Barua ya Wazi kwa Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

Wazo la kabwela

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2013
Posts
1,901
Reaction score
1,511
Barua ya Wazi kwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

Mheshimiwa Mkuu wa Chuo,
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,

Kwa heshima na taadhima, napenda kuchukua fursa hii kwa niaba ya wanafunzi wa kitivo cha elimu kukupongeza kwa dhati kwa kuteuliwa kwako kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Uteuzi wako ni ishara ya imani kubwa waliyonayo viongozi na jamii ya kielimu juu ya uongozi wako thabiti, hekima na maono chanya kwa maendeleo ya elimu ya juu nchini. Tunakuombea mafanikio mema katika kutekeleza majukumu yako.

Hata hivyo, sambamba na pongezi hizi, napenda kwa unyenyekevu mkubwa kuwasilisha malalamiko ya wanafunzi wa kitivo cha elimu tunaosoma shahada za uzamili na uzamivu kuhusu changamoto sugu ya ucheleweshaji wa kazi za utafiti unaofanywa na baadhi ya wasimamizi. Wasimamizi hawa wamekuwa wakichelewesha kwa makusudi kabisa kupitia kazi za wanafunzi, kuchelewa kutoa mrejesho au hata kutotoa majibu kwa mawasiliano ya mara kwa mara kutoka kwa wanafunzi.

Tabia hii isiyo ya kitaaluma imekuwa ikiwavunja moyo wanafunzi, kuwachelewesha kuhitimu kwa muda uliopangwa, na hata kuleta msongo wa mawazo miongoni mwao. Kwa mtazamo wetu, ucheleweshaji huu si wa bahati mbaya tena, bali ni wa makusudi, jambo linalodhoofisha lengo la chuo la kuwahudumia wanafunzi kwa njia ya haki na kwa wakati.
Mheshimiwa Mkuu wa Chuo, kwa kuzingatia dhamira yako ya kuboresha elimu, tunapendekeza hatua zifuatazo:
1. Kuweka miongozo yenye muda maalum wa kupokea, kupitia na kujibu kazi za wanafunzi.
2. Kuwabana wasimamizi kwa kuweka mfumo wa tathmini ya utendaji wao unaoshirikisha mrejesho wa wanafunzi.
3. Kuwepo kwa chombo maalum cha kushughulikia malalamiko ya wanafunzi kwa haraka na kwa siri.
4. Kuchukua hatua za kinidhamu kwa msimamizi yeyote atakayekiuka kwa makusudi majukumu yake.

Tunaamini chini ya uongozi wako mpya, matatizo kama haya yatapatiwa suluhisho la kudumu kwa ajili ya maendeleo ya elimu na ustawi wa wanafunzi wote.
NI SISI WAHANGA WA KITIVO CHA ELIMU CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA
 
Hahaha siyo chuo kikuu huria tu ni kote. Kuna watu walishasoma miaka 7 masters pale chuo cha ustawi wa jamii kijitonyama. Hayo yalifanyika huku wakuu wa chuo wakiwepo na wanadunda tu kwenye magari yao na viyoyozi tena waliosoma ULAYA na AMERIKA.
Mmoja alishawahi kuniambia HAWA CHADEMA wanaongea sana. Wakati wa JPM Kwa bahati mbaya akapewa kuwa kamishna wa ustawi wa jamii.
Mtu yule alifika pale Dodoma akawahamisha watu wote aliowakuta pale akabaki na timu yake. Akasema siyo STAWI TENA NI MAENDELEO YA JAMII.
AKARUDISHWA DAWATINI.
SASA YUPO HAPO OPEN ANASUBIRI KUSTAAFU MASHAVU YAMEMTUNA KWA KIHORO.
DR UPO? MBONA HUJATUAMBIA KWAMBA UPO OPEN BAADA YA KUONDOSHWA KWA AIBU HAPO DODOMA MZEE???
 
Watanzania wengi ni wavivu, fikra hohehahe, hawana utu na wanaroho mbaya sana.

Ukikutana na msomi mwenye sifa hizo una bahati mbaya sana.
 
