Barua ya wazi kwa Sheikh Mziwanda na Dr. Sule: Acheni kutetea dhulma dhidi ya Watanzania wenzenu

Sheikh Mziwanda yeye hukaa pale, akiona fukuto la joto la wananchi kuingia barabarani kudai haki tu basi atakuja na ushawishi kibao kwa waislamu wa "amani", "utulivu", "mbona rais akiwa mkiristo haiwi hivi, haiwi vile". Sijawahi kumuona hata siku moja akiteyea wananchi dhidi ya Udhalimu wa watawala
 
kukariri Quran ndio inakuwaje ni zaidi ya kila kitu ikiwa mambo ya kawaida tu masheikh wanatia aibu? Tangu lini mtu anaekariri akawa na akili?
Mkuu una hoja ila tuzidi kuwekeza fikra katika hoja yako....

Ni kweli wako wanaokariri tu na wasielewe maana yake.....

Ni kweli wako wanaopoteza muda kukariri elimu yoyote ile ila wasiielewe kwa undani na kuiishi......

Wako waarabu wanaojua kiarabu na wameshindwa kukariri hiyo Qur'an.....na wako waliokariri na wakaelezwa maana ya kila aya na wakafahamu vyema ila bado wakashindwa kuilewa maana yake ya ndani (Batin)....ndio wale wanaounga mkono UGAIDI na hata wakajilipua na kuwahiliki wengine......

Sheikh Ahmad Zarruq katika kushajiisha juu ya uelewa mpana wa elimu yoyote iwayo akasema maneno haya yafuatayo :

"Never give wisdom to unworthy as it unjust to the knowledgeables".

WISDOM.....

Unapoitafuta elimu ,usitumie tu nguvu kuipata bali nguvu na maombi kwa Mungu uyaelekeze akupe BUSARA juu ya hiyo elimu....

#Do Not Do Harm😍

#Milele ardhi tukufu ya Tanzania😍
 
Baadhi ya masheikh wananisikitisha sana yaani wapo "kimkakati" sana.

Utafikiri wamepewa maelekezo maalum na kitengo kutuliza mambo, au kutumika kwenye ile "wagawe uwatawale"

Au pengine wanajipendekeza tu kwa watawala!
Mada zako kuhusu maswala haya huwa unazipa tafakuri kubwa inayo stahili. Hizi ni mada ngumu sana kuzijengea ukuta wa kutoonyesha unako lalia mwenyewe.

Pamoja na kukubaliana na lawama unakozielekeza wewe; kwa viongozi wa kidini binafsi kama hao mashekh wawili ulio waandikia, binafsi lawama ninazielekeza kwanza kabisa kwa hao viongozi wa kisiasa; hasa huko ndani ya CCM. Tatizo linaanzia huko na huko ndiko litakapo malizikia au litakapo lipukia iwapo litaendelea kurutubishwa.
 
Unawezaje kuwatofautisha ikiwa tunaambiwa waislamu ni wamoja?
Unaweza kuwatofautisha kutokana na hizo kauli zao uislamu unapinga dhulma bila ya kujali hiyo dhulma imefanywa na nani muislamu wa kweli hawezi kuunga mkono dhulma
 
Ndugu Masheikh
Nimewajibika kuandika barua hii kuwaomba kwa unyenyekevu mkubwa ACHENI KUTETEA dhulma dhidi ya watanzania wenzenu ktak madhila yanayowakumbuka.

NIANZE NA SULE
Wakati wa sakata la Ngorongoro, Mwanamihadhara ndugu Sule aliandaa clip ambayo ilisambazwa katika makundi ya kijamii ikieleza kuwa wamasai waishio ngorongoro ni wakenya waliovamia maeneo hayo kutoka Kenya. Katika kauli hizo akajaribu kuwaaminisha watanzania kuwa hao wamasai walioko ngorngoro hawastahili kuonewa huruma pindi serikali ikijaribu kuwatoa kwa sababu ni Wakenya.
Kauli hii ilikuwa ni ya ajabu sana hasa ukizingatia kwanza ni uongo, maana wamasai walioko ngorongoro walihamishiwa hapo na serikali hiyohiyo ili kupisha uanzishwaji wa hifadhi ya Serengeti miaka ya 1960's. lakini ukiachilia mbali hilo ile ni kauli isiyo na chembe ya huruma kwa watanzania wenzetu waishio ngorongoro ambao, walikuwa wananyimwa kila aina ya haki za kiraia na utawala huu wa Samia ili kuwapa maisha magumu waondoke. Kusema uongo ni kinyume cha Agizo la Mwenyezi Mungu anayetaka watu waseme ukweli!
Hata hivyo ndugu Sule amekuwa akilalamikiwa na waislamu wenyewe kwa kulete mafundisho ambayo wao wanaita ni Shirki, kwa kutangaza pete za Majini kuwa eti zina msaada kwa watu kitu ambacho masheikh wenzie wamempnga vikali kuwa asilete SHIRKI katika dini.

