Barua ya wazi kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe: CHADEMA Isikubali kuonewa

Barua ya wazi kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe: CHADEMA Isikubali kuonewa

Chadema na watanzania bado waoga Sana kudai haki,ushaur kaeni kimya tu kuliko kujiaibisha hv Jana wamepiga mkwara ohooo kongamano lipo lkn ukumbini hakutokea hata mmoja,wengine wamekamatwa kama kuku kilichofuata ni kupiga kelele mtandaoni,cdm mna kelele sn mtandaoni lkn field ni utopolo kabisa,tulien siku mkiona mna uwezo wa kupambana na police ndo mdai
Siyo waoga ila watanzania wana subira sana. Unfortunately watawala wameiabuse vya kutosha hii subira, It is a matter of time tu kabla hawa watu hawajaonyeshwa hasira ya wananchi
 
Kama kweli ni vidume, waanze ktk viwanja vya biafra, wajitokeze mbele Mbowe, Kigaia, Mnyika, Lwaitama na Mwalimu, msigwa, wote hao wanao uhakika wa familia zao kula bila shida yoyote, tabu ni wafuata upepo tutaabisha familia zetu bure.
Sikia nikwambie hutobaki mzima ,Kama sio kesho ila bado utakufa , Sasa nikwambie sio mda nitaandamana mwenyewe mpaka chamwino ikulu , liwalo na liwe why kuogopa kivuli mlicho kutengeneza wenyewe

Uoga wako peleka KWA mkeo , usituletee sie, au mimi
 
Mbowe, msaanii tu wafuasi wake nyie Pro-Chadema JF na kule Twitter kina kigogo na kundi, unakumbuka Mbowe aligombea urais akapata kura laki 4, mnajazana ujinga tu kama una uchungu ingia barabarani.

Chama chochote kishike dola mambo ni hayo hayo wacha Samia akupigeni spana hamtaki kumuheshimu na mnamzonga,ndio Kwanza miezi minne mnampanda kichwani
Akili fupi kama minyoo ya bilharzia [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]we ka mtu bwana
 
Mimi naamini ishu ya maandamano, kama yakiandaliwa vizuri yanaweza kufanyika lakini in phases

1. Lazima yawe incremental, spontaneous, yanayoongezeka kila day after day

2. Initially yawe decentralized, yaani kila kundi la watu let say kumikumi kila moja kuandamana kivyake katika mahali wanapoona wanaweza kufikisha ujumbe wao mpaka hapo baadae itakapoamuliwa

3.Ukisharegister mafanikio ya awali, inajengwa momentum kwa ajili ya maandamano mengine ambayo nayo ni ya watu makundinakundi kila moja ikitarget eneo lake na intensity inaongezeka

4. Ngoma ikishaitika yanaitishwa maandamano makubwa makubwa

Lazima tuelewe falsafa ya jeshi la polisi nchini ktk kuzuia maandamano

1. Nguvu nyingi huwa ni kuzuia yasianze kuliko kuthibiti yakishaanza, njia wanayofanya ni kukamata influencers, organisers, viongozi wakubwa, etc
 
Hii njia yako namba mbili naona itakuwa easier kuharibiwa na polisiccm, na ikashasambaratishwa itakuwa ngumu kuitisha maandamano makubwa zaidi, mimi naona hili jambo lingekuwa kama shambulio la kushtukiza, wawe wengi, ili polisiccm wakose pa kuanzia kutawanya waandamanaji.
 