Pale mwanafunzi anapomlaumu Supervisor,basi na yeye mwanafunzi ahakikishe anafanyia kazi yale yote anayoambiwa na Supervisor wake..
Wanafunzi wengi sisi tumejaa lawama sana kuliko uhalisia wa mambo..
 
Barua ya Wazi kwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

Mheshimiwa Mkuu wa Chuo,
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,

Kwa heshima na taadhima, napenda kuchukua fursa hii kwa niaba ya wanafunzi wa kitivo cha elimu kukupongeza kwa dhati kwa kuteuliwa kwako kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Uteuzi wako ni ishara ya imani kubwa waliyonayo viongozi na jamii ya kielimu juu ya uongozi wako thabiti, hekima na maono chanya kwa maendeleo ya elimu ya juu nchini. Tunakuombea mafanikio mema katika kutekeleza majukumu yako.

Hata hivyo, sambamba na pongezi hizi, napenda kwa unyenyekevu mkubwa kuwasilisha malalamiko ya wanafunzi wa kitivo cha elimu tunaosoma shahada za uzamili na uzamivu kuhusu changamoto sugu ya ucheleweshaji wa kazi za utafiti unaofanywa na baadhi ya wasimamizi. Wasimamizi hawa wamekuwa wakichelewesha kwa makusudi kabisa kupitia kazi za wanafunzi, kuchelewa kutoa mrejesho au hata kutotoa majibu kwa mawasiliano ya mara kwa mara kutoka kwa wanafunzi.

Tabia hii isiyo ya kitaaluma imekuwa ikiwavunja moyo wanafunzi, kuwachelewesha kuhitimu kwa muda uliopangwa, na hata kuleta msongo wa mawazo miongoni mwao. Kwa mtazamo wetu, ucheleweshaji huu si wa bahati mbaya tena, bali ni wa makusudi, jambo linalodhoofisha lengo la chuo la kuwahudumia wanafunzi kwa njia ya haki na kwa wakati.
Mheshimiwa Mkuu wa Chuo, kwa kuzingatia dhamira yako ya kuboresha elimu, tunapendekeza hatua zifuatazo:
1. Kuweka miongozo yenye muda maalum wa kupokea, kupitia na kujibu kazi za wanafunzi.
2. Kuwabana wasimamizi kwa kuweka mfumo wa tathmini ya utendaji wao unaoshirikisha mrejesho wa wanafunzi.
3. Kuwepo kwa chombo maalum cha kushughulikia malalamiko ya wanafunzi kwa haraka na kwa siri.
4. Kuchukua hatua za kinidhamu kwa msimamizi yeyote atakayekiuka kwa makusudi majukumu yake.

Tunaamini chini ya uongozi wako mpya, matatizo kama haya yatapatiwa suluhisho la kudumu kwa ajili ya maendeleo ya elimu na ustawi wa wanafunzi wote.
NI SISI WAHANGA WA KITIVO CHA ELIMU CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA
unapoteza muda njia rahisi ya upata masters ana phd ndani ya muda mfupi ni kupata scholarship nje ya nchi nimekutana na Mtanzania ana Phd ya Ux design ana miaka 29 na aliipata akiwa na miaka 27 kaajiriwa kama professoor huku ujerumani.
 
90% wapo hivyo. Fikiria mtu anakuwa supervisor halafu hapokei cmu ya mwanafunzi anayemsimamia???
Anakushikilia kwa miaka mitatu mpaka mitano bila hata huruma yoyote kuwa unapoteza fedha.

Hii ni roho mbaya tu hakuna tafsiri nyingine.
 