KWA SHEIKH MZIWANDA
Ndugu Sheikh mziwanda, umesikika ukidai kuwa wanaotekana nchini ni CHADEMA wenyewe, na ukatoa mfano wa Clip ya Dr Slaa ya miaka takriban minne akizungumzia tukio la kutekana katika chama. Kinachonisikitisha unanasibisha matukio ya sasa kwa kusema kuwa ni CHADEMA wanafanyiana hayo.
Ndugu Mziwanda, Muogope ALLAH, Tafadhali sana ndugu yangu, Wewe mwenyewe umesema una listi ya watu zaidi ya 100 waliotekwa kipindi cha Magufuli, Je Ndugu mziwanda hao wote walitekwa na CHADEMA?- Mo Dewji alitekwa na CHADEMA?,Roma mkatoliki alitekwa na CHADEMA?, Azory Gwanda alipotezwa na CHADEMA?

Kwenye kauli yako ukasikika unasema kuwa kipindi cha Magufuli walipotea zaidi ya watu 100, ukahoji kuwa mbona hakukuwa na maandamano?- Kwa hiyo ndugu Mziwanda, unataka kutwambia kuwa kwa kuwa watu hawakuandamana kudai jambo fulani kipindi cha nyuma basi ni makosa watu hao kuandamana kutaka jambo fulani leo hata kesho?. Sisi tunapata mashaka ndugu Mziwanda kuwa unataka kuchomeka hisia za udini, unataka watu waone kuwa kwa kuwa mtawala wa sasa ni muislamu basi kila dai lolote la msingi ambalo raia wa nchi hii wanalo basi eti wanaweka presha kwa sababu rais ni muislamu. NDugu mziwanda hiki unachokifanya ni kibya mno, si chema na kwa kweli kinagawa watu kuliko kujenga!

MZIWANDA, wewe hujitokeza mara nyingi wananchi wanapokuwa na ishu na serikali yao, wewe husimama kuitetea serikali tena kwa kuwagawa waislamu wajitenge na madai ya msingi ya kitaifa. Ulifanya hivyo katika mimbari kutetea uuzwaji wa bandari, ukadai kuwa mama anashambuliwa kwa imani yake.
Leo Umma unataka kutumia haki zao za kikatiba kuandamana ili mauaji na utekwaji vikomeshwe, wewe unakuja na kuongea na waislamu eti wajitenge na mambo hayo. SHEIKH HIVI UNASIMAMIA HAKI AU UNAWALINDA WATAWALA?

Sheikh: Kwani mtume si alisema ukiona jambo baya/ovu liondoe kwa mkono wako, ukishindwa kemea uovu huo, na kama kukemea huwezi si mtume alisema chukia?- SASA WEWE unasimamia wapi katika hayo matatu kuhusiana na matendo ya kutekwa, kupotezwa na kuuawa watu?. Je hutaki watu waingie mitaani kukemea uovu huo unataka wafanyeje?. Umesema kuwa wakati wa Magufuli walipotea watu zaidi ya 100, LINI WEWE UMEWAHI KUKEMEA JAMBO HILO WAZIWAZI UMMA UKAKUSIKIA?

SHEIKH MZIWANDA SI KWA SABABU SAMIA NI MUISLAMU BASI UNAJARIBU KUMLINDA NA KUMKINGIA KIFUA KWA KILA KITU KIBAYA!.

Ndugu Mziwanda, Mwenyezi Mungu katika Qur'an anasema kuwa sema kweli hata kama ukweli huo "unakunyooshea kidole" wewe mwenyewe. Sasa kama mtu inabidi ujishuhudie ukweli hata kama ukweli huo uko dhidi yako kwa nini unamkingia Kifua Samia eti kwa sababu Samia ni muislamu mwenzako tu?.
Je umesahau Khalifa mmoja wa kiislamu amewahi kumpa haki Myahudi licha ya kuwa kuna shauri mbele yake lililetwa linalomhusu muislamu na myahudi. Kwa nini alimpa haki myahudi badala ya muislamu mwenzie?

