Barua ya wazi kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe: CHADEMA Isikubali kuonewa

Chairman, mmeonewa kiasi cha kutosha, mmenyanyaswa kiasi cha kutoshao sasa fanya jambo, tumechoka
CHADEMA leo hii ipo, kwa sababu waliweza kuepuka mitego yote waliyowekewa ili wamalizwe moja kwa moja kama chama endapo wangetumia papara.
Hatari hiyo haijaisha, ipo inaendelea sana hadi leo, kwa hiyo ni kazi kubwa wanayotakiwa CHADEMA kuendelea kuifanya kuepukana na mitego hiyo.

Nashukuru sana kwamba mada yako umejaribu sana kuepuka kuwachochea CHADEMA wafanye mambo yatakayosababisha chama kisambaratishwe kabisa.

Lakini pia, kumbuka bila uwepo wa viongozi kadhaa ndani ya chama hicho, hasa Mbowe mwenyewe, na wengine wachache, hawa wakizuiliwa, shughuli za chama ndipo zitakuwa zimefifia sana. Kwa hiyo, pamoja na kufanya kila linalowezekana katika kukataa uonevu huu wanaofanyiwa CHADEMA, ili CHADEMA iendelee kuwa kiongozi wa mageuzi, viongozi wake ni lazima wawe ni sehemu muhimu wa kuchochea mapinduzi hayo.

Ndiyo, ni kweli, Mbowe na baadhi ya viongozi wa juu wakiondolewa na kuwekwa ndani, dunia italichukulia tendo hilo kwa uzito wake na Tanzania haitakuwa tena nchi isiyokuwa na wafungwa wa kisiasa. Lakini kuondoka kwao katika uwanja wa mapambano kutakuwa kumefifisha sana mapambano hayo bila ya uwepo wa kuibuka kwa viongozi watakaochukua nafasi za kuendeleza mampambano hayo.

Naunga mkono hoja zako zote, niliyoandika hapa ni kutoa tahadhari tu ili ifahamike kwamba mapambano hayatafana bila kuwepo kwa viongozi wa kuyasimamia mapambano hayo.
Ningependa kuona viongozi wengi ndani ya chama hicho, na hasa vijana ambao wapo tayari kuchukua nafasi zao katika kuendeleza mapambano hata bila uwepo wa viongozi waliopo sasa.
 
Unapoweka mambo ya Muumba nadhani hata wapinzani siyo watakatifu.

Hasa linapokuja suala la fursa, na maslahi wanasiasa wote lao ni moja.

Hakuna mwanasiasa anaepambania HAKI out of nowhere, isiyo na attachment yoyote yenye maslahi yake.

Sasa hivi ukiwasikiliza wapinzani wote waliokuwa wabunge, ni kama bado wana hangover ya ubunge maana ni pesa za bure bure.

Mimi naamini watu wabaya wako vyama vyote na watu wema wako vyama vyote.

Mfano: Nyalandu aliyekuwa CCM ni binadamu mwenye utu kuliko Selasini au Mwita Waitara waliokuwa CDM.

Kitu kingine kinachoweza kusababisha CCM ipoteze uungwaji mkono mkubwa wa kutisha ni Rais kukatalia madarakani.

Ila kama wataendelea kuwa na 10 years limit, ni ngumu kuwatoa. Maana kisaikolojia binadamu ni mtu wa matumaini, ukiona watu wanaandamana kwa fujo maana yake wamekosa matumaini kabisa.
 
Mimi nadhani ushauri muhimu katika mada nzima iliyowasilishwa hapa ni kwamba, sasa ni lazima yawepo mabadiliko katika mbinu za upambanaji.
Kule kuendelea kuombaomba kumeshindikana, wanaoombwa hawana nia yoyote ya kuwepo kwa mabadiliko.
CHADEMA hawana jeshi la kupambana kivita na wenye silaha zote za wananchi wa Tanzania, ila wana watu ambao, kama wamedhamiria pawepo mabadiliko, hakuna silaha na jela zitakazozuia hilo lisitokee.

Akina Mbowe hawawwezi kwenda kupigwa risasi na kufia mbali kwa kuhimiza watu wakatae hadaa za watawala. Kwa kufanya hivyo watawekwa kizuizini, na kama wapo akina mbowe elfu hamsini, hawa wote watawekwa kizuizini? Hili ndilo litakalokuwa suluhisho la tatizo lililopo?

