Barua ya wazi kwa Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi: Manung'uniko ya Waislamu lazima yafanyiwe kazi


Kama la masheikh lina ugaidi , kaisaidie polisi kupeleka kesi mahakamani labda mwenzetu unao ushahidi, ili hawa watu washitakiwe
 

Tanzania haina dini lakini Wakiristo ni wanufaika zaidi wa ajira na teuzi za serikali.
Kutokana na kunufaika huko wengi miongoni mwao wananufaika na mishahara iliyostable, Bima ya Afya nzuri, Pensheni za uzeeni, mikopo benki n. k
Matokeo yake wanao uwezo wa kusomesha watoto wao shule nzuri, kuwa na makazi stable.
Wakati huo Waislamu kutokana na kutonufaika ipasavyo na keki hiyo ya Taifa ya ajira za serikali , maisha yao yanakuwa siyo bora kama wakiristo, hawanufaiki na bima mzuri ya Afya, pensheni, na faida nyingi zitokanazo na mishahara ya serikali. Sasa katika hali kama hiyo Waislamu wanakuwa kama raia daraja la pili katika nchi yao. Hili halikubaliki, na lazima lifanyiwe kazi ili kuweka usawa na kuondoa manung'uniko ambayo kwa kweli ni madai ya msingi!. Hata mtu ujifanye vipi kuyapuuza, lakini ni madai halali na ya msingi sana!
 
Kama la masheikh lina ugaidi , kaisaidie polisi kupeleka kesi mahakamani labda mwenzetu unao ushahidi, ili hawa watu washitakiwe
Wewe ambae unaona wanaonewa nenda kawatoe tuishi nao uraiani.
 
Kama sababu ni hiyo kwanini usibadili dini ukaungana na unaodhani wanapata upendeleo ili nawe unufaike? Hii ni inferior complex ambayo mara nyingi insumbua sana makundi ama watu wasiojiamini!
Nenda kwa takwimu utueleze ni wapi ndani ya Jamhuri hii ya Muungano ambapo kundi fulani liliitwa kwenye usahili kwa nafasi fulani ila likabaguliwa kwa msingi wa dini.
 
Mimi ni mkristo ila nawaunga mkono kina shekh ponda kwasababu maaskofu wetu waliowengi wako kimya maboko kibao yanafanyika wao wako kimya wanasubiri rais mwislamu aingie madarakani ndio waanze kumsumbua.

Imagine polisi wanavyoonea chadema unreasonably.

Kupigwa risasi 32 kea lisu maaskofu wapo kimya .

Ben Saanane mpaka leo hatujui you mifupa au yupo safe house maaskofu kimya.

Azory kapotea maaskofu Aina ya pengo kimya .

Leo hii mtumishi wa uuma anaepaswa kuwa unbiased anachukua fomu kwa CCM maaskofu kimya.

Ikifika jumapili wanataka tuwapelekee our hard earned money kirahiiiiisiiii pumbav.

Nawapongeza wachache Aina ya bagonza hao Mungu awabariki .
 

Hakuna cha inferiority complex hapa. Huwezi kuteua 80% watu wa dini moja halafu ukaona hilo siyo tatizo!

Wote ni Watanzania, walipa kodi nchi hii, lazima keki ya Taifa igawanywe kwa haki.

Angekuwa rais Muislamu akateua 80% Waislamu nchi hii ingetawalika? , si mgechonga sana humu mitandaoni kama mlivyochonga kipindi kile JK alivyokuwa akiwapa vijinafasi waislamu angalauangalau hata kama kiujumla Wakiristo walikuwa bado ni wengi zaidi kwenye hizo nafasi?
 
Hahahahaaaaq!

Hv huu waraka mbna ww wakristo kule zanzibar tunapata tabu!

Jino kwa jino (mamamamamamamamamamamamamamaaaaaye)
 
Hii sio lazima ajibu Bashiru Ally

1. Kwani Udom hakuna wahadhiri waislamu kwa sasa? Mimi najua wapo wengi nawafahamu.
Kuhamishwa wahadhiri,kwani wamefukuzwa kazi? Acheni utoto ktk mambo ya maana.