NDUGU MZIWANDA: Umekuwa ukijaribu kuwatenga waislamu wasiungane na watanzania wenzao kwa hoja za 1. Amani, 2. Mbona wakati wa magufulihaikuwa hivi
Ningependa kukwambia tu kuwa wanaotekwa, kupotezwa na kuuawa siyo wakiristu tu bali hata waislamu pia. Mo Dewji ni muislamu, Mzee Ally kibao ni muislamu. Sasa kwa nini hutaki waislamu waungane na waislamu wenzao kupaza sauti kukataa udhalimu huu?

SHEIKH MZIWANDA: Napenda nikukumbushe tu kuwa ukizuia WENGI KUDAI HAKI basi mtu mmoja mmoja kwa siri au kwa dhahiri ataamua kuidai peke yake, Je unajua kitakachotokea pale mtu mmoja bila kushawishiwa na mwingine, au kwa kumshirikisha mwingine ataamua kulipa kisasi?.

SHEIKH tafadhali tetea haki ya watu, usitetee "ULUA" wa watawala!
Asante Mkuu.

Maandamano ya kujikomboa kutoka kwa watesi ni ‘ Kuacha kutoa sadaka’

Mungu yupo kila mahali. Maandiko yanasema ‘’usalipo sirini… Ombeni nanyi mtapewa..’ Fanyeni ibada majumbani mwenu, toeni sadaka kwa wenye uhitaji mfano mahospitalini, kwa yatima na wajane etc.

Sio kila mhubiri ni mtumishi wa Mungu wa kweli! Nyumba za ibada ni nyumba za biashara za watu.

Siku tukilitambua hili basi tutakombolewa.

Nyumba za ibada zimegeuka mshale na msumari wa moto kwa ukombozi wa mwafrika…
 
Quran inatutaka kabla ya kuzungumza jambo kwanza tulifanyie utafiti wa kutosha
Au masheikh kama kweli wamefanya hayo wanatakiwa watubu. Sio muongozo wa dini.

Katika Qur'an, kuna aya kadhaa zinazosisitiza umuhimu wa kufanya uchunguzi wa jambo kabla ya kutoa uamuzi au kuamini kitu.

Moja ya aya maarufu ni kutoka Surah Al-Hujurat (49:6), ambapo Allah anasema:"Enyi mlioamini! Mkiletewa habari na fasiki yoyote, ichunguzeni kwa makini, msije mkawadhuru watu kwa ujahili, na mkawa wenye kujuta kwa mliyoyatenda."
(Qur'an 49:6)

Aya hii inatoa mwongozo wa kidini kwa waumini kuhusu umuhimu wa kufanya uchunguzi wa habari au jambo lolote kabla ya kuchukua hatua, ili kuepuka kufanya maamuzi mabaya au kuumiza wengine bila sababu. Hii inahimiza kuwa na tahadhari na kufanya utafiti wa kina kabla ya kuchukua hatua yoyote.

AO MASHEIKH WAMEFANYA UTAFITI ?
 
Ukweli ni kwamba katika Uislam kuna taratibu zilizowekwa katika kuamiliana na watawala. Haifai kuminyamana na watawala. Tumeamrishwa kuwatii watawala katika yasiyo ya haramu na kuwa na subra katika dhulma ya mtawala.

Na haifai kumkosoa mtawala hadharani, anayetaka kumnasihi mtawala amshike mkono au amuandikie kwa siri amnasihi. Umekutana na mtawala uso kwa macho hapo sasa ndio umepata fursa ya kumnasihi, basi mnasihi kwa busara iwapo kama ni kweli unataka kutoa nasaha. Au muandikie. Haifai kumtukana.

Lakini haifai kuwapinga na kuwakosoa hadharani. Sikuambii kuwafanyia uasi ndio kabisa.

Na kuhusu maandamano sijui mapinduzi hayafai. Sisi tumefundishwa kuwa na subra kunako dhulma ya mtawala. Hawawi madhalimu watawala ila kwa sababu ya dhulma za raia.

Dhulma ikidhihiri miongoni mwa watu; kukajaa washirikina wanaoabudu wengine pamoja na Allah au wakawaabudu wengine badala ya Allah, au kukajaa wazinifu, wezi, wadokozi, matapeli, waonevu na wenye kupokonya haki za watu na kadhalika basi Allah atawaoneshea athari ya maovu yao kupitia watawala wao. Watayaona hayo kwa watawala wao. Hivyo wakitaka kuondolewa watawala madhalimu, basi waache wao kwanza dhulma.

