Barua ya Wazi Kwa Comrade Ally Saleh, Uchaguzi Umekwisha, Yaliyopita Si Ndwele, Tugange Yaliyopo na Yajayo, Pelekeni Majina, Muijenge Zanzibar Yenu!

Barua ya Wazi Kwa Comrade Ally Saleh, Uchaguzi Umekwisha, Yaliyopita Si Ndwele, Tugange Yaliyopo na Yajayo, Pelekeni Majina, Muijenge Zanzibar Yenu!

Atakaerudi na kuunga mkono juhudi za kutaka angalau harufu ya upinzani kuingia kwenye serikali haramu huyo ni mbeba laana na msaidizi wa dhambi walizozichuma CCM.

Labda ipigwe kura ya maoni kwa wana ACT wazalendo wote waishio Zanzibar.

Lipi au kipi kinatafutwa ? Ni wazi Serikali ya Mwinyi haina hatua refu sana itaanza kupata mitihani na kama Magufuli atamsaidia na kumshika mkono,lipo deni la Zanzbar kwa serikali ya Muungano likilipwa hili Mwinyi atavuka.

CCM imeshikwa pabaya hivyo kama ACT viongozi watakuwa wenye tamaa ya fisi na kuingia siku hiohio CCM serikali wataandika bonge la barua kuiarifu dunia kuwa ,ACT wamekubali au wameukubali uchaguzi na matokeo yake na wameingia kwenye kuunda serikali kwa mujibu wa katiba hivyo hatuna shida na hapo ruhusa ya kufungua milango itakuwa wazi na CCM Zanzibar watapeta kirahisi,huku waunga juhudi wakilambwa vichogo,kwani wametupiwa fupa na kulivamia.
 
Vitu vingine sio issue ya fulani kukuelewa, ni kuangalia na kutanguliza mbele maslahi ya taifa. Kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu ni kuangalia maslahi ya taifa.
Naamini Comrade Zitto hayumo kwenye kundi hili la viongozi nilio wazungumza hapa
p
ushauri mzuri,lakni wana zitto wote wako busy kushadadia mabeberu mda huu uli tz iwekewe vikwazo🤔
 
Wanabodi,

Hii ni Barua yangu ya Wazi kwa Ndugu yangu Mwana fani mwenzangu wa tasnia ya habari na mwanasheria Mwenzangu, Ally Saleh, ambaye kwenye mambo ya Zanzibar, tumetoka naye mbali, toka wakati akiwa reporter wa BBC kule Zanzibar na mimi nikiwa reporter wa DTV ya Dar.

Wakati wa vurugu za Zanzibar za January 2001 kufuatia uchaguzi mkuu wa mwaka 2000, mimi, mwandishi wa gazeti la Majira na Ally Saleh tulionja nae kidogo ladha ya Mwembe Madema kule Zanzibar ile January 2001!. Sijui ni waandishi wangapi wa habari wa bara na Visiwani wamewahi kuionja Mwembe Madema!. Na kwa vile hii ni issue ya Zanzibar, naomba nisizungumzie mambo ya Mwembe Madema, kwa wabara mnaweza msielewe, Mwembe Madema ni nini, ni wapi, na hiyo ladha ya Mwembe Madema tuliyoonja mimi, Ally Saleh na mpiga picha wa gazeti la Majira wa enzi hizo Khalfan Said ni ladha ya kitu gani, hilo tuwaachie wenyewe Wazanzibari ndio wanajua Mwembe Madema ni wapi na kuna nini.

Barua hii ya wazi kwa Ally Saleh ni kufuatia kuisoma barua yake kwa JPM kabla ya uchaguzi na leo nimesoma tena maoni yake kwa kilichotokea Zanzibar kwenye uchaguzi huu.

