PostGE2025 Barua ya wazi kwa Othman Masoud na Jussa - Mtoseni Samia muinusuru Zanzibar

PostGE2025 Barua ya wazi kwa Othman Masoud na Jussa - Mtoseni Samia muinusuru Zanzibar

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
17,047
Reaction score
63,206
Salam ndugu Othman Masoud na Jussa

Bi mkubwa kwa sasa ni rais asiyekubalika na wananchi kwa hiyo kufanya siasa zozote za kumlinda na kumsaidia "mwenzetu" apate ahueni ya kutawala hakutaisaidia Zanzibar na wala hakuisaidii ACT, sanasana kunaisaidia CCM.

Nasema hivi kwa sababu sasa hivi bi mkubwa anapambana na mambo makuu mawili, mosi kutumia muda wake mwingi kuficha ushahidi wa uhusika wake na watu wake wa karibu dhidi ya mauaji holela ya maelfu ya wananchi wasio na silaha katika maandamano ya october 29. Na pili kuna kundi ndani ya CCM linawaza urais wa 2030, Hili kundi litaanza kuchachamaa baada ya miaka miwili au mitatu ijayo , litakuwa busy na ishu za uchaguzi huo na hivyo Bi mkubwa atakuwa hana nguvu wala control ya kutosha ya kiserikali kwenye ishu za maendeleo na hivyo hata Zanzibar haitonufaika kivile.

Na pia lazima mfahamu kuwa ili bi mkubwa awe salama baada ya kustaafu lazima atahikikisha Huko Zanzibar mwaka 2030 anawezesha figisu katika uchaguzi wa Zanzibar ili iendelee kukaa CCM madarakani pande zote mbili za muungano ili astaafu kwa amani. Kwa hiyo ACT itaendelea kuchezewa figisu hata katika chaguzi zijazo.

Sasa cha kufanya, ni lazima mpandishe joto la kisiasa nchini kwa kuleta mbele madai yenu ya mamlaka kamili ili kwenye suala la katiba mpya ambalo bi mkubwa anakusudia kulianzisha basi awakute tayari muwe grounded katika madai yenu. Huu ukimya wenu wa kimkakati kwa ajili ya kumsaidia "Mwenzetu" ili atawale smoothly kwa sasa haufanyi kazi tena, na mkiendelea nao mtajikuta mmekamatwa offguard na kushindwa kutetea maslahi ya Zanzibar ipasavyo kwa sababu joto la kisiasa huko Zanzibar litakuwa limepozwa na CCM ikisaidiwa na nyie kwa kujua au bila kujua.

Pili chama chenu cha ACT kimepoteza mvuto mno kwa umma kwa sababu ya kushiriki uchaguzi ambao mnajua, Tanzania inajua na Afrika inajua kuwa kamwe usingeweza kuwa huru na haki. Hata hivyo mliingia mkidhani mnamsaidia "dada" na kwa maslahi mapana ya Zanzibar, Hivi sasa baada ya uchafuzi ule na mauaji ya oct 29, ACT imepoteza uungwaji mkono mno Tanganyika na hata Wazanzibar wameanza kujiuliza je kweli mpo kuichallenge CCM au mpo tu kwa ajili ya nafasi chache za SUK za kugawiwa mkate kidogo na CCM mtulie?.

Sasa basi nawaandikieni haya ili muweze kuinusuru Zanzibar na ACT.

