Barua ya wazi kwa Waziri wa Mazingira na NEMC- Kelele mitihani ni tishio la afya za wananchi na Ustawi wa Taifa

Yaani utadhani nchi hii haina serikali kabisa. Huwezi kuuona Ujinga huu kwenye nchi za watu wanaojielewa.
Pita tu kariakoo pale. Uchafuzi wa kelele ni mkubwa sana. Watu hawana ustaarabu na serikali haijali kabisa kwa sababu watawala wana maeneo yao yasiyo na kelele.
 
Barua yako ina mashiko tatizo linakuja kwetu sisi wenyewe, mwanzo kulianzishwa msako wa makelele kwenye mabaa na kumbi za starehe wananchi wakaanza kelele maradioni watu kama walikua wanaandamana hivi na Jamaa wakaona isiwe tabu wakatuachia kelele zetu, so atupaswi kulalamika tena.
Uwajibikaji HAUPO tangu A Hadi Z !
 
Kama vile hakuna anayejali mwenye dhamana ya kudhibiti kelele. Vigodoro vimezidi vya kukesha hasa maeneo ya wazaramo
 
Mleta uzi umepiga henyewe hongera kwa hoja hii. Kelele sikuhizi imefanywa sehemu ya maisha ya mtanzania, si masokoni, kwenye usafiri wa umma (Mabasi na daladala), nyumba za ibada nazo ni makelele tuu (baadhi hasa hizi za kileo) nk. Kiufupi uchafu wa kelele umetapakaa na hivyo tusishangae kuona afya za akili za watanzania zikiyumba na hivyo tutaendelea kushuhudia matukio ya kushangaza yakifanyika sababu mojawapo ni uchafu wa ubongo unaosababishwa na makelele.
 
Kwa kelele hizi zilizopita kiasi mitaani, HAKUNA MIND za Watanzania zitakazokuwa na utulivu wa kutosha Kufikiri vyema, Kuinnovate. Kwa Hiyo tutaendelea kuwa na Jamii yenye ujinga mwingi.
 
Hakuna viongozi wa kulikemea hilo. Kila mmoja ni muoga sana, mji umekuwa mchafu sana. Hakuna utulivu kabisa.

Zamani ilikuwa unaweza kutoka na familia kwenda sehemu na kufurahi nao. Lakini sasa kila sehemu ni uchafu wa kelele tu.
Ukweli Dar es salaam ya sasa ni chafu sana tofauti na kipindi kile anaongoza Mkuu wa mkoa Makamba.
 
Ndugu mheshimiwa Waziri naandika haya kukujuza kuwa. Kwa sasa nchini kiwango cha kelele mitaani kinatisha, ni jukumu la serikali kuchukua hatua ili kulinda Afya za wananchi na ustawi wa Taifa.

Ndugu Waziri, leo hii kwenye vituo vya mabasi, masokoni, mitaani, kelele zimekuwa ni nyingi na tena kubwa kupita kiasi.

Ndugu Waziri, nafahamu ofisini kwako ziko taarifa mbalimbali za Tafiti ya hali ya kelele nchini, zilizofanywa na taasisi mbalimbali za Elimu na utafiti nchini. Na miongoni mwa Tafiti zetu ni ile iliyofanywa na chuo kikuu cha Muhimbili kwa kushirikiana na UDOM mwaka 2019 ikionyesha kuwa zaidi ya asilimia 58 ya wafanyakazi wa viwanda vya nguo nchini WAMEPOTEZA USIKIVU.

Pia Tafiti zikaendelea kusema kuwa maeneo ya Mgahawa kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na SUA umevuka hadi kufikia 73dBA ambayo imezidi kiwango cha 55dBA ambayo ndiyo inayotakiwa.

Na tafiti nyingine ikasema kuwa maeneo yanayozunguuka mashine za kusaga kiwango cha kelele kinafika hadi 103dBA ambacho ni kiwango kikubwa sana cha kelele ambacho kinaathiri pakubwa mno uwezo wa kusikia.

Disco siku hizi limegeuka ndiyo mtindo wa matangazo ya biashara.

Ndugu waziri, siku hizi kila ansyetaka kutangaza biashara zake basi anatafuta spika kubwa na muziki mkubwa anauweka masokoni, anapita na maspika barabarani na kufungulia muziki mkubwa non stop utadhani yuko ndani ya Disco. Hali hii siyo tu kwamba inaumiza masikio bali inakosesha utulivu kabisa. watoto wanaathirika, wagonjwa wanaathirika na hata raia wa kawaida nao wanaathirika.

