drevaHiace
New Member
- Sep 15, 2021
- 1
- 1
YAH: CHANGAMOTO YA KUONGEZEWA GHARAMA ZA KAZI YETU ZA KUBEBA ABIRIA KUTOKA OFISI YA MKURUGENZI YA MANISPAA YA SUMBAWANGA
Mh. Waziri Mkuu,
Sisi ni madreva tunaoendesha magari madogo ya abiria maalum kama Hiace yanayofanya safari kuanzia Sumbawanga kwenda wilaya za Mkoa wa Rukwa ambayo ni bonde la ziwa Rukwa Wilaya ya Sumbawanga na kwa upande wa juu tunakwenda Matai Wilaya ya Kalambo na Namanyere Wilaya ya Nkasi
Mh. Waziri Mkuu, gari zote tulizotaja hapo juu zinazoanzia Manispa ya Sumbawanga kwenda maeneo hayo tumepata changamoto kubwa ya kuongezewa gharama za uendeshaji na ofisi ya Mkurugenzi Manispa ya Sumbawanga ambayo utatuzi wake tumeona ni ofisi yako inaweza kutusaidia kwa kuwa tumejaribu kuongea na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga imeshindikana, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga na Mkoa kote hatujapata msaada.
Mh. Waziri Mkuu, kwa nini tunaomba ofisi yako itusaidie, kwa sababu tumeona jambo hili ni mtambuka, Madreva tunaosafirisha abiria kwenda maeneo tajwa hapo juu tumeongezewa gharama za uendeshaji mara mbili baada ya stendi mpya ya mabasi yaendayo Mikoani ya Katumba kufunguliwa ambayo ipo umbali wa Kilomita 17 kutoka Sumbawanga Mjini barabara ya kuelekea Mbeya.
Mh. Waziri Mkuu, kutoka Manispa ya Sumbawanga kwenda Matai Wilaya ya Kalambo kuna umbali wa Kilomita takribani 45 ambapo tulikuwa tunapakia abiria kwa nauli ya shilingi 2,500. Baada ya Stendi mpya ya mabasi Katumba kufunguliwa gari zote tuliambiwa lazima tuanzie huko bila kujali gharama zinazo ongezeka kutokana na kuongezeka kwa umbali, mfano kwa gari zinazokwenda Matai, umbali ulio onezeka ni kilomita 34 kwenda na kurudi hivyo kuwa na jumla ya kilomita 89 lakini nauli ni ileile ya awali ya 2500 ambayo lililenga kilomita 45 tu. Lakini pia katika eneo hilo lililo ongezeka la kilomita 34 haturuhusiwi kubeba abiria na kama utapakia ukikamatwa faini ni shilingi 500,000 hadi 1,000,000
Mh. Waziri Mkuu, kwa umbali huo tunatumia lita 7 za mafuta ambayo gharama yake ni shilingi za Kitanzania 18,165 ambapo haturuhusiwi kubeba abiria hali ambayo imeongeza gharama za uendeshaji, Mh. Waziri Mkuu, lita 7 za mafuta kwa magari madogo hutumika kutoka Sumbawanga mjini hadi Matai Wilayani Kalambo, kwa hiyo kwenda na kurudi kwa sasa tunatumia kwa ajili ya mafuta tu shilingi 36,330, kwa hiyo kuna ongezeko la shilingi 18,165 zinazotumika bure baada ya katazo la kubeba abiria maeneo ambayo abiria hupatikana, Mh. Waziri Mkuu, abiria wanatoka maeneo tuliyotaja hapo awali wanakuja Sumbawanga mjini wakiwa na shida mbalimbali ikiwemo kuja kupata huduma za afya ukiwaambia waende umbali wa Kilomita 17 barabara kuu ya kuelekea Mbeya, kwenda kupanda gari ili warudi walikotoka hawawezi kukubali kutokana na kuongezeka kwa nauli ambazo wanatozwa kwenye bajaji ili wafike stendi kuu, na huladhimika kubaki maeneo jirani na mjini ili waweze kurudi makwao.
Mh. Waziri Mkuu, toka katazo hili kutoka ofisi ya Mkurugenzi, tuliomba ofisi yake kufanya kukaa naye ambacho kilifanyika tarehe 22/8/2021, kikao hicho hakikuzaa matunda, Mh. Waziri Mkuu waajiri wetu mwezi Septemba ni kipindi cha kulipa kodi kwa robo ya tatu ya mamlaka ya mapato (TRA) kulingana na changamoto hii inayotukabili itawasumbua namna ya kulipa kodi baada ya ongezeko la gharama ya uendeshaji.
Mh. Waziri Mkuu, katika maeneo tuliyoorodhesha hapo juu, kuna jumla ya gari 195, kodi inayolipwa na gari hizi si haba, gari moja inalipa shilingi 75,000 kwa mwezi ambayo kwa gari zote kwa mwaka, mamlaka ya mapato Mkoa wa Rukwa inakusanya jumla ya shilingi za Kitanzania 175,500,000. Lakini pia kuna taasisi zingine za Serikali zinakusanya kutoka kwenye gari hizi kupitia leseni mbalimbali mfano LATRA inatoza shilingi 45,000 kwa gari moja kwa mwaka ili kuruhusu itembee barabarani, inakusanya jumla ya shilingi 8,775,000, kuna mashirika ya bima, kwa gari inayobeba abiria 14 zina kusanya jumla ya shilingi 265,500, kwa gari zote, kwa mwaka jumla ya shilingi 51,675,000 hukusanywa, mbali na hiyo ili gari ipewe stika(leseni) kutoka LATRA lazima ipite Jeshi la polisi upande wa usalama barabarani na kukaguliwa, gharama ni shilingi 15,000 kwa kila gari ambapo jumla ya shilingi 2,925,000 hukusanywa, pia ofisi ya Mkurugenzi hukusanya pindi gari inapotoka stendi, kama kwa siku sitafanya kazi gari 50, gari moja hutozwa shilingi 1,000 hivyo jumla ya shilingi 50,000 hutozwa kwa siku na kwa mwaka hukusanywa shilingi 18,000,000. Kwa hiyo Jumla ya shilingi za Kitanzania 256,875,000 hukusanywa na Taasisi za Serikali.
Mh. Waziri Mkuu, kutokana na ongezeko la gharama za uendeshaji kuwa kubwa, sisi madreva wa gari ndogo zinazofanya safari za kwenda bonde la ziwa Rukwa Wilaya ya Sumbawanga, Mathai Wilaya ya Kalambo na Namanyere Wilaya ya Nkasi tunaomba turuhusiwe kutumia Stendi ya zamani ili kuepuka gharama kubwa za uendeshaji hasa upande wa mafuta ambapo tunaenda umbali ambao nauli inaingia mara mbili ya nauli iliyopo kwa sasa iliyopangwa na LATRA na sisi tupo tayari kulipa ushuru kama sheria za nchi zinavyotutaka.
Mh. Waziri Mkuu, tumeleta ombi letu kwako baada ya kuona changamoto yetu ni mtambuka inahusisha ofisi ya Mkurugenzi ambayo iko chini ya OR TANISENI, Jeshi la Polisi liko chini ya Wizara ya Mambo ya ndani ambalo linatukamata tukibeba maeneo ambayo abiria wanapatikana, Wizara ya Fedha inayohusika na ukusanyaji wa mapato kupitia TRA pamoja LATRA inayohusika na usimamiaji wa usafirishaji kupitia Wizara ya Uchukuzi na Usafirishaji ambao wanafahamu hasara tunayopata baada ya kulazimishwa tutembee umbali mrefu kwa nauli ya awali ambayo ni mahususi kwa umbali wa kilomita 45 tu, pia LATRA ndio wanaojua kupanga nauli kulingana na umbali wa gari inakokwenda lakini kwa masikitiko makubwa hawajatoa ufafanuzi wa gharama zinazotugharimu baada ya kuongezewa umbali tunaotembea.
Mh. Waziri Mkuu, umbali uliongezeka mfano ni sawa na gari Itoke Dar es Salaam kwenda Morogoro, gari hiyo irudi tena kutoka Morogoro hadi Dar es Salaam kwa nauli ya awali tu yaani Dar es Salaam hadi Morogoro.
Mh. Waziri Mkuu, hali hii inatugharimu sana hasa upande wa mafuta, pesa nyingi zinaishia kwenye kununua mafuta. Mh. Waziri Mkuu, hali hii inatishia ajira zetu kwa kuwa wajili wetu wanapata hasara. Kwa tunavyofahamu sisi, Serikali inasimamia ustawi wa wanachi wake kwa kuweka mazingira rafiki kwa kufanya kazi ili wapate kipato na kasha walipe kodi.
Mh. Waziri Mkuu, tunatanguliza shikrani zetu za dhati kwako na tunakutakia Afya njema katika majukumu yako.
Ni sisi madreva wa gari ndogo za kwenda bonde la ziwa Rukwa, Matai na Namanyere