Barua ya Wazi kwa familia ya Ali Hassan Mwinyi

Barua ya Wazi kwa familia ya Ali Hassan Mwinyi

Mzee Mwinyi hana kosa lote kuhusu hili suala,ni kosa la madhalimu wa CCM
Kosa analo kwa kuimba mapambio kwa watawala wa CCM huko majukwaani wewe umemsikia na mimi nimemsikia na wote tumemsikia na Allah pia amemsikia yote hayo ili mwane abebwe kwa mbeleko utawala wa Zanzibar
 
Hebu ripotini bas kinachoendelea huko maana mie naona amani tu..kama kuna shar semeni na ushahid
 
Tusiwachague akina Mwinyi tena wametawala mda mrefu na hakuna mabadiliko.
 
Kwani familia zao zinaishia wapi kwa nn tunalia lia hapa inabidi tulie ndugu zake naye wakamatwe ili maumivu yawe reciprocal
 
Familia ya Mwinyi haihusiki. Wazanzibari watampigia kura au kutompigia kura Hussein mwinyi na siyo familia ya Mwinyi. Ungeeleza namna gani hii ni dulma dhidi ya Wazanzibari kwa kutumia rational arguments na siyo arguments based on emotions and/or religious reasoning.
 
Tulia mnyolewe, Zanzibar imekombolewa kwa damu na jasho. Hatutaki utumwa urudi. Mwambie babu yenu alee wajukuu
 
Itendee haki nafsi yako kesho ni siku maalumu ya kulipiza kisasi kwa mabaya yote uliyotendewa na Utawala huu dhalimu.Weka tiki (vema) kwenye jina la mwisho la mgombea, hakikisha hiyo vema ama tiki yako haitoki nje ya kibox (kisanduku). Pia usitoboe macho kwa mgombea number moja kwa hasira maana kufanya hivyo utakuwa umeharibu kura yako.
 
Mmewachochea vijana wa watu waende kulivamia gari lililo beba vifaa vya NEC tena gari linalo lindwa na polisi alafu mlivyo wanafiq wameumia mna anza kuilaumu serikali.
 
Mmewachochea vijana wa watu waende kulivamia gari lililo beba vifaa vya NEC tena gari linalo lindwa na polisi alafu mlivyo wanafiq wameumia mna anza kuilaumu serikali.
Wapuumbaaaf Sana hao..wametumwa na wakoloni waje watugawanye ili waweze kututawala...wanaona wivu maendeleo tunayoyafanya
 
Kwenu Familia ya Ali Hassan Mwinyi

1. Mzee Ali Hassan Mwinyi
Ulijiuzulu miaka ya 1970 kwa sababu ya mauaji ya watu wasio na hatia wakiwa katika mikono ya dola, leo napenda nikufahamishe mzee wetu kuwa kuna wananchi wa Zanzibar, wasio na hatia wanauawa Zanzibar bila haki, bila sababu za msingi isipokuwa tu ili mwana aliyetoka katika viuno vyako awe mtawala bila ridhaa ya wananchi wa Zanzibar.

Mzee Mwinyi, Ule uungwana ambao Watanzania walikufahamia, leo hii napenda upate taarifa kuwa kuna Wazanzibar leo damu zao zinagusa ardhi pasi na haki ili tu mwanao awe mtawala.

Umefanya nini mzee wetu mzee Mwinyi kuzuia dhulma hii ya watu wasio na hatia?. Utamueleza nini ALLAH wewe mzee wetu kwa kubariki na kushiriki kumuandalia mwanao utawala huko Zanzibar kwa kujitia upofu, kujisogeza karibu na watawala wa sasa, kuimba mapambio ili tu mwanao awe mtawala wa huko?

Mzee wetu mzee Mwinyi utawala uliopatikana kwa damu za watu kumwagika utaisaidiaje familia yako hapa duniani na ahera?

