Barua ya wazi kwa viongozi/wanasiasa wa juu

Barua ya wazi kwa viongozi/wanasiasa wa juu

fokonola bokoyoka

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2015
Posts
966
Reaction score
638
Siasa zenye tija na manufaa kwa nchi yetu.

Vyama vyote vya siasa vyenye nia njema na watu wa Nchi hii ni muda muafaka kutembelea maeneo ya vijijini na vitongojini ili kujionea hali ya maendeleo, bado changamoto ni kubwa sana tena kwenye yale mambo ya msingi kabisa hasa Maji, Umeme, Afya, Elimu, Kilimo/Ufugaji na Miundombinu.

Kwa haraka kabisa kwenye KAMPENI ya mwaka huu vyama vyote kwa maana ya Chama Tawala na vyama vya Upinzani hakuna MGOMBEA ambaye amepita huko zaidi wanakatiza tu kwenye Barabara Kuu wakati kipindi hiki kingesaidia vyama na wagombea kujua changamoto wanazokumbana nazo watu wa Vijijini na Vitongojini. Kule hali ni mbaya sana cha kusikitisha ni kwamba viongozi wetu waliopo madarakani na wale ambao wanaomba kupewa dhamana hamna ambaye anafanya ziara huko.

Barabara, Shule, Afya, Maji kwa kweli yanasikitisha sana. Ni vyema VIONGOZI wa juu kabisa hasa RAIS, WAZIRI MKUU na MAKAMU wa RAIS na kwa Vyama vya UPINZANI wale Viongozi wa juu hasa MGOMBEA URAIS, MAKAMU, MWENYEKITI NA KATIBU kufika kujionea hali halisi badala ya kuishia mijini na kwenye viunga tu. Watanzania wa huko wanaishi maisha magumu sana sana laiti kama VIONGOZI wa JUU wangekuwa wanafika huko naamini tusingesikia kabisa mtu anaahidi NDEGE au SGR maana kule hakuna huduma ya Afya, Zahanati inapatikana Kilomita mpaka 20 wakati huo huo njia hazipitiki, Shule ni mbovu pia hakuna waalimu na maisha ni magumu huwezi laumu MTUMISHI, Maji yanapatikana Kilomita mpaka 15 tena sio salama ni yale ya MABWAWA, Barabara ndio usiseme ni huzuni mpaka unajiuliza kweli na huku ni sehemu ya TANZANIA, Umeme ndio kabisa wala hamna matumiani.

Inawezekana viongozi wa juu hawafahamu hii hali maana wawakilishi wa huku wanajali zaidi matumbo yao au wakiwasilisha matatizo hawaeleweki, ushauri ni vyema viongozi wetu wa juu hasa RAIS, MAKAMU, WAZIRI MKUU wakafanya ziara kwenye haya maeneo ili wajionee wenyewe hali ilivyo naamini wataboresha SERA zao zaidi kwa kusaidia hawa WATANZANIA wenzetu.

Kwa kuendeleza haya maeneo Nchi yetu itakuza Uchumi wake kwa kasi sana, suala la msingi ni hawa viongozi wetu wa juu wakatembelea kwanza haya maeneo ya ndani ili wajionee kwanza. Ni rahisi sana wanaweza wakachagua baadhi ya mikoa hata kumi tu kama CASE STUDY ili wajue jinsi ya kutatua haya matatizo.

Ni muda muafaka kuacha KUAHIDIANA kwenye majukwaa ya SIASA/KAMPENI huduma MUHIMU kama Maji, Afya, Elimu Bora, Umeme, Kilimo/Ufugaji Bora, Miundombinu tena angalau ya Changarawe au Barabara zilizochongwa tu.

Mambo ya KUAHIDIANA ni kama SGR, NDEGE, TECHNOLOGIA na mengine kama hayo sio huduma za msingi Kama zilizotajwa juu.

MIAKA 59 YA UHURU HALI BADO NI MBAYA SANA.

Nawasilisha.
 
..nadhani dhana ya chama tawala na vyama vya upinzani ni tatizo hapa nchini.

..ni vizuri tukaviita vyama vya siasa, ili kuweka haki na usawa kwa vyama vyote.
 
Back
Top Bottom