Barua ya wazi kwa Rais: Mhesimiwa, Mungu ametusikia sasa na wewe tusikie

Barua ya wazi kwa Rais: Mhesimiwa, Mungu ametusikia sasa na wewe tusikie

Zakawaida zipi ??? Mheshimiwa misaili,labda uziweke hapa tuzitafakari na kila Mtanzanaia ataona Mheshimiwa usibanie unachokijua na kuona kitafaa labda serikali imeghafilika.
Angalizo :Siku serikali ikisema atakaekamatwa hajavaa barakoa atapigwa faini shilingi 50000/ mtarudi hapahapa na kusema serikali kandamizi
Inaelekea hujasoma barua nzima, rudia tena kusoma, utaziona ziko clear kama mwezi mpevu
 
Mheshimiwa Rais

Yesu anasema kuwa, kabla hamjaomba chochote kutoka kwa Baba yenu aliyeko mbinguni yeye ameshatambua mkitakacho!

Tulipofunga na kusali kwenye wimbi la kwanza la korona, Mungu alitusikia na alituonyesha kitu gani cha kufanya kwenye hili tatizo ili tunusurike.

Mheshimiwa Rais, kwenye wimbi la kwanza la Korona Taifa Zima na Serikali yao tulichukua tahadhari. Kwenye wimbi hilo serikali yako ilichukua hatua zifuatazo:

1. Ilifunga mashule kuwalinda watoto na pia kuzuis watoto kuusambaza ugonjwa kutokea mashuleni

2. Ilizuia michezo

3. Iliweka uraratibu wa vyombo vya usafiri kuwa na level seat

4. Serikali yako kwa tamko lako wewe binafsi ulitangaza kuviomba vyombo vya habari viwe wadau na vishiriki kuuleisha umma juu ya ugonjwa huu

5. Serikali yako ilihimiza watu kunawa, na wananchi wakaitikia kwa wingi kwa kuweka ndoo za maji kila kona ya nchi

6. Baada ya kelele nyingi za wananchi Serikali yako ilifunga mipaka.

7. Serikali yako ikshimiza maombi kwa Mungu atusaidie

Mheshimiwa Rais, ukiangalia orodha hizo hapo juu utaona kuwa katika wimbi la kwanza Serikali yako ilifanya kitu, ilichukua hatua za msingi za kuzuia tatizo hili kusambaa na kwa kweli tulifanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Mheshimiwa Rais, kwa bahati mbaya kwenye wimbi hili la pili la huu ugonjwa serikali yako inataka kujitoa katika wajibu wa kuhakikisha usalama wa wananchi katika maambukizi haya mapya!

Mheshimiwa Rais, kama serikali yako inachukua hatua

1. Kwanini mpaka hivi sasa serikali haitamki Ugonjwa wa COVID-19 kwa uwazi kabisa na kwa jina lake?, Wananchi watajuaje kuwa kuna COVID-19 kama huo ugonjwa hamuutamki kwa jina lake?

2. Kwanini pamoja na kutambua kuwa Korona haijaisha duniani serikali yako iliendelea kuruhusu watalii kuja nchini tena wengine kutoka katia nchi ambazo zilikuwa zikiripoti kuwa korona imechachamaa mathalani nchi ya uingereza?

3. Kwanini mpaka hivi sasa serikali yako haichukui hatua, japo baadhi ya zile ilizochukua katika wimbi la kwanza ikiwemo kuzuia mashabiki kujazana michezoni, mbona katika nchi nyingine ambazo timu zetu zinakwenda kucheza mashabiki hawaingii uwanjani?

4. Kwanini viongozi wa serikali yako ukiwemo wewe mwenyewe ukiwa kwenye public hamuongozi kwa mfano ili wananchi waweze kuwa na kigezo kizuri kutoka kwenu, kwa mfano hamvai barakoa wala kuweka social distance, Je maneno yenu ya kuwaabia wananchi wachukue tahadhari yatatafsirika vipi kama nyie wenyewe hamuyaishi in public?