Ila migomo, maandamano, uasi na mapinduzi unazidisha shari na uharibifu na kuondoa amani.

Nimeandika haya sio kwa sababu hao "dokta" Sule na Sheikh Mziwanda ni masheikh zangu. Hapana. Allah awaongoze.

Allah atuongoze katika njia iliyonyooka. Allah atengeneze mioyo ya watawala wetu, awaongoze katika njia iliyonyooka, awafanyie wepesi na awape hikma na uadilifu. Allah aidumishe amani tuliyonayo, Yaa Hayyu Yaa Qayyum. Ameen.
 
Asante Mkuu.

Maandamano ya kujikomboa kutoka kwa watesi ni ‘ Kuacha kutoa sadaka’

Mungu yupo kila mahali. Maandiko yanasema ‘’usalipo sirini… Ombeni nanyi mtapewa..’ Fanyeni ibada majumbani mwenu, toeni sadaka kwa wenye uhitaji mfano mahospitalini, kwa yatima na wajane etc.

Sio kila mhubiri ni mtumishi wa Mungu wa kweli! Nyumba za ibada ni nyumba za biashara za watu.

Siku tukilitambua hili basi tutakombolewa.

Nyumba za ibada zimegeuka mshale na msumari wa moto kwa ukombozi wa mwafrika…

No, tutafuata Dini yetu Uislam.
 
Mashekhe wote wabongo njaa kuanzia kishiki,mziwanda na wengine waliobaki wenye misimamo shekhe ponda wengi ni empty bin
Kishki, Mziwanda, "dokta" Sule wote hawajasimama sawa. Huyo Ponda naye hajasimama sawa na ni mwanaharakati tu. Allah atuongoze sisi na wao.

Masheikh waliosimama sawa ni wale walio katika njia ya Salaf
 
Ndugu Masheikh
Nimewajibika kuandika barua hii kuwaomba kwa unyenyekevu mkubwa ACHENI KUTETEA dhulma dhidi ya watanzania wenzenu ktak madhila yanayowakumbuka.

NIANZE NA SULE
Wakati wa sakata la Ngorongoro, Mwanamihadhara ndugu Sule aliandaa clip ambayo ilisambazwa katika makundi ya kijamii ikieleza kuwa wamasai waishio ngorongoro ni wakenya waliovamia maeneo hayo kutoka Kenya. Katika kauli hizo akajaribu kuwaaminisha watanzania kuwa hao wamasai walioko ngorngoro hawastahili kuonewa huruma pindi serikali ikijaribu kuwatoa kwa sababu ni Wakenya.
Kauli hii ilikuwa ni ya ajabu sana hasa ukizingatia kwanza ni uongo, maana wamasai walioko ngorongoro walihamishiwa hapo na serikali hiyohiyo ili kupisha uanzishwaji wa hifadhi ya Serengeti miaka ya 1960's. lakini ukiachilia mbali hilo ile ni kauli isiyo na chembe ya huruma kwa watanzania wenzetu waishio ngorongoro ambao, walikuwa wananyimwa kila aina ya haki za kiraia na utawala huu wa Samia ili kuwapa maisha magumu waondoke. Kusema uongo ni kinyume cha Agizo la Mwenyezi Mungu anayetaka watu waseme ukweli!
Hata hivyo ndugu Sule amekuwa akilalamikiwa na waislamu wenyewe kwa kulete mafundisho ambayo wao wanaita ni Shirki, kwa kutangaza pete za Majini kuwa eti zina msaada kwa watu kitu ambacho masheikh wenzie wamempnga vikali kuwa asilete SHIRKI katika dini.

KWA SHEIKH MZIWANDA
Ndugu Sheikh mziwanda, umesikika ukidai kuwa wanaotekana nchini ni CHADEMA wenyewe, na ukatoa mfano wa Clip ya Dr Slaa ya miaka takriban minne akizungumzia tukio la kutekana katika chama. Kinachonisikitisha unanasibisha matukio ya sasa kwa kusema kuwa ni CHADEMA wanafanyiana hayo.
Ndugu Mziwanda, Muogope ALLAH, Tafadhali sana ndugu yangu, Wewe mwenyewe umesema una listi ya watu zaidi ya 100 waliotekwa kipindi cha Magufuli, Je Ndugu mziwanda hao wote walitekwa na CHADEMA?- Mo Dewji alitekwa na CHADEMA?,Roma mkatoliki alitekwa na CHADEMA?, Azory Gwanda alipotezwa na CHADEMA?