nimeona umeandika sentensi kadhaa hapa kama vile " kuwin huruma ya wananchi" , "kuvuna sapoti ya wananchi"
hizi sentensi zako zinaonesha wazi kabisa kwamba haya mambo mawili( huruma ya wananchi na sapoti ya wananchi) havipo upande wenu. Hapa napata swali kwamba kwa nini wananchi hawajawapa sapoti ya kutosha mpaka sasa pamoja na nguvu nyingi mnazozitumia?
Umezungumzia kudai katiba mpya itakuwa ni turufu kwenu ukionesha wazi kabisa kwamba katiba mnayoidai ni ile ya manufaa binafsi ya wanasiasa na si ile ya matakwa halisi ya wananchi.
Ushauri wangu ni kwamba shughulikieni kwanza changamoto za ndani ya chama chenu ndipo mje kwa wananchi kuwaeleza nini hasa mnachokihitaji.
Vinginevyo umeonekana ktk uandishi wako ukiwa na hasira kali kitu ambacho ktk uandishi unatoka nje ya mstari.
 
Mimi naamini ishu ya maandamano, kama yakiandaliwa vizuri yanaweza kufanyika lakini in phases

1. Lazima yawe incremental, spontaneous, yanayoongezeka kila day after day

2. Initially yawe decentralized, yaani kila kundi la watu let say kumikumi kila moja kuandamana kivyake katika mahali wanapoona wanaweza kufikisha ujumbe wao mpaka hapo baadae itakapoamuliwa

3.Ukisharegister mafanikio ya awali, inajengwa momentum kwa ajili ya maandamano mengine ambayo nayo ni ya watu makundinakundi kila moja ikitarget eneo lake na intensity inaongezeka

4. Ngoma ikishaitika yanaitishwa maandamano makubwa makubwa

Lazima tuelewe falsafa ya jeshi la polisi nchini ktk kuzuia maandamano

1. Nguvu nyingi huwa ni kuzuia yasianze kuliko kuthibiti yakishaanza, njia wanayofanya ni kukamata influencers, organisers, viongozi wakubwa, etc
Tatizo hapa mleta mada amesema kabisa kwamba hakuna sapoti ya kutosha kutoka kwa wananchi. Sasa hapo ni nani atakaeandamana?
Angalia tu ishu ya UKUTA ikivyoyeyuka kama theruji.
 
Hii njia yako namba mbili naona itakuwa easier kuharibiwa na polisiccm, na ikashasambaratishwa itakuwa ngumu kuitisha maandamano makubwa zaidi, mimi naona hili jambo lingekuwa kama shambulio la kushtukiza, wawe wengi, ili polisiccm wakose pa kuanzia kutawanya waandamanaji
Hii approach yako ni lazima ufikie critical mass ya raia waliochefukwa sana ndo wanaingia kitaa.

Na ili raia waingie front kwa wingi lazima kwanza uvunje myth kuwa raia wa Tanzania huwa hawaandamani, kwa hiyo ili kuvunja hii myth lazima yawepo maanadamano madogo madogo mengi nchi nzima.

Hili likishafanikiwa mass inakuwa na confidence ya kuingia mtaani.

Unajua huwa hakuna maandamano yanaoyotokea hivihivi bila kuratibiwa, kupangwa na kuwa executed!, kitu ambacho huwa hakina control ni aftermath ya maandamano.

Sasa ili kupata watu wengi at once either
1. Serikali ifanye jambo moja baya sana likasirishe wananchi kupita kiasi kiasi kwamba hata serikali iwe kwenye defensive side, ikose hata moral authority ya kutumia maguvu mengi.
2. Au Serikali izembee iruhusu uratibu wa maanadamano hayo yafanikiwe, Kwa experience ya jeshi la polisi la TZ huwa ni wazuri sana kwenye preemption, yaani ni wazuri sana kwenye "Kinga ni bora kuliko tiba", ndiyo maana hufanya wawezalo kudistrupt leadership ya maandamano husika
 
Mh Mbowe chukua ushauri huu, Kama mbwai mbwai
Hakuna kitu ambachoMbowe na CHADEMA hawajafanya.

Wameshajaribu zaidi ya mara 4 kuingiza watu barabarani kwaajili ya maandamano bila mafanikio.

Watu hawako tayari.

Na Mbowe hana ushawishi huo mkubwa mnaodhani anao.

