Barua ya wazi kwa Boniface Mwamposa

Barua ya wazi kwa Boniface Mwamposa

The Whistleblower

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2022
Posts
247
Reaction score
434
Kwako mtumishi wa Mungu, nakuomba Tafadhali sana usipuuze andiko langu, hili ni andiko la Mungu mwenyewe.

Wewe hakika ni mtumishi wa Mungu,ni kweli kabisa Mungu alikuita ili ufanye kazi yake, wanaokudharau na kukusimanga ni wa kuonea sana huruma, kwa sababu mimi nina ushahidi wa zaidi ya 100 %,kuwa kweli wewe ni mtumishi wa Mungu.

Niende kwenye hoja ya mada yangu kwako.

Mungu anapokuita shetani huwa anafanya vikao kuzimu ili aharibu kazi ya Mungu, na shetani ana mbinu zaidi ya milioni moja za kuangusha watumishi wa Mungu.

Wewe Mwamposa, shetani anahangaika ili aharibu kazi ya Mungu aliyokupa uifanye, alichokifanya shetani kwako ni kuwaleta watawala wa Tanzania kuanzia Rais hadi wakuu wa mikoa watengeneze ukaribu kwako kwa maslahi yao ya kisiasa.

Walipojua maelfu ya watanzania wanakufuata ili waombewe basi wakaona ni bora waanze kukutumia ili wapate mtaji wa kisiasa.

Yaani uwashawishi watu waichague CCM, Mwamposa achana kabisa na harakati za kisiasa zitakuharibia kazi ya Mungu.

Siyo vibaya wewe kuwaheshimu viongozi wa serikali, lakini habari za siasa kwa chama chochote achana nazo, wewe piga injili na ufungue watu waliofungwa na shetani.

Narudia tena, Mwamposa achana na siasa ,fanya kazi ya Mungu aliyokuitia,muige mzee Mwakasege ,huyu mzee huwezi kumsikia ulimi wake ukiongelea siasa kwa namna yotote ile.

Narudia tena, Mwamposa achana kabisa na siasa,iko siku utaitwa Ikulu (kama alivyowahi kuitwa Gwajima) na utapewa jimbo la kugombea ubunge,hapo ndo itakuwa anguko lako kamili kwenye kazi ya Mungu na utabaki historia.

Shetani hajachoka kukufuatilia ili akuangushe, kwa sababu umeharibu kazi nyingi mno za shetani shetani kwa hiyo ana kisasi kikubwa mno na wewe.

Hiyo madhabahu unayoongoza siyo ya kwako ni ya Mungu,Mungu amekuamini wewe kuisimamia tu, ndo maana inaitwa madhabahu ya Mungu, siyo madhabahu ya Mwamposa, kwa hiyo acha kuichafua madhabahu ya Mungu kwa kukaa unaifanyia kampeni CCM.

Mungu ana watu wemgi mno, anaweza kuinua mwingine kufanya kazi yake endapo utaendelea kumkera.

Watu wanaenda kusali na kupokea uponyaji siyo kusikiliza kampeni za CCM kwenye madhabahu ya Mungu.

Mwamposa achana kabisa na siasa fanya kazi ya Mungu.
ALIYE KARIBU NA MWAMPOSA AMPELEKEE HUU UJUMBE.
 
Kwako mtumishi wa Mungu, nakuomba Tafadhali sana usipuuze andiko langu, hili ni andiko la Mungu mwenyewe.
Wewe hakika ni mtumishi wa Mungu,ni kweli kabisa Mungu alikuita ili ufanye kazi yake,wanaokudharau na kukusimanga ni wa kuonea sana huruma,kwa sababu mimi nina ushahidi wa zaidi ya 100 %,kuwa kweli wewe ni mtumishi wa Mungu.
Niende kwenye hoja ya mada yangu kwako.
Mungu anapokuita shetani huwa anafanya vikao kuzimu ili aharibu kazi ya Mungu,na shetani ana mbinu zaidi ya milioni moja za kuangusha watumishi wa Mungu.
Wewe Mwamposa, shetani anahangaika ili aharibu kazi ya Mungu aliyokupa uifanye ,alichokifanya shetani kwako ni kuwaleta watawala wa Tanzania kuanzia Rais hadi wakuu wa mikoa watengeneze ukaribu kwako kwa maslahi yao ya kisiasa.
Walipojua maelfu ya watanzania wanakufuata ili waombewe basi wakaona ni bora waanze kukutumia ili wapate mtaji wa kisiasa.
Yaani uwashawishi watu waichague CCM, Mwamposa achana kabisa na harakati za kisiasa zitakuharibia kazi ya Mungu.
Siyo vibaya wewe kuwaheshimu viongozi wa serikali, lakini habari za siasa kwa chama chochote achana nazo, wewe piga injili na ufungue watu waliofungwa na shetani.
Narudia tena, Mwamposa achana na siasa ,fanya kazi ya Mungu aliyokuitia,muige mzee Mwakasege ,huyu mzee huwezi kumsikia ulimi wake ukiongelea siasa kwa namna yotote ile.
Narudia tena, Mwamposa achana kabisa na siasa,iko siku utaitwa Ikulu (kama alivyowahi kuitwa Gwajima) na utapewa jimbo la kugombea ubunge,hapo ndo itakuwa anguko lako kamili kwenye kazi ya Mungu na utabaki historia.
Shetani hajachoka kukufuatilia ili akuangushe, kwa sababu umeharibu kazi nyingi mno za shetani shetani kwa hiyo ana kisasi kikubwa mno na wewe.
Hiyo madhabahu unayoongoza siyo ya kwako ni ya Mungu,Mungu amekuamini wewe kuisimamia tu,ndo maana inaitwa madhabahu ya Mungu, siyo madhabahu ya Mwamposa,kwa hiyo acha kuichafua madhabahu ya Mungu kwa kukaa unaifanyia kampeni CCM .
Mungu ana watu wemgi mno, anaweza kuinua mwingine kufanya kazi yake endapo utaendelea kumkera.
Watu wanaenda kusali na kupokea uponyaji siyo kusikiliza kampeni za CCM kwenye madhabahu ya Mungu.
Mwamposa achana kabisa na siasa fanya kazi ya Mungu.
ALIYE KARIBU NA MWAMPOSA AMPELEKEE HUU UJUMBE.
Mwanzo wa andiko lako umesema hili andiko ni la Mwenyezi Mungu cha kushangaza mwisho unasema aliyekaribu na Mwamposa ampelekee huu ujumbe!! Pia ndani ya andiko lako limejaa mambo ya siasa tu kwani Mungu hataki siasa!! Pia vipi Askofu Mwamakula anayehubiri siasa kupitia Chadema?
 
Mwamposa tegemeo lake ni ccm&serikali tu wala siyo mungu

Ova
 
Mwanzo wa andiko lako umesema hili andiko ni la Mwenyezi Mungu cha kushangaza mwisho unasema aliyekaribu na Mwamposa ampelekee huu ujumbe!! Pia ndani ya andiko lako limejaa mambo ya siasa tu kwani Mungu hataki siasa!! Pia Askofu Mwamakula anayehubiri siasa kupitia Chadema?

Binadamu tumeumbiwa kusahau, huyu ni mwenzetu.
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Back
Top Bottom