Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Ndugu mheshimiwa Waziri naandika haya kukujuza kuwa. Kwa sasa nchini kiwango cha kelele mitaani kinatisha, ni jukumu la serikali kuchukua hatua ili kulinda Afya za wananchi na ustawi wa Taifa.
Ndugu Waziri, leo hii kwenye vituo vya mabasi, masokoni, mitaani, kelele zimekuwa ni nyingi na tena kubwa kupita kiasi.
Ndugu Waziri, nafahamu ofisini kwako ziko taarifa mbalimbali za Tafiti ya hali ya kelele nchini, zilizofanywa na taasisi mbalimbali za Elimu na utafiti nchini. Na miongoni mwa Tafiti zetu ni ile iliyofanywa na chuo kikuu cha Muhimbili kwa kushirikiana na UDOM mwaka 2019 ikionyesha kuwa zaidi ya asilimia 58 ya wafanyakazi wa viwanda vya nguo nchini WAMEPOTEZA USIKIVU.
Pia Tafiti zikaendelea kusema kuwa maeneo ya Mgahawa kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na SUA umevuka hadi kufikia 73dBA ambayo imezidi kiwango cha 55dBA ambayo ndiyo inayotakiwa.
Na tafiti nyingine ikasema kuwa maeneo yanayozunguuka mashine za kusaga kiwango cha kelele kinafika hadi 103dBA ambacho ni kiwango kikubwa sana cha kelele ambacho kinaathiri pakubwa mno uwezo wa kusikia.
Kutumia mtindo wa kupiga mziki mkubwa utadhani Disco siku hizi limegeuka ndiyo mtindo wa matangazo ya biashara.
Ndugu waziri, siku hizi kila anayetaka kutangaza biashara zake basi anatafuta spika kubwa na muziki mkubwa anauweka masokoni, anapita na maspika barabarani au anasimika maspika makubwa mahali na kufungulia muziki mkubwa non stop utadhani yuko ndani ya Disco. Hali hii siyo tu kwamba inaumiza masikio bali inakosesha utulivu kabisa. watoto wanaathirika, wagonjwa wanaathirika na hata raia wa kawaida nao wanaathirika.
ATHARI ZA HIZI KELELE.
Wataalamu wanasema kuwa Sauti inayofikia 75dB inaathiri uwezo wa kufikiri na kufanya kazi. Hii inamaanisha kuwa kwa kushindwa kudhibiti hizi kelele tunatengeneza Taifa la watu wenye uchovu wa kufikiri na hata tija ya utendaji wao wa kazi unashuka. Hii inashusha uwezo wa kuzalisha na hivyo kupelekea cycle ya umasikini kuendelea.
Wataalamu wanasema kuwa kiwango cha kelele kikishafika 90dB hii inaweza kupelekea watu kupoteza uwezo wa kusikia vizuri.
Uchunguzi wangu kuhusu kiwango cha sauti mitaa ya Dar
Kwa kutumia kifaa cha kupima sauti, nimepita katika maeneo ya mkusanyiko wa watu wengi katika soko la Bunju, na Kituo cha mabasi ya Makumbusho. Hapa kiwango cha sauti kinafika kati ya 85dB mpaka 87dB. Maeneo haya yamesheheni spika kibao, Makumbusho kuna Spika ya kutangaza biashara ya kampuni ya Simu ya Yas, Wanapiga DISCO mtindo mmoja, ni makelele ya kufa mtu.
Ndugu waziri hatuwezi kuwa Taifa la makelele. Hakuna mind iliyoproductive inayoweza kuwa bunifu, yenye fikra tunduizi, inayoweza kufanya kazi sawasawa katika mitaa iliyojaa makelele.
Najua Ipo sheria ya kudhibiti Kelele ya NEMC ya mwaka 2004 lakini sheria hiyo haisimamiwi. Serikali za mitaa hazifanyi kazi ipasavyo, na manispaa zinazotoa vibali vya matangazo hazifanyi kazi sawasawa kwenye hii ishu.
Ndugu Waziri na mhusika wa NEMC fanyieni kazi hili.
Nawasilisha!