Kwanza pole sana ndugu yangu, kaka yangu na mwanafani mwenzangu Ally Saleh kwa juhudi zako binafsi kuepusha shari, na poleni ndugu zetu Wazanzibari kwa kilichotokea, ikiwemo kuugharimikia uchaguzi mkuu wenu kwa machozi, jasho na damu, maadam this time ushahidi wa picha na video zipo, I hope this time mtafanya the right thing na sio kuishia kupiga tuu kelele kama uchaguzi wa 2015 ambapo niliuliza

Kupitia matokeo ya NEC ya uchaguzi Mkuu wa 2015, yameonyesha mgombea wa CCM, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hakushinda Zanzibar, aliyeongoza kwa kura za Wanzanzibari kwenye uchaguzi wa rais wa JMT, ni mgombea wa upinzani, Edward Lowassa, na wapiga kura ni wale wale, then by proxy, kama uchaguzi wa Zanzibar usingefutwa, then CCM ingeshindwa na mshindi angekuwa ni Maalim Seif Sharif Hamad

Kutokana na matokeo hayo, then kuna possibility siku zote huwa anashinda lakini hapewi, jee mliwahi kufanya utafiti kwanini mtu wenu huwa anashinda lakini hapewi, ili kabla hamjaingia kwenye uchaguzi mwingine tena, mjiridhishe kuwa hizo sababu sasa hazipo, hivyo this time akishinda atapewa?.

Mimi ni member wa mtandao maarufu wa Jamiiforums na japo nina chama, lakini naandika kama mchambuzi huru, hivyo kabla ya uchaguzi kule jf niliandika bandiko hili

Kwenye bandiko hilo, nilisema
" kama Mwana JF, be the first to know kuwa CCM ndio inakwenda kushinda uchaguzi mkuu huu kwa a landslide victory ya ushindi wa kishindo, kwa pande zote mbili za Muungano!.

Ushindi huu ni kufuatia mimi mwana JF mwenzenu, Pasco Mayalla, nimesikia sauti ndani ya moyo wangu, yaani voices from within, kuwa katika uchaguzi huu, mshindi ni CCM!. Hii voices from within, is never wrong, maana ni sauti yake YEYE mwenyewe!

Kwa upande wa Tanzania Bara, CCM itashinda kwa kishindo kwasababu ya track record ya Magufuli, itaibeba CCM na kushinda kwa kishindo.

Kwa upande wa Zanzibar, kwa mujibu wa katiba, rais wa Zanzibar ni mjumbe wa cabinet ya JMT, Muundo wa serikali ya JMT, hatuna serikali ya mseto, ushindi ni by a simple majority, hata akishinda kwa kura moja, ni mshindi, and the winner takes it all. Hivyo mshindi wa Zanzibar lazima iwe ni CCM!"

Nilimaliza andiko langu kwa maneno haya
"Nawatakia maandalizi mema ya October 28, sio kwenda kuchagua, bali kwenda tuu kuthibisha kilichochaguliwa tayari kwa ajili tuu ya kukamilisha taratibu za mchakato wa kukamilisha uchaguzi, kama ni kuchagua, watu siku nyingi, wameisha chagua mioyoni mwao, tarehe 28 ni kukamilisha tuu taratibu".

Sasa kwa vile hayo yametokea na sio mapya, na uchaguzi umekwisha, uchaguzi mwingine ni 2025, na kwasababu hakuna kitu kingine chochote kinachoweza kufanyika sasa kubadili matokeo, nakushauri, washauri chama chako, hata kama mmedhulumiwa na hamjaridhika na matokeo, ili kuweza kuendelea na mapambano, tumieni kanuni ya " If you can't beat them,
join them", kanuni hii hutumika kwenye vita, ukiona unashindwa au anaelemewa, kuliko kuendelea ku fight and be wiped out, sometimes it's wise to retreat kwenda kujijenga upya, or to surrender and join them. Hivyo natoa wito kwako na chama chako, yaliyopita sii ndwele, kubalini matokeo, join them na kutoa ushirikiano, pelekeni jina la Makamu wa Kwanza wa rais, na majina 2 ya mawaziri kwenye serikali ya Umoja wa Kitaifa, muijenge Zanzibar yenu.

Kwa kuendelea kususa, you have everything to loose and nothing to gain, your will be wiped out completely and buried 6ft under!, hivyo there will be no one at all uchaguzi wa 2025, hivyo ni busara to join them for survival hadi 2025.

By joining them, you'll have everything to gain and nothing to loose, yaliyopita sii ndwele, gangeni yaliyopo na yajayo. The choice is yours.
I wish you all the best.