Mkuu hakuna mtu anayawaza hayo. Kijana mmoja alishikilia kazi yangu kwa muda mrefu sana. Siku moja namfuata ofsini baada ya kumpigia bila mafanikio na email nyingi bila majibu siku moja nikaenda ofsini kwake bila taarifa namkuta yupo ofsini na mwanafunzi wa diploma tena wa kike wakiongea ya kawaida kama vile hakuna kitu.
Ah umekuja kazi yako sijaisoma unajua nipo bize sana. Wakati anatongoza mke wa mtu???
 
unapoteza muda njia rahisi ya upata masters ana phd ndani ya muda mfupi ni kupata scholarship nje ya nchi nimekutana na Mtanzania ana Phd ya Ux design ana miaka 29 na aliipata akiwa na miaka 27 kaajiriwa kama professoor huku ujerumani.
Tatizo kupata sasa
 
Wanafunzi wenyewe mnaweza kuchelewa kuhitimu mnakaa hadi miaka 7 kisa ubize au ada kusuasua sasa wakufunzi kuchelewesha kidogo tu imeshaandikwa na barua. Mngeenda campus kama mlikuwa na haraka, wakufunzi waliaathiriwa na mienendo ya usomaji wa wanafunzi wao.
 
Ni vizuri misingi ya taaluma ifuatwe na iwe na muda katika utekelezaji, kama matokeo yanatakiwa yatoke ndani ya siku 3, na iwe hivyo.
Changamoto inawezekana iko kwa wakufunzi kutokupenda kazi zao.
 
Umeongea ukweli kabisa.Wanafunzi sisi tunafanya mambo ilmradi liende tu,sasa supervisor anataka mtu aive uandishi kazi yake anaikagua na kutoa marekebisho ila mwanafunzi hayafanyii kazi..
 
Tusihukumu wa upande mmoja... Maana tuko sisi wengine supervisor anashikilia kazi yako hata kwa miezi mitatu mnne... Inakera... Kazi yake ni kufanyia kazi tafiti zetu na ndio maana tunalipa ada tena kwa wakati... Kama anaona kazi yangu hairidhishi si ananiambia tuu then narekebisha... Mbona vyuo vya private hawana huu uhuni???
 
Wanafunzi wenyewe mnaweza kuchelewa kuhitimu mnakaa hadi miaka 7 kisa ubize au ada kusuasua sasa wakufunzi kuchelewesha kidogo tu imeshaandikwa na barua. Mngeenda campus kama mlikuwa na haraka, wakufunzi waliaathiriwa na mienendo ya usomaji wa wanafunzi wao.
Achana na hao ambao wanachelewa kwa sababu zao binafsi ... Hebu fikiria sisi tunaokwamishwa .... Kumbuka hakuna mwanafunzi aliyesimama kusoma kwa matakwa yake anayelalamika ... Tunaelalamika ni sisii tunaokwamishwa fikiria mtu unasoma masters kwa miaka 5 hadi 7 ni haki kweli???
 
Umeongea ukweli kabisa.Wanafunzi sisi tunafanya mambo ilmradi liende tu,sasa supervisor anataka mtu aive uandishi kazi yake anaikagua na kutoa marekebisho ila mwanafunzi hayafanyii kazi..
Mwanafunzi asipofanyia kazi, tatizo ni lake.
 
Hahaha siyo chuo kikuu huria tu ni kote. Kuna watu walishasoma miaka 7 masters pale chuo cha ustawi wa jamii kijitonyama. Hayo yalifanyika huku wakuu wa chuo wakiwepo na wanadunda tu kwenye magari yao na viyoyozi tena waliosoma ULAYA na AMERIKA.
Mmoja alishawahi kuniambia HAWA CHADEMA wanaongea sana. Wakati wa JPM Kwa bahati mbaya akapewa kuwa kamishna wa ustawi wa jamii.
Mtu yule alifika pale Dodoma akawahamisha watu wote aliowakuta pale akabaki na timu yake. Akasema siyo STAWI TENA NI MAENDELEO YA JAMII.
AKARUDISHWA DAWATINI.
SASA YUPO HAPO OPEN ANASUBIRI KUSTAAFU MASHAVU YAMEMTUNA KWA KIHORO.
DR UPO? MBONA HUJATUAMBIA KWAMBA UPO OPEN BAADA YA KUONDOSHWA KWA AIBU HAPO DODOMA MZEE???
Duh miaka7 masters huku ujerumani masters ni 1.5 years na hapo inategemea juhudi zako. Kama ukikaza sana unamaliza masters ndani ya mwaka mmoja. Watu hawapo serious aisee.
 
Back
Top Bottom