Pre GE2025 Barua ya wazi kwa mheshimiwa ex mayor wa ubungo na mwenyekiti wa chadema kanda ya Pwani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
CDM wanasema wao ni demokrasia wamefanya uchaguzi mzuri kabisa na team ya TAL imeshinda kinyongo cha nini?? cha mhimu mtulie mjenge chama chenu acheni mambo meengi wengi wenu bila cdm hata wewe boni yai hutakua wa maana ndani ya ccm nakuambia ukweli hamjui tu..NJoo ccm uone kama utaongea kitu usikizwe!! mmeshindwa kuvali yaishe kama hamtaki anzeni kwenda chauma
 
Tuhuma zozote nzito kama hizi ushahidi mwanana ni muhimu sana
kwenye siasa huwa hatuhitaji water tight evidence kuthibitisha jambo. balance of probability inatosha. Kwa taifa la hovyo kama Tz rushwa na ufisadi sio tuhuma kubwa kama unavyotaka kumaanisha. Vinginevyo kuna majitu mengi tu yangekuwa jela saivi.
USHAURI: ondoeni mioyo yenu kwa Mbowe, mwenyekiti wa chama sasa ni Lissu, tumuunge mkono.
 


Acheni uwongo. Mbowe alifanyiwa nini na Lisu? Kwa kusemwa vibaya, naamini Lisu alisemwa vibaya kuliko alivyosemwa Mbowe. Lisu si ndiye aliambiwa kuwa ĥawezi kuwa hata kiongozi wa nyumba 10? Si ndiye aliambiwa ni mropokaji? Si ndiye aliambiwa eti hata kuteuliwa kuwa mgombea Urais, ilikuwa kwa sababu alifanana kwa tabia na Hayati?

Ukiwa mtu mwenye hekima, kauli za hovyo wakati wa uchaguzi unazipuuza maana watu wengine hawana uwezo wa kushawishi waoiga kura bila ya kutoa kauli za kuwabeza wapinzani wao.
 

Kama huyu Rangai aamini katika box la kura na kuendelea itumikia Chadema, then sisi tunajua hafai maana ni kwa Ccm ki falsafa, wana mageuzi uamini kwenye democrasia
 
Ndio maana mm sipigagi kura. Labda atokee makenga wa Tanganyika. Hawa wapinzani wapo kupiga hela tu Tanzania. Wakizibiwa mirija ya hela wananuna. Mtu anatangaza maandamano alafu siku moja kabla yeye anapelekwa lockup sehemu salama ili nyie mfanywe chambo watoto wenu waumizwe.
 
Ila mwamba alikuwa na mvuto flan hivi pale CDM.....Yani chama kilikuwa oinaonekana kina standard flan hivi...

Ila Sasa hivi ni vurugu tuu
Mwamba alikuwa kiongozi,akiongea watu wanatafakari hata wiki,sasa hivi Kiongozi anaongea saa hiyohiyo watu wanasahau
 
Kuna wakati unaongea point 💪
 
Tusisahau pia kuwa Boniface alikuwa mhesabu kura za Mbowe, nadhani maumivu yalianzia pale aliona live. Sasa ni wakati wa kuishi demokrasia wanayohubiri kila mara.

Tusisahau haya maumivu yapo kwa Mbowe pia, alitumia hekima kukubali matokeo na akachukua point 3 za mwanademokrasia, ila ukweli ni alipigwa chini baada ya miaka za ya 20.
 
Siasa chafu alizofanya Lisu na team yake dhidi ya team Mbowe yale majeraha kupona sio rahisi

Kuna vidonda vya kawaida na donda ndugu

Bon yai alichofanya ni sahihi ku block kabisa simu nk za wahuni

Tuwe fair Mbowe alichofanyiwa na Lisu sicho kabisa

Mbowe kapigwa kwenye sanduku la kura, tena Boniface akiwa msimamizi wake, kuhusu kampeni timu ya Mbowe hawakuwa na hoja za ushawishi sana, na public haikuwa upande wao, timu Lissu hija ziliwabeba na umma pia.

Na ukiwa kwenye kampeni ni kusema madhaifu ya mpinzani wako, na ndivyo Lissu alivyofanya.

Chadema nje ya chaguzi wanazopambana na CCM, hawakuwahi kuwa na chaguzi za ndani zenye ushindani kama hizi, ndio maana kila kitu kimekuwa kama kipya kwao, na ndio maana maumivu ni makubwa.
 
Freeman Anaipenda sana Chadema, Atakuja kuwasaidia wakihitaji msaada wake, hajawahi kuwa na kinyongo
Kwa katiba ya Chadema, anakuwa mjumbe wa kudumu wa kamati kuu ya chama, yeye bado ni sehemu ya chama ni mwanachama. Labda yeye aamue kukimbia wajibu wake.
 
Yaani nyie maccm mnataka kuifundisha chadema jinsi ya kuendesha chama?
Kama ni kuwafundisha ufisadi sawa, kwa sababu hiyo ndiyo fani mliyobobea.
Sina chama cha siasa. Hata hivyo, nina uhuru wa kushauri pale ambapo naona inafaa. Kwa mwenendo huu, SSH kashashinda uchaguzi, CHADEMA ijikite kwenye uchaguzi wa madiwani na wabunge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…