2. Waislam hawajaweka Elimu dunia kama kipaumbele chao,nenda kilwa,Pwani yote na miji inayofanana na hiyo hawasomi elimu dunia,dhamira yao kubwa ni kwenda kwa mungu. Mkoa wa Lindi na Mtwara hasa elimu IPO chini sababu wengi ni waislamu(natokea huko)

3. Ukichukua takwimu za wasomi wa nchi hii,utakuta wakristo ni wengi kuliko waislamu,ukiondoa wachache wanaoibuka sasa hivi. Mfano nikiwa chuo kikuu tulikuwa wanafunzi 33 darasani ila waislamu ni 5 tu,nikiwa A level wanafunzi zaidi ya 18000,ila waislamu walikuwa 30% tu,
Kwa takwimu hizi unategemea nini.

4. Halafu Ponda amesahau kuleta na takwimu ya idadi ya waislamu against ya wakristo Tanzania,alichofanya ni kukurupuka tu.

5. Chuo kikuu cha waislamu kipo morogoro lakini ukiangalia udahili pale hukuti mkristo hata mmoja,vyuo vya kikristo wanasoma na waislamu,wakristo hawapigi kelele,ila ingekuwa viceversa ungeona maandamano ya waislamu.

6. Waislamu waache inferiority complex na wachape kazi, tunaishi nao,tunajua wanasisitiza nini zaidi ya elimu dunia.


Mwisho,niseme nimejibu sio kwa kufuata series ya maswali yake.
Ila Naomba yafuatayo:-

1. Idadi ya wakristo against waislamu

2. Idadi ya wasomi wakristo against waislamu.

3. Tuletee idadi ya wahadhiri/wafanyakaxi wa udom waislamu against wakristo.

Ahsante
Ni Mimi Stesheni
Mwananchi
 
Hahahahaaaaq!

Hv huu waraka mbna ww wakristo kule zanzibar tunapata tabu!

Jino kwa jino (mamamamamamamamamamamamamamaaaaaye)

Zanzibar ni nchi, wana serikali yao, wana bunge lao(baraza la wawakilishi), kuna kazi huko Zanzibar hata uwe muislamu wa Tanganyika huwezi pewa!, kwa hiyo wacha Wazanzibari wajisemee wenyewe kwenye mambo ya nchi yao, na sisi huku Tanganyika tujisemee yetu
 
Tujiulize kabla ya uhuru kulikuwa na Seminary za kikristo ngapi na sasa zipo ngapi na shule za umma kabla ya uhuru zilikuwa ngapi na sasa zipo ngapi? Je mitazamo ya dini zetu katika elimu ikoje? Wachina wameendelea sana sababu ya kufanya kazi na sio kuleta mambo ya dini kwenye taasisi za uma, hivi kweli kuna mtu anaweza kuwa na elimu ya kutosha na utaalam akaachwa kuajiriwa kwa ajili ya dini yake?

Binafsi huwa namshangaa sana binadamu anayekuwa na fikri za kikabila, ukanda, rangi na dini tunasahau ya kuwa binadamu wote ni sawa na tumezaliwa katika mfumo unaofanana na damu zetu wote ni nyekundu. Tukianza ubaguzi tutajikuta hata tunaojiona tunafanana hatufanani tena, tutaanza kujitenga wale wenye group O negative la damu nao wataanza kulalamika kwa nini wao ndio wanawajibika kuongezea damu kila mtu, wale wenye group zingine nao watahisi O anawasimanga.
 

Hayo ya Inferiority complex unayajua wewe lakini teuzi za 80% watu wa dini moja siyo jambo la kawaida hilo kuna harufu kali ya udini hapo!

Haiwezekani ubague watu kwa misingi ya dini kisha wakihoji uwape majibu ya nyodo, kuita madai yao ni "utoto", " inferiority complex", "hawajasoma" wala haisaidii.

