MNYOO JOGOO
Senior Member
- Apr 2, 2012
- 195
- 94
BARUA YA WAZI KWA MWALIMU NYERERE, Mei, 2013
Mpendwa Mwalimu,
Tangu uondoke hali hapa Tanzania imebadilika.
Siku hizi mlima Kilimanjaro upo Kenya,
ziwa Nyasa liko Malawi,
Tanzanite iko Kenya,
TANESCO ni ya mtu binafsi na Rais wetu anaishi airport.
Mwl huku historia imebadilika kuwa Tanzania imetokana na visiwa vya Pemba, Unguja na Zimbabwe.
Mwl huku tumeingia katika rekodi ya maajabu ya Dunia kwani mwanafunzi anahitimu darasa la saba hajui kusoma wala kuandika na anafaulu mtihani anaingia Sekondari.
Mwl huwezi kuangalia TV mpaka uwe na kisambuzi (nikija nitakueleza maana yake) kutizama ligi ya matusi Bungeni.
Mwl baada ya wanafunzi kufeli sana mwaka 2012, serikali inaangalia
uwezekano na mpango mpya wa kunusuru waliofeli kwa kutumia viwango vifuatavyo:
A=40% - 100%
B=20% - 39%
C=10% -19%
D=3% - 9%
F=0% - 2%
Bado hawajaamua wafanyeje.
Pumzika huko huko uliko Mwalimu maana ukija utakufa tena ghafla.