BARUA YA WAZI KWA MWL NYERERE, Mei , 2013

MNYOO JOGOO

Senior Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
195
Reaction score
94
BARUA YA WAZI KWA MWALIMU NYERERE, Mei, 2013

Mpendwa Mwalimu,

Tangu uondoke hali hapa Tanzania imebadilika.

Siku hizi mlima Kilimanjaro upo Kenya,
ziwa Nyasa liko Malawi,
Tanzanite iko Kenya,
TANESCO ni ya mtu binafsi na Rais wetu anaishi airport.

Mwl huku historia imebadilika kuwa Tanzania imetokana na visiwa vya Pemba, Unguja na Zimbabwe.

Mwl huku tumeingia katika rekodi ya maajabu ya Dunia kwani mwanafunzi anahitimu darasa la saba hajui kusoma wala kuandika na anafaulu mtihani anaingia Sekondari.

Mwl huwezi kuangalia TV mpaka uwe na kisambuzi (nikija nitakueleza maana yake) kutizama ligi ya matusi Bungeni.

Mwl baada ya wanafunzi kufeli sana mwaka 2012, serikali inaangalia
uwezekano na mpango mpya wa kunusuru waliofeli kwa kutumia viwango vifuatavyo:
A=40% - 100%
B=20% - 39%
C=10% -19%
D=3% - 9%
F=0% - 2%

Bado hawajaamua wafanyeje.
Pumzika huko huko uliko Mwalimu maana ukija utakufa tena ghafla.
 
barua nzuri sana. natamani kama kanaatakaye mfikishia. Pumzika kwa AMANI MWL.
 
Mwambie pia katibu mkuu wa chama chake anatuhumiwa kwa ujangiri wa pembe za ndovu
 

Umesahau kumwambia haya.
Ule udini ulioupanda sasa ndio umekolea.
 
Umesahau jambo mmoja kubwa kwamba misingi aliyoiacha imefanya watanzania wengi kuwa namimba za kufikiri,hawapendi kufikiri na wengi wao wamewakabidhi akili zao wanasiasa na viongozi wadini, wao kiakili wako likizo tangu 1961,na hii mbegu ulipandwa wewe mwalim,usisahau kumwambia na hili.
 
Usisahau kumwambia kuwa ccm siku hizi inatumia mapolis kwa ajili ya kupambana na wapinzani wake, na kupokonya ushindi wa wapinzani hasa vijijini kama wenyeviti wa vijiji waliochaguliwa kwa vyama vya upinzani!
 
Umwambie pia siku hizi kwenye chama chake sifa kubwa ya kuwa kiongozi wa juu ni kujua kutukana matusi makubwa ya nguoni hasa kuwatukana wasiokubaliana na chama, kuwa katibu wa chama ni lazima uwe na rekodi nzuri ya uhujumu uchumi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…