Your Media Comrade, and fellow Learned Brother
Paskali.
Hivi Pasksli bila kukebehi Wazanzibari unajiskia vibaya?
Hivi wewe unastarehe sana kutosha madonda yetu!
Unasema yaliopita wakati unajua mpaka sasa bado wapo vijana wake kwa waume chungu mzima jela na kamatakamata inaendelea hadi Leo
Tafadhali achana na sisi
 
ACT kujiunga SUK Zanzibar ni fursa kwa chama chao kuwa sehemu ya dola na kukikomaza. It's up to them kama wanataka kukomaa au wanataka uanaharakati.

Fursa kama hii angeipata mtu kama Mbowe hata asingejiuliza mara mbili.
 
CCM si ilishinda kwa kishindo kote Bara na Visiwani? Wananchi si wamewakubali wao ndiyo pekee wanastahili kuongoza Tanzania? Sasa kwa nini wanalazimisha wapinzani waingie? Ondoa huo ujinga wa serikali ya mseto maana wananchi wameukataa kupitia kura, huku Bara futa hivyo viti maalum wabaki wapiga makofi bungeni peke yao. Au mimi ndiyo sielewi, kwa nini sisiemu wanahangaika na wapinzani waliokataliwa?
 
Nikimuangalia seif ni mkomavu kisiasa yupo tayari kwa maslahi mapana ya nchi ila haya mafisi kenda machogo huku bara ndio tatizo!
 
Kama marehemu Mloo angekuwepo siasa za Zanzibar zingekuwa zimebalance matokeo ya sasa ni kutokana na ulimbukeni wa Seif.

Kitendo cha yeye kugoma na kuwazuia wawakilishi wake kwenye serikali iliyopita ndio kiliwapa mwanya ccm kuweka sheria za kuwasaidia wao lakini angekubali kushirikiana nao angeweza kuzuia njama zao.

Seif amekosa mtu wa kumwambia ukweli ndani ya chama chake badala yake kila anachoamua hata kama si sahihi wanakifuata na hayo ndio matokeo waliyoyapata.
 
ACT kujiunga SUK Zanzibar ni fursa kwa chama chao kuwa sehemu ya dola na kukikomaza. It's up to them kama wanataka kukomaa au wanataka uanaharakati.

Fursa kama hii angeipata mtu kama Mbowe hata asingejiuliza mara mbili.
Zanzibar upizani ulisha komaa kisiasa na kiuongozi. Suala la uwanaharakati rabda bara.

Mpaka inawekwa SUK ndani ya katiba CCM walisha jua kuwa they are facingi strong and organazed opposition in zanzibar.
Ccm walisha timiza malengo ya kunyakua dola Znz sasa wanataka legitimacy tu.

Yeyeto atakae wapa bure bila political cost .hata akiwa maalim atageuzwa km lipumba kwenye siasa za Zanzibar.

Kama ni fursa ni hukoo si zenj
 
Kama marehemu Mloo angekuwepo siasa za Zanzibar zingekuwa zimebalance matokeo ya sasa ni kutokana na ulimbukeni wa Seif.
Kitendo cha yeye kugoma na kuwazuia wawakilishi wake kwenye serikali iliyopita ndio kiliwapa mwanya ccm kuweka sheria za kuwasaidia wao lakini angekubali kushirikiana nao angeweza kuzuia njama zao.
Seif amekosa mtu wa kumwambia ukweli ndani ya chama chake badala yake kila anachoamua hata kama si sahihi wanakifuata na hayo ndio matokeo waliyoyapata.
Viti kwenye baraza la wawakilishi ni issue ya nani katangazwa na tume.
Mtaji wa kisiasa ni watu mkuu sio guns and tanks .
Sisiem km hawataki fair ground basi si washashika tayar na wajenge nchi sasa.
 
ACT kujiunga SUK Zanzibar ni fursa kwa chama chao kuwa sehemu ya dola na kukikomaza. It's up to them kama wanataka kukomaa au wanataka uanaharakati.

Fursa kama hii angeipata mtu kama Mbowe hata asingejiuliza mara mbili.
Rejea 2015 - 2020 Nani alikua SUK na Sasa yupo wapi?

Hakuna chakukomaza pale unawekwa ule tu Wala hauna kazi yoyote
 
Back
Top Bottom