Barua ya Wazi Kwa Comrade Ally Saleh, Uchaguzi Umekwisha, Yaliyopita Si Ndwele, Tugange Yaliyopo na Yajayo, Pelekeni Majina, Muijenge Zanzibar Yenu!

Atakaerudi na kuunga mkono juhudi za kutaka angalau harufu ya upinzani kuingia kwenye serikali haramu huyo ni mbeba laana na msaidizi wa dhambi walizozichuma CCM.

Labda ipigwe kura ya maoni kwa wana ACT wazalendo wote waishio Zanzibar.

Lipi au kipi kinatafutwa ? Ni wazi Serikali ya Mwinyi haina hatua refu sana itaanza kupata mitihani na kama Magufuli atamsaidia na kumshika mkono,lipo deni la Zanzbar kwa serikali ya Muungano likilipwa hili Mwinyi atavuka.

CCM imeshikwa pabaya hivyo kama ACT viongozi watakuwa wenye tamaa ya fisi na kuingia siku hiohio CCM serikali wataandika bonge la barua kuiarifu dunia kuwa ,ACT wamekubali au wameukubali uchaguzi na matokeo yake na wameingia kwenye kuunda serikali kwa mujibu wa katiba hivyo hatuna shida na hapo ruhusa ya kufungua milango itakuwa wazi na CCM Zanzibar watapeta kirahisi,huku waunga juhudi wakilambwa vichogo,kwani wametupiwa fupa na kulivamia.
 
ushauri mzuri,lakni wana zitto wote wako busy kushadadia mabeberu mda huu uli tz iwekewe vikwazo🤔
 
Hivi Pasksli bila kukebehi Wazanzibari unajiskia vibaya?
Hivi wewe unastarehe sana kutosha madonda yetu!
Unasema yaliopita wakati unajua mpaka sasa bado wapo vijana wake kwa waume chungu mzima jela na kamatakamata inaendelea hadi Leo
Tafadhali achana na sisi
 
ACT kujiunga SUK Zanzibar ni fursa kwa chama chao kuwa sehemu ya dola na kukikomaza. It's up to them kama wanataka kukomaa au wanataka uanaharakati.

Fursa kama hii angeipata mtu kama Mbowe hata asingejiuliza mara mbili.
 
CCM si ilishinda kwa kishindo kote Bara na Visiwani? Wananchi si wamewakubali wao ndiyo pekee wanastahili kuongoza Tanzania? Sasa kwa nini wanalazimisha wapinzani waingie? Ondoa huo ujinga wa serikali ya mseto maana wananchi wameukataa kupitia kura, huku Bara futa hivyo viti maalum wabaki wapiga makofi bungeni peke yao. Au mimi ndiyo sielewi, kwa nini sisiemu wanahangaika na wapinzani waliokataliwa?
 
Nikimuangalia seif ni mkomavu kisiasa yupo tayari kwa maslahi mapana ya nchi ila haya mafisi kenda machogo huku bara ndio tatizo!
 
Kama marehemu Mloo angekuwepo siasa za Zanzibar zingekuwa zimebalance matokeo ya sasa ni kutokana na ulimbukeni wa Seif.

Kitendo cha yeye kugoma na kuwazuia wawakilishi wake kwenye serikali iliyopita ndio kiliwapa mwanya ccm kuweka sheria za kuwasaidia wao lakini angekubali kushirikiana nao angeweza kuzuia njama zao.

Seif amekosa mtu wa kumwambia ukweli ndani ya chama chake badala yake kila anachoamua hata kama si sahihi wanakifuata na hayo ndio matokeo waliyoyapata.
 
ACT kujiunga SUK Zanzibar ni fursa kwa chama chao kuwa sehemu ya dola na kukikomaza. It's up to them kama wanataka kukomaa au wanataka uanaharakati.

Fursa kama hii angeipata mtu kama Mbowe hata asingejiuliza mara mbili.
Zanzibar upizani ulisha komaa kisiasa na kiuongozi. Suala la uwanaharakati rabda bara.

Mpaka inawekwa SUK ndani ya katiba CCM walisha jua kuwa they are facingi strong and organazed opposition in zanzibar.
Ccm walisha timiza malengo ya kunyakua dola Znz sasa wanataka legitimacy tu.

Yeyeto atakae wapa bure bila political cost .hata akiwa maalim atageuzwa km lipumba kwenye siasa za Zanzibar.

Kama ni fursa ni hukoo si zenj
 
Viti kwenye baraza la wawakilishi ni issue ya nani katangazwa na tume.
Mtaji wa kisiasa ni watu mkuu sio guns and tanks .
Sisiem km hawataki fair ground basi si washashika tayar na wajenge nchi sasa.
 
ACT kujiunga SUK Zanzibar ni fursa kwa chama chao kuwa sehemu ya dola na kukikomaza. It's up to them kama wanataka kukomaa au wanataka uanaharakati.

Fursa kama hii angeipata mtu kama Mbowe hata asingejiuliza mara mbili.
Rejea 2015 - 2020 Nani alikua SUK na Sasa yupo wapi?

Hakuna chakukomaza pale unawekwa ule tu Wala hauna kazi yoyote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…