4. Mheshimiwa Rais Kwanini mara nyingi umesikika ukiipiga vijembe barakoa, au ukiwapongeza wasiozivaa in public. Je hatua yako hiyo inasaidiaje mapambano dhidi ya Korona?

Mheshimiwa Rais, Mtume Muhammad amefundisha kuwa, Mfunge Ngamia wako asikimbie kisha Muombe Mungu amlinde ili asikimbie, siyo umuache hivihivi kisha eti ukazane na maombi Mungu amlinde!

Mheshimiwa Rais, umeuliza kuhusu kurudi kwa wimbi hili la pili kuwa tumekosea wapi?

Tulipokosea ni kwamba tuliacha kuwa serious kwa kitu ambacho Mungu ameshatuonyesha ukweli wake. Tumekuwa tukikataa kuwa hakuna korona nchini wakati tunajua ipo. Tumekuwa tukikejeli njia za kujikinga kama vile kuzipiga vijembe barakoa, Tumekuwa hatutaki kuuita ugonjwa hata kwa jina lake halisi, Tumekuwa tukiruhusu wageni kutoka nchi zilizoathirika na ugonjwa kuingia nchini kisa tunataka fedha, Tumekuwa hatutaki kujenga awareness kwa kumobilize nguvu zote za serikali kuuelimsha umma kuhusu kuchukua tahadhari za ugonjwa huu.

Mheshimiwa Rais, Mungu anajua ayafanyayo, katupa bongo tuzitumie, katupa utashi wa maamuzi, katupa zawadi ya wataaamu miongoni mwetu baadhi yao ni madaktari, Sasa basi Kumuomba Mungu ni jambo jema lakini tunatska kuona unachukua hatua na uwajibikaji katika hili suala!

Mheshimiwa Rais, Unahoji kama tuna imani kwa Mungu la, jibu ni naam Imani tunayo na tunamuomba alinde maboma yetu lakini tunafunga maboma yetu usiku kabla ya kulala, Sasa na wewe ndiye mkuu wa hili boma liitwalo Tanzania, wakati ukitaka kila mtu achukue hatua, Pia umbuka na wewe unaowajibu kama mkuu wa boma hili la Tanzania kuchukua hatua za kulinda boma zima!

Mheshimiwa Rais, unasema kufa kupo, magonjwa yapo kwa hiyo tuondoe hofu!. Mheshimiwa hatuondoi hofu kwa sababu ya kuamini hayo magonjwa yapo, tunaondoa hofu tukiamini kuwa ipo serikali responsible itakayofanya kila inayoweza kutunusuru huku na sisi tuitimiza wajibu wetu kujinusuru. Bila ya kuona kuwa seriali inafanya vitu fulanifulani vya msingi kama nilivyoekeza huko juu tutaendelea kuwa na hofu, maana huwezi kupambana na ugonjwa wa halaiki wewe peke yako ni lazima nchi nzima muwe vitani. Sasa serikali itakwepaje wajibu wake hapo?

Mheshimiwa Rais, Mungu anafanya yake na kwa muda wake, sasa na wewe chukua hatua sahihi kulinda Taifa hili dhidi ya hili janga!
Kwamba Maalim (rip) au hata mshirika wako wa karibu kabisa kwenye doctrine yako ya hofu Balozi Kijazi (rip) wamefeli kwa sababu ya hofu? Mbona itakuwa ni kuwacheza shere wahanga wa ugonjwa huu?

Wahanga wote wameshindwa kupumua! Kupumua = hofu ?

Labda kama wanadhani tu watoto wadogo:

 
Hospital ya uhuru Dom kuna ze nyungus? Nafuatilia michango yako kama umekengeuka

Nimekujibu kwenye hiyo Id yako nyingine. Soma huyo kiazi mwenzako niliyemquote kaandika nini, na nimemjibu nini.
 
Nimekujibu kwenye hiyo Id yako nyingine. Soma huyo kiazi mwenzako niliyemquote kaandika nini, na nimemjibu nini.
Umefanya nicheke bure. Kwa hiyo wewe ni mtalaamu wa id za Jf? Mbona unakwama?
 
Umenena vema. Ni jibu sahihi kwa swali la Rais - wapi tumekosea.
 