Kwenye kauli yako ukasikika unasema kuwa kipindi cha Magufuli walipotea zaidi ya watu 100, ukahoji kuwa mbona hakukuwa na maandamano?- Kwa hiyo ndugu Mziwanda, unataka kutwambia kuwa kwa kuwa watu hawakuandamana kudai jambo fulani kipindi cha nyuma basi ni makosa watu hao kuandamana kutaka jambo fulani leo hata kesho?. Sisi tunapata mashaka ndugu Mziwanda kuwa unataka kuchomeka hisia za udini, unataka watu waone kuwa kwa kuwa mtawala wa sasa ni muislamu basi kila dai lolote la msingi ambalo raia wa nchi hii wanalo basi eti wanaweka presha kwa sababu rais ni muislamu. NDugu mziwanda hiki unachokifanya ni kibya mno, si chema na kwa kweli kinagawa watu kuliko kujenga!

MZIWANDA, wewe hujitokeza mara nyingi wananchi wanapokuwa na ishu na serikali yao, wewe husimama kuitetea serikali tena kwa kuwagawa waislamu wajitenge na madai ya msingi ya kitaifa. Ulifanya hivyo katika mimbari kutetea uuzwaji wa bandari, ukadai kuwa mama anashambuliwa kwa imani yake.
Leo Umma unataka kutumia haki zao za kikatiba kuandamana ili mauaji na utekwaji vikomeshwe, wewe unakuja na kuongea na waislamu eti wajitenge na mambo hayo. SHEIKH HIVI UNASIMAMIA HAKI AU UNAWALINDA WATAWALA?

Sheikh: Kwani mtume si alisema ukiona jambo baya/ovu liondoe kwa mkono wako, ukishindwa kemea uovu huo, na kama kukemea huwezi si mtume alisema chukia?- SASA WEWE unasimamia wapi katika hayo matatu kuhusiana na matendo ya kutekwa, kupotezwa na kuuawa watu?. Je hutaki watu waingie mitaani kukemea uovu huo unataka wafanyeje?. Umesema kuwa wakati wa Magufuli walipotea watu zaidi ya 100, LINI WEWE UMEWAHI KUKEMEA JAMBO HILO WAZIWAZI UMMA UKAKUSIKIA?

SHEIKH MZIWANDA SI KWA SABABU SAMIA NI MUISLAMU BASI UNAJARIBU KUMLINDA NA KUMKINGIA KIFUA KWA KILA KITU KIBAYA!.

Ndugu Mziwanda, Mwenyezi Mungu katika Qur'an anasema kuwa sema kweli hata kama ukweli huo "unakunyooshea kidole" wewe mwenyewe. Sasa kama mtu inabidi ujishuhudie ukweli hata kama ukweli huo uko dhidi yako kwa nini unamkingia Kifua Samia eti kwa sababu Samia ni muislamu mwenzako tu?.
Je umesahau Khalifa mmoja wa kiislamu amewahi kumpa haki Myahudi licha ya kuwa kuna shauri mbele yake lililetwa linalomhusu muislamu na myahudi. Kwa nini alimpa haki myahudi badala ya muislamu mwenzie?

NDUGU MZIWANDA: Umekuwa ukijaribu kuwatenga waislamu wasiungane na watanzania wenzao kwa hoja za 1. Amani, 2. Mbona wakati wa magufulihaikuwa hivi
Ningependa kukwambia tu kuwa wanaotekwa, kupotezwa na kuuawa siyo wakiristu tu bali hata waislamu pia. Mo Dewji ni muislamu, Mzee Ally kibao ni muislamu. Sasa kwa nini hutaki waislamu waungane na waislamu wenzao kupaza sauti kukataa udhalimu huu?

SHEIKH MZIWANDA: Napenda nikukumbushe tu kuwa ukizuia WENGI KUDAI HAKI basi mtu mmoja mmoja kwa siri au kwa dhahiri ataamua kuidai peke yake, Je unajua kitakachotokea pale mtu mmoja bila kushawishiwa na mwingine, au kwa kumshirikisha mwingine ataamua kulipa kisasi?.

SHEIKH tafadhali tetea haki ya watu, usitetee "ULUA" wa watawala!
HAWA WAGANGA WA KIENYEJI TU, WANATAFUTA WATEJA WAPUMBAVU HAWA.
 