Mara ya mwisho walitangaza maandamano baada ya uchaguzi mkuubwa 2020 na hakuna aliyejitokeza, kila mtu anaandamana ONLINE 🤣

CHADEMA waache ubinafsi, washawishi makundi mengi ya kijamii yawaunge mkono. Hivyo ndivyo hata UHURU ukivyopatikana.

Hii mentality ya CHADEMA kujiona wao ndio wao, wao ndio wapigania HAKI, wengine wasaliti Yaani kama una shida wewe ndio unapaswa kuwaunga mkono ni ya kipumbavu na itaishia kumtajirisha Mbowe tu kwa kuvuna ruzuku tu basi.
 
Tatizo hapa mleta mada amesema kabisa kwamba hakuna sapoti ya kutosha kutoka kwa wananchi. Sasa hapo ni nani atakaeandamana?
Angalia tu ishu ya UKUTA ikivyoyeyuka kama theruji.
Wapo wananchi wa kutosha wenye kuwahurumia na kukubaliana na madai ya msingi ya katiba mpya, ILA kupata huruma na uungwaji wa wale ambao walikuwa hawakuungi mkono hapo mwanzo ni ushindi mkubwa
 
Hakuna kitu ambachoMbowe na CHADEMA hawajafanya.

Wameshajaribu zaidi ya mara 4 kuingiza watu barabarani kwaajili ya maandamano bila mafanikio.

Watu hawako tayari.

Na Mbowe hana ushawishi huo mkubwa mnaodhani anao.

Mara ya mwisho walitangaza maandamano baada ya uchaguzi mkuubwa 2020 na hakuna aliyejitokeza, kila mtu anaandamana ONLINE 🤣
Walikuwa na uratibu poor wa hayo maandamano.

Yale ya UKUTA viongozi wa dini waliingilia kati kuyasimamisha na bahati mbaya CHADEMA waliyumba pale

Yakiratibiwa vizuri kwa strategy nzuri, wananchi wanaweza kuingia kitaa mpaka ukashangaa
 
Hii approach yako ni lazima ufikie critical mass ya raia waliochefukwa sana ndo wanaingia kitaa.

Na ili raia waingie front kwa wingi lazima kwamba uvunje myth kuwa raia wa Tanzania huwa hawaandamani, kwa hiyo ili kuvunja hii myth lazima yawepo maanadamano madogo madogo mengi nchi nzima.

Hili likishafanikiwa mass inakuwa na confidence ya kuingia mtaani.

Unajua huwa hakuna maandamano yanaoyotokea hivihivi bila kuratibiwa, kupangwa na kuwa executed!, kitu ambacho huwa hakina control ni aftermath ya maandamano.

Sasa ili kupata watu wengi at once either
1. Serikali ifanye jambo moja baya sana likasirishe wananchi kupita kiasi kiasi kwamba hata serikali iwe kwenye defensive side, ikose hata moral authority ya kutumia maguvu mengi.
2. Au Serikali izembee iruhusu uratibu wa maanadamano hayo yafanikiwe, Kwa experience ya jeshi la polisi la TZ huwa ni wazuri sana kwenye preemption, yaani ni wazuri sana kwenye "Kinga ni bora kuliko tiba", ndiyo maana hufanya wawezalo kudistrupt leadership ya maandamano husika
Bila kutumia ukabila ( ni ngumu hapa kwetu ) au dini siyo rahisi watu kuingia barabarani nchi nzima.

Ni ngumu kwa Mkerewe kuingia barabarani kupigwa virungi na risasi kwasababu ya mchagga Mbowe, ila ni rahisi kwa Wazulu kuandamana kwasababu ya Zuma au Wajaluo kuandamana kwasababu ya Odinga.
 
Halafu kumbuka, maandamano yanayoweza kuleta impact siyo ya siku moja.

Ni maandamano hata ya mwezi mfulululizo mwezi mzima ila shughuli za kiuchumi zisimame na serikali ianguke.

