Barua ya Wazi Kwa Comrade Ally Saleh, Uchaguzi Umekwisha, Yaliyopita Si Ndwele, Tugange Yaliyopo na Yajayo, Pelekeni Majina, Muijenge Zanzibar Yenu!

Barua ya Wazi Kwa Comrade Ally Saleh, Uchaguzi Umekwisha, Yaliyopita Si Ndwele, Tugange Yaliyopo na Yajayo, Pelekeni Majina, Muijenge Zanzibar Yenu!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Hii ni Barua yangu ya Wazi kwa Ndugu yangu mwana fani mwenzangu wa tasnia ya habari na mwanasheria Mwenzangu, Ally Saleh, ambaye kwenye mambo ya Zanzibar, tumetoka naye mbali, toka wakati akiwa reporter wa BBC kule Zanzibar na mimi nikiwa reporter wa DTV ya Dar.

Wakati wa vurugu za Zanzibar za January 2001 kufuatia uchaguzi mkuu wa mwaka 2000, mimi, mwandishi wa gazeti la Majira na Ally Saleh tulionja nae kidogo ladha ya Mwembe Madema kule Zanzibar ile January 2001!. Sijui ni waandishi wangapi wa habari wa bara na Visiwani wamewahi kuionja Mwembe Madema!. Na kwa vile hii ni issue ya Zanzibar, naomba nisizungumzie mambo ya Mwembe Madema, kwa wabara mnaweza msielewe, Mwembe Madema ni nini, ni wapi, na hiyo ladha ya Mwembe Madema tuliyoonja mimi, Ally Saleh na mpiga picha wa gazeti la Majira wa enzi hizo Khalfan Said ni ladha ya kitu gani, hilo tuwaachie wenyewe Wazanzibari ndio wanajua Mwembe Madema ni wapi na kuna nini.

Barua hii ya wazi kwa Ally Saleh ni kufuatia kuisoma barua yake kwa JPM kabla ya uchaguzi na leo nimesoma tena maoni yake kwa kilichotokea Zanzibar kwenye uchaguzi huu.


Kwanza pole sana ndugu yangu, kaka yangu na mwanafani mwenzangu Ally Saleh kwa juhudi zako binafsi kuepusha shari, na poleni ndugu zetu Wazanzibari kwa kilichotokea, ikiwemo kuugharimikia uchaguzi mkuu wenu kwa machozi, jasho na damu, maadam this time ushahidi wa picha na video zipo, I hope this time mtafanya the right thing na sio kuishia kupiga tuu kelele kama uchaguzi wa 2015 ambapo niliuliza

Kupitia matokeo ya NEC ya uchaguzi Mkuu wa 2015, yameonyesha mgombea wa CCM, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hakushinda Zanzibar, aliyeongoza kwa kura za Wanzanzibari kwenye uchaguzi wa rais wa JMT, ni mgombea wa upinzani, Edward Lowassa, na wapiga kura ni wale wale, then by proxy, kama uchaguzi wa Zanzibar usingefutwa, then CCM ingeshindwa na mshindi angekuwa ni Maalim Seif Sharif Hamad

Kutokana na matokeo hayo, then kuna possibility siku zote huwa anashinda lakini hapewi, jee mliwahi kufanya utafiti kwanini mtu wenu huwa anashinda lakini hapewi, ili kabla hamjaingia kwenye uchaguzi mwingine tena, mjiridhishe kuwa hizo sababu sasa hazipo, hivyo this time akishinda atapewa?.

Mimi ni member wa mtandao maarufu wa Jamiiforums na japo nina chama, lakini naandika kama mchambuzi huru, hivyo kabla ya uchaguzi kule jf niliandika bandiko hili

Kwenye bandiko hilo, nilisema
" kama Mwana JF, be the first to know kuwa CCM ndio inakwenda kushinda uchaguzi mkuu huu kwa a landslide victory ya ushindi wa kishindo, kwa pande zote mbili za Muungano!.

Ushindi huu ni kufuatia mimi mwana JF mwenzenu, Pasco Mayalla, nimesikia sauti ndani ya moyo wangu, yaani voices from within, kuwa katika uchaguzi huu, mshindi ni CCM!. Hii voices from within, is never wrong, maana ni sauti yake YEYE mwenyewe!