Ukweli ni kwamba katika Uislam kuna taratibu zilizowekwa katika kuamiliana na watawala. Haifai kuminyamana na watawala. Tumeamrishwa kuwatii watawala katika yasiyo ya haramu na kuwa na subra katika dhulma ya mtawala.

Na haifai kumkosoa mtawala hadharani, anayetaka kumnasihi mtawala amshike mkono au amuandikie kwa siri amnasihi. Umekutana na mtawala uso kwa macho hapo sasa ndio umepata fursa ya kumnasihi, basi mnasihi kwa busara iwapo kama ni kweli unataka kutoa nasaha. Au muandikie. Haifai kumtukana.

Lakini haifai kuwapinga na kuwakosoa hadharani. Sikuambii kuwafanyia uasi ndio kabisa.

Na kuhusu maandamano sijui mapinduzi hayafai. Sisi tumefundishwa kuwa na subra kunako dhulma ya mtawala. Hawawi madhalimu watawala ila kwa sababu ya dhulma za raia.

Dhulma ikidhihiri miongoni mwa watu; kukajaa washirikina wanaoabudu wengine pamoja na Allah au wakawaabudu wengine badala ya Allah, au kukajaa wazinifu, wezi, wadokozi, matapeli, waonevu na wenye kupokonya haki za watu na kadhalika basi Allah atawaoneshea athari ya maovu yao kupitia watawala wao. Watayaona hayo kwa watawala wao. Hivyo wakitaka kuondolewa watawala madhalimu, basi waache wao kwanza dhulma.

Ila migomo, maandamano, uasi na mapinduzi unazidisha shari na uharibifu na kuondoa amani.

Nimeandika haya sio kwa sababu hao "dokta" Sule na Sheikh Mziwanda ni masheikh zangu. Hapana. Allah awaongoze.

Allah atuongoze katika njia iliyonyooka. Allah atengeneze mioyo ya watawala wetu, awaongoze katika njia iliyonyooka, awafanyie wepesi na awape hikma na uadilifu. Allah aidumishe amani tuliyonayo, Yaa Hayyu Yaa Qayyum. Ameen.

Kama mtawala kaingia madarakani kwa utaratibu fulani aliokula kiapo kuuheshimu basi utaratibu huo ni mkataba.

Mkataba wetu ambao ni katiba yetu na sheria za nchi unaruhusu kumkosoa, mtawala, na unaruhusu maandamano.

Na kabla mtawala hajapewa hatamu anakula kiapo kuviheshimu hivyo vitu. Kwa hiyo inabidi aviheshimu tu kama hataki basi aachie tu hiyo nafasi.

Mfumo wetu wa utawala siyo Ukhalifa, ni Jamhuri
 
Kishki, Mziwanda, "dokta" Sule wote hawajasimama sawa. Huyo Ponda naye hajasimama sawa na ni mwanaharakati tu. Allah atuongoze sisi na wao.

Masheikh waliosimama sawa ni wale walio katika njia ya Salaf

Hao Salaf walijuaje kuwa wao ni Salaf.Na wewe unawajuaje kuwa ni Salaf?. Wana shahada yao iliyo tofauti?
 
Hivi kwa nini tunaishi kwa hisia. Hao wenye intelejensia yao kwa nini wasifanye uchunguzi watoe majibu, nani mtekaji?
 
Mkuu una hoja ila tuzidi kuwekeza fikra katika hoja yako....

Ni kweli wako wanaokariri tu na wasielewe maana yake.....

Ni kweli wako wanaopoteza muda kukariri elimu yoyote ile ila wasiielewe kwa undani na kuiishi......

Wako waarabu wanaojua kiarabu na wameshindwa kukariri hiyo Qur'an.....na wako waliokariri na wakaelezwa maana ya kila aya na wakafahamu vyema ila bado wakashindwa kuilewa maana yake ya ndani (Batin)....ndio wale wanaounga mkono UGAIDI na hata wakajilipua na kuwahiliki wengine......

Sheikh Ahmad Zarruq katika kushajiisha juu ya uelewa mpana wa elimu yoyote iwayo akasema maneno haya yafuatayo :

"Never give wisdom to unworthy as it unjust to the knowledgeables".

WISDOM.....

Unapoitafuta elimu ,usitumie tu nguvu kuipata bali nguvu na maombi kwa Mungu uyaelekeze akupe BUSARA juu ya hiyo elimu....

#Do Not Do Harm😍

#Milele ardhi tukufu ya Tanzania😍
Sule ni muhuni tu hamtakiwi kusikilizwa na mtu mwenye akili
 
Back
Top Bottom