Sasa hali ya hivyo usifikiri inaweza kuletwa na mwanasiasa aina ya Mbowe au kutokana na agenda zilizoasisiwa na Mbowe mwenyewe anavyojisikia.
 
Hii approach yako ni lazima ufikie critical mass ya raia waliochefukwa sana ndo wanaingia kitaa.

Na ili raia waingie front kwa wingi lazima kwamba uvunje myth kuwa raia wa Tanzania huwa hawaandamani, kwa hiyo ili kuvunja hii myth lazima yawepo maanadamano madogo madogo mengi nchi nzima.

Hili likishafanikiwa mass inakuwa na confidence ya kuingia mtaani.

Unajua huwa hakuna maandamano yanaoyotokea hivihivi bila kuratibiwa, kupangwa na kuwa executed!, kitu ambacho huwa hakina control ni aftermath ya maandamano.

Sasa ili kupata watu wengi at once either
1. Serikali ifanye jambo moja baya sana likasirishe wananchi kupita kiasi kiasi kwamba hata serikali iwe kwenye defensive side, ikose hata moral authority ya kutumia maguvu mengi.
2. Au Serikali izembee iruhusu uratibu wa maanadamano hayo yafanikiwe, Kwa experience ya jeshi la polisi la TZ huwa ni wazuri sana kwenye preemption, yaani ni wazuri sana kwenye "Kinga ni bora kuliko tiba", ndiyo maana hufanya wawezalo kudistrupt leadership ya maandamano husika
Hawa polisi wanaowazuia watu kufanya hata mikutano ya ndani sidhani kama wataruhusu maandamano ya vikundi vichache, mchezo utakuwa ni kuwindana kama paka na panya, na kwa mtindo huo sidhani kama kuna jambo litakalofanikiwa, but all in all, kwangu bora execution iwepo na itekelezwe, iwe ya maandamano mafupi ya watu wachache, au ya watu wengi kwa pamoja muhimu watanzania waamshwe usingizini.
 
Bila kutumia ukabila ( ni ngumu hapa kwetu ) au dini siyo rahisi watu kuingia barabarani nchi nzima.

Ni ngumu kwa Mkerewe kuingia barabarani kupigwa virungi na risasi kwasababu ya mchagga Mbowe, ila ni rahisi kwa Wazulu kuandamana kwasababu ya Zuma au Wajaluo kuandamana kwasababu ya Odinga.
Dini nakubaliana na wewe, ni force inayobind watu katika soul zao, ila waliokuwa na guts za kuingia mtaani zaidi ni waislamu ndiyo maana serikali ikawawekea BAKWATA na kuwaweka viongozi wake wakubwa kwenye payroll
Ukabila siyo sana, kwa sababu majority ya watu wa kabila fulani wako confined ktk mkoa mmoja. Kwenye mikoa mingine wako sporadic

Hapa Tanzania kuna vitu vifuatavyo:

1. Watu wafikie pointi washindwe kupata hata mlo mmoja kwa siku (Hii bado serikali ya CCM inawaumiza kichwa, at the moment watu wanaweza kuafford kula japo mlo mmoja, ila CCM wameanza kuvuruga kwa kuchukua hatua za kikodi zenye kuongeza umasikini nchini).

2. Vijana wawe frustrated mitaani washindwe kufanya shughuli zao ndogondogo, wakate tamaa ya maisha(Magufuli alideal na hii point kwa kuwaachia wamachinga wafanye watakavyo)

3. Itokee political force yenye ushawishi mkubwa ya kuonyesha kuwa njaa ya wananchi inatokana na utawala mbaya, uongozi mbaya, katiba mbaya etc hata hivyo hiyo force wananchi shurti waiamini kuwa ni genuine, isiyoogopa (Magufuli alijaribu kudeal na point hii kwa kuwanunua wapinzani, strategy yake ililenga kuzigawa ranks za wapinzani, kuwaondolea imani kwa wananchi).