Kwa upande wa Tanzania Bara, CCM itashinda kwa kishindo kwasababu ya track record ya Magufuli, itaibeba CCM na kushinda kwa kishindo.

Kwa upande wa Zanzibar, kwa mujibu wa katiba, rais wa Zanzibar ni mjumbe wa cabinet ya JMT, Muundo wa serikali ya JMT, hatuna serikali ya mseto, ushindi ni by a simple majority, hata akishinda kwa kura moja, ni mshindi, and the winner takes it all. Hivyo mshindi wa Zanzibar lazima iwe ni CCM!"

Nilimaliza andiko langu kwa maneno haya
"Nawatakia maandalizi mema ya October 28, sio kwenda kuchagua, bali kwenda tuu kuthibisha kilichochaguliwa tayari kwa ajili tuu ya kukamilisha taratibu za mchakato wa kukamilisha uchaguzi, kama ni kuchagua, watu siku nyingi, wameisha chagua mioyoni mwao, tarehe 28 ni kukamilisha tuu taratibu".

Sasa kwa vile hayo yametokea na sio mapya, na uchaguzi umekwisha, uchaguzi mwingine ni 2025, na kwasababu hakuna kitu kingine chochote kinachoweza kufanyika sasa kubadili matokeo, nakushauri, washauri chama chako, hata kama mmedhulumiwa na hamjaridhika na matokeo, ili kuweza kuendelea na mapambano, tumieni kanuni ya " If you can't beat them,
join them", kanuni hii hutumika kwenye vita, ukiona unashindwa au anaelemewa, kuliko kuendelea ku fight and be wiped out, sometimes it's wise to retreat kwenda kujijenga upya, or to surrender and join them. Hivyo natoa wito kwako na chama chako, yaliyopita sii ndwele, kubalini matokeo, join them na kutoa ushirikiano, pelekeni jina la Makamu wa Kwanza wa rais, na majina 2 ya mawaziri kwenye serikali ya Umoja wa Kitaifa, muijenge Zanzibar yenu.

Kwa kuendelea kususa, you have everything to loose and nothing to gain, your will be wiped out completely and buried 6ft under!, hivyo there will be no one at all uchaguzi wa 2025, hivyo ni busara to join them for survival hadi 2025.

By joining them, you'll have everything to gain and nothing to loose, yaliyopita sii ndwele, gangeni yaliyopo na yajayo. The choice is yours.

Na kwa upande wa Zanzibar kwa vile mnachagua mtu na sio chama, na mtu wenu ni Maalim Seif Sharif Hamad, now at 77 years, ushiriki wake uchaguzi huu ndio the grand finale or final finale, mshauri atumie ile kanuni ya "if you can't get what you want, just take what you get", tunajua aliutaka sana urais, lakini akakoseshwa, sasa kilichopo ni u Makamu, mshauri akubali tuu kuwa Makamu at 77 years, he has everything to gain and nothing to loose, na japo mimi sio Mungu, mtu kukataa u Makamu wa rais at 77 years of age, he'll have everything to loose and nothing to gain and he'll be the biggest loser!.

I wish you all the best.

Your Media Comrade, and fellow Learned Brother
Paskali.
 
Sidhani kama Zitto atakuelewa!
Vitu vingine sio issue ya fulani kukuelewa, ni kuangalia na kutanguliza mbele maslahi ya taifa. Kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu ni kuangalia maslahi ya taifa.
Naamini Comrade Zitto hayumo kwenye kundi hili la viongozi nilio wazungumza hapa
p
 
Vitu vingine sio issue ya fulani kukuelewa, ni kuangalia na kutanguliza mbele maslahi ya taifa. Kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu ni kuangalia maslahi ya taifa.
Naamini Comrade Zitto hayumo kwenye kundi hili la viongozi nilio wazungumza hapa
p
Zitto pale ACT wazalendo ni sawa na Mtei pale CHADEMA.
 
Vitu vingine sio issue ya fulani kukuelewa, ni kuangalia na kutanguliza mbele maslahi ya taifa. Kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu ni kuangalia maslahi ya taifa.
Naamini Comrade Zitto hayumo kwenye kundi hili la viongozi nilio wazungumza hapa
p
Hongera kwa analysis nzuri sana
 
Nilimuheshimu sana Pascal miaka iliyopita, Nilimsoma sana na kujifunza vitu vingi sana.