Kwa hiyo, kazi ya akina Mbowe sasa hivi ni kuhakikisha tu kwamba wapo akina Mbowe wengi watakaochukua nafasi zao wao watakapoondolewa na kuwekwa kizuizini.
 
Yaani wakiaandaa mkutano waandae kila kata nchi nzima tuone kama police wataweza kuwakamata kata zote Tanzania
Issue ni kwamba Police huwa wanayacontrol maandamano na kuyazima kabla hayajatokea kwa kupita mitaani na magari ya kutisha na gwaride plus mazoezi.

Siku ya maandamano hakuna anayetokeza.

Kwanza huyo anaye-organize mwenyewe atakamatwa hata siku ya maandamano haijafika.
 
Muumba namuweka kwa ajili ya wananchi siyo wanasiasa, wanasiasa ni vyombo tu

Upande unaosimamia haki kwa dhati pamoja na mapungufu yake Mungu huuinua!
 
Mkuu, sasa hivi kilicho wazi na kinachoonekana ni ubaya wanaofanya CCM, huo wa CHADEMA, pamoja na kwamba unaweza kuwepo ubaya kwao pia, hayo ni makisio yako tu?
Kama na wao au wengine wakipewa fursa ya kuongoza, wakifanya ubaya tutauona na itakuwa haki yetu kuukataa kama tunavyokataa huu sasa wanaofanya CCM.

Hatuwezi kuogopa kuwasema CCM ambao ubaya wao uko wazi, eti kwa kuogopa ubaya ambao CHADEMA hatujaona wakiufanya.
 
Hii ni Challenge kubwa ambayo wapinzani huwa wanakutana nayo!.

Njia ya kuvunja hii, ni maandamano ambayo ni incremental kwanza kabla ya kujenga momentum ya maandamano makubwa siku za baadae
Yaani watu waandamane sporadically katika makundi ya watu wachache wachache nchi nzima ili kuvunja hiyo myth kuwa watu huwa hawaandamani.

Kwa mfano show za Polisi hufanywa mijini, lakini pembezoni mwa miji na vijiji huwa hawafiki. Sasa maandamano ya Makundi ya watu yanaweza kufanywa huko pembezoni mwa miji na vijiji kama initial phase ya maandalizi ya maandamano makubwa.
Huko vijijini watu waandamane waende ofisi za serikali za vijiji, watendaji, etc
Baadae hiyo myth ikiwa shattered , itazidi kujenga awareness kwa raia wengi na baadae oneday umma utaingia mtaani tu!
 
Nimeanza kuogopa huenda Mbowe ni mamluki, kuna fursa nyingi kisiasa zinajitokeza lakini hazitumiwibipasavyo.
1. Tozo
2. Kukamatwa kwa wafuasi
3. Kuboronga kwa watawala kwa kutotii katiba hizi zote ni fursa kwa wapinzani kupata pa kuwaunganisha wananchi kupaza sauti kwa pamoja.
Mbowe ni mpinzani kweli au tunazugwa????
 
Unajua kipindi cha kudanganyana kimepita wanasiasa wote wanatafuta kula wao na familia zao ikibidi kusaza hakuna mtu asiye jua, mimi nampongeza Mbowe kwa kuwa muelewa wa mambo ya pesa, Unatoa ushauri mleta mada kama raia wa kawaida huko juu hari haiko hivyo.
Mboe anajua anachokifanya amekuwepo Ikulu tangia anamiaka 13 anasoma, anamsingi mkubwa na taifa hili muwe mnatafuta historia za watu kabla ya kuwaamini azawaizi anles mtakuwa mnapiga mak taimu.
 
Peleka akili zako za kuku kulee
 
Muumba namuweka kwa ajili ya wananchi siyo wanasiasa, wanasiasa ni vyombo tu

Upande unaosimamia haki kwa dhati pamoja na mapungufu yake Mungu huuinua!
Wananchi hawajahitaji mabadiliko. Wakiyahitaji yatakuja ndani ya wiki moja tu. Labda huwajui wananchi.

Na tatizo kubwa agenda za wapinzani hazina attachment kubwa na wananchi.

Fanya mikutano ya hadhara nzima uwasikilize wananchi, agenda zao ni tofauti kabisa.

Wengi watasema Afya, maji, elimu, ardhi, mafao, bei za mazao n.k.

Watu kama hao kuwaambia waandamane kwasababu ya katiba mpya siyo rahisi.