Nimekuandikia haya kwa sababu Hussein ni mwanao, laiti ungemkanya kuwa jambo analoshiriki lina viashiria vyote vya dhulma na hivyo aache angekusikiliza.

Lakini sasa itasaidia nini mnaswali, mnafunga, mnaenda kuhijji Makka lakini mwanao anashiriki dhulma ya waziwazi?

2. Kwako Hussein Mwinyi
Mwenyezi Mungu anasema kwenye Qur'an kuwa "Inna Llaha la yuflihu dhalimuun", Ikimaanisha hakika ya Mwenyezi Mungu hawafanyi madhalimu kuwa ni wenye kufaulu. Hebu tusemezane Hussein, Uko tayari damu kiasi gani ya Wananchi wasio na hatia wa Zanzibar imewagike ilimradi tu uwe raisi?

Uraisi una faida gani kwako kama ili uufikie lazima upande miili ya wananchi wa Zanzibar waliolazwa barabarani kwa risasi?

3. Kwako Abdullah na Abbasi Mwinyi
Mmemshauri nini Mzee wenu na Kaka yenu aachane na Uraisi huu unaoonekana umejaa damu za Wazanzibar zisizo ba hatia?
Je mko tayari familia yenu ikumbukwe na Watanzania na Wazanzibari kama familia ya dhulma?

Je mlimshauri kaka yenu aachane na jambo hili ambalo kimsingi linakwenda kumpa madhambi makubwa kwa kushiriki kwake kwenye dhulma ya kutisha?

Nyinyi kama familia mna shida gani, kama Majumba mnajengewa, kama pensheni ya mzee iko palepale, asilimia 80% ya mshahara wa rais wa sasa anapata. Sasa kutaka madaraka yote hata kutojali uhai wa wananchi wa Zanzibar mnatafuta nini?

4. Kwako mama yetu Sitti Mwinyi
Mama, Wazanzibar wanakufa mama, wanapigwa risasi, watu wanakua wajane, watu wanapoteza mama, baba zao huko Zanzibar, kwa sababu mwanao Hussein anataka madaraka kwa gharama yoyote!

Mama Umechukua hatua gani kumwambia mwanao aachane na jambo lenye dhulma ndani yake?
Ufalme na mamlaka utamsaidia nini kama ili kuufikia shuruti damu za watu zimwagike?

Mama ukweli ni kuwa mwanao hakubaliki Zanzibar, ni nguvu tu ya dhulma inatumika ili kumsimika madarakani.
Mama mwambie Hussein aachane na biashara hii ya uraisi si njema kwake, si njema kwa sababu njia anayopita imejaa mateso, manyanyaso, dhulma ya kutisha kwa watu waz Zanzibar.

Nimalizie kwa kuwakumbusha ndugu zangu wa familia ya Mzee Mwinyi

Allah anasema katika Qur'an tukufu
"Laa Tudhlim walaa tudhlmuun"
Maana yake Msidhulumu na wala msidhulumiwe

Sasa ni jukumu lenu enyi familia ya Mwinyi kujipima na kuona kama ndugu yenu Hussein Mwinyi anashiriki katika dhulma dhidi ya Wazanzibar na mjiangalie dhima yenu mbele ya ALLAH ni ipi, maana mtaulizwa, mlikuwa wapi wakati dhulma ikifanywa na mmoja wa wana familia yenu akishiriki kikamilifu na nyie mlifanya nini kuizuia? !

Nimefikisha kwenu!
Zanzibar ndo chanzo cha mitandao kuzimwa. Tungeyaona ya zanzibar basi bara tungeitikia
 
Ukubwa ni mtamu jamani, mwinyi hawezi sikia lolote kwa sasa ilimradi mwanae ashinde tu. Hussein mwenyewe alikua anasubiri miaka yote hii halafu leo mnataka aachie. Zanzibar ina wenyewe bora mtulizane dawa iingie
 
Back
Top Bottom