1. Pandisheni joto la kisiasa Zanzibar kwa kutoingia ktk SUK. Na hoja zenu ziwe ni uchaguzi haukuwa huru na haki. Mkifanya hivi wananchi angalau warawaheshimu kuwa japo CCM haikuheshimu kura zao kwa kuzichakachua nyie mmeziheshimu. Hii itarudisha imani ya wananchi kwenu

2. Dada yenu sasa hivi anapambana kujinusuru, msimuonee huruma, huyu sasa hawezi kuwapa changes za kikatiba mnazozitaka kwenye silver plate. Pandisheni joto la kisiasa visiwani, Throw her under the bus, ili kwenye negotiating table ya mambo ya katiba muangalie future ya Zanzibar kuliko kulinda mtu. Kumbukeni huyu mama kesho na keshokutwa anaondoka kwenye hicho kiti ataingia mtanganyika. Msipokuwa wakali kama pilipili now huyo mtanganyika ajaye atawachelewesha sana. Kwa hiyo now is the time muwashe moto wa kisiasa huko Zenji. Msikubali kughilibiwa na wazee watakaotumwa kuwapoza. CCM ndo mbinu yao hiyo, tayari wana wazee wao wa kupoza mambo wakishaharibu.

Nawatakieni siku njema.
 
Act ni mpango wa kando wa sisisemu kuua upinzani wa kweli,kumbuka Mh.Polepole alishasema hivyo ni vyama rafiki.
 
Hao akina Jusa hata hao wapemba hawawaamini kama walivyokuwa wanamkubali Seif. Lakini kitendo cha wao kukubali kuingia kwenye uchaguzi na mapungufu haya, kumewapunguzia imani sana kwa wapiga kura wao. Labda warukie agenda ya mamlaka kamili ili wabakishe imani ya wananchi wao, kinyume na hapo ndio imetoka hiyo.
 
Mbona walishagoma kujiunga SUK na hata wawakilishi wao wamegoma kuapa!!

Licha ya hilo Othman Masoud alikua serikalini kabisa kabla ya kutimkia ACT namuonaga kama mtu wa mfumo ndio maana mwaka huu licha ya wao kukiri kuibiwa kura hakukuwa na maandamano tofauti na miaka yote ilikua lazima kuwe na mshike mshike baada ya uchaguzi.
 
Nilisikia wamegomea kuungia kwenye Serekali, lakini kwa tone ya chini sana, hawana lile vibe la miaka yote. Na sababu hasa ya kujifanya kuvuta kamba ni haya machafuko yaliyotoea huku bara. Iwapo huku Tanganyika kusingefanyika kilichitokea baada ya uchaguzi, wangeingia haraka kwenye SUK. Wapo nje wakipima upepo.
 
Hao akina Jusa hata hao wapemba hawawaamini kama walivyokuwa wanamkubali Seif. Lakini kitendo cha wao kukubali kuingia kwenye uchaguzi na mapungufu haya, kumewapunguzia imani sana kwa wapiga kura wao. Labda warukie agenda ya mamlaka kamili ili wabakishe imani ya wananchi wao, kinyume na hapo ndio imetoka hiyo.

Kete ya mamlaka kamili ndiyo kete peke ya kuwarudishia imani ya Wazanzibari
 
Mbona walishagoma kujiunga SUK na hata wawakilishi wao wamegoma kuapa!!

Licha ya hilo Othman Masoud alikua serikalini kabisa kabla ya kutimkia ACT namuonaga kama mtu wa mfumo ndio maana mwaka huu licha ya wao kukiri kuibiwa kura hakukuwa na maandamano tofauti na miaka yote ilikua lazima kuwe na mshike mshike baada ya uchaguzi.
Yule ni hana tofauti na Lipumba, na zitto kabwe waliishapokea chao wakaambiwa washiriki uchaguzi ili kutoa legitimacy ya uchaguzi huru na haki kwa Dr.Mwinyi.

Hata ukimuangalia kwenye kampeni alikuwa anaongea kama mshenga.

Jusa naweza kumuamini lakini sio othman masoud.

Kumbuka bila ACT hata Zanzibar ingekuwa worse than Tanganyika.

Wapiga kura wasingekuwepo kabisa.

Na 2030 utashuhudia hili.
 
Othman Masoud na Samia hawakukutana barabarani.

Lakini akiweka urafiki wao mbele akaacha maslahi mapana ya Zanzibar basi atakuwa hawatendei haki wazanzibari na watamuona msaliti.
 
Back
Top Bottom