Pre GE2025 Barua ya wazi kwa mheshimiwa ex mayor wa ubungo na mwenyekiti wa chadema kanda ya Pwani

Pre GE2025 Barua ya wazi kwa mheshimiwa ex mayor wa ubungo na mwenyekiti wa chadema kanda ya Pwani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
CDM wanasema wao ni demokrasia wamefanya uchaguzi mzuri kabisa na team ya TAL imeshinda kinyongo cha nini?? cha mhimu mtulie mjenge chama chenu acheni mambo meengi wengi wenu bila cdm hata wewe boni yai hutakua wa maana ndani ya ccm nakuambia ukweli hamjui tu..NJoo ccm uone kama utaongea kitu usikizwe!! mmeshindwa kuvali yaishe kama hamtaki anzeni kwenda chauma
 
Tuhuma zozote nzito kama hizi ushahidi mwanana ni muhimu sana
kwenye siasa huwa hatuhitaji water tight evidence kuthibitisha jambo. balance of probability inatosha. Kwa taifa la hovyo kama Tz rushwa na ufisadi sio tuhuma kubwa kama unavyotaka kumaanisha. Vinginevyo kuna majitu mengi tu yangekuwa jela saivi.
USHAURI: ondoeni mioyo yenu kwa Mbowe, mwenyekiti wa chama sasa ni Lissu, tumuunge mkono.
 
Siasa chafu alizofanya Lisu na team yake dhidi ya team Mbowe yale majeraha kupona sio rahisi

Kuna vidonda vya kawaida na donda ndugu

Bon yai alichofanya ni sahihi ku block kabisa simu nk za wahuni

Tuwe fair Mbowe alichofanyiwa na Lisu sicho kabisaa


Acheni uwongo. Mbowe alifanyiwa nini na Lisu? Kwa kusemwa vibaya, naamini Lisu alisemwa vibaya kuliko alivyosemwa Mbowe. Lisu si ndiye aliambiwa kuwa ĥawezi kuwa hata kiongozi wa nyumba 10? Si ndiye aliambiwa ni mropokaji? Si ndiye aliambiwa eti hata kuteuliwa kuwa mgombea Urais, ilikuwa kwa sababu alifanana kwa tabia na Hayati?

Ukiwa mtu mwenye hekima, kauli za hovyo wakati wa uchaguzi unazipuuza maana watu wengine hawana uwezo wa kushawishi waoiga kura bila ya kutoa kauli za kuwabeza wapinzani wao.
 
Salaam na heshima kwako mheshimiwa Boniface Jacobo Mayor mstaafu na Mwenyekiti wa Kanda ya pwani chama Cha demokrasia na maendeleo CHADEMA.

Kiongozi kabla ya kusema niliyowiwa kuyasema naomba kutambua unao washauri wengi sana wenye vyeo na nafasi kubwa kuliko Mimi ila naomba unipe dakika chache tu kusoma barua hii.

Kiongozi kabla ya uchaguzi mkuu wa chama ulikuwa mtu muhimu sana katika chama na nikiri huo umuhimu wako upo , pengo lako tunaliona ndio maana nimewiwa kuandika barua hii ya wazi kwako .

Kiongozi Kuna matukio mengi sana yametokea nchini ambayo sio kawaida tukose tweet mbili tatu kuyahusu na kuna matukio mengi sana ya kichama ambayo hatukuoni wala kuona mchango wako kwa sasa

Kiongozi naomba nikukumbushe tukio la wewe kurudisha fomu ya kugombea uenyekiti Kanda ya pwani. Wanachama wengi tulikusindikiza kurudisha fomu wengine hata hutufahamu na usisahau hatukukusindikiza kwa sababu ya ukaribu wako na Mbowe tambua hili Kuna wengi tu walipendezwa na Lissu wakati wa uchaguzi na walikuwa wengi tu huenda zaidi ya wafuasi wa mbowe waliokusindikiza . Hivyo tambua tunaokuamini hatukuamini kwasababu yoyote zaidi ya kuwa mwanachama wa chadema na mwenye uwezo mkubwa katika harakati za chama .

Tunatambua umeumia sana kutokana na demokrasia ilivyoamua ila fikiria vizuri sidhani kama mheshimiwa Mbowe anafurahia ukimya wako . Tafadhali ni muda wa kurudi sasa. Tusamehe tuliotoa maneno makali wakati wa uchaguzi wa chama nikiwemo umeniblock kabisa. Uchaguzi umekwisha . Ushapumzika vya kutosha . Pengo lako linakusubiri ulizibe Tafadhali lizibe tusonge mbele.

Nisikuchoshe kwa barua ndefu. Tafadhali rudi kama awali maisha yaendelee

Mwanachama mtiifu wa CHADEMA
Na mwanaharakati wa haki
Assenga

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kama huyu Rangai aamini katika box la kura na kuendelea itumikia Chadema, then sisi tunajua hafai maana ni kwa Ccm ki falsafa, wana mageuzi uamini kwenye democrasia
 
Ndio maana mm sipigagi kura. Labda atokee makenga wa Tanganyika. Hawa wapinzani wapo kupiga hela tu Tanzania. Wakizibiwa mirija ya hela wananuna. Mtu anatangaza maandamano alafu siku moja kabla yeye anapelekwa lockup sehemu salama ili nyie mfanywe chambo watoto wenu waumizwe.
 
Ila mwamba alikuwa na mvuto flan hivi pale CDM.....Yani chama kilikuwa oinaonekana kina standard flan hivi...

Ila Sasa hivi ni vurugu tuu
Mwamba alikuwa kiongozi,akiongea watu wanatafakari hata wiki,sasa hivi Kiongozi anaongea saa hiyohiyo watu wanasahau
 
Mkuu ni vigumu sana kufanya kazi na watu uliowatukana hadharani na kuwasingizia kula Rushwa ya Samia, kwa mfano Lissu amesema si mara moja kwamba Sugu alimshinda Msigwa kwa Rushwa, bila ushahidi wowote, ushahidi unaotolewa ni kwamba Mrema alihongwa bia 10 (bia moja ya kitanzania ni elfu 2 tu, hii maana yake ni kwamba Mrema alihongwa elfu 20), Je tuamini kwamba hii ndio rushwa ya uchaguzi? , hata kama ni kweli , hivi Mrema ni mpiga kura?

Sasa Sugu ni Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa na Msigwa ni Mwanaccm, Sasa unafanyaje kazi na Sugu kwa namna hii katika hali ya Ukweli wa kibinadamu? Unayemtetea Msigwa yuko ccm, tena alihama akiwa kakata rufaa na watu wakijiandaa kuijadili.

Tujifunze kuheshimu viongozi wengine kama sisi tunavyotaka kuheshimiwa, Hakuna Kiongozi anayeweza kuongoza Chama Peke yake kwa kutumia akili zake tu

Haya ni Mapungufu na ni lazima yarekebishwe ili kama chama twende pamoja
Kuna wakati unaongea point 💪
 
Tusisahau pia kuwa Boniface alikuwa mhesabu kura za Mbowe, nadhani maumivu yalianzia pale aliona live. Sasa ni wakati wa kuishi demokrasia wanayohubiri kila mara.

Tusisahau haya maumivu yapo kwa Mbowe pia, alitumia hekima kukubali matokeo na akachukua point 3 za mwanademokrasia, ila ukweli ni alipigwa chini baada ya miaka za ya 20.
 
Siasa chafu alizofanya Lisu na team yake dhidi ya team Mbowe yale majeraha kupona sio rahisi

Kuna vidonda vya kawaida na donda ndugu

Bon yai alichofanya ni sahihi ku block kabisa simu nk za wahuni

Tuwe fair Mbowe alichofanyiwa na Lisu sicho kabisa

Mbowe kapigwa kwenye sanduku la kura, tena Boniface akiwa msimamizi wake, kuhusu kampeni timu ya Mbowe hawakuwa na hoja za ushawishi sana, na public haikuwa upande wao, timu Lissu hija ziliwabeba na umma pia.

Na ukiwa kwenye kampeni ni kusema madhaifu ya mpinzani wako, na ndivyo Lissu alivyofanya.

Chadema nje ya chaguzi wanazopambana na CCM, hawakuwahi kuwa na chaguzi za ndani zenye ushindani kama hizi, ndio maana kila kitu kimekuwa kama kipya kwao, na ndio maana maumivu ni makubwa.
 
Freeman Anaipenda sana Chadema, Atakuja kuwasaidia wakihitaji msaada wake, hajawahi kuwa na kinyongo
Kwa katiba ya Chadema, anakuwa mjumbe wa kudumu wa kamati kuu ya chama, yeye bado ni sehemu ya chama ni mwanachama. Labda yeye aamue kukimbia wajibu wake.
 
Yaani nyie maccm mnataka kuifundisha chadema jinsi ya kuendesha chama?
Kama ni kuwafundisha ufisadi sawa, kwa sababu hiyo ndiyo fani mliyobobea.
Sina chama cha siasa. Hata hivyo, nina uhuru wa kushauri pale ambapo naona inafaa. Kwa mwenendo huu, SSH kashashinda uchaguzi, CHADEMA ijikite kwenye uchaguzi wa madiwani na wabunge.
 
Back
Top Bottom