Mwananchi ambaye anaamka asubuhi anenda shambani, ziwani kuvua au kuchunga ng'ombe hawezi kuona ni kwa namna gani katiba mpya itamsaidia kwenye shughuli zake.

Kundi pekee litakalokwambia linataka Katiba mpya ni tabaka la kisiasa.
 
Spirit ya kipindi cha Slaa iliondoka na Slaa?
Chadema ilikuwa moto
 
Anyway, mimi sioni chochote wanachofanya CCM ambacho CDM hawajakifanya. Hasa kwenye eneo la Nepotism, Siasa chafu, ubaguzi, chuki, Impunity na Demokrasia.

Mwisho wa siku vitabadilika vyama, ila watu ni wale wale tu.

Uhuru Kenyatta wa KANU ndio huyo huyo wa Jubilee.

Hata Lowassa wa CCM ndio huyo huyo wa CHADEMA.
 
EeenHeeee!,
Utaniwia radhi kama itaonekana ninakufuatilia kila sehemu, lakini naona mabandiko yako yana mvuto nisioweza kujizuia kuujibu.

Yaani mkuu, unasubili, au unayo matumaini ya wachuga ng'ombe/mbuzi/wavuvi, n.k., WOTE wafikie hatua ya kuingia barabarani ndipo waweze kushiriki kuleta mabadiliko?

Hali ya namna hiyo uliwahi kuiona wapi duniani?

Ninakuhakikishia, nchi hii wakipatikana watu laki tano, waliodhamiria kabisa kuleta mabadiliko, utayaona mabadiliko, na hao wengine watakuwa ni washiriki wakubwa kwenye hatua za kumalizia mapambano hayo.
Usitegemee wote hao uwaone leo barabarani, au kutowaona barabarani ukadhani kwamba hawataki mabadiliko.
 
Vijijini watu wana maisha yao mengine kabisa.

Ni ngumu kwa mtu kuacha shughuli zake za kuchunga mifugo, kulima au palizi akaandamane kudai katiba mpya.

Unless kama utamwambia hiyo katiba itamsaidiaje kulinda mifugo yake na ardhi.

Ishtoshe vijijini kuna tawala tofauti na za kimila au Yowe zinazoheshimika sana, ambazo sidhani kama Chadema wana ushawishi huko.
 
Mimi sijawaona CHADEMA waking'ang'ania kubaki madarakani, na hata kukataa kabisa kuboresha katiba ili kura za wananchi ziweze kuwa na nguvu ya kuwabakisha madarakani au kuwaondoa.

Katika mambo yote, pengine hili kwangu ni la muhimu zaidi.
 
Wote CCM hao... Uchaguzi wa 2020 ni fundisho kubwa kwa upinzani. They should be ready for a bigger sacrifice. Amani itapatikana kwa ncha ya upanga tu. Vinginevyo, watakuwa ni kama NGO ya mambo ya siasa hadi mwisho wa dunia. The timing is right. Inategemea na jinsi watavyocheza karata zao.
Hata mimi nashangaa, kuna watu Wanataka Chadema itii tu amri ambazo siyo za haki.

Chadema wakiikubali hii hali maana yake ni kuwa kamwe hakitopata fursa ya kuwafikia wwnanchi ipasavyo na kutafuta kuungwa mkono.

CCM wanataka kuilimit Chadema isikue
 
Atanyea debe maisha yake yote, mdanganye!

Kwenu hakuna utawala ulio mzuri? Mkapa hakuwafaa, kikwete hakuwafaa kwamba alikuwa lazy, Magufuli kwenu alikuwa dictator, Madame president hafai tena kwenu?? mnataka nchi iongozwe na nani???

Kiukweli ni bora Tadea kuliko mawazo yenu, badilikeni...
 
Mimi sijawaona CHADEMA waking'ang'ania kubaki madarakani, na hata kukataa kabisa kuboresha katiba ili kura za wananchi ziweze kuwa na nguvu ya kuwabakisha madarakani au kuwaondoa.

Katika mambo yote, pengine hili kwangu ni la muhimu zaidi.
Ni nani anaeweza kumchallenge Mbowe leo akabaki salama.

Ni kwanini vifungu vya kikatiba vyote vilivyoonekana kumsumbua Mbowe alivibadili ?

Ni kwanini linapotokea jambo ambalo Mbowe huwa anaona lina maslahi kisiasa katiba huwa anaweka pembeni. Mfano halisi ni Lowassa kupewa fomu ya kugombea yeye peke yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…