4: Itokee madhehebu makubwa ya dini yawape moral authority wananchi dhidi ya sera za serikali (Serikali huwa inadeal na viongozi wa dini kwa favors mbalimbali ikiwemo kuwaweka ktk payroll, Ila Madhehebu Makubwa kama wakatoliki wakiingilia kati serikali huwa inapwaya,mfano ni pale Kanisa Katoliki na lile la Kilutheri walipomgomea Magufuli kwenye ishu ya Korona lile wimbi la pili, JPM alijikuta overnight hana control ya narrative ya ishu ya Korona)
 
Nakubaliana na wewe. Na ndio maana unaona namna ambavyo safari bado ni ndefu.

Vile vile ugumu wa safari unaongezwa na mambo yafuatayo:

- Ubinafsi wa wapinzani wenyewe kwasababu vyama vimegeuka vitega uchumi na sehemu ya ajira na fursa kwa wahusika.

Leo CDM, NCCR, ACT, CUF wote wanataka katiba mpya lakini hawakai pamoja kwasababu hawaaminiani na wanashutumiana.

- CCM mpaka leo bado imeyakumbatia na kuyahodhi makundi yote muhimu ya kijamii kama vyama vya wafanyakazi, makundi ya kidini, Wasanii, wanataaluma, media n.k
 
CCM inahodhi makundi hayo kwa sababu ni chama dola, hiyo ni teknic yao ya survival

Pamoja na yote hayo tusisahau kitu kimoja

INVISIBLE HAND

CCM wamejenga kiburi kuwa hakuna wa kuwagusa, kwamba nyumba yao ya mamlaka ni imara isiyotikisika na kwa kufanya hivyo wamekuwa na kiburi ndiyo maana walivuruga uchaguzi serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

Kwa Kiburi chao hiki wanaweza kujikuta wanakosa Kibali cha Muumba Mbingu na nchi, kwa hiyo tusiwabeze wapinzani kama watakuwa na nia njema na kupigania haki, wanahitaji kuwa consistent
 
Ndugu Freeman!
Mara nyingi umesikika ukitaka sana siasa za uungwana, siasa za akupigaye shavu la kushoto basi mgeuzie la kulia. Hilo ni jambo zuri lakini hiyo falsafa yako inafanya kazi katika nchi za watawala ambao ni sober minded, siyo katika nchi ambayo watawala wameamua liwalo na liwe kwenye kusimika mifumo ya dhulma, uonevu ukandamizaji na kufanya lolote ilimradi waendelee kubaki madarakani hata kama si kwa ridhaa za wananchi.

Ndugu Mbowe
Tone yako ya kupenda maridhiano watawala wanaitafsiri kama uoga.

Huu uonevu mnaofanyiwa na watawala wa kunyimwa haki zenu za kufanya siasa kinyume cha katiba mtaendelea kufanyiwa mpaka siku mtakapoamua kusema sasa inatosha!

Ndugu Mbowe, Huu ni muda sasa wa kuvunja confidence hii ya watawala ambayo kimsingi wameshajiaminisha kuwa hamna uwezo, wala guts za kufanya chochote. Hii chain mkiifanikiwa kuivunja mtakuwa katika position nzuri za kuadvance haki zenu za kisiasa nchini.

Huu ni muda muafaka wa kuraise stake katika utawala wa nchi hii ili waone kuwa kutawala kinyume cha sheria na katiba ni kitu chenye gharama, kwa hiyo lazima ufanye yafuatayo:

1. Ni muda muafaka sasa wewe kuhimiza Wafuasi wako wasitii maagizo batili
Toa maagizo yako kwenye machinery nzima ya chama chako, Viongozi na wanachama wa chama chako wasitii maagizo haramu ya watawala katika maeneo yao. Kwa mfano kama Wamezuia mikutano, wewe waagize wafanye mikutano. Wewe usijali wala kuhofu maagizo yako yatafanyiwa kazi kwa kiwango gani, lakini wewe toa agizo la kichama, vikao na mikutano ifanyike. Katika hili kuna watakaofanikiwa kufanya hiyo mikutano kuna watakaoshindwa kwa sababu mbalimbali, lakini ni lazima tuvunje hii chain ya utii haramu wa maagizo haramu yaliyo kinyume cha sheria

