Barua ya wazi kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe: CHADEMA Isikubali kuonewa

Ndio gharama za demokrasia, hata Mandela alinyea debe kwa 27yrs, na akageuka shujaa kuliko yule dhalimu aliyeko motoni.
Wewe umefanya kitu gani cha maana au kuchochea wenzako wakanyee debe? Toka na wewe tukuone unanyea debe!
 
Ndio gharama za demokrasia, hata Mandela alinyea debe kwa 27yrs, na akageuka shujaa kuliko yule dhalimu aliyeko motoni.
ni makosa la jinai kuwafananisha hawa wahuni na mandela.
 
Jitokeza siyo kuunga mkono tu. Wakati ule Mbowe ananyea debe ulimsaidia nini au ulikuwa uko nyuma ya keyboard kama kawaida yako??!!

Tujitokeze mara 2? Mbowe tulimchangia fedha lukuki baada ya hukumu.
 
Chadema na watanzania bado waoga Sana kudai haki,ushaur kaeni kimya tu kuliko kujiaibisha hv Jana wamepiga mkwara ohooo kongamano lipo lkn ukumbini hakutokea hata mmoja,wengine wamekamatwa kama kuku kilichofuata ni kupiga kelele mtandaoni,cdm mna kelele sn mtandaoni lkn field ni utopolo kabisa,tulien siku mkiona mna uwezo wa kupambana na police ndo mdai
 
Hivyo unaona mazuri yanatofanywa na maharami pekee.
mimi ni muumini wa siasa za kistaarabu zenye kuzingatia maslahi ya nchi yangu kwanza.
Tanzania ni Muhimu zaidi kuliko chama chochote kile.
siko tayari kunyamaza ninapoona chokochoko za kuhatarisha amani yetu maana likiharibika hakuna atakaye salimika.
 
Kwahiyo hicho cha maharamia ndio chama Chako na ndio kinachoona na kuzingatia maslahi ya taifa.?
 

Ww sio muumini wa siasa za kistaarabu, bali ni bendera fuata upepo kwa matamko ya viongozi. Watu wanafanya mkutano wa ndani kusema matakwa yao halali, je ni ustaarabu au chokochoko gani wameleta?
 

Karata za CCM ziko hapa:

1. CDM hawako tayari kupambana hadi kutumia nguvu.
2. Sana sana CDM watasusia chaguzi.

Zote mbili hazina madhara kwa CCM kwani zitawaacha wakiwa madarakani.

Ni muda sasa mahusiano haya kubadilika. Hiyo ndiyo lugha sahihi kwao watakayo ielewa.

 

Umeongea ukweli.

Kujivutavuta kwa CHADEMA katika kudai haki yao ndo kunawachelewesha kupata haki yao wanayostahiki.

CHADEMA lazima itafute namna ya kupandisha joto la kisiasa nchini.

CHADEMA lazima iwape CCM tough time. Initially CCM itajaribu kutumia majeshi kuzima joto hilo lakini CHADEMA ikikomaa, majeshi yatawaambia CCM kuwa haya ni masuala ya kisiasa yamalizeni nyie wenyewe kwa wenyewe kisiasa.

Ila hatua hii ya Majeshi kuwambia CCM wafanye siasa badala ya kuwategemea wao itakuja tu kama CHADEMA wataonyesha resolve ya kutorudi nyuma kwenye kudai haki zao za kikatiba!
 
Ww sio muumini wa siasa za kistaarabu, bali ni bendera fuata upepo kwa matamko ya viongozi. Watu wanafanya mkutano wa ndani kusema matakwa yao halali, je ni ustaarabu au chokochoko gani wameleta?
weka ushabiki pembeni, waulize kina Lwaitama, kina msigwa na viongozi wengine walio kuwa wanahamasisha wananchi wahudhurie kikao cha ndani, hivi kweli kilikiwa kikao cha ndani au mkutano wa hadhara?!
unajua chadema mara nyingi wanawachukulia Askari wetu kama watu fulani hivi wasio jielewa! yaani huwa wanawadharau sana askari na kujiona wao wana akili zaidi.
sasa ngoja wakabiliane na mkono wa sheria. maaana nchi hii inafuata utawala wa sheria, ukivunja sheria lazima ushughulikiwe.
 


Hii nchi si ya Mbowe wala CDM peke yao.

Mbowe na CDM wanatakiwa kupewa amri tu na sisi tuliochoshwa na huu upumbavu. Tunataka mahusiano mapya (new rules of engagement):

1. Nia yetu ni kujadiliana kwa amani ila tunayo haki ya kutumia nguvu kama ikiwa lazima kulinda haki zetu.
2. Kwamba hatutashiriki chaguzi tena ieleweke kuwa hakuna uchaguzi mkuu tena utakaofanyika bila kuwapo tume huru.

Huu utakuwa mwanzo sahihi wa kumwajibisha kila mtu kuanzia chini hadi juu.

Amri moja!
 

Nasema hivi huna jipya, huo ni mkutano wa ndani, una shida gani? Kuna kosa lolote mkutano wa ndani kuhamasisha watu wahudhurie? Acha kulazimisha tafsiri zako zisizo na msingi wowote. Ingekuwa wamekutana kwa siri hapo ndio kungekuwa na shaka, lakini wametangaza kweupe maana hawana ajenda yoyote ya siri. Ww ndio uweke pembeni mahaba ya siasa za hila.
 

Pana aina za lugha ambazo huzielewa zaidi. Acha waendelee kuzipalilia.
 
Sasa hivi tuko hapa:

Na bado.

Cc: Missile of the Nation
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…