ATHARI ZA HIZI KELELE.

Wataalamu wanasema kuwa Sauti inayofikia 75dB inaathiri uwezo wa kufikiri na kufanya kazi. Hii inamaanisha kuwa kwa kushindwa kudhibiti hizi kelele tunatengeneza Taifa la watu wenye uchovu wa kufikiri na hata tija ya utendaji wao wa kazi unashuka. Hii inashusha uwezo wa kuzalisha na hivyo kupelekea cycle ya umasikini kuendelea.

Wataalamu wanasema kuwa kiwango cha kelele kikishafika 90dB hii inaweza kupelekea watu kupoteza uwezo wa kusikia vizuri.

Uchunguzi wangu kuhusu kiwango cha sauti mitaa ya Dar

Kwa kutumia kifaa cha kupima sauti, nimepita katika maeneo ya mkusanyiko wa watu wengi katika soko la Bunju, na Kituo cha mabasi ya Makumbusho. Hapa kiwango cha sauti kinafika kati ya 85dB mpaka 87dB. Maeneo haya yamesheheni spika kibao, Makumbusho kuna Spika ya kutangaza biashara ya kampuni ya Simu ya Yas, Wanapiga DISCO mtindo mmoja, ni makelele ya kufa mtu.

Ndugu waziri hatuwezi kuwa Taifa la makelele. Hakuna mind iliyoproductive inayoweza kuwa bunifu, yenye fikra tunduizi, inayoweza kufanya kazi sawasawa katika mitaa iliyojaa makelele.

Najua Ipo sheria ya kudhibiti Kelele ya NEMC ya mwaka 2004 lakini sheria hiyo haisimamiwi. Serikali za mitaa hazifanyi kazi ipasavyo, na manispaa zinazotoa vibali vya matangazo hazifanyi kazi sawasawa kwenye hii ishu.

Ndugu Waziri na mhusika wa NEMC fanyieni kazi hili.

Nawasilisha!
Umaskini na tamaa vinadumaza uwezo wa kufikiria. Mtu anauza duka lake lakini anaruhusu wale vijana wanaweza kompyuta na kurusha nyimbo, wanapiga miziki kwa sauti ya juu kuanzia asubuhi mpaka jioni. Na kweli hao vijana wanapata pesa ya kula.

Matajiri anzisheni viwanda vidogo vidogo na vya kati ili vijana wakapate ajira viwandani waachane na mambo ya kurusha nyimbo na muvi mitaani
 
Ndugu mheshimiwa Waziri naandika haya kukujuza kuwa. Kwa sasa nchini kiwango cha kelele mitaani kinatisha, ni jukumu la serikali kuchukua hatua ili kulinda Afya za wananchi na ustawi wa Taifa.

Ndugu Waziri, leo hii kwenye vituo vya mabasi, masokoni, mitaani, kelele zimekuwa ni nyingi na tena kubwa kupita kiasi.

Ndugu Waziri, nafahamu ofisini kwako ziko taarifa mbalimbali za Tafiti ya hali ya kelele nchini, zilizofanywa na taasisi mbalimbali za Elimu na utafiti nchini. Na miongoni mwa Tafiti zetu ni ile iliyofanywa na chuo kikuu cha Muhimbili kwa kushirikiana na UDOM mwaka 2019 ikionyesha kuwa zaidi ya asilimia 58 ya wafanyakazi wa viwanda vya nguo nchini WAMEPOTEZA USIKIVU.

Pia Tafiti zikaendelea kusema kuwa maeneo ya Mgahawa kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na SUA umevuka hadi kufikia 73dBA ambayo imezidi kiwango cha 55dBA ambayo ndiyo inayotakiwa.

Na tafiti nyingine ikasema kuwa maeneo yanayozunguuka mashine za kusaga kiwango cha kelele kinafika hadi 103dBA ambacho ni kiwango kikubwa sana cha kelele ambacho kinaathiri pakubwa mno uwezo wa kusikia.

Disco siku hizi limegeuka ndiyo mtindo wa matangazo ya biashara.