2. Ni lazima CHADEMA iendelee kuwin huruma ya wananchi
Haya matendo mnayofanyiwa ya uonevu na ukandamizaji, wananchi wanayaona. Sasa ni muda muafaka wa kuyadocument vizuri, kuyaamplify ili wananchi wengi wayaone. Uonevu ambao watawala wanawafanyia kama mtaweza kuwashitakia, uungwaji mkono utakuwa ni mkubwa, na utaendekea kukua siku baada ya siku

3. Ndugu Mbowe ni muda wa Uongozi wa CHADEMA kusacrifice zaidi
Ndugu Mbowe, kama nilivyokueleza huko juu, kuna ulazima wa kuvunja chain hii ya uonevu, hili halitifanyika bila uongozi wa CHADEMA kujitoa mhanga(kusacrifice), Ni lazima uongozi wa CHADEMA uitishe mikutano ya wazi ambayo ni ya haki kisheria, ikizuiwa kinyume cha sheria Viongozi wa CHADEMA wasitii, Kubalini kusacrifice hata Jela lakini haki yenu kama Chama muipate. Na hii mikutano isiwe one day event, itisheni hii mikutano mara kwa mara mpaka watawala waone kuwa gharama za kupambana na CHADEMA ni kubwa kuliko kutenda haki.

Ndugu Mbowe, Hii chain ya nyie kuonewa hamtaivunja mpaka msacrifice, muwe tayari kwenda jela kwa ajili ya course hiyo

4. Ni lazima CHADEMA itumie fursa za serikali ya CCM kuboronga kwenye uchumi ili kuvuna sapoti ya wananchi
Ndugu Mbowe, Kimsingi, CCM wanajua measures zao za kiuchumi ni unpopular kwa wananchi, pia wanajua legitimacy yao ya kisiasa kwa wananchi ni ndogo sana, kwa hiyo wanachokifanya ni kujaribu kwa nguvu zote kuweka ukuta baina yenu na wananchi ili msiwape hao watawala kibano cha kisiasa. Ni lazima message yenu sasa muiegemeze katika ugumu wa maisha ambayo wananchi wanapitia na kwenye fact kuwa tumefika hapa kwa sababu ya utawaka mbovu wa CCM na wananchi hawana wawakilishi waliotokana na ridhaa zao. Tumieni kila opportunity, tengenezeni talking points za matatizo ya kiuchumi muzisambaze hadi huko chini kwa viongozi wenu wa ngazi za chini ili waweze kuwaeleza wananchi kwa ufasaha kabisa madhila ya utawala wa CCM kwenye maisha yao, na namna CCM inavyopekekea wao kuwa na maisha Magumu

5. Ni muda muafaka wa kumuomba kila mwanachadema afanye kazi ya kusambaza ujumbe wa Chama
Ndugu Mbowe, CCM wanadhani wanaweza kudhibiti moto wa CHADEMA kwa kuthibiti uongozi ambao uko structured, kwamba wakidhibiti let say viongozi wa matawi, mashina, kanda na viongozi Taifa basi wataweza kukithibiti Chama. Sasa ni muda muafaka wa Chadema kutoa muongozo kwa kila mwanachama na shabiki na Chadema kufanya kazi za chama za kusambaza jumbe na sera za chama. Agiza kila mtu, afikishe ujumbe na sera za chama kwa marafiki, kwa majirani n. k. Yaani kwenye suala la kusambaza jumbe za CHAMA isiwe muda wote centralized bali nyakati kama hizi ngumu mnazozuiwa kuorganise iwe ni decentralized. Hii itawezesha ujumbe kufika pale ambapo watawala hawataki mfike!