Walioweka lokidowni wote wamezifungua na bado tatizo lipo,mnapomsikiliza Raisi mengine naona yanawapita na mnachagua yale mliyotulia nayo,

Mnataka Raisi afanye au aseme kitu gani ? Akili zenu zipo wapi ? afunge mashule ? Afunge safari za kuingia na kutoka mkoa kwa mkoa,wilaya kwa wilaya kijiji kwa kijiji mtaa kwa mtaa ??

Kuna shemu mmekosea mliambiwa habari ya nyungu mmeachana nayo,mbona wimbi la mwanzo wanancho nyote mlikuwa mnapiga nyungu,mlipozoea na kuona mafanikio mkawacha,sasa Rais akisema yeye kila siku anapiga nyungu mtasemaje ? Na tunamuona anachanganyika na watu kila aina.
Nyungu ni zoezi endelevu.
Nyungu ni upuuzi, nyungu siyo tiba. Nyungu haina mchango wowote positive katika kupambana na corona.

Nyungu wanaweza kupiga watu kama fashion mpya ya kuwafurahisha waganga wa kienyeji lakini siyo kuambana na corona. Kasome jinsi corona inavyoshambulia halafu utaona nafasi ya nyungu katika kuhatarisha maisha ya mgonjwa.

Nawaambieni ndugu zangu:

USITHUBUTU KUMWEKA MGONJWA WAKO KWENYE NYUNGU, UTAHARAKISHA SAFARI YAKE YA KUELEKEA KABURINI. ANAYEHAMASISHA NYUNGU KWA WAGONJWA WA CORONA, NI MUUAJI.
 
Huyo mtu ni mtu wa ajabu kuwahi kupewa nafasi aliyonayo.Kuwa mtu wa ajabu ni jambo la kawaida.Ila kuwa mtu wa ajabu mwenye madaraka ni hatari sana.Kuna usemi wa kuwa kuna watu elimu haijawasaidia hususani kwenye kufikiria kama wasomi.Miongoni mwao ni huyu mtesi wetu.Bora hofu ya Corona kuliko hofu waliyonayo watendaji wako ya kuogoba kutinduliwa kwa kuumwaga ukweli kuwa corona tunayo
 
Nyungu ni upuuzi, nyungu siyo tiba. Nyungu haina mchango wowote positive katika kupambana na corona.

Nyungu wanaweza kupiga watu kama fashion mpya ya kuwafurahisha waganga wa kienyeji lakini siyo kuambana na corona. Kasome jinsi corona inavyoshambulia halafu utaona nafasi ya nyungu katika kuhatarisha maisha ya mgonjwa.

Nawaambieni ndugu zangu:

USITHUBUTU KUMWEKA MGONJWA WAKO KWENYE NYUNGU, UTAHARAKISHA SAFARI YAKE YA KUELEKEA KABURINI. ANAYEHAMASISHA NYUNGU KWA WAGONJWA WA CORONA, NI MUUAJI.

Anayeamini nyungu sio muuaji tu, bali ni mshirikina wa nguvu.
 
Walioweka lokidowni wote wamezifungua na bado tatizo lipo,mnapomsikiliza Raisi mengine naona yanawapita na mnachagua yale mliyotulia nayo,

Mnataka Raisi afanye au aseme kitu gani ? Akili zenu zipo wapi ? afunge mashule ? Afunge safari za kuingia na kutoka mkoa kwa mkoa,wilaya kwa wilaya kijiji kwa kijiji mtaa kwa mtaa ??

Kuna shemu mmekosea mliambiwa habari ya nyungu mmeachana nayo,mbona wimbi la mwanzo wanancho nyote mlikuwa mnapiga nyungu,mlipozoea na kuona mafanikio mkawacha,sasa Rais akisema yeye kila siku anapiga nyungu mtasemaje ? Na tunamuona anachanganyika na watu kila aina.
Nyungu ni zoezi endelevu.

IMG_20210218_174254_207.jpg


Eti kwamba walikokuwa lockdown wamezifungua hali iko pale pale. Habari hizi huwa mnadanganyiana Lumumba?
 
Back
Top Bottom