Teuzi za serikalini hazihitaji watu mamilioni, zinahitaji mamia kadhaa na idadi hiyo Waislamu wanayo ya kutosha tu!.

Pia siku hizi waislamu waliosoma ni wengi, hata Nyerere mwaka 1985 kwenye hotuba yake ya kuaga pale diamond Jubilee ailikiri kuwa Waislamu waliosoma waliongezeka sana kulinganisha na mwaka 1961, Sasa kwa nini watu wa imani moja wawe overrepresented kuliko watu wa imani nyingine, kama siyo udini ni kitu gani?
 
Mkuu, hilo la uwiano ktk teuzi serikalini ni ukweli mtupu. Kwa jamii yenye makundi makubwa mawili ya kiimani, pale inapotokea kundi moja likionekana dhahiri likiwa na teuzi chache mno kulinganisha na lingine, kwa vyovyote vile huwezi kukwepa hisia kama hizi, kwa kuwa kundi kama hilo huku na likitemgwa na hata kukosa "ownership"

Waraka wa Ponda kimantiki ulipaswa kuchukuliwa kama kichocheo cha fikra ktk kutaka kujitathimini yenyewe ktk jambo hilo. Ponda hakutaka kuwa mnafiki bali kupaza sauti ili kile kinachozungumzwa mafichoni kikapate kusikika. Hii ni Tanzania iliyo makazi ya wananchi wote, ijapokuwa serikali yetu haina dini, bali ni lazima iyaangalie kwa umuhimu wa are na yake makundi mbalimbali ya kidini yenye watu wengi ndani ya mifumo yake.

Kundi kubwa la Waisilamu lina wasomi wengi mno, tena wa viwango tofauti. Visitafutwe visingizio ile kukwepa kulizungimzia suala hili kwa uzito wake. Mbona wakati wa utawala wa awamu ya nne, tulishuhudia nyaraka na malalamiko kama hayo kutoka kwa Wakristo ijapokuwa Mzee Kikwete alijitahidi mno kuzingatia uwiano huu?
 
Ujitambui kweli wewe inamana wewe ni muelewa Sana kuliko Samia Suluhu, Majaliwa,
 
Yes, ni vicious circle! Tatizo letu kubwa ni 'mfumo kristo' ambao kwa sehemu kubwa unatufanya tusione dhulma mbalimbali. Ni kama mfumo dume tu unavyofanya kazi. ...inahitaji tafakari kubwa kuweza kuziona dhulma mbalimbali. Ndio sababu hata kiongozi akiwa muislamu, mfumo huo unamfanya asione hizo dhulma. Ni kama ilivyo kwa mfumo dume, hata viongozi wanawake wanajikuta wakitenda kulingana na mfumo unavyotaka.

Sasa badala ya kuwafunga midomo watu wanaweza kutuonesha dhulma hizo na udhaifu wa mfumo uliopo, tungewaacha waseme ili kuweza kufanyia marekebisho. Hata kama hatukubaliani na wanayosema au kuyataka, lakini ni muhimu kusikiliza perspectives zao kwa sababu kuna kitu tutajifunza.

Bahati nzuri nchi yetu imechanganyika sana. Mimi ni mkristo, lakini ninao ndugu wa damu waislamu. Ninaamini watu wengi pia tupo hivyo.

Tuwasikilize wanachosema......kati yake zipo hoja zenye mashiko tu kama tukiamua kusikiliza objectively.
 

Tatizo hamna umoja thus mnaburuzwa,lipeni kisasi October ili kukomesha udhalimu.
 
Ndio watu wa aina yako wapewe vyeo kweli? Umejibu nini hapo. Tafuta data ujue unachoandika.
Ponda ana kesi ya kujibu,kuna sheria ya takwimu ilipitishwa bungeni.

Analo hilo
Jibu swali na sio blabla
Wanaotaka kwenda mbinguni wasomee huko na wanaosomea ajira wasomee huko.
Tutasomana tu.
Soma vizuri nilichoandika mwanzo utaelewa tu. Wewe umesoma tu inferiority complex, mengine hujaona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…