6. Ni lazima kuionyesha sura halisu ya Rais Samia, ajulikane kabisa kuwa naye anaenjoy "urahisi wa Udikteta" na anachukia "ugumu wa demokrasia"
Demokrasia siyo kazi nyepesi, inahitaji kutumia akili zaidi, kujizuia zaidi, kuwa na subira zaidi, maridhiano zaidi. Sasa hayo ni mambo magumu kuliko udikteta ambao madikteta hawataki kuumiza kichwa sana kwenye utawala, wao wanataka kutumia miguvuguvu tu
Sasa Samia inaonekana kabisa anataka kufuata njia za Mtangulizi wake, hataki tabu, anataka kutawala kwa mteremko. Lakini wakati huohuo anataka kuudanganya ulimwengu kuwa yeye ni mwanademokrasia, Hataki kuitwa "DICTATOR". Sasa CHADEMA isikubali kumpa hii blank cheque, kama anafanya Udikteta aitwe dikteta, asakamwe kwa udikteta wake.
Na hapa naungana na John Heche, Acheni kumuita Samia MAMA. hii inampa soft power, na moral authority ambayo connotation ya mama inabeba. Kiufupi kama anavunja katiba ya nchi basi haistahili kuendelea kutumia hilo jina mama, muiteni kwa jina lake halisi, kama ni dikteta basi aitwe Dikteta.

7. Madai ya Katiba mpya ni turufu inayopaswa kutumika kwa nguvu zote
Ndugu Freeman, katika vitu ambavyo wananchi wengi wanakubali, bila kujali mirengo yao ya kisiasa ni katiba mpya. Hii ni turufu kubwa ambayo hata CCM wanashindwa waihandle vipi. Sasa ni muhimu sana nyie kuiframe agenda hii kuwa ni kwa ajili ya masilahi ya wananchi zaidi, katika kufanya hivyo nashauri nyie kama chama mkae muandae points za namna gani Katiba mpya inagusa maisha ya watu moja kwa moja. Hizi talk points zisambazwe kwa makada wenu wote nchi nzima. Lengo hapa ni kuondoa ile spin kuwa nyie mnapigania katiba mpya kwa ajili ya madaraka tu.

Elezeni faida za bunge na mahakama huru, elezeni katiba mpya inapambanaje na ufisadi, elezeni katiba mpya ina uhusiano gani na maji yao, elimu ya, afya yao. Namna hii mtaweza kuwashawishi wananchi wawe active zaidi na zaidi katika kuidai na kuilszimisha serikali ya CCM ilete hiyo katiba mpya. Msiishie tu kuzungumzia ishu ya tume huru ya uchaguzi na madaraka ya rais jinsi yasivyo fair bali onyesheni jinsi vitu hivyo vinavyopelekea maisha ya watu kuwa magumu zaidi.

Mwisho kabisa ndugu Mbowe napenda kukwambia kuwa sasa ni muda muafaka wa kuraise joto la kisiasa nchini, lipndisheni kwa kugomea amri haramu. Fanyeni mikutano hata kama imezuiwa kinyume cha sheria. Hawa hawana mabomu, waka askari wa kutosha wa kuweza kupambana na HAKI

Chairman, mmeonewa kiasi cha kutosha, mmenyanyaswa kiasi cha kutoshao sasa fanya jambo, tumechoka!
Yaani wakiaandaa mkutano waandae kila kata nchi nzima tuone kama police wataweza kuwakamata kata zote Tanzania
 
Yaani wakiaandaa mkutano waandae kila kata nchi nzima tuone kama police wataweza kuwakamata kata zote Tanzania

Hapa polisi huwa inatumia technic za kupiga mkwara, kuzunguusha mapolisi mitaani na vifaa vya kijeshi kutisha watu

Huzunguukia makazi ya viongozi na kuwakamata etc.
 
Back
Top Bottom