Kwa sasa siwezi kusoma S maandiko yake, yamejaa unafiki,uongo,kujipendekeza nk.

Tumekuonya kuwa umri umekutupa, uteuzi kwako haupo. Acha kujipa kazi ngumu kuliko Watanzania wote.

Zamani tuliamini kila mzee ana Hekima.
 
Mkuu
Nimehisi kama huja address problems
Suala la GNU ipo kikatiba na ACT hawajaipinga.
Hebu vuta picha ndugu yako wa damu ameuwawa kisha anakuja mtu yule anakwambia yaishe twendwe mbele. Ni rahisi kama hivyo KWELI PASCAL
Hapa lazima kuwe na hakikisho la kuto kurudiwa
1.mauwaji na mateso
2.Uchaguzi unaofata uwe huru na jumuiya ya kimataifa ishiriki kufikia suluhisho hilo
3 .walio uwa wawajibishwe
4.waathirika walipwe fidia
Kama CCM hawataki hayo waendeleee kutawala TU .opposition in Zanzibar is here to stay wala sio lazima ruzuku.
Km ACT watakubali bila mageuzi makubwa basi kundi lile alosema Nyerere
Wanasiasa malay.. malay.. wananunulika hawana ajenda wala muelekeo
 
Kama kuna kitu wapinzani watachemsha ni kukubali huu ushauri mfu, ni bora hivyo vyama vife kama uhai wake unategemea kushirikiana na wauaji na wezi wa kura, kuliko kujiunga na watu wa aina hiyo. Na iwapo viongozi watakubali kujiunga na serikali za damu, wajue fika watapoteza uungwaji mkono na wananchi, kwani watakuwa wameamua kubariki umwagaji damu.
 
Naona unatoa wazo kama la Neville Chamberlain kumtaka Wisnton Churchill akae na Hitler wayamalize!

Mawazo na ushauri wako hayasaidii kupatikana kwa Zanzibar yenye heshima bali ni appeasement kwa mfumo ovu ambao unatakiwa uwe fought kwa nguvu zote na kuudismantle siyo kuupa legitimacy!

Appeasement kwa watu na mifumo miovu haitatui tatizo kamwe, inalilea!

Mtu mwenye akili akikupa wazo la kipumbavu na wewe ukalikubali wazo hilo basi atakudharau!

Maalimu kuingia kwenye serikali ya aina hiyo ni kuhalalisha haramu ambayo kimsingi ni haramu ambayo inabidi ipigwe vita iondoke siyo kuilealea ibaki! . Zanzibar sasa hivi inahitaji tume huru ya uchaguzi, na hiyo tume huru ya uchaguzi haipatikani kwa wapinzani kupewa viti viwili vya kuzugia na maalimu kupewa msosi, ale, atulie halafu mambo yaendelee kuwa business as usual. Yaani kila baada ya miaka mitano, wahuni wanapeleka majeshi zanzibar, wanapira haki za wananchi, wanatesa, wanaua, wanabaka halafu baada ya hapo wapinzani wanaingia kwenye serikali haramu.

Maalim alisema, safari hii hawakubali Ukhanithi,akiingia kwenye serikali hiyo CCM watamuona Khanithi.
 
Huu ushauri bado nauona ni mbinu tu za kujaribu kushawishi wapinzani wakubali kuingia na hatimaye kuhalalisha haramu. Chama chako kiliona inafaa ima fa ima wawe peke yao na njama zikapangwa wenye mamlaka wakasimamia ikawa walivyotaka sasa imeonekana bunge linakosa uhalali kikatiba na kikanuni mmeanza kujifanya washauri wa wapinzani. Tuache CCM waendelee kula kibudu.
 
Vitu vingine sio issue ya fulani kukuelewa, ni kuangalia na kutanguliza mbele maslahi ya taifa. Kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu ni kuangalia maslahi ya taifa.
Naamini Comrade Zitto hayumo kwenye kundi hili la viongozi nilio wazungumza hapa
p
Kwa hiyo, Siasa inatoa nafasi uwafanyie washindani wako uhuni kwa Maslahi ya Taifa na haitoa nafasi na wengine washinde kwa kisingizio cha Maslahi ya Taifa?
 
Back
Top Bottom