoja nchini?

4. Suala la kuhamisha wahadhiri na watumishi 11 wa Imani moja Chuo cha UDOM na kuleta wengine 11 wa imani nyingine linahitaji uchunguzi
Ndugu katibu mkuu, nilistushwa sana na hili suala kama ambavyo lilielezwa kwa kina kwenye waraka wa Sheikh Ponda.
Nimejiuliza kuwa iweje katika utumishi uhamishe watu kwa mkupuo halafu ionekane wote ni wa imani moja halafu waletwe wengine 11 na wote wawe wa imani moja, hili linatoa picha gani, limebeba ajenda gani, hao waliofanya uhamisho huo walitaka kuachieve kitu gani?

Wazungu wana msemo kuwa, ukiona inatweta kama bata, inatembea kama bata na inalia kama bata basi hiyo ni bata. Inawezekana vipi kwa kanuni zozote zile za nasibu uondoe watu 11 wenye kufuata mrengo wa dini moja sehemu halafu wakati huohuo ulete wengine 11 wa dini nyingine kama maamuzi ya kufanya hivyo hayakusukumwa na udini uliokubuhu katika kufanya maamuzi hayo basi ni kitu gani?. Cha kusikitisha zaidi waraka ukaenda mbele na kusema wazi kuwa wengine katika wale waliohamishwa walienda kupewa nafasi za chini kuliko hadhi yao.

Ndugu katibu mkuu, tunakitaka chama chako kifanye uchunguzi au kiilazimishe serikali yake ichunguze na iwaeleze Watanzania ni sababu gani za msingi hatua hiyo ilifikiwa na kwa nini ionekane watu wa dini moja ndiyo wanakumbwa na zoezi la kuondolewa mahali na wakaletwa wengine wote wa imani ya dini nyingine.

Hoja kuwa serikali inaweza kumhamisha yeyote na kumleta yeyote katika utumishi wa umma ni kweli lakini kwa muktadha huu haina mashiko maana inaonyesha kuwa kuna msukumo fulani wa maamuzi ambayo yameacha question marks na kwa kuwa kuna umma hususan wa kiislamu unadhani kuwa kuna nia isiyo njema imesukuma maamuzi hayo, tunakitaka chama cha Mapinduzi kitoe maelezo kwa nini uamuzi tata huo ulifikiwa ili kusafisha hali hii inayoweza kupelekea hisia hasi zinazoweza kupelekea kuvunjika kwa amani.

5. Chama cha mapinduzi na serikali yake kijifunze kwa maandamano yanayotokea marekani kupinga ubaguzi
Huko Marekani kulikuwepo na manung'uniko ya muda mrefu, watu weusi wakilslamika hadharani na sirini kuhusu ubaguzi wa kimfumo dhidi yao, walilamika kuhusu ubaguzi katika uchumi, katika mifumo ya utoaji haki nchini humo, walilamika hadi upataji wa ajira katika serikali ya Shirikisho na hata za majimbo.

Manung'uniko yao yalikuwa yakipuuzwa kwa madai kuwa marekani hakuna ubaguguzi wowote bali ni inferiority complex yao tu na uvivu wao wa kutofanya kazi. Ikawa inatolewa mifano michache kuwa mbona fulani na fulani ni weusi na matajiri, ni wacheza kikapu maarufu, ni wacheza sinema maarufu n. k. Hata hivyo pamoja na kauli hizi donge lilikuwa bado limo katika mioyo ya wamarekani weusi maana wanasema yule avaaye kiatu, yeye ndiye anayeona wapi kinambana. Leo Marekani hali imekuwa tete baada ya wamarekani weusi na wale wapenda haki kuingia mitaani kuonyesha ghadhabu yao juu ya matendo hayo baada ya kifo cha kikatili cha George Floyd kilichosababishwa na ukatili wenye dalili zote za ubaguzi wa rangi.

Ndugu Katibu Mkuu, madai haya ya Waislamu hapa nchini haijalishi ni ya kweli au siyo kweli lakini yapo, madai haya yanahitaji majibu au hatua ya kuyarekebisha ili yasije kuendelea kujenga ghadhabu ya kimya kimya ambayo siku moja ikitoka nje, sisi kama taifa tutakuja kuwa na wakati mgumu sana. Kamwe tusijenge Kiburi kuwa vyombo vya usalama vitawashughulikia wote hao wenye kuleta madai haya. Ndugu katibu mkuu hata katika hivyo vyombo vya usalama kunaweza kukawemo watu walioaminishwa dhana hizo iwapo zitaachwa bila kushughulikiwa na ikitokea hali hiyo Taifa liktakuwa katika sintofahamu kubwa. Wahenga walisema Kinga ni bora kuliko tiba, yatupasa kama Taifa kulitafutia ufumbuzi suala hili badala ya kujidai kuwa halipo.

6. Ni muda muafaka sasa Masheikh walioko jela waachiwe huru bila masharti yoyote
Ndugu katibu mkuu, ni mwaka takriban wa 8 sasa Masheikh wapo jela bila kuhukumiwa na mahakama yoyote, Makosa yao hayajathibitishwa mahakamani, kwa hiyo madai na hoja zilizosomwa na Sheikh Ponda zina. mashiko
Tunakitaka chama cha mapinduzi kiisimamie serikali yake izingatie utawala wa sheria.

Chama kiulize serikali yake, inaendelea kuwashikilia Masheikh hao kwa uhalali upi wa kisheria?. Kama uchunguzi haujakamilika, kama huo uchunguzi haujakamilika miaka 8 utakamilika lini? Je, haki inatendeka kwa hawa masheikh au kuna namna yoyote ya kuamua kuwakomoa?

Ndugu katibu mkuu hawa Masheikh walikamatwa Zanzibar, kama lengo ni Justice au haki kwa nini ilazimishwe washitakiwe Tanzania bara na si hukohuko Zanzibar walipotenda kosa lolote inalodaiwa walitenda?

Hitimisho:
Ndugu katibu mkuu, yapo madai ambayo waislamu wamekuwa wakidai miaka nenda rudi, na kuna mambo wamekuwa wakiyawekea question mark kama vile teuzi katika awamu hii.

Sasa sisi kama raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunaona kuwa haya madai yasipojibiwa huenda yakaitia nchi katika uwezekano wa kuvunja mshikamano wa kitaifa na kuvunja amani huko mbele.

Sasa kwa kuwa watu wa aina yangu tunaipenda nchi yetu, si busara kuacha kutoa mchango wa mawazo katika mambo kama haya hata kama ni tata kiasi gani(controversial). Ndiyo maana kwa muktadha huu tunakitaka chsma cha Mapinduzi kijibu hoja za waislamu ili kutunza huo mshikamano!

Ndugu Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi waislamu wana hoja zijibuni

Wako katika ujenzi wa Taifa.

Missile of the Nation (Kombora hatari kabisa la ulinzi wa Taifa)

Nakala kwa:
1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2. Waziri Mkuu
3. Mkurugenzi Usalama wa Taifa
 
SUALA LA ELIMU WAISLAMU WENGI HAWALIPI KIPAUMBELE TUACHENI KUSINGIZIA WAKRISTO. ELIMU DUNIA SI KIPAUMBELE KWETU. KWA NINI TUNAFUCHA UDHAIFU?

Waislamu wanaipa elimu kipaumbele kama wenzao Wakristo.

Hicho ulichokisrma ilikuwa ni enzi za ukoloni ambapo shule za mission zilikuwa zikitoa elimu huku zikibatiza watoto. Ila wale walioamua kufunika kombe na kukomaa kusoma hivyohivyo wakaishia kuwa waislamu "poa"

Enzi hizo ndo wazee wa kiislamu hawakupenda kupeleka watoto wao shule kuhofia hilo, ila baada ya uhuru wazazi wa kiislamu walikuwa na mwamko mkubwa sana wa kusomesha watoto wao ila pamoja na mwamk huo,mavyuoni idadi yao iliendelea kuwa kiduchu
 
Mi naona mleta mada ndo msing kwa sababu zifuatazo unapoteua au kuajiri unaangalia taaluma ya unarmuajir au kumteua sio dini sababu dini haiend kufanya kazi. Jingine ni kwamba waislam weng wanasema sana dini kuliko elim dunia sasa apo wanaofika chuo ni wachache ilo ni swala la wao kuhimizana kusoma sio kulalamikia chama cha Ccm . Mim sio ccm ila kwa hili mtailaumu bure ccm yani ufeli wew class lawama uipe ccm hii ni sawa???

Hii ni hoja dhaifu, na propaganda iliyopitwa na wakati

Ukiteuwa huteuwi malaki au mamilioni ya watu bali unateua mamia kama si maelfu.

Idadi hiyo ya kutosha ya wenye vigezo waislamu pia wanayo kama wenzao wakiristo
 
Huyo mwislam mwenzenu hana lolote, anamuogopa meko. Yani meko kawakamatawaislam wote kilichobaki ni kuwlisha kitimoto tu.

N mmetulia tulii na ataendeea kuwaklia kooni na kuwashika shika
 
Kwa nini tunapenda kupanda mbegu za udini? Je, tuamini kuwa ni kiki ya kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu?

Kuhusu CCM chama kilicho madarakani, Rais wa kwanza alikuwa Mkiristo, aliyemufuata Mzee Mwinyi, Muislamu. Rais wa Tatu, Mzee Mkapa, Mkristo akafuatiwa na Rais Kikwete, Muislamu. Rais aliyeko madarakani, Dr Magufuli ni Mkristo lakini Makamu wake, Mama Samia na Waziri Mkuu ni Waislamu. Hata Katibu Mkuu wa Chama ni Muislamu. Yaani viongozi wote hao hawatambui jamii ya Kiislamu isipokuwa wewe
Tufike mahali tuheshimu kuwepo kwa dini zingine na si Uislamu tu, kwamba kuna uonezi!
 
Back
Top Bottom