Ndugu waziri, siku hizi kila ansyetaka kutangaza biashara zake basi anatafuta spika kubwa na muziki mkubwa anauweka masokoni, anapita na maspika barabarani na kufungulia muziki mkubwa non stop utadhani yuko ndani ya Disco. Hali hii siyo tu kwamba inaumiza masikio bali inakosesha utulivu kabisa. watoto wanaathirika, wagonjwa wanaathirika na hata raia wa kawaida nao wanaathirika.

ATHARI ZA HIZI KELELE.

Wataalamu wanasema kuwa Sauti inayofikia 75dB inaathiri uwezo wa kufikiri na kufanya kazi. Hii inamaanisha kuwa kwa kushindwa kudhibiti hizi kelele tunatengeneza Taifa la watu wenye uchovu wa kufikiri na hata tija ya utendaji wao wa kazi unashuka. Hii inashusha uwezo wa kuzalisha na hivyo kupelekea cycle ya umasikini kuendelea.

Wataalamu wanasema kuwa kiwango cha kelele kikishafika 90dB hii inaweza kupelekea watu kupoteza uwezo wa kusikia vizuri.

Uchunguzi wangu kuhusu kiwango cha sauti mitaa ya Dar

Kwa kutumia kifaa cha kupima sauti, nimepita katika maeneo ya mkusanyiko wa watu wengi katika soko la Bunju, na Kituo cha mabasi ya Makumbusho. Hapa kiwango cha sauti kinafika kati ya 85dB mpaka 87dB. Maeneo haya yamesheheni spika kibao, Makumbusho kuna Spika ya kutangaza biashara ya kampuni ya Simu ya Yas, Wanapiga DISCO mtindo mmoja, ni makelele ya kufa mtu.

Ndugu waziri hatuwezi kuwa Taifa la makelele. Hakuna mind iliyoproductive inayoweza kuwa bunifu, yenye fikra tunduizi, inayoweza kufanya kazi sawasawa katika mitaa iliyojaa makelele.

Najua Ipo sheria ya kudhibiti Kelele ya NEMC ya mwaka 2004 lakini sheria hiyo haisimamiwi. Serikali za mitaa hazifanyi kazi ipasavyo, na manispaa zinazotoa vibali vya matangazo hazifanyi kazi sawasawa kwenye hii ishu.

Ndugu Waziri na mhusika wa NEMC fanyieni kazi hili.

Nawasilisha!
Mleta mada na wewe acha kelele

Hamia maeneo yasiyo kuwa na kelele.kama hupendi kelele
 
Zamani ilikuwa unaweza kutoka na familia kwenda sehemu na kufurahi nao. Lakini sasa kila sehemu ni uchafu wa kelele tu.
Ukweli Dar es salaam ya sasa ni chafu sana
Hujalazimishwa kuishi Dar hama
 
Wako bize na uchaguzi 2025!
Hawana muda wala nafasi ya kutusikiliza!
 
Kwa kelele hizi zilizopita kiasi mitaani, HAKUNA MIND za Watanzania zitakazokuwa na utulivu wa kutosha Kufikiri vyema, Kuinnovate. Kwa Hiyo tutaendelea kuwa na Jamii yenye ujinga mwingi.
Ingekuwa utulivu unasaidia ugunduzi wasandawe wangegundua ndege
 
Kwa hili tunakubaliana kama nchi tumefeli. Kama ambavyo hakuna tulichofaulu.

Kila mmoja mmoja mchukia kelele apambane na familia yake kuhamia eneo lisilo na kelele. Mi nimehami ushuani, tatizo kuna barabara ya kwenda hospital, ni lazima ambulance ipite mara kwa mara hivyo kelele hii ni lazima haikwepeki 😂😂😭😭
 
Hicho kinaitwa kibomba,,,Hadi ombaomba wanavimiliki
 
Attachments

  • Screenshot_20250216-104152.jpg
    Screenshot_20250216-104152.jpg
    115.5 KB · Views: 1
Ndugu mheshimiwa Waziri naandika haya kukujuza kuwa. Kwa sasa nchini kiwango cha kelele mitaani kinatisha, ni jukumu la serikali kuchukua hatua ili kulinda Afya za wananchi na ustawi wa Taifa.

Ndugu Waziri, leo hii kwenye vituo vya mabasi, masokoni, mitaani, kelele zimekuwa ni nyingi na tena kubwa kupita kiasi.

Ndugu Waziri, nafahamu ofisini kwako ziko taarifa mbalimbali za Tafiti ya hali ya kelele nchini, zilizofanywa na taasisi mbalimbali za Elimu na utafiti nchini. Na miongoni mwa Tafiti zetu ni ile iliyofanywa na chuo kikuu cha Muhimbili kwa kushirikiana na UDOM mwaka 2019 ikionyesha kuwa zaidi ya asilimia 58 ya wafanyakazi wa viwanda vya nguo nchini WAMEPOTEZA USIKIVU.

Pia Tafiti zikaendelea kusema kuwa maeneo ya Mgahawa kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na SUA umevuka hadi kufikia 73dBA ambayo imezidi kiwango cha 55dBA ambayo ndiyo inayotakiwa.

Na tafiti nyingine ikasema kuwa maeneo yanayozunguuka mashine za kusaga kiwango cha kelele kinafika hadi 103dBA ambacho ni kiwango kikubwa sana cha kelele ambacho kinaathiri pakubwa mno uwezo wa kusikia.

Disco siku hizi limegeuka ndiyo mtindo wa matangazo ya biashara.

Ndugu waziri, siku hizi kila ansyetaka kutangaza biashara zake basi anatafuta spika kubwa na muziki mkubwa anauweka masokoni, anapita na maspika barabarani na kufungulia muziki mkubwa non stop utadhani yuko ndani ya Disco. Hali hii siyo tu kwamba inaumiza masikio bali inakosesha utulivu kabisa. watoto wanaathirika, wagonjwa wanaathirika na hata raia wa kawaida nao wanaathirika.

ATHARI ZA HIZI KELELE.

Wataalamu wanasema kuwa Sauti inayofikia 75dB inaathiri uwezo wa kufikiri na kufanya kazi. Hii inamaanisha kuwa kwa kushindwa kudhibiti hizi kelele tunatengeneza Taifa la watu wenye uchovu wa kufikiri na hata tija ya utendaji wao wa kazi unashuka. Hii inashusha uwezo wa kuzalisha na hivyo kupelekea cycle ya umasikini kuendelea.

Wataalamu wanasema kuwa kiwango cha kelele kikishafika 90dB hii inaweza kupelekea watu kupoteza uwezo wa kusikia vizuri.

Uchunguzi wangu kuhusu kiwango cha sauti mitaa ya Dar

Kwa kutumia kifaa cha kupima sauti, nimepita katika maeneo ya mkusanyiko wa watu wengi katika soko la Bunju, na Kituo cha mabasi ya Makumbusho. Hapa kiwango cha sauti kinafika kati ya 85dB mpaka 87dB. Maeneo haya yamesheheni spika kibao, Makumbusho kuna Spika ya kutangaza biashara ya kampuni ya Simu ya Yas, Wanapiga DISCO mtindo mmoja, ni makelele ya kufa mtu.

Ndugu waziri hatuwezi kuwa Taifa la makelele. Hakuna mind iliyoproductive inayoweza kuwa bunifu, yenye fikra tunduizi, inayoweza kufanya kazi sawasawa katika mitaa iliyojaa makelele.

Najua Ipo sheria ya kudhibiti Kelele ya NEMC ya mwaka 2004 lakini sheria hiyo haisimamiwi. Serikali za mitaa hazifanyi kazi ipasavyo, na manispaa zinazotoa vibali vya matangazo hazifanyi kazi sawasawa kwenye hii ishu.

Ndugu Waziri na mhusika wa NEMC fanyieni kazi hili.

Nawasilisha!
 
Hawajali, hii restaurant hapo wanapopikia chakula. mafuta ya kupikia yanatiwa kwenye maji taka.
Takataka zinatupwa ovyo
Jamaa wakipita wanapewa chao hawajali afya za watu
 
Attachments

  • VID_20250104_063837.mp4
    13 MB
Hawa wajinga ndio wameamua hivyo maana hata kwenye mikutano yao wanaleta waimbaji
Usitegemee mabadikiko kwani watakuambia ni wapiga kura wetu msiwanyanyase
Ni nchi inayoenda kwa kuogopa wananchi wake, hata sheria kutunga wanaziogopa
Ila kuna wajinga wengine huwa wanawatetea na sababu ni ushamba tu
Hawajawahi kutoka nje ya nchi na kuona nchi zingine zilivyo na sheria kali kwa ujinga huu wa makelele

Mtu anafurahia kelele za mziki kwenye Bus
Huku nje hata simu tu pameandikwa heshimu wengine kwa kuongea polepole
Nchi maskini ni Laana
 
Back
Top Bottom