Barua ya wazi kwa Mheshimiwa Rais Dr. John Pombe Magufuli

Barua ya wazi kwa Mheshimiwa Rais Dr. John Pombe Magufuli

Hakuna kitu kinauma kama siku unakutana na mwenzako kapiga kivazi (kombati)alafu ukicheki mlikua nae wewe ukarudi uraiani na isitoshe hata kwenye gwaride alikuwa nanga[emoji16][emoji16]
Ila wawafikirie waende tu RTS kama watashindwa au kufa juu yao maana ni wamependa wenyewe vijana

Ninawaona maafisa wengi tu wa nyota mbili wakiwa na miili ya magonjwa hayo ya Bp, moyo wakati Mtu Wa nyota mbili ni mpiganaji Kama private tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni swala ambalo ni gumu kdg kulizungumzia hum kiundani zaidi lakn kikubwa kilio chetu tunahitaji kimfkie mheshimiwa Rais Ntashkuru kma utakua na msaada na hlo hata kuweza kushare.
Umeumizwa halafu unakingia kifua kufichua uozo uliosababisha mchujo wa kinafiki na upendeleo wa kushenzi?

Nani asiyejua kujiunga na jeshi kunatumika rushwa na kujuana?

Nikuhakikishie, hao wote mkifanyiwa re examination, robo3 ni wazima, ila nafasi zenu zimewekwa kibindoni ajili ya kuzawadia watoto wa wakubwa wadio na sifa, watakaochomekwa kinyemela ama nafasi hizo kuuzwa.

Sasa wewe endelea kufichaficha, mahali ambapo unatakiwa kumwaga mtama ili msaidiwe, maana haukusaidiwa na mamlaka hiyo.

Mara nyingi kumekuwa na upinzani wa kimyakimya rais atoapo maelekezo ya ajira kwa amri.

Wanayapokea maagizo yake kwa shingo upande huku wakiwaza namna ya kufanikisha waliyoyazoea, maana anakuwa kaziba mirija yao ya ulaji.

Mwaka jana tuliona tena tangazo la Mkuu wa majeshi akiagiza vijana waliojenga ukuta wa Mererani wakapewa zawadi ya ajira kisha kurudishwa majumbani, waripoti kwenye chuo cha mafunzo!

Ni nini maana ya mkanganyiko huu sasa, ni nani huyo aliyepingana na amri halali ya CinC kuwarejesha majumbani badala ya kuwapeleka chuo cha mafunzo!

Ajira hiyo ilitangazwa kama zawadi kwenu ni haki yenu vijana mliojitolea kwa nidhamu na jasho kufanikisha miradi iliyopewa jeshi kutekeleza na kupelekea jeshi hilohilo kupewa sifa na kuaminika.

Je walipowapima walipeleka ripoti kwa rais juu ya u unfit wenu na hatua gani zichukuliwe za kuwasaidia?

Maana hiyo ni ajira maalumu ya tamko la rais, hawezi kutokea tu kiongozi hapo katikati akapindisha tamko la rais bila kupeleka taarifa Ikulu.

Sasa wanatumia mbinu za kuwapa alama za unfit kutimiza malengo yao hayo niliyoeleza.

Lalamiko lenu likisongeshwa likamfikia Jpm na likafanyiwa kazi, kisha mkarudiwa kupimwa kwa kutumia majopo mengine ya madaktari, litaumbua myororo mzima wa kifisadi, kisha waliofanya huo unyama washitakiwe na kuwajibishwa bila kujali cheo cha mtu, maana nyie wote hao hamuwezi kuwa ma unfit inapopatikana ajira, lakini kwenye kujitolea mlikuwa physically fit.

Pole sana kijana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wenzeni ambao walikuwa unfit wakalazimisha si wamekufa kibaha sijui chakinze?
 
Yani ukuta wa Ikulu mpya ya Tz iliyopo Dodoma mlijenga nyie JKT??.
Kaka kiukweli kama wamewafanyia hv watoto wa masikin laaana itawatafuna kuanzia ngazi za juu za jeshi na usalama kiujumla ,jwtz inasifiwa kwa sababu ya hawa vijana,watoto wanapga kazi ucku na mchana wanaumia wanakuja kuwadump kwa staili hii.kaka huo ukuta wa ikulu dodoma umejengwa na vijana hao hao ndugu
 
Mkuu copy ya barua nyingine nakushauri ipeleke kwa sanduku la posta,kuna ndugu yangu hapo Ikulu huwa anatumia S.L.P 9120 Dar es salaa.
Nackia hadi ikulu walienda mkuu kupeleka barua lakn hazimfikii mzee bora walivyojilipua
 
TODAYS, Naongezea wazo kidogo kama Mh Rais huwa anachungulia humu ama kuna wasaidizi wake najua wapo humu walichukue hili hakuna kitu kizuri kama kutumia Akili+Hekima= MAARIFA ukitumia hii falsafa utaona mafanikio yake hii Nchi ya Tanzania hakika Tumshukuru Mungu kwa kujaaliwa Ardhi kubwa yenye rutuba udongo mzuri na rasilimali za kila aina,

Hao vijana wa jkt waliomaliza serikali inao uwezo wa kuwagawanya wakatenga maeneo ya ufugaji wakajenga kiwanda na kuwajiri hawa kwa ajili ya kusindika na kuuza nje hela itayopatikana itatosha mishahara yao na nyingine kutumiwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ,

Pili watenge mashamba makubwa kwa kilimo cha kisasa wawaweke hawa vijana walime kilimo cha kisasa mazao yakivunwa mengine yatauzwa nje hela itapatikana uchumi utakuwa ajira zitaongezeka yaani kuna kitu nakiona lakini naona wengine hamkioni fursa zipo pengine ni uthubutu tu na wakiweza hili naimani tutafanikiwa Umoja ni Nguvu( Masikini hana hela lakini ana mawazo)


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasaidiwe wapate haki yao ili wasijeshawishika kuunda jeshi lao kwa shauku ya kudhihirisha kwamba siyo unfit.
 
Wamewaambia mpo UNFIT. Sasa mnataka nini kingine?...Rais mwenyewe atawashangaa.....Fanyeni shughuli nyingine mnazidi kupoteza tu muda.


Sent using Jamii Forums mobile app
acha ujinga....sheria inataka aliyepata madhara kazini lazima afidiwe....sasa mbona hawa wametupwa kama vile takataka? halafu kuna uwezekano wa kuwa FIT tena kama wakipata huduma stahiki na wakarudishwa kazinai kama rais alivyoamrisha
 
Poleni sana wazee kwa hiyo mitihani iliowakuta .
Wanajamvi inabidi tusaidie kufikisha hiki kilio cha hawa wadogo zetu maana mtaani ni kugumu japo sijajua wapo UNFIT kw kigezo kipi, Kama wameonyesha uzalendo huo mdau alivyoeleza katika barua yake hatuna budi kutoa mchango ata wa mawazo kipi kifanyike.

Kama ilivyodesturi ya kulipa fadhira kwa wanajeshi wanapopata matatizo wakiwa vitani kwa hili naona kifanyike kitu kama hiko waitwe wapatiwe matibabu na kuingizwa kwenye mfumo wa ajira ambao ni rafiki kwao, maana inawafanya wasononeke mara mbili zaid. kwanza kuikosa ajira na kuona wenzao wakiajiriwa, pili kuwa na matatizo ya kiafya ambayo kama jeshi wameshindwa kuwatibia je familia binafsi za hawa wahanga wataweza kugharamia hayo matibabu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasaidiwe wapate haki yao ili wasijeshawishika kuunda jeshi lao kwa shauku ya kudhihirisha kwamba siyo unfit.
jeShini ukiambiwa unfit unaelezwa Vizuri eneo uko unfit hasa kiafya. Naona mleta mada wala hilo hapingi na kakiri waliambiwe unfit wakajitibie anacholalamika ni kuwa hawana sip hawana Maradhi wanayo ila pesa ya kujitibia hawana ndio maana wanaomba kazi ili wapate pesa Za kujitibia!!!! Na Jeshi huwa haliajiri wagonjwa na si jeshi tu ni serikali yote na hata waajiri binafsi

Uzima wa afya sasa hivi ni mtaji mkubwa mno kuanzia kwenye ajira hadi kupanda vyeo nk

Vijana wahamasishwe kutunza afya zao.Afya mdororo yaweza mkosesha mtu kazi hata awe na sifa zipi
 
Hakuna kitu kinauma kama siku unakutana na mwenzako kapiga kivazi (kombati)alafu ukicheki mlikua nae wewe ukarudi uraiani na isitoshe hata kwenye gwaride alikuwa nanga[emoji16][emoji16]
Haikuwa riziki unatumia ujuzi ulioupata kupambana kitaa
 
jeShini ukiambiwa unfit unaelezwa Vizuri eneo uko unfit hasa kiafya. Naona mleta mada wala hilo hapingi na kakiri waliambiwe unfit wakajitibie anacholalamika ni kuwa hawana sip hawana Maradhi wanayo ila pesa ya kujitibia hawana ndio maana wanaomba kazi ili wapate pesa Za kujitibia!!!! Na Jeshi huwa haliajiri wagonjwa na si jeshi tu ni serikali yote na hata waajiri binafsi

Uzima wa afya sasa hivi ni mtaji mkubwa mno kuanzia kwenye ajira hadi kupanda vyeo nk

Vijana wahamasishwe kutunza afya zao.Afya mdororo yaweza mkosesha mtu kazi hata awe na sifa zipi
Kwani wanaposailiwa jkt si huwa wanapimwa huo u Unfit ni kabla ya kusajiliwa jkt au baada ya kusajiliwa jwtz
 
Nakumbuka enzi hizo sisi tulikuwaga tunaimbaga kawimbo haka “” KATOTO KADOGO KANALI****a Jimama “”.

Chenja zile sitokaa nizisahau aisee, full morali,

TANZANIA YANGU EE, NAKUPENDA.

Poleni sana vijana, na imani mweshimiwa litamfikia hili ombi lenu, Mnasitahili kwakweli .
 
Kiwarhoapandenga, ulichoongea ni sahihi lkn watapita km hawaoni ifike mahala taasisi za kifedha wa invest kwenye idea...km.....nje na serikali iweke mkono wake....mfumo wa scheme plantation urudishwe usimamiwe chakula kiuzwe nje pesa ipatikane watu walipwe naisha yaende wakati mwingine tuige mawazo ya waliotunyanyasa(wakoloni) serikali ikiweka kambi kama wafanyavyo jkt kwenye kilimo.

unabeba watu mtaani wanapiga kazi kwann tuwe maskini wakati tunakila kitu...kwann tuwe na tamaa kwa kujiangalia mimi...ebu ona hawa vijana wameachwa baada ya wao ma alwatani kunufaika wamesha wadump!...siasa ziwekwe pembeni tuishi uharisia wa maisha....mnataka watu wawe wezi kwann hatumuogopi MUNGU ifike mahala wanasiasa waache kuroga wasimamie ukweli na wakifanyie kazi na MUNGU atafungua njia.

Sio kupata uongozi wa madawa afu mnabaki kujiineemesha wenyewe....mpk hapa TZ ikiamua kujismamia wenyewe tunafika mbali ila mpango wa kilimo ni sanaa tupu hakuna kiongozi tena hawa wanojiita wana PHD. hakuna wanaozungumzia kupaumbele kwenye kilimo wote ni kujineemesha na kufidia jinsi alivyosota kusoma shuleni.

hakuna elimu inayomnufaisha mwanafunzi,mtaani hakuna kinachomnufaisha mwananchi serikali inataka watu wafanyenn haya maisha mpk lini...kila siku nafuu ya jana....nini dhamila ya serikali kwa wananchi wake...ebu angalieni hawa vijana ndio tegemeo katika nchi yoyote tuwe wazalendo kwenye nchi yetu.

tuingiwe roho ya upendo na kuthamini nchi yetu tujivunie kile tulichonacho na kukisimamia...utaona pesa hakuna lkn kipindi hiki cha uchaguzi pesa ipo kuhadaa watu....ebu tuweni wazalendo...kuanzia RAISI MPAKA MWANANCHI WA MWISHO tuipeperushe bendera ya TANZANIA popote pale kwa manufaa, mnisamehe kutofata alama za uandishi na MUNGU anisamehe nmeandika kwa hasira sana....ila naipenda nchi yangu TANZANIA.

HOT
 
acha ujinga....sheria inataka aliyepata madhara kazini lazima afidiwe....sasa mbona hawa wametupwa kama vile takataka? halafu kuna uwezekano wa kuwa FIT tena kama wakipata huduma stahiki na wakarudishwa kazinai kama rais alivyoamrisha

Kwani walikua na mikataba